Mudi alikua anawekwa vizuri tu yaani sio swala la kuuliza.
Matoleo ya Biblia ya Kingereza
Katika utangulizi wa toleo la Biblia linalotumika sana, la Revised Standard Version, mtunzi ameandika yafuatayo:
"Biblia ya Revised Standard Version, ni marekebisho yaliyoidhinishwa ya toleo la American Standard Version, lilochapwa 1901, na ambalo nalo pia lilikuwa ni marekebisho ya toleo la King James Version, lilochapwa 1611...
Toleo la King James Version lililazimika kushindana na Biblia ya Geneva Bible (1560) juu ya kutumiwa na watu wengi; lakini hatimaye lilienea, na kwa zaidi ya karne mbili na nusu hakuna tafsiri ya Biblia kwa Kingereza iliyoandikwa na kuidhinishwa. Toleo la King James Version likawa ndilo "toleo lililoidhinishwa" kwa wanaoongea Kingereza... Ndio,
Toleo la King James Version lina dosari kubwa mno. Kufikia katikati ya karne ya kumi na tisa, maendeleo ya tafiti za Kibiblia vilevile kugunduliwa kwa miswada mingi ambayo ni ya kale zaidi kuliko ile iliyotegemewa na Toleo la King James Version, yamefanya toleo hilo kuwa ni wazi kuwa lina dosari nyingi na mbaya mno na kusababisha kuitishwa kufanyika marekebisho ya tafsiri ya kingereza. Kazi ikafanywa, kwa idhini ya Kanisa la Uingereza, mwaka 1870.
Toleo la Biblia la English Revised Version lilichapwa mwaka 1881 – 1885; na Toleo la American Standard Version, lahaja zake zimejiingiza katika upendeleo wa wanazuoni wa Kimarekani walioshiriki katika kazi hiyo, nalo lilichapishwa mwaka 1901.
Toleo la King James Version la Agano Jipya liliegemea matini za kigiriki zilizovurugwa kimakosa, ikiwemo kujilimbikizia makosa ya karne ya kumi na nne ya kunukuu miswada.
Nalo kimsingi, lilikuwa ni matini ya Kigiriki ya Agano Jipya kama lilivyoandikwa na Beza, 1589, ambaye kwa ukaribu zaidi alifuata chapa hiyo ya Erasmus, 1516 – 1535, iliyoegemea juu ya miswada ya zama za kati. Mswada wa kwanza na ulio bora zaidi miongoni mwa miswada minane aliyoishirikisha ulikuwa ni wa karne ya kumi, naye akautumia kidogo mno mswada huo kwa sababu unatofautiana sana na matini za kawaida zilizopokelewa; Beza alipata miswada miwili ya thamani kubwa mno, ikiwa ni ya karne ya tano na ya sita, lakini aliitumia kidogo mno kwa sababu inatofautiana na matini iliyochapwa ya Erasmus."
"... Toleo la American Standard Version lilipewa haki miliki ya kuzuia matini yake isibadilishwe bila idhini. Mnamo 1928 haki hiyo ilipatikana kutoka katika Baraza la Kimataifa la Elimu na Dini, na kwa hiyo likawekwa katika umiliki wa makanisa ya Marekani na Canada yaliyoshiriki katika baraza hilo kwa kupitia bodi zao za elimu na uchapaji.
Baraza hilo liliainisha kamati ya wasomi kusimamia matini ya ya Toleo la American Standard Version na kufanya uchunguzi na kujua kama marekebisho zaidi yanahitajika... [Baada ya miaka miwili] uamuzi ulifikiwa; nao ni kuwa; kunahitaji marekebisho kikamilifu katika toleo la 1901, ambalo litabakia kuwa lipo karibu na mapokeo ya Tyndale-King
James kama itakavyokuwa... Mnamo 1937 na marekebisho yalipewa idhini kwa kura ya Baraza hilo."
"Wasomi therathini na wawili walitumika kama wanakamati wa kamati iliyotakiwa kufanya marekebisho hayo, nao waliyalinda mabadiliko na kuishauri Bodi ya Ushauri ya wawakilishi hamsini wa madhehebu ili kushirikiana kufanya kazi hiyo... Toleo la Agano Jipya la
Revised Standard Version lilichapwa mwaka 1946."
Toleo la Biblia la Revised Standard Version, linajumuisha Agano la Kale na Jipya, nalo lilichapwa mnamo Septemba 30, 1952, na likakubalika sana."
Katika Toleo la Biblia la Revised Standard Version, idadi kubwa ya mistari muhimu kutoka katika Toleo la King James Version ya Agano la Kale na Jipya, ambayo wasomi waliiona kuwa imeongezwa katika karne za baadaye, iliondoshwa kutoka katika matini na kuwekwa katika tanbihi. Kwa mfano, kifungu maarufu sana katika Injili ya Yohana 8:7
kinachohusu mzinzi aliyetakiwa kupigwa mawe. Inasemakana Yesu amesema: "Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe."
Tanbihi za Toleo la King James (1952) zinaeleza "Mamlaka za kale mno zinaondosha aya za 7:53 – 8:11"
Kwa kuwa mswada namba 1209 wa Vatikani na mswada wa Sinaitic ya tangu karne ya nne haina aya kumi na
mbili hizo, wasomi wa Biblia wamefikia uamuzi wa kuwa maneno hayo hayatoki kwa Yesu. Mfano mwingine ni kifungu kinachohusishwa na Yesu na kinachotumika kama ushahidi wa rejeo la Utatu katika Maandiko matakatifu. Katika 1 Yohana 5:7, Inasemakana Yesu amesema: "Kuna watatu wanaoshuhudia huko mbinguni, Baba, Neno na Roho Mtakatifu: na watatu hawa ni mmoja"
Msomi maarufu sana wa Biblia, Benjamin Wilson, anaandika kuwa; maandiko haya yanayohusu "ushahidi wa
mbinguni" hayamo katika mswada wowote wa Kigiriki ulioandikwa kabla ya karne ya kumi na tano! Kwa hiyo, katika Toleo la Biblia la Revised Standard Version, mstari huu umefutwa na kutolewa katika matini tena bila ya kuwekewa tanbihi.
Hata hivyo, ili kuwe na idadi ya mistari iliyosawa baina ya Toleo la Biblia la Revised Standard Version, na ile ya Toleo la Biblia la King James Version, warejeaji wameugawa mstari wa sita na kuwa mistari miwili.