(not debating, just leaving this here for Genuine Truth Seekers)
Proof of Jesus
HAKUNA mtu aliyeacha
nyayo nyingi kwenye historia kama Yesu Kristo,
HAKUNA!
Yesu Kristo ndiye Mtu
mashuhuri kupita wote kwenye historia,
nakuhakikishia.
1) Kwanza dini zote (ikiwemo dini ya atheism) zinamkubali Yesu Kristo, halafu Yesu anajikubali mwenyewe tu.
Wayahudi wanasema Yesu alikuwa Rabi/mwalimu.
Waislamu wanasema Yesu alikuwa nabii.
Wabuddha wanasema Yesu ni mtu aliyeangaziwa (enlightened).
Wahindu na imani za huko Mashariki wanasema Yesu alikuwa udhihirisho wa Mungu, mungu flani aliyechukua umbo la binadamu, mwalimu, mtawa, mtu mtakatifu aliyeamua kuachana na ya ulimwengu n.k.
New age spiritualists wanaohubiri power of the mind, wanasema Yesu alikuwa ni mtu aliyefuzu kwenye hiyo sekta.
Waamini
sayansi kuwa ndo itawapa majibu ya kila kitu (wakana Mungu) wanasema Yesu alikuwa jamaa mjanja mjanja, mwanasiasa flani ambaye alianzisha chama chake na kupata wafusi.
Kuna
viazi vichache vinasema Yesu hakuwepo kabisa.
YESU KRISTO hamtaji yeyote yule, anasema yeye pekee:
• ndiye
Njia inayotafutwa na watu,
ndiye
Kweli inayotafutwa na watu,
ndiye
Uzima wa binadamu
unakopatikana,
• ndiye
Mwanga kwenye ulimwengu
huu wenye giza,
• ndiye
Ufufuo kwani kifo sio mwisho,
• ndiye
Mlango wa kuingilia
Next
Level,
• ndio
Jina pekee tunalopaswa kuliitia,
sio majina ya watu waliokufa,
• ndiye
Mchungaji mwema atatupa kila tunachohitaji,
• ndiye
Mwana wa Mungu, Muumba aliyeingia ndani ya uumbaji wake mwenyewe, akawa
Mwana wa. Binadamu
• ndiye
Kristo/
Masihi/
Mwokozi, anayetuokoa na uharibifu (dhambi) na kifo ambacho binadamu anahangaika kukiepuka.
View attachment 3555599
(
kuna mtu atakwazika kisa YESU ni ngozi nyeupe. Acha ushamba! Katafute ngozi nyeupe uoe uachane na hizi hoja za bei rahisi)
2) Hakuna mtu mwenye
rekodi nyingi kumhusu kwenye historia kama Yesu Kristo.
-
Waongo na
wazushi wanasema hamna uthibitisho. Ni nini hasa
kinastahili kuwa uthibitisho?
Shida sio kuwa hamna uthibitisho, shida ni
hawapendi kuona wanachoona.
Yesu angekuwa ni mwalimu tu mwenye hekima ambaye hakuzaliwa na bikra, hakufanya miujiza, hakufufuka na kupaa mbinguni,
hakuna ambaye angepinga kuwa hakuna mtu mwengine kwenye historia ambaye kumbukumbu zake zilitunzwa kwa wingi kama Yesu.
- Kwa sasa tuna takriban hati za zamani
6000 za
agano jipya katika lugha ya
Kigiriki peke yake! Wastani wa hati moja ni
kurasa 450!
- Tukiongeza na nakala zilizotafsiriwa
karne za kwanza kwa
kilatini,
kiCoptic,
kiSyriac n.k tunakuwa na
makumi ya maelfu ya nakala za agano jipya. NI AIBU kwa waongo na wazushi!
-
Hakuna maandiko yoyote kwenye historia yenye
shehena la nakala kama agano jipya!
HAKUNA.
View attachment 3555597
View attachment 3555598
3) Vitabu vya Injili viliandikwa na watu
walioshuhudia hayo matukio.
Mpelelezi wa mauaji,
James Warner Wallace (J.W.W), mkana Mungu aliyegeuka na kumwamini Yesu anasema akiitwa kwenye tukio la mauaji, maelekezo ya kwanza anayotoa kwa polisi ni kuwa wawatenganishe
walioshuhudia hilo tukio. Maana wakikaa wote wataanza kujadili hilo tukio mpaka aje afike atakuta wana maelezo yanafanana fanana.
Lakini wakitenganishwa, akija kuwahoji mashahidi, maelezo yao huwa ni
shagala bagala, huenda yakaonekana hata kuwa
yanapingana. Lakini hiyo haimaanishi kuwa yanapingana.
Tena ukija
kuchanganya maelezo yao yanayoonekana kupingana ndo unapata picha vizuri kwasababu kila mtu anakuwa anasimulia kutokana na
mazingira aliyokuwepo wakati wa tukio, alichokuwa ana
focus,
hamu yake,
mtazamo wake,
makuzi yake n.k.
- Sasa basi, kitabu cha
Luka kinasema kabisa anayoandika daktari Luka ni shuhuda za
mashahidi alioenda kuwahoji (Luka 1).
- Mathayo na Yohana wanasema waliyoandika
walishuhudia kwa macho yao.
- Injili ya Marko inakubalika na wachambuzi kuwa ni Marko alikuwa akiandika kwa niaba ya mtume Petro aliyekuwa
anamsimulia, akimsaidia kutafsiri kwenda Kigiriki.
View attachment 3555593
Je kuna sababu yoyote ya
kushuku shuhuda hizi?
a) Utasikia "haiwezani kitabu cha 1 Petro kiwe kiliandikwa na mtume Petro kwasababu kimeandikwa kwa Kigiriki cha
kisomi kabisa na mtume Petro alikuwa
mvuvi kutoka Galilaya".
Sasa kwanini asijue kigiriki wakati maisha yake yote aliishi eneo ambalo watu waliongea kigiriki! !
Lakini pia inaoneka kuwa Petro alikuwa anamsimulia mtu anamuandikia.
Kama wazee wa kanisa (church fathers) wa
karne ya kwanza na ya pili kwenye barua zao walikuwa
wanarejea maandiko na wanakubaliana kuwa yaliandikwa na flani na flani, unakataa nini? ?
View attachment 3555592
b) Au utasikia "maandiko yenyewe yameandikwa
mamia ya miaka baada ya matukio kwahiyo yamebadilishwa au kutungwa ".
i) Kwanza
hatuna nakala halisi zilizoandikwa kwa mikono ya mitume wenyewe, sababu ni wazi:
•
Nyenzo walizotumia (ngozi) hazingeweza kudumu.
•
Muda mrefu umepita.
Nakala za historia zilikuja kuanza kudumu wakati walipoanzisha
taasisi za kutunza nakala hizi, ndomana unapokuja kukutana na
nakala yoyote ya historia ya zamani zaidi iliyotunzwa unaweza kukuta ni ya miaka zaidi ya 90, 300, 1000 baada ya kuandikwa kwa
nakala ya kwanza kabisa.
ii) Pia Nakala nyingi ziliharibiwa na waliochukia ujumbe wa Wakristo.
iii) Inawezekana pia waliiga utamaduni wa Wayahudi ambao
waliharibu nakala za zamani zilizochakaa kila waliponakili maandiko kwenye sehemu mpya.
View attachment 3555591
c) Kama watu wangetaka kubadilisha biblia, ingebidi wapitie njama za viwango vitatu:
i) Kwanza
njama ya hati - ingebidi wachukue zaidi ya
hati 6000 za kigiriki agano jipya wazibadilishe na wafiche ushahidi kuwa wamefuta wino wakabadilisha.
ii) Pili
njama ya lugha - Kisha itabidi wakatafute
maelfu ya hati za agano jipya zilizotafsiriwa kwenda
kilatini, kiCoptic na
kiSyriac wazibadilishe zote ziendane na uongo waliyoandika kwenye zile za
Kigiriki.
iii) Tatu
njama ya maoni ya wazee wa kanisa (early church fathers) - wazee wa kanisa wa karne za kwanza walikuwa na
utamaduni wa kuandika maoni/
uchambuzi kuhusu biblia.
Tukisema tutupe biblia zote, tunaweza kuunda
asilimia 95 ya agano jipya kwa kutumia
maandishi ya wazee wa kanisa tu! Kwahiyo wanaotaka kubadilisha biblia ingebidi pia wapitie
barua zote za wazee wa kanisa wabadalishe iendane na uongo walioandika kwenye
Kigiriki na kilatini, kiCoptic na kiSyriac.
Kusema kuwa Biblia imebadilishwa ndio
Conspiracy Theory kubwa kuliko zote kwenye karne yetu (ikifuatiwa na Evolution)
View attachment 3555590
d) Bila kusahau kopi tulizonazo za Injili
zinakaribiana umri na nakala halisi, mfano tuna kopi za miaka
100AD.
Linganisha na nakala zingine za kihistoria, mfano za mwanahistoria
Josephus ambaye kopi yake ya zamani kabisa tuliyonayo ni ya
miaka 1000 baada ya Josephus! ! !
Au za
Julius Caesar na vita zake kopi tuliyonayo ya zamani kabisa kumhusu ni ya
miaka 900 baada ya Caesar mwenyewe! ! !
Au
Aristotle, kopi yake ni ya
miaka 1400 baaya ya Aristotle! ! !
View attachment 3555588
e) Je tunaweza kujua wakati ambapo
nakala ya kwanza kabisa iliandikwa?
Kwa mfano, kitabu cha Matendo kilichoandikwa na Luka kinaongelea
utabiri wa kuharibiwa kwa Yerusalemu (Matendo 6:14). So tunaweza kuhitimisha kuwa kiliandikwa
kabla ya 70AD.
Kwenye kitabu cha Luka, Luka anasimulia jinsi Yesu
alivyotabiri kuwa Yerusalemu itakuja kuharibiwa.
Hakuna kitabu chochote kwenye agano jipya kilichosimulia tukio la kuharibiwa kwa Yerusalemu, zaidi ya kutoa
unabii kuhusu kuharibiwa kwa Yerusalemu (70AD)!
Unakuta mtu badala ya mtu kuhitimisha kuwa Yesu
anaweza kutabiri kwa usahihi, mtu anasema hivyo vitabu viliandikwa baada ya tukio kwasababu
haiwezekani kutabiri! ! !
Kwahiyo mtu
ameshaamua akilini kwake miujiza
haiwezekani kwahiyo akiona simulizi la utabiri uliokuja kutimia maana yake liliandikwa baada ya tukio! Hapo tayari umeleta
ubaguzi (bias) kwenye kupima
umri wa hizi nakala za kihistoria.
Kingine, wakati vitabu vya Matendo na Luka vinaandikwa bado kina Paulo, Petro, Yakobo
walikuwa hai (miaka ya vifo vyao unajulikana), wakati
vifo vya wafuasi wengine wa Yesu kama Stephano na Yakobo kaka ya Yohana vinatajwa.
Inawezekana mtu aandike historia ya Tanzania ya miaka ya 90
asitaje kifo cha Nyerere?
View attachment 3555585
f) Sasa tutajuaje kuwa nakala hizi za agano jipya zilizonakiliwa vizazi baada ya vizazi
hazijabadilika?
Tutafuata
mlolongo wa ulinzi (chain of custody).
Kwa mfano, aliyeandika kitabu cha
Yohana,
alimpa nani hiyo nakala?
Tunawajua baadhi ya
wanafunzi wa Mtume Yohana:
Ignatius,
Polycarp,
Papius.
Hawa wanafunzi nao wana wanafunzi wao
wanajulikana.
So tunaangalia kwenye huu mlolongo wa wanafunzi, Je simulizi kumhusu Yesu
linabadilika? Je Yesu alianza kama
mtu wa kawaida kadri muda ulivyoenda akageuka kuwa
Mungu mtu?
Hapana! Tangu kitabu cha Yohana hadi barua za wanafunzi wake (wazee wa kanisa) na wanafunzi wao, simulizi ni
lilelile: Yesu alizaliwa na bikra, alifanya miujiza, alikufa, akafufuka! ! !
Kitabu kama
1 Wakorintho kinakadiriwa kuwa cha miaka ya
50AD, na kinaongelea Ufufuo wa Yesu (1 Wakorintho 15). So Ufufuo wa Yesu ni habari iliyokuwepo tangu
karne ya kwanza, haikutungwa baada ya miaka kupita!
[ATTACH type="full" size="2550x1644"]3555584[/ATTACH]
Hata kuhusu vitabu vilivyokuja kurasimishwa kwenye
Baraza la Laodicea (363AD), ndo hivyo hivyo vilivyokuwa vinanakiliwa kwenye barua za wazee wa kanisa tangu
karne ya kwanza, na vilikuwa vinaitwa hivyo hivyo vinavyoitw -
Injili ya Luka, ya Mathayo n.k.
Baraza halikuja kuamua lolote jipya kuhusu vitabu zaidi ya
kukataa vitabu vilivyokuja kuibuka baadae ambavyo wazee wa kanisa
hawakuvitambua!
g) Kingine cha kutujuza kuwa nakala hazijabadilika ni uwepo wa
mamia na maelfu ya nakala za awali kabisa za agano jipya kwa visehemu au nzima nzima, kwa lugha zaidi ya nne tofauti.
Zingekuwepo kopi mbili tu kungekuwa na utata. Lakini ni maelfu ya nakala tena kwa lugha nne tofauti! !
View attachment 3555582
h) Utasikia "kitabu cha Mathayo hakijasema kimeandikwa na Mathayo kwa hiyo
hatujui nani kakiandika na hakiaminiki".
Unajua ni historia kiasi gani itabidi
tuitupilie mbali tukitumia hii hoja?
Hakukuwa na utamaduni wa mtu kuandika jina lake kwenye makala zake.
Tumeona hapo juu
(f), uhalali wa waandishi wa nakala hizi tunaupata kupitia
mlolongo wa umiliki (chain of custody).
i) Vipi kuhusu zinazodaiwa kuwa ni utata (
contradictions) zinazoonekana kwenye zile Injili nne?
Kwanza contradiction maana yake
haziwezi kupatanishwa. Kilichopo kwenye Injili ni tofauti (
variation) sio contradiction.
Kwa mfano, kwenye
ukoo wa Yesu, Mathayo 1:16 inasema baba ya Yosefu ni Yakobo huku Luka 3:23 inasema baba ya Yosefu ni Heli. Mtu anakimbilia kusema ni contradiction.
Lakini
Mathayo kafuata ukoo wa Yesu kupia
Solomon Mwana wa Daudi (Mathayo 1:6),
huku
Luka akifwata ukoo kupitia
Nathani mwana wa Daudi (Luka 3:31)!
Njia mbili tunazoweza
kupatanisha kisa hiki:
a)
Mathayo anafuata ukoo wa Yesu kupitia
Yosefu baba yake mlezi huku
Luka akifwata ukoo kupitia
Maria mama yake.
Ndomana Luka anasema "...na watu
walidhani yeye ni mtoto wa Yosefu mwana wa Heli...." (Luka 3:23 BHN).
Yosefu anakuwa mwana Heli kupitia
ndoa yake na Maria, hivyo Yesu anakuwa
mwana wa Daudi kupitia Maria
kisheria.
b) Au kupitia ile Sheria ya
kurithi mke (levirate marriage), kwamba Heli na Yakobo walikuwa Ndugu, kisha
Heli alikufa bila mwana kwahiyo Yakobo akamuoa mjane wake akamzaa Yosefu, kwahiyo
Yosefu alikuwa mwana wa Heli kisheria.
Unaweza kutafiti zaidi.
Je maelezo haya hayapatanishi Injili hizo?
View attachment 3555581
Mfano mwingine, kulikuwa na malaika mmoja au wawili kwenye kaburi la Yesu?
Mathayo 28 na Marko 16 inasema mmoja. Luka 24 na Yohana 20 inasema wawili.
Mpelelezi J.W.W anakwambia hajawahi kusikia mashahidi wawili wa tukio
wakikubaliana kila kitu.
Kwanza chochote atakachojibu shahidi
kinategemea swali ulilomuuliza, ndomana anaweza asitaje jambo muhimu sana kwenye kesi, ukija kuumuliza kulihusu anakwambia
hukuniuliza!
Na ndo anachoona kwenye kisa hiki cha malaika kwenye kaburi la Yesu. Waandishi wanaonekana kujibu
maswali tofauti.
Mathayo na Marko
hawajasema kulikuwa na malaika mmoja tu! Lakini Yohana na Luka wanasema waliwepo wawili.
Sasa kama kuna wawili si kuna mmoja! !
Hakijaharibika kitu.
Ili kuwe na contradiction, Mathayo na Marko waseme alikuwepo
mmoja tu.
Ukisoma vizuri utaona Mathayo na Marko walikazia issue ya
tetemeko na jiwe la kaburi.
Mathayo anaonekana kujibu swali "Ni nini kilisababisha tetemeko"?
Marko anaonekana kujibu swali "ni nani aliondoa jiwe kwenye kaburi"?
Luka anaonekana kukazia fikra kupotea kwa mwili kwenye kaburi.
Yohana yeye alikazia fikra ripoti ambayo wanawake hao walienda kutoa.
J.W.W anasema anavyoona jinsi ambavyo waandishi wa Injili hizi
hawakujihangaisha kulinganisha masimulizi yao Ili yafanane, ni
uthibitisho kuwa masimulizi haya ni ya
kutegemeka.
Hata yangefanana neno kwa neno,
wazushi wangekataa pia! Wangesema hawa watu
wametunga.
View attachment 3555580
4) Masimulizi kwenye agano jipya (na la kale) ni yenye
kutegemeka kihistoria.
Kuna taarifa nyingi za zisizo za kikristo za kihistoria kwenye biblia. Yani kama utamsoma Josephus (36-100AD)
ukamwamini na usijiulize mara mbili kama yuko sahihi au la, basi hata Injili unaweza kusoma bila kujiuliza.
Ukikuta tofauti kwenye taarifa fulani ya kihistoria (mfano issue ya sensa ya Quirinus wakati Yesu alipozaliwa) sio unampuuza Luka na kumsikiliza Josephus, maandishi ya Josephus
hayana mamlaka yoyote zaidi ya Luka.
Kwanza
Injili inakuwa na mamlaka zaidi kwakuwa yalionekana kuwa maandiko yenye thamani kubwa kwahiyo
yalilindwa sana, yalitunzwa, yalisambazwa na
kutafsiriwa!
Tofauti na maandishi ya wanahistoria kama Josephus ambaye hakuwa na watu
waliofuatilia na kulinda maandishi yake! ! Kama kuna
uongo amesema hakuna wa kumpinga!
Daktari Luka anasema: "....Watu wengi wamejitahidi kuandika juu ya mambo yale yaliyotendeka kati yetu. Waliyaandika kama tulivyoelezwa na wale walioyaona mambo hayo kwa macho yao tangu mwanzo, na waliotangaza ujumbe huo.
Inafaa nami pia, Mheshimiwa, baada ya kuchunguza kwa makini mambo yote tangu mwanzo, nikuandikie kwa mpango, ili nawe uweze kujionea mwenyewe ukweli wa mambo yale uliyofundishwa." (Luka 1:1-4 BHN)
Mtume Petro naye anasema: "Wakati tulipowafundisheni juu ya ukuu wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo,
hatukutegemea hadithi tupu zisizo na msingi. Sisi tuliuona utukufu wake kwa macho yetu wenyewe." (2 Petro 1:16 BHN)
Mtume Paulo anasema: "....alizikwa, akafufuka siku ya tatu kufuatana na Maandiko Matakatifu; kwamba
alimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea wale kumi na wawili. Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya 500 kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa." (1 Wakorintho 15:4-6 BHN)
Biblia ni nyaraka zenye
kutegemeka kabisa za historia.
Sio
hekaya au
hadithi!
Biblia sio
Gilgamesh epic!
Biblia iliandikwa na
mashahidi wa matukio halisi ya historia, wakishuhudiwa na mashahidi wenzao wa hayo matukio.
View attachment 3555579
5) Bila kusahau kuenea kwa ukristo karne za kwanza kulihusisha
mateso makali sana kwa wakristo.
Walichohitaji ni
kumkana Yesu halafu waepuke kifo waendelee na maisha yao,
lakini
mamia na maelfu walikubali kuuawa: walisulubiwa, walipigwa mawe hadi kufa, walichomwa moto wakiwa hai, walitupwa waliwe na wanyama!
Kuna
faida waliyokuwa wanapata kwa kushikilia hiyo Imani?
Pesa? Mamlaka? Wanawake?
Zaidi ya
mateso na
kudharaulika!
Au wote walikuwa
wanaota?
Ni nini kilichowasukuma?
Na kuna tofauti ya mtu
kukufuata kukuua kwasababu ya imani yako, na mtu aneyeenda
kujitoa kafara kwasababu ya imank yake.
View attachment 3555562
View attachment 3555578
6) Tuna
uthibitisho wa kutosha kabisa wa kukubali masimulizi ya Yesu
bila shaka yoyote (beyond reasonable doubt).
Haiwezekani kuwa na uthibitisho
bila shaka kabisa (beyond possible doubt).
Hiyo itahitaji kujua
KILA KITU na haiwezekani kujua kila kitu.
Hakuna anayeishi maisha kwa kiwango hicho cha
bila shaka kabisa maana hata nyumbani tusingetoka hadi mtu uwe na uhakika
bila shaka kabisa kwamba
hutogongwa na gari kesho,
hutopigwa na radi,
hutotekwa n.k.
Hata hukumu za wahalifu wabaya kuliko wote wanaohitaji kunyongwa
hazihitaji uthibitisho
bila shaka kabisa.
Nafasi ndogo iliyobaki kati ya
uthibitisho bila shaka yoyote na
uthibitisho bila shaka kabisa ndo nafasi ya maswali yako yasiyokuwa na
majibu.
Ni nafasi ya wewe kuchukua hatua moja tu, ya
IMANI.
Sio
Imani kipofu: ni
Imani yenye uthibitisho usio na shaka yoyote!
Kuwa na TUMAINI sio kuwa na
matamanio ya kufikirika.
Ni kuwa na uhakika wa mambo unayoyatarajia kutokana
uthibitisho usio na shaka uliopata.
"Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye."
Yohana.6.28-29.SRUV
"Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa maana kila mtu anayemwendea Mungu ni lazima aamini kwamba Mungu yuko, na kwamba huwatuza wale wanaomtafuta."
Waebrania.11.6.BHN
"Pimeni kila kitu: Zingatieni kilicho chema."
1Wathesalonike.5.21.BHN
View attachment 3555561