Dunia ya sasa ukiwa na watoto wengi kuliko mali ulizonazo wewe ni Maskini

Dunia ya sasa ukiwa na watoto wengi kuliko mali ulizonazo wewe ni Maskini

Mcanada

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2020
Posts
982
Reaction score
1,942
Dunia ya leo ni tofauti sana na ile dunia ya miaka 1000 iliyopita dunia ya leo kadiri unavyoongeza watoto unagundua ndivyo unavyojiongezea mzigo wa malezi, matunzo na nguvu ya ulinzi ya watoto wako kiroho na kimwili, Dunia ya leo upebari ndio unaoitawala na kuiongoza dunia kuliko ule mfumo wa Kijamaa ..

Kwa asilimi 99% ya wazazi wengi leo wana matatizo ya akili kuliko wasio na watoto kwasababu rasilimali walizonazo haziwatoshelezi watoto wao kiasi cha kuwafanya wafurahie maisha.

Watoto wengi leo wanapata malezi chini ya kiwango kutoka kwa wazazi wao kwasababu wazazi wanatumia muda mwingi kupambana kuongeza rasilimali zitakazotosha familia lakini wanagundua hata hicho wanachokitafuta hakitoshi kwasababu kadiri muda unavyokwenda mahitaji yanaongezeka na maisha yanakuwa magumu kwasababu mali tulizonazo hazitutoshi.

Asikudanganye mtu usizae bila mipango ukijidanganya kuwa kila mtoto anakuja na baraka yake dunia ishabadilika sana now days.. zaa watoto kulingana na uhitaji wako lakini pia angalia mali ulizonazo jee zinawatosha/zitawatosha? usije kuleta watoto kisha waje kuteseka kwasababu ya mzazi kushindwa kuwaandalia mazingira mazuri ya maisha yao yajayo. Mithali 13:22 (NENO); Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi,

Uwe na asubuhi Njema!
Ontario, Canada.
 
Niwe na angalau saba
artificialbloom-monkey.gif
 
Mimi kama kuna uwezekano na hakuna factor yoyote inayosumbua ( when pesa is kept constant), ninaweza kuwa nao hata tisa.

Napenda mno watoto.
 
Mtoto ni commitment sio tu kiuchumi, mtoto anahitaji maandalizi ya kiuchumi na kisaikolojia
 
Huu ni msemo wa hovyo sana, ingekuwa ni hivyo tusingeona watoto omba omba mitaani na barabarani.
Kama unawaona barabarani basi ujue ridhki ya mtu ipo miguuni mwake.

Watoto wa mitaani husababishwa na mambo mengi ikiwemo kufa kwa wazazi.

Mzazi mmoja kukataa mtoto na mwingine Hana uwezo.

Umasikini kwa familia zao

Tabia mbovu walizonazo

N.B unaweza kuzaa mmoja na Bado akawa mtoto wa mtaani
 
Back
Top Bottom