Duniani kote usafiri wa reli ndiyo rahisi kuliko wote. SGR tulitegemea kuwa kiama cha usafiri wa mabasi na malori, imeshindikana

Duniani kote usafiri wa reli ndiyo rahisi kuliko wote. SGR tulitegemea kuwa kiama cha usafiri wa mabasi na malori, imeshindikana

Pole sana kama jina la title ya thread hii limekukwaza. Bila shaka kama ingaliandikwa, "Duniani kote isipokuwa nchi chache kama USA, usafiri wa reli ndiyo rahisi kuliko wote ....", bila shaka haungalikwazika.

Licha ya maneno kuwa mengi, title kama hiyo ingalikosa nguvu na kupuuzwa on the spot na hawa jamaa zetu walengwa ambao wamekuwa wakituzengua sana hapa nchini Tanzania kila siku kwa masilahi yao binafsi. Jamaa hawa ni pamoja na TRC, LATRA, wafanya biashara wakubwa wa usafiri wa mabasi, semi trailer lorries na baadhi ya wanasiasa. Jamaa hawa wamekuwa wakiwaaminisha wananchi wetu kila kukicha kwamba America na nchi za EU ndiyo dunia. Na kwamba kinachofanyika America na ulaya ndiyo nasisi tunapaswa kukifanya. Wamefika hadi kututishia kwamba tutashitakiwa kwenye dunia tukishindwa kile dunia inataka tukifanye au tuishi. Hawa jamaa wanajifanya ni waumini wa mwimbaji maarufu wa USA, Michael Jackson aliyeimba, "We are the world" akiimanisha USA ndiyo dunia. Nadhani nimeeleweka.


Naomba tu usema facts na kama ni mawazo basi sema kwa mawazo yangu usiongee mawazo kama vile ni facts! Na kama ni facts weka data example nauli etc au uliza kwanza. Tumekuwa na tabia ya kuandika mawazo binafsi kama facts hivyo hili sio tatizo lako pekee ni utamaduni mbaya ambao najaribu kuutoa hasa hapa
 
Wacha wee...

Tuna Bush Lawyers, na bila shaka tunao Bush Economists!

Huoni aibu unavyojaribu kulinganisha labor intensive state vs highly advanced states?!

Unalinganisha nchi zinazozalisha malaki ya ajira kwa mwaka na hivyo kuwezesha labor movements among sectors of economy wakati nchi yako haina uwezo huo!!

Unalinganisha nchi ambazo zina malaki kwa malaki ya fursa huku nchi yako ikiwa na limited opportunities...

In short, as usual, uelewa wako katika masuala ya uchumi ni duni!!

Acha kukariri... tunazungumzia Tanzania na sio kwingineko duniani!!

All economic practices zinazofanyika kwa kuangalia kwingine duniani badala ya kuangalia mazingira ya nchi husika kwa kawaida ni practices zinazoishia kufeli.

Na ndo maana, back in 1993, akihutubia Jukwaa la Uongozi, Afrika, Lee Kuan Yew, aliyeipaisha Singapore alielezea jukwaa hilo sera zake zilzoifanya Singapore kuwa ilipo. Baada ya kueleza mengi, kisha akasema haya:-



Kozi zipi?

We jamaa mbona MUONGO SANA wewe?!

Kwahiyo hapo ndo tayari unadhani unafahamu vema masuala ya teknolojia na impact yake kwenye uchumi, ama?!

Before 2015 nimefanya sana kazi za freelancing, na moja ya lucrative gigs ilikuwa Translation kabla ya Wakenya hawajavamia.

Pamoja na kwamba zilikuwa translation softwares lakini bado ALL TIME Clients walilisisitiza Manual Translation!

Nalazimika kutoa hiyo mifano ingawaje hapakuwa na sababu za msingi kwa sababu hapa tunazungumzia ni namna gani unaweza kushabikia suala la kuondoa mabasi 500 kwenye mzunguko bila kuangalia economic impact. Hata hivyo, hapa unaishia kutoa mifano ambayo ni VERY IRRELEVANT.

Mfano mwingine IRRELEVANT... Jikite kwenye hoja!

Sasa kwa akili zako hizo si utasema huko nako tutumie robot kwenye huu ambao tunaelekea kwenye Agricultural AI !

Kwanini yasiendelee kutumika huko kwenye mabasi kisha tukaangiza mafuta mengine kwa ajili ya huko kwingine?

Kausome uchumi, na uuelewe!

Uchumi ni moja ya nyanja ambazo hazitaki kukariri bali kuelewa!

Ni wapi Mafisadi wanaweza kufaidika zaidi kati ya kuondoa mabasi barabarani na kuyaacha mabasi barabarani?

Kama reliable mode of transportation itabaki kuwa treni peke yake ina maana major players watakuwa Wanasiasa na Government Officials...

Hao ndio watatoa tenda za ku-supply nishati ili treni iendelee kuwa operational...

Hao ndio watatoa tenda za vyakula ili treni ziweze kuuza vyakula

Hao ndo watakamatia ajira kwenye sekta ya usafiri...

Hao ndo watakamatia tenda za kuagiza mabehewa mengi zaidi kwa sababu demand ni kubwa kutokana na monopoly..., and so on!

What about mabasi?

Kusoma
hujuji, ina maana hata picha ukutani huzioni?
Sasa wewe freelancer, huo uchumi nani kakufundisha au umepewa kazi ya kuwapigia debe hao matajiri wa malori na mabasi? Mbona huongelei juu ya maelfu ya roho za watanzania zinazopotea kila mwaka kwa ajali za malori na mabasi hayo barabarani? Mbona huongelei maelfu kwa maelfu wanappata ulemavu kila mwaka kutokana na ajali hizo Mbona huongelei uharibifu mkubwa wa barabara zetu unaofanywa na mabasi na malori hayo ambao unatugharimu matrilioni ya pesa?

Kwa taarifa yako, ulimwengu wa leo, ikiwamo Tanzania, unabadilika haraka sana kwa kasi kubwa. Mabadiliko haya yanasabishwa na kasi kubwa ya maendeleo ya teknolojia duniani kote. Tanzania ya leo ni tofauti sana na Tanzania ya enzi za Mwalimu Nyerere au Mkapa au Kikwete. Hizo enzi sasa hivi zinahesabika kama enzi za zamadamu.

Ulimwengu wa sasa umeingia zama ya Artificial Intelligence, robotechnology, genomics, genetic engineering/technology na automated systems. Ni ulimwengu ambao binadamu sasa wanaweza kupandikizwa micro chips za artificial intelligence vichwani mwao na hivyo kuwafanya kuwa superhumans. Hizi siyo fiction tena wala ndoto kama zilizokuwa zikisimuliwa enzi hizo. Kazi nyingi zilizokuwa zinafanywa na binadamu kwa mikono (manually), sasa zinaendelea kuchukuliwa na kufanywa na automated systems na functional intelligent robots kwa ufanisi mkubwa zaidi:
  • Hivi leo hata huko kwenye kazi yako hiyo ya freelancer, upatikanaji wa habari ni rahisi sana. Enzi hizo za zamadamu ilibidi mkazitafute SHIHATA. Leo kazi ya SHIHATA inafanywa na mtu mmoja tu anayeitwa Msigwa, wengine wote walishapoteza kazi na Msigwa pekee anazifanya kazi hizo kwa ufanisi mkubwa.
  • Leo hii huhitaji kwenda kununua magazeti (printed newspapers) kupata habari. Habari ye yote unaipata kiganjani kwako kwenye simu janja au tv. Hapo wafanyakazi wengi wa magazeti na uchapishaji walishapoteza ajira zao.
  • Leo habari na matukio mengi unayapata live kwenye tv yako au simujanja. Hauhitaji ma freelancers kama akina Chege waje wakusimulie. Hata burudani zote unazipata live ukiwa po pote pale. Huhitaji kusafiri hadi Qatar kuangalia kombe la dunia.
  • Leo viwanda vingi vinatumia automated systems kwa ufanisi mkubwa. Kiwanda kama cha textile kilichokuwa kinahitaji wafanyakazi zaidi ya 100 kwa shift, sasa kinahitaji wafanya kazi wasiozidi kumi tu kwa sababu shughuli nyingi zinafanywa na automated systems. Automated systems pia zinaepusha malalamiko ya wafanyakazi kupandishwa mishahara, migomo, ubadhilifu, rushwa etc
  • Leo hii ndege zinaendeshwa bila kuwa na rubani kwa ufanisi mkubwa zaidi. Hata hiyo ajali ya ndege ya Bukoba haingalitokea kama ndege hiyo ingalikuwa inaendeshwa na automated systems. Sasa hivi ndege za aina hii ndizo zinatumika zaidi kwenye uwanja wa vita. Muda si mrefu zitatumika uraiani na marubani wengi wa ndege watapoteza kazi. Tayari kuna magari yayosafiri bila ya kuwa na dreva. Hivyo kwenye enzi hii ya superhumans gari ndogo, malori, mabasi, treni, ndege na meli hazitakuwa na madreva au marubani. Zitaendeshwa na automated systems.
  • Leo hii kazi za bank tellers na cashiers zinafanywa na automated teller machines bila wizi na janja janja zingine. Wengi wa fani hizo wamepoteza kazi. Sasa hivi unaweza kuchukua au kuweka hela yako kwenye account ya benki yako ukiwa nyumbani na kuituma utakako. Huhitaji kwenda kujipanga benki. Na sasa crypto currency inakuja kumaliza utumiaji wa hayo makaratasi ya manoti ya mabenki kuu ambayo nayo wafanyakazi wao wengi watapoteza kazi.
  • Leo hii masanduku ya posta hayana kazi na wafanyakazi wengi wa posta walishapoteza ajira zao. Watu wanatumia emails, whatsapp mails, sms etc kwa ufanisi mkubwa kuliko hayo mabarua ya posta!
  • Leo kumbi za mahoteli mengi za mikutano hazina kazi. Zimebaki za kufanyia chereko chereko tu za birthdays na harusi. Mikutano mingi inafanyika live kimtandao.
  • Leo watu wote wenye komputa na simu janja wanajua kutumia keyboard na kuna automated softwares za voice recognition and dictation. Hivyo typists na secretaries wengi wameshapoteza ajira.
  • Leo ukataji wa tickets, travel bookings na hotel bookings zinafanyika kwa mtandao. Hivyo wafanya kazi wengi wa travel agents walishapoteza ajira.
  • Leo magari, treni, ndege, meli na mitambo mbali mbali ya viwandani inazidi kutengenezwa ambayo inatumia umeme badala ya dizeli au petroli. Hivyo muda si mrefu dunia itaachana na matumizi ya mafuta haya ya dizeli na petroli kama ilivyoachana na matumizi ya makaa ya mawe kwa kiasi kikubwa. Nchi na makampuni yanayomiliki biashara hii yamafuta yamejaribu kuzuia kwa nguvu nyingi na kwa muda mrefu ili hili lisitokee lakini nguvu ya maendeleo ya teknolojia imeshinda. Sembuse hawa wafanyabiashara wa mabasi na semi trella ndiyo watatushinda? Never over our dead bodies!
  • Na mengine mengi tu bwana freelancer ambayo hayaepukiki in this new era.
 
Back
Top Bottom