King Suleiman,
Mag3,
Nguruvi3,
Ningependa kujadili hoja zenu kwa pamoja.
Kero za muungano ambazo rais Kikwete juzi Alitamka Kwamba sasa zimeondolewa, kero hizi zimekuwepo kwa miaka 50 sasa, yani tangia kuundwa kwa taifa letu la "Tanzania". Hakuna Ukweli wowote Kwamba rasimu ya Mafichoni ya CCM imezitatua. Mfumo wa serikali Mbili umetumika kwa miaka 50 sasa, lakini Tazama idadi ya manung'uniko, malalamiko na hata hujuma za kuvunja muungano.
Hata rais alikiri Katika hotuba yake bungeni Wakati wa kuzindua BLK Kwamba - kuna utata mwingi kwenye mjadala wa suala la "Zanzibar ni nchi kamili inayojitegemea au ni sehemu ya jamhuri ya muungano". Cha ajabu ni Kwamba, Wakati wa makabidhiano ya rasimu ya mafichoni juzi, rais wa Zanzibar dr shein akatamka Kwamba "Zanzibar ni sehemu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania", jamani, what's going on??? Ina maana hata shein hajui Kwamba katiba aliyoapa kuilinda Kule Zanzibar inatamka Kwamba Zanzibar ni "nchi"????
Kina Sitta, lukuvi, Wassira, Chenge, migiro, na hata marais Kikwete na shein, hawa wote ni wanachama wa CCM. Na wanajua Kwamba ibara ya (1) ya mkataba wa muungano (1964) Inasema kuwa - jamhuri ya Tanganyika na jamhuri ya Watu wa Zanzibar zinaungana na kuwa nchi moja yenye mamlaka ya Kidola. Ibara ya (1) ya katiba ya muungano Inasema Kwamba "jamhuri ya muungano wa Tanzania ni nchi moja", lakini mabadiliko ya katiba Zanzibar (2010) yanaitambua Zanzibar Kama nchi kamili ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Lakini sio hivyo tu, ndani ya mabadiliko hayo, Zanzibar imekuwa nchi huru, imejiundia bendera yake, Wimbo wake wa taifa, Ina mihimili yake mitatu kamilifu - serikali, bunge, Mahakama, kwa Mujibu we katiba yake ili itambulike kuwa ni nchi kamili. Kwanini CCM wanataka kuchezea Watu akili?
Kuzima hoja ya serikali Tatu kwa namna wanavyofanya muda sio mrefu kutaufanya upande wa pili wa muungano Kuhoji nini kinaendelea. Tume ya jaji warioba ilifanya kazi nzuri sana ya kujaribu kutegua bomu hili. Katiba ya Zanzibar inaunda majeshi kwa Mwamvuli wa "idara maalum za serikali ya mapinduzi ya Zanzibar". Majeshi hayo yapo Katika ibara ya 12 ya katiba ya Zanzibar. Kitendo Hiki ni Kinyume cha katiba ya JMT ambayo inapiga marufuku mtu yoyote au shirika lolote au kikundi chochote kuunda na kuweka jeshi nchini/ndani ya JMT. Kwa maana hii, ni Wakati Rasmi sasa kwa CCM kuacha kutumia jina la mwalimu nyerere na mzee karume kutetea Mfumo wa muungano kwa Mujibu wa rasimu ya CCM ya mafichoni kwani Malengo ya serikali Mbili kwa nchi moja yalishakufa siku nyingi na kuzikwa pamoja na waasisi wa muungano. Ni taahira tu ndiye anayeweza kukubali Kwamba unaweZa kuwa na serikali Mbili Katika nchi Mbili. Ndani ya nchi Mbili AMA kuna serikali moja au serikali Tatu, basi!
Hoja Kwamba Kitendo cha Tanzania bara kuvaa koti la muungano hivyo kujinufaisha binafsi au kutumia rasimali za Zanzibar haiwezi kuzimwa kwa kuipa Zanzibar "uhuru wa bandia" wa kujiamulia masuala yake. Vile vile Mgawanyo wa Mapato ya muungano na uchangiaji wa gharama za muungano Kati ya serikali ya muungano na serikali ya Zanzibar hakuwezi patiwa ufumbuzi kwa kuwaambia Raia wa nchi Jirani ya Zanzibar Kwamba sasa mna uhuru wa kukopa nje, Kujiunga na Jumuiya za kimataifa, kuagiza bidhaa na kuendesha uchumi wenu bila ya kupitia Tanzania bara. CCM inatakiwa ijiulize - je, inapopinga serikali Tatu na kuleta serikali Mbili zile zile za miaka 50, je sasa Zanzibar wataridhika na Hali hiyo? Hawataibua Madai Mapya kuhusu Zanzibar kuwa nchi kamili? Je kuna mamlaka kamili Zanzibar bila ya uwepo wa Tanganyika?
Je tuseme Zanzibar wakanyamaza, je upande wa Tanzania bara, wao hawatadai Tanganyika Yao? Je, Hali ya hewa ya kisiasa ya 1984 haitajirudia, Tena Wakati huu kwa kuvunja Kabisa muungano?
CCM wanatakiwa kukaa chini na kutafakari haya:
Chama kijiulize, kwanini viongozi wa Zanzibar wamebadili msimamo ghafla kutoka serikali Tatu na sasa Wanaunga Mkono serikali Mbili Wakati kitovu cha malalamiko dhidi ya serikali Mbili kwa miaka 50 ni za zibT na sio Tanganyika? Kwa akili ndogo tu, CCM Inabidi iamke na kutambua Kwamba wake wote waliokuwa wanapigia chapuo katiba inayopendekezwa ni waumini wa serikali Tatu, sio serikali Mbili. Nitafafanua:
iwapo wangekuwa kweli ni waumini wa serikali Mbili, basi wasingesema Kwamba Zanzibar ni nchi kamili ndani ya muungano. Dr shein hawezi kutamka Kwamba Zanzibar ni sehemu ya muungano akiwa nchini Zanzibar, hayo anayatamka akiwa kwenye ziara nje ya nchi yake Yani nchini Tanganyika Kama alivyofanya juzi Wakati wa kupokea katiba inayopendekezwa.
iwapo viongozi wa Zanzibar wangekuwa kweli ni waumini wa serikali Mbili, baraza la wawakilishi lisingepitisha azimio la kutaka Mfumo wa serikali Tatu.
iwapo viongozi wa Zanzibar wangekuwa kweli ni waumini wa serikali Mbili, baraza la wawakilishi lisingeamuru Kwamba Sheria zote zinazotungwa na bunge la muungano ni lazima zipitiwe kwanza na baraza la wawakilishi Kabla ya Sheria hizi kutumika Zanzibar.
iwapo viongozi wa Zanzibar wangekuwa kweli ni waumini wa serikali Mbili, wasingevimega vitu vya pamoja vya muungano.
iwapo viongozi wa Zanzibar wangekuwa kweli ni waumini wa serikali Mbili, wasingetaka wapate bendera Yao, majeshi Yao, Wimbo wao wa taifa pamoja na uraia.
iwapo viongozi wa Zanzibar wangekuwa kweli ni waumini wa serikali Mbili, wasingesema Kwamba umaskini wa wazanzibari umesababishwa na muungano.
iwapo viongozi wa Zanzibar wangekuwa kweli ni waumini wa serikali Mbili, wasingedai wapi kuna fedha, wapi kuna rasilimali, Mafuta, gesi, na wasingepanga mikakati ya kutumia rasilimali hizi na pia sekta ya utalii kwa manufaa ya wazanzibari.
iwapo viongozi wa Zanzibar wangekuwa kweli ni waumini wa serikali Mbili, wasingedai mipaka ya Utawala Kati ya SMZ na serikali ya muungano.
iwapo viongozi wa Zanzibar wangekuwa kweli ni waumini wa serikali Mbili, wasingefanya mabadiliko ya katiba Yao 2010 kufanya serikali ya muungano kuwa Kama mbia wa Zanzibar huku katiba ya JMT 1977 ikitamka wazi Kabisa Kwamba rais wa muungano ni mtawala hadi Zanzibar.
iwapo viongozi wa Zanzibar wangekuwa kweli ni waumini wa serikali Mbili, wasingesema Kwamba Tanganyika imevaa koti la muungano, hivyo serikali inayotawala muungano ni serikali ya Tanganyika, huku serikali hii ikituhumiwa Kwamba inanufaika zaidi na rasilimali za pamoja.
Sent from my iPhone using JamiiForums