Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Barubaru,

Nashangaa sana kwanini umekuwa ni shabiki wa historia iliyopotoshwa na inayozidi kupotoshwa.
Nikulize, kwako wewe, nini ni legal foundation ya muungano? Jibuu dhahiri kwa waelewa wa historia ya kweli ni mkataba wa muungano (1964) ambao tume ya katiba imegundua kwamba historia ni kitu ambacho hakiwezi kwepeka; kumbuka mkataba huu ulikuwa na hadhi na pia uhalali wote wa kisheria za kimataifa.

Nikuulize swali lingine: Je articles of the union zinataja Tanganyika na Zanzibar kama nini kati ya haya - nchi shiriki (jamhuri mbili huru ) au serikali mbili shiriki? Jibu kwa swali hili pia kwa waelewa wa historia ni kwamba mkataba (1964) unataja Tanganyika na zanzibar kama jamhuri mbili huru, na katika ibara ndani ya hizi articles, unatambua kwamba jamhuri huru ya Tangayika ina serikali yake na watendaji wake wa kuendesha Taifa la Tanganyika as of April 1964, ndio maana mkataba ule ukasema pawe na kipindi cha mwaka mmoja kama kipindi cha mpito ambapo katiba ya jamhuri ya Tanganyika yenye serikali yake full functional ifanyiwe marekebisho ili iwe ni katiba ya muda ya JMT (kwa mwaka mmoja) na sheria kadhaa zifanyiwe marekebisho ili zitumike zanzibar kwa masuala yasiyokuwa ya muungano wakati zanzibar nayo ikijipanga kikatiba kusimamia masuala hayo kwani bado haikuwa na katiba yake kama jamhuri as of april 1964. Pia ikaelezwa kwamba rais wa muungano katika kipindi cha mpito asimamie masuala ya Tanganyika (kwa muda wa mwaka mmoja tu ambapo ndani ya hicho kipindi cha mpito, jamhuri ya muunngao ilitakiwa ianze mchakato wa katiba mpya. Lakini kilichotokea ni kwamba kile kipindi cha mpito ambapo rais wa jmt alitakuwa asaidiane na makamu wake (kutoka zanzibar) kuteua tume ya katiba na baraza la kutunga katiba, haya hayakufanyika a badala yake zikaja sheria za muungano kwa nia ya kuufunika mkataba, huku pia suala la tume ya katiba na baraza la kutunga katiba vikiachwa bila utekelezaji. Hizi ndio zikawa ni hatua za mwanzo za kukiuka mkataba wa muungano. Kilichofuatia ni katiba ya muda kutangazwa siku chache kabla ya kipindi cha mpito to expire.

Swali langu kwako barubaru: Je unajua asili ya jina na Tanzania Bara ni nini? Jibu ni kwamba miaka miwili baada ya katiba ya muda kupitishwa (yani 1967), uchakachuaji wa mkataba ukazidi kushika kasi ambapo sheria namba 22 ya mwaka 1967 ilipitishwa kwa nia ya kuifukia Tanganyika na kuweka jina la Tanzania Bara kama mbadala. Sambamba na hili, tukumbuke kwamba TANU ilishajiingiza kwenye suala la muungano kupitia sheria za muungano 1965 (kinyume na mkataba wa muungano ambao hautaji vyama), hivyo TANU ikasubii upenyo kupitia sheria batili, na tangia hapo chama hiki kikachukua majukumu ya kusimamia masuala ya muungano na yasiyo ya muungano huku ikisema Tanzania ni nchi ya chama kimoja wakati znz kulikuwa na ASP. Hapa hoja yako juu ya kutofautisha serikali na chama ndio inakuja - TANU ikawa serikali na serikali ikawa TANU, hivyo kimsingi tofauti unayomuuliza Nguruvi3 haikuwa na maana tena.

Hadi hapa, serikali ya Tanganyika ilikuwepo ila jina Tanganyika (kiserikali) likafutwa na sheria tajwa hapo juu lakini kimsingi majukumu yake yakahamishiwa kwenye chama cha siasa ambapo katiba ya 1965 ilikipa chama hiki madaraka ya juu kabisa ya kuendesha nchi. Kwa maana hii, majukumu ya Tanganyika kiserikali yaliendelea kuwepo kupitia chama - mwanzo wa kiini macho.

Hapo juu unajadili juu ya Tanzania bara na kusema Tanganyika haipo, Je unajua kwamba kuna wakati pia kulikuwa hakuna zanzibar bali Tanzania Visiwani? Ni muhimu ukawa na uelewa kwamba kupitia katiba ya JMT ya 1977, katiba hii ilikuja na sheria za kuua zanzibar (kama sheria namba 22 ilivyoua Tanganyika 1967), hivyo sheria ya 1977 ilifuta zanzibar a na kuzalisha Tanzania visiwani. Miaka miwili baadae, Zanzibar ikaja na Katiba yake ya kwanza kama Taifa huru baada ya mapinduzi, na katika mabadiliko yaliyofuatia baadae kikatiba nadhani 1981, wakarudisha jina zanzibar na kulifuta Tanzania visiwani, hivyo kurudisha heshima ya mkataba. Tanganyika ilitakiwa irudi kwa mtindo kama huu wa zanzibar kwa kuipatia Tanganyika katiba yake separate na ile ya JMT. Kwa bahati mbaya Tanganyika haikuweza fanya hivyo kwani Tanganyika ilifanywa ndio Tanzania na kubeba koti la muungano.

Kwa maana hii basi, lazima uelewe hoja ya nguruvi3 hapo juu kwamba Tanganyika imekuwepo throughout kama serikali na vile vile kama nchi kwani legal foundation ya muungano pamoja na uwepo wa katiba ya 1977 iliendelea na inaendelea kuwa mkataba wa 1964 ambao unatambua Tanganyika na znz kama two sovereign states zilizo surrender baadhi tu ya mambo huku yaliyosalia yakitakiwa kuendelea kuwa chini ya nchi shiriki ambapo Tanganyika ilikuwa pia na serikali yake, na znz iliazima sheria za hapa na pale (modified) huku nao wakijipanga kuwa na serikali yao yenye katiba yao ndani ya mwaka mmoja. Kwahiyo basi the fact kwamba nchi iliendelea kutawaliwa chini ya serikali mbili kupitia katiba ya jmt 1977 haina maana kwamba serikali ya muungano had legitimacy kikatiba. Legitimacy yake ilitokana na other things - azimio la arusha, historia ya tanu na asp kutetea wanyonge ndani na nje ya nchi (hasa tanu) na charismatic and integrity ya nyerere. Umma ulikiamini chama na serikali bila kujali katiba. Those days are long gone, ndio maana bila ya uhalali wa kikatiba, ccm haiwezi kuishi kwa amani, kwani umma unataka kushirikishwa katika kujenga uhalali huu, na uhalali huo unazidi kuonyesha kwamba utategemea sana kuheshimiwa kwa legal foundation of the union (mkataba wa 1964) ambao bado unatambua Tanganyika na zanzibar kama two sovereign states zinazotakiwa kuwa na serikali zake kusimamia masuala yao yaliyo nje ya muungano, hence logic ya serikali tatu kwenye rasimu ya katiba.

Huu ni wakati muafaka wa taifa kuongozwa nna serikali ambazo source zake za legitimacy ni katiba, na sio utashi wa vyama vya siasa na mambo mengine ya ovyo.

Mkuu Nguruvi3, historia imepotoshwa sana na wada kama Mkandara inaonekana sio tu kwamba wameafiki upotoshaji huo bali wameanza kuujengea uhalali. Hili ni tatizo. Tutalijadili zaidi ukija na mjadala wako ulioahidi hapo juu ambapo nitatumia fursa hiyo kujibu baadhi ya hoja za mkandara.

Cc JokaKuu


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi heshima mbele kiongozi, wanasema vijana wa leo

Upotoshaji ninaouona hapa ni wa kiwango cha juu sana. Kwamba ipo znz na JMT. Hatuelezwi muungano unakuwepo vipi kama hakuna washirika. Mkandara anasema mshirika mmoja ni znz halafu mwingine ni muungano! Jamani, jamani!

Tumeambiwa kuna Tanzania bara, nimemuuliza Mkandara Tanzania bara ni nchi gani, ilianza lini na kwa utaratibu gani.
Hilo hana jibu, na nilijua hana kwasababu Kinana, Pinda na Nape hawana pia.

Anasema JMT inainyonya znz, sasa nimeuliza hivi itaionyanyaje wakati JMT na znz imo?
Wakasema kuna mambo yasiyo ya muungano, nikakubaliana nao na kuwauliza nani ashughulikie hayo yasiyo ya muungano?
Hakuna jibu.

Historia inasimama yenye hata kama itapindishwa kwa nuclear energy. Historia haiumbwi au kufanyiwa modificatiions, ipo tu na inajitengeneza na kujisamimia yanyewe
 
Walioomba kwa niaba ya SMT ni kina nani? maana ujue hii habari ya Kinyemela ni msemo tu wa watu sisi hatujui ni kina nani walihusika na nadhani hata Wazanzibar wachodai ni kuwepo kwa vitu hivyo pasipo ridhaa yao. Hata habari ya serikali 3 ilianzishwa upya na kina Sharrif Hamad na wafuasi wa CUF na sii BLM sisi tulisha isahau toka malecela na Jumbe walipowekwa pembeni.

Hivyo tusiseme vitu kwa sababu tunamsikia sana Jussa akipiga makelele. hata Mtikila kisha tukana sana juu ya Wahindi wafukuzwe sidhani kama anawakilisha mawazo ya Watanzania. Hivyo, tuwe makini sana na swala hili ndio maana nasema Muungano wetu ulikuwa wa pekee na tusirukie vitu kwa sababu tu mnawasikia kina Jussa na Maalim Seif wenye sauti kubwa ZnZ kama Lema na Arusha yake. Lema hawakilishi mawazo ya Watanzania wala wana chadema wote ni wajinga tu ndio watamsifia.

Na ndio maana mimi nasimamia kusema hivi ikiwa hayo mambo 11 mengine yaloongezwa yalipitishwa na BLM basi ni halali kwa sababu BLM ndio pekee wenye mamlaka hayo. Hili la Elimu ya juu kufikia mwaka 1969 sisi tulikuwa na vyuo gani? maana tusiseme tu habari hizi wakati sisi wenyewe hadi tunapata Uhuru tulikuwa na wasomi walokwenda kusoma nje wengi wao ikiwa Uganda na Kenya. Na Zanzibar ilikuwa na wasomi wengi kutuzidi huo ndio ukweli.labda Kwa hiyo tuwe na fact kwanza maana Nassor Moyo alikuwa mjumbe wa BLM hivyo naweza kuamini kuwa iliongezwa mapema miaka ya 70 kufuatia labda mipango ya Ujenzi wa vyuo Tz bara.

Nachokuomba kufahamu ni ya kwamba kero za Muungano zimetokana na kiburi chetu sisi wote. Aidha tumekuwa tukijineemesha sisi bara kwa jina la Jamhuri ama wao wamechukua hatua mbaya kujibu kero hizo na sasa watu wanatazama reactions kufikia maamuzi ya kuunda serikali 3 pasipo kuitazama source ya kero hizi. kuunda kwa serikali 3 hakuondoi kero za Wazanzibar wala Watanganyika.

Nitakupa mfano mwingine. Tuseme wewe umeoa mke na kwa bahati mbaya mkeo anadai kila siku kunyimwa haki zake za kike, iwe kwenda sokoni, Kitchen party au mipango ya Upatu lazima umwekee kizuizi lakini wewe mwanamme unashinda nje ktk Mabar hadi usiku wa manane ukirudi umelewa na usiulizwe (rushwa na Ufisadi)! Ikafika mwanamke kaamua aidha apate naye uhuru kamili wa kujiamulia mambo yake kama wewe ama laa basi ndoa hiyo ife ijulikane kabisa kila mtu huru maana kachoka na kunyanyaswa ktk maswala yake ya kike ama hata kukujulia hali yako mwenyewe ktk ulevi imekuwa ni kosa lake.

Wewe kwa hasira ya majibu hayo ya mkeo na pasipo kupima kwanza kwa nini mkeo kafikia kuomba uhuru wake ktk maswala ya kike unasema, taraka sitoi ila unapendekeza separation ili kila mmoja wenu awe huru kabisaa. In a real fact, ni kwamba separation ni njia ya kuelekea kuvunja ndoa na sii kuiimarisha. Kisha basi kwa nini usitazame mgogoro wenyewe haswa ni kipi? kama hataki wewe ushinde bar hadi usiku mkubwa kwamni kuna taabu gani kuacha tabia hiyo? na kama ikiwa hupendi mkeo aende ktk hizo Kitchen party na Kuchanga Upatu mwambie kwa njia nzuri zaidi na sio kwamba kule wanawake wote malaya tu watakufundisha mambo mengine mabaya. hapo unakuwa hujataka ku solve proble ya ndoa ila unachukua njia ilo kuwa rahisi zaidi kulingana na matamanio yako.

Hivyo ndio kusema serikali 3, kwa jinsi navyoelewa muundo wa serikali za nchi hakuna litakalo badilika kwa Zanzibar maana tayari wanavyo vyombo vyote isipokuwa kinachoongezeka hapa ni kuzaliwa upya kwa Tanganyika. Yale matatizo na sumu ya Muungano hatukuyagusa kwa sababu separation au divorce sio suluhu ya Ndoa ila ni hitimisho baada ya kushindwa kupatana.

Kwa maoni haya ya serikali 3, Tanganyika itabidi kuunda upya katiba yake, na mihimili mitatu kujengwa hapo tunazungumzia wizara zisizopungua 20. Mahakama yake na bunge lake.. Sasa ikisha kuwa hivyo ina maana katiba hii mpya haitafaa tena maana kuna vipengele ambavyo vitahitaji kutokuwa vya Kitaifa bali kila nchi ina mamlaka navyo.

Kutokana na kuzaliwa kwa tanganyika katiba mpya mnayoiandika leo haitafaa tena itabidi tuanze Upya Alif kwa ujiti. Hii akili kweli..Kwa nini tusirudi nyuma tukaziangalia hizo kero za Wazanzibar halafu nasi Bara tuziweke zetu ili tupate suluhisho ya hizi kero badala ya kuamua kuvunja ndoa.

Nachosema mimi matatizo ya ndoa yapo kwa kila nyumba, kinachotakiwa ni kuya face matatizo yenyewe uso kwa uso na sii kuyakwepa kwa kutafuyta njia ilokuwa rahisi wakati kosa sii la ndoa bali nyinyi wenyewe mloingia ktk ndoa. Ndoa hata siku moja haiwezi kuwa mbaya au haramu haramu ni nyie mloingia ktk ndoa.
 
Mkuu umesema sisi tunataka kuipotosha Historia japo sijui ni wapi nilipoipotosha historia ila nakuomba nionyeshe mahala popote ktk katiba ya mwaka 1977, 1984 au 2010 inayosema ama kuitangaza nchi ya Tanzania visiwani maana katiba ndio mwongozo. Leo hii Tanzania bara inaitwa Bongo sijui nayo vizazi vyetu huko mbele vitakuja kudai kuwa nchi ya Bongo ilikuwepo kikatiba au?

Bila shaka mtu anapotaka kuzitambulisha nchi zilizomo ktk Muungano wetu tulitumia Tanzania Bara na Tanzania visiwani lakini hizi sio nchi zinazotambulikana kikatiba wala kkisheria. Ni mwelekeo wa kufikia tu Tanzania moja hatua kwa hatua. Hakuna wala haikuwepo nchi ya Tanzania bara wala Tanzania visiwani ni msemo rarisi ulotumika kutofautisha nchi zetu ktk muungano.

Nguruvi3, sijasema mshirika mmoja ni Zanzibar na mwingine ni JMT. Muhimu unielewe kwanza kabla ya kuropoka maana JMT ina nchi mbili ambazo ni Tanganyia na Zanzibar yenye mihimili yake kama Taifa moja. Huwezi kuiondoa Zanzibar ktk JMT kama mnavyotaka isomeke kuwa JMT ni Tnganyika - hapana. JMT ni nchi mbili na ndio maana husikii Zanzibar wala Bara ila JMT, isipokuwa kuna serikali ya pili ambayo ni serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tanganyika haipo tena na ndio maana bara hatuna serikali, mahakama wala bunge letu na ndio maana ya shinikizo la kuirudisha linapamba moto wewe ukiwa mpambanaji mtia maji.

Unaposema neno JMT hakuna yalokuwa ya Zanzibar wala ya bara ila ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali yake ni serikali kuu, federal hakuna serikali ya Tanganyika ndani ya JMT. Rais JK ni rais wa JMT sio rais wa Bara ama Mwinyi alikuwa Visiwani. Bunge lake ni la JMT na sii kwa bara wala Znz tu na kadhalika. Mnapenda sana kupotosha maandishi ya mtu ili isomeke vibaya wakati ni wewe mwenyewe hukuelewa nilichoandika.
 
Last edited by a moderator:
Kama ni nchi mbili Tanganyika na Zanzibar iweje leo tuna Zanzibar hatuna Tanganyika. Hebu twende kwa hatua.Tuonyeshe Tanganyika ilitoweka vipi kwa wawili hao na leo tuna Tanzania na Zanzibar.
 
Kama ni nchi mbili Tanganyika na Zanzibar iweje leo tuna Zanzibar hatuna Tanganyika. Hebu twende kwa hatua.Tuonyeshe Tanganyika ilitoweka vipi kwa wawili hao na leo tuna Tanzania na Zanzibar.
Alaa mku wangu unapika chai kuaweka maji sukari na maziwa sii umepika chai tayari sasa unaponiuliza maji yako wapi nikujibu nini?.. zanzibar ni kama sukari unaiweka upendavyo ukitaka kijiko kimoja viwili juu yako lakini inapoingia kwenye mchangyiko wa chai haiwi sukari tena wala hakuna maji au maziwa. Chai ni Chai kubali iitwe ya maziwa haitapotoshi kuwepo mkwa majiwala sukari! hahaha..haha hahaa!
 
Mkuu nimepitia kumbu kumbu kuna mahali umesema tuna nchi 2, Zanzibar na JMT. Bado unaamini hivyo?

Pili, kama chai ni ya maziwa na sukari, nimekuuliza unaposema znz wanameminywa kujiunga na OIC, kwani walikuwa wajiunge kama nchi au wajiunge kama sehemu ya chai ya maziwa yenye sukari.

Tatu, kama ipo SMZ katika chai, Serikali ya Tanganyika ipo wapi.
Mkuu hapa kinachotakiwa ni kuonyesha Tanganyika ipo wapi kiserikali na kama haipo ilitioweka kwa mujiza gani.

Twende taratibu
 
Tuna nchi mbili ndani ya muungano, na kuna nchi moja nje ya Muungano hivyo tuna serikali 2, moja ni ile ya Znz na nyingine ni ya Jamhuri. kama nimesema tuna nchi 2 na kuiita ile ya muungano ni kutokana na matumizi ya hili neno ndio maana nika switch to Taifa. taifa ni moja na kuna nchi ya Zanzibar hivyo Mzanzibar anafungwa na katiba ya Znz na pia katiba ya JMT. Sisi kwa upande wetu hatuna nchi tena ila Tanzania na ndio maana hatutumii Utanganyika wala Ubara isipokuwa ktk mazungumzo.

2. Swala la sukari nimeliweka kukupa tu mwanga kuhusu jina la Tanganyika. hata hivyo sikosi jibu maana tambua tu yakwamba ni sukari ikatumike wapi, Ipo ktk chai na sasa inataka kutumika ktk Urojo ambao wananchi wake wanaupenda sana. Sisi hatukatazwi kunywa Urojo ukipenda utakunywa. Hivyo basi sukari inatumika kote kaa maji yanavyoweza kutumika kote iwe kupika Ugali au Mtori.

3. Serikali ya Tanganyika haiwezi kuwepo ikiwa tumekubali kubadilisha jina na mipaka yetu kuwa Tanzania. Swala hapa ni kutazama je Tanganyika inapoteza nini tunapotumia jina la Tanzania ilihali Tanganyika ipo ndio maana nikasema Maji hayatajwi ktk chai ya maziwa isipokuwa chai na Maziwa, haina maana maji hayana umuhimu anma yatajwe ndio uhalali wa chai hiyo unapatikana. Ukitaka kujua ukweli tazama ingredience zake na sii kutazama jina tu ukaanza kulalamikia chai nzima kuwa maji hayamo.

labda nikukumbushe vizuri kama wewe ni Old school au middle school ya kwamba Tanganyika ni nchi kubwa sana na kulionekana hatari ya kuimeza Zanzibar kama tungekuwa na serikali 3. Ni sawa na mezani unakula na mtoto na hivyo kila tonge lako ni sawa na mlo mzima wa mtoto na akitaka kuku utamwambia kula kwanza ugali unenepe wee miguu ya kuku, maini na firigisi ni za watu wazima. Hivyo basi ndio kuwepo kwa serikali 2 ambazo mtoto Zanzibar ana bakuli lake na anaweza kuchota toka sahani kubwa. Sisi hatuna haja wala sababu ya kuchota sahani la mtoto ila kuna mchango wake ktk menu hiyo.

kama nilivyokwisha sema Wazanzibar hawajui ama wanafanya makusudi kabisa kuomba serikali 3 kwa sababu nina hakika BLM halitapendelea mfumo huo. Na mfumo huo utakuwa Mzito sana kwa Wazanzibar kuliko wanavyofikiria na hakika muungano utavunjika kwa sababu bara itazuia vitu vyake kwa roho ya kimaskini maana tunachogawana ni umaskini. Leo hii Wazanzibar wanafanya choyo kwa kitu wasichhokuwa nacho (roho ya maskini) na bara hatudhuriki maana tuna ardhi kubwa, maliasili na rasilimali za kutosha lakini itakapo geukia kwao hapo ndipo watakiona cha moto na sio wao tu ita affect Muungano mzima. Hivi Mtoto, mwanao kweli akililia wembe kweli unatakiwa umpe?

Taabu itakuwa kwao Wazanzibar maana nchi yenyewe ndogo, hesabu kubwa ya Wazanibar iko bara na nje, hao wakirudi pale patakuwa kama Rwanda, sasa je ndivyo mnavyotaka?.. Jibu jingine ni serikali 1, lakini hili haliwapendezi Wazanzibar wote iwe wa BLM ama BLW hivyo ni kinyume cha makubaliano yalounda nchi yetu. Hatuwezi kuuvunja muungano ama kuufanyia majaribio Muungano hili nalikataa kwa sababu Tanzania haitakuwa Tanzania tena, tutafika walikofika Sudan au Ethiopia. Tusitake kuibadilisha Historia hapa katikati wakati Zanzibar ina historia yake na Tanganyika tunayo ambayo sisi tumekubali kuondokana na Tanganyika na kuchukua kipya kinyemi Tanzania - Chai ya Maziwa!.

Hizi kero zitakuwepo tu, hata Marekani kero wanazo. Leo Ukraine inatawaliwa na Nazis tena ma red skin unaona nchi zote za EU na Marekani wanawapongeza Utawala huo kama walivyofanya juu ya Apartheid, hawa wenzetu wanaangalia maslahi yao kwanza na ndio maana walipongeza referendum ya Sudan, Bosnia na kusema referendum ni haki ya wananchi leo huko Cremia sii haki ya wananchi wake. double standard lkn kwa manufaa ya western countries sisi ndio kwanza tunachochea ugonvi na utengano.

nachotaka kusema hapa ni sisi kutazama interest za TAIFA letu hata kama hatukubaliani. Swala ni kuzitanmbua kero zenyewe na kisha kuzitafutia suluhu sio kuunda serikali 3 au 1 kutokana tu na kero za wanasiasa wala sii wananchi maana wananchi wamejazwa ujinga huu na hivyo hawatumii tena akili zao.
 

Mkuu Mkandara, wewe ni moja ya great thinkers wanaoheshimika humu, ndio maana huwa nakuwa muangalifu kabla sijajadili hoja zako. Je, nikuulize:

*whats the legal foundation of our union? Au hatuna haja ya kuangalia the legal foundation?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwanza nashukuru kwa utangulizi wako na hakika sote inabidi tuwe makini hasa tunapozungumzia swala hili la uhai wa nchi yetu.

Kuhusu legal foundation mkuu wangu tunaitaka ili iweje? Hivi kweli tunaweza ku question legal foundation ya ndoa ya wazazi wetu na tukisha jua ndio tutafanya nini! mimi hushindwa hata kuelewa wale wanaotaka kuisona Artical of Union kwa lengo la kutafuta makosa na sii kuelemika hujiuliza - WHY?

Hivyo nadhani jibu langu hapa hapa ni kama alivyosema Mwl. Nyerere siku alokwenda UN kuiwakilisha nchi yetu ama alivyosema Karume ktk mikutano yake na yote unaweza ku summerize into - Pan Africanism. Haijalishi kama ni legal au laa na hata kama ikiwa kuna sababu nyinginezo tofauti za kisiasa bado muungano wetu ulifikiwa makubaliano ya pande 2 wakapitia miundo yote ya serikali 1 na 3 na kupendekeza hii ambayo imedumu kuliko miungano yote ya nchi za Kiafrika ya 1 na 3.

Tupeane sifa badala ya kuendelea kujishusha mahala tunapopongezwa na mataifa. Muungano wetu unatugusa wengi iwe ni kwa Historical, Culture, geogtaphic, objective na kadhalika, Sisi ni Wamoja toka kabla ya Uhuru wa Tanhanyika au Mapinduzi ya Zanzibar na tunazidi kupanua wigo la mahusiano maana leo hii mimi Mkandara hapa Mkerewe nina ndugu wa damu na Wazanzibar leo mkatutenganishe kwa sababu za kisiasa?. tena juu ya yote hamtaki kunipa Uraia kwa sababu naishi Ughaibuni! jamani nitakimbilia wapi miye mwee!

Kama unakumbuka vizuri historia ZNP na Afroshiraz walikuwa chama kimoja baada ya mkutano wa Pan African mjini Mwanza, hii ni kabla ya Uhuru wa Zanzibar. Lakini Shamte na kundi lake wakaingia tamaa, wakaja wageuka ASP na kuungana na ZPPP ya Sultan dakika za mwisho na kuwapa ushindi ZPPP. Hivyo mipango ya kuungana nchi za Kiafrika ilikuwepo toka awali ya Uhuru wenyewe na sisi tuliapa hatutakuwa huru hadi Afrika nzima imekombolewa. Sasa tunahitaji legal foundation ipi maana sisi wengine sio wasomi hatukufundishwa na Prof. Shivji au Prof. Haroub Othman - (Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi) ila tuna kumbukumbu nzuri tu ilotujenga kuamini ktk Umoja wa nchi za Kiafrika.

Muungano huu ndio pekee umebakia ktk nchi za Kiafrika na umeweza kudumu kwa miaka 50, leo hii watu wanachukia tulichonacho (serikali 2) kwa sababu tunayajua mabaya na mazuri yake kwa kuishi ndani ya mfumo huo. Lakini kati ya wabunge wote wa bunge la katiba, hakuna hata mmoja wao anayejua mazuri na mabaya ya serikali 3 au 1 kwa sababu hawaishi wala kuongoza ktk mifumo hiyo. Ni rahisi kuchambua serikali 2 na ubaya wake leo hii lakini wasitudanganye kuwa wanajua mazuri na mabaya ya serikali 3 ama 1 kwa sababu serikali moja ilikuwepo kati ya mwaka 1961 hadi 64 kwa bara na Zanzibar ni siku 20 tu. Wao wanajuaje mabaya na mazuri ya serikali hizo kwa Tanzania yetu?..Wajumbe wengi kama sii wote walikiuwa madarasani shule za msingi wakisoma na kaptula za kaki leo wanavaa suti kuja tuvuruga!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu maelezo haya yanapaswa yaambatane na maelezo.
Hiyo Tanganyika ilitoweka vipi kiasi sisi tukawa hatuna nchi bali nchi mpya ya Tanzania.
Naomba ueleze jamvi Tanzania ilipata uhuru lini
Serikali ya Tanganyika haiwezi kuwepo ikiwa tumekubali kubadilisha jina na mipaka yetu kuwa Tanzania. Swala hapa ni kutazama je Tanganyika inapoteza nini tunapotumia jina la Tanzania ilihali Tanganyika
Mkuu kama unakubali Tanganyika ipo, unakataa nini kwamba hakuna nchi hiyo?Mkuu mipaka ya Tanzania siyo mipaka ya Tanganyika. Huu ni upotoshaji kwa vijana, nachelea kutambua wengi wa vijana wanaweza feli mitihani. Mkuu tuwasaidie siyo kuwaingiza porini.Tanganyika ni kitu tofauti na Tanzania
labda nikukumbushe kwamba Tanganyika ni nchi kubwa na kulionekana hatari ya kuimeza Zanzibar kama tungekuwa na serikali
Wazanzibar wanasema tumeungana nchi mbili sawa na hivyo uwepo usawa.
Wewe unabadilisha kauli mbiu yao na kuwafanya dhalili
Wazanzibar hawajui ama wanafanya makusudi kuomba serikali 3, nina hakika BLM halitapendelea mfumo huo.
Umefunguka, nakuhakikishia this is the point of no return. Someone opened the Pandora box.Who let the dogs out!Unachozungumzia ndiyo basis ya wale wanaotaka serikali 2, siyo wananyonywa, wanaonewa, wanaburuzw na mengine ya aibu kama hayo.
Baada ya kuonyesha data wznz hawana la kusema,Watanganyika wameelewa uzito wa mzigo waliobeba .


Mkandara anashauri Watanganyika waendelee kubeba mzigo huu ukiambatana na matusi, malalamiko na madai yasiyo na msingi eti kwa vile Zanzibar ikiwa na machafuko nasi tutaingia. Hizo ni mbinu za kuwatishaWatanganyika.

Tunataka serikali ya tatu kila nchi ihudumie watu na eneo lake bila kumnyonya mwingine.
Tuna mambo 7 yanayotuunganisha kama kuna uwezekano yapunguzwe au tuvunje muungano kabisa.

Wznz kwa ubinafsi, uchoyo na chuki kwa Watanganyika wameharibu mahusiano.
Hakuna cha maelewano, kilichopo ni Tanganyika ishughulikie watu wake

Roho ya masikini hakuileta Mtanganyika aliyeuza utaifa wake, ni mznz asiyetosheka.Madai ya wznz ni game changer, Tanzania will not be the same to znz. Tanganyika ni kwa Watanganyika na hatujali.
Mtanganyika ambaye ni adui nambari moja visiwani haridhiki tena na uwepo wa wznz, ni fact. Tumekubali unyonge huo kwa miaka 50, sasa basi.
Tanganyika itarudi Dodoma au mtaani.
Itarudi kwasababu wazanzibar wanadhani ni raia bora na wanastahili kila haki hata isiyokuwa yao.

Hatujali nini kitawakumba, tunajali malalamiko yao.
Siku nyingi wameomba kuvunja muungano, wengine serikali 3 na wengine mkataba.

Sisi tunasema muda wa kuendelea kupigizana kelele basi. Tunataka Tanganyika yetu ili tushughulikie ufisadi, umasikini, ujinga na maradhi.Hatuwezi kuacha kujadili mambo muhimu kwasababu tu wznz wanataka nafasi 30 za mabalozi.

Tumekubali matakwa yao, wao waamue kuendelea kuvunja muungano hilo hiari yao.
Sisi tuna kazi moja tu, kuipigania Tanganyika. Dodoma wakikataa tutachukua ownership mitaani huko hakuna control. Tutapigania Tanganyika kama wznz wanavyopigania znz yao. Tanganyika haizuiliki inacheleweshwa tu
Wanaotaka kujitenga ni wazanzibar. Mkandara umeonyesha jinsi wanAvyonyonywa. Hutataki wateseke.Hatutaki tuwe koloni la weusi, wala hatutaki laana zao.
Wznz wanamlaani Nyerere Laanatullah, hatutaki waendelee kusononeka. Tunataka waishi kwa amani na nchi.
Uhuni waliofanya miaka 10 iliyopita hauvumiliki.

Kwa leo Tanganyika ni suala la muda, itarudi tu iwe Dodoma au katika viunga vya minazi.
Iwe kwa majadiliano au msuguano! Tanganyika itarudi na znz yenye malaka kamili itakuwepo.
Huwezi kuishi na mwiba mguuni. No way, tutatengana kila mtu afanye lake.

Tanganyika itazinduka nakuhakikishia, iwe kwa heri au kwa namna nyingine, it is coming
Mkuu kero! Hivi tutakaa tunajadiliana nafasi za mabalozi ambazo ni 30. Hizo ni kero kweli!Watu wamekwenda kwa Fatma kuulizia nafasi za ubalozi.Hawa wanatusaidia nini to be honest.

K
inachoitwa kero ni njia za kumtwisha Mtanganyika gharama. Hatuna kero nao. Tunataka Tanganyika yetu
Nasema iwe Dodoma au mtaani Tanganyika haikwepeki.
 
Mkuu Mkandara, kwanza tambua kuwa Tanganyika hatuna kero na znz.
Pili, Hatutaki kuwanyima uhuru wao wa kujitawala.
Tatu, Hakuna mazuri ya serikali 2 kwa Tanganyika.

Kuhusu kujaribu, Nyerere na Karume walikuwa na guts za kuunganisha nchi. Miaka 50 Mkuu anatutisha kuhusu serikali 1 au 3. Mbona hizo zina nafuu, vipi kuhusu kuvunja jahazi kugawana mbao.

Zanzibar hawataki muungano waache wakajenge nchi yao. Uwepo wao ni tatizo letu, hatuwahitaji kwa lolote kwa chochote. Kama kuna kero Tanganyika ni midomo ya wznz, hatuna dai lingine kwao.

Wala usipotoshe kuwa tukae pamoja tuongelee kero. Tanganyika haina kero tuongelee nini.
Kero ni shida za znz hivyo usituweke katika mizani moja. Kama wana matatizo waseme, sisi hatuna kero na znz, hatudai kitu kule, na hakuna sababu za kudai.

Mkandara unajenga picha kuwa Tanganyika inawategemea wazanzibar hivyo tukae meza moja tuongelee kero. Si kweli hatuna kero na wala hatuna sababu za kukaa meza moja. Wao waje mezani tulipokaa kama hawataki juu yao. Tumewachoka sana.

Mbona wakati wamewachoma moto Watanganyika hukusema kitu. Majadiliano wiki nzima sasa hilo husemi kwasababu limefanywa na Wazanzibar. Hivi kukataliwa OIC kuna uzito sana kuliko kuchomwa moto Watanganyika.

Tanganyika haikwepeki hapa tulipo. Inazinduka kwa serikali au mitaani kwa hoja kwa viroja.
Popote na itakapobidi tunahitaji Tanganyika yetu kwa gharama yoyote.
Muda wa kupigazana kelele za nafasi za ubalozi ndio kero hiyo! tukae tunaongea hilo!!!
 

Nguruvi3,

Labda nikusaidie zaidi. Suala la kuchangia muungano kwa sasa bado linashughulikiwa na kufanyiwa kazi na Tume maalum iliyoundwa chini ya Afisi ya makamo wa Rais Muungano ikijumuisha Waziri mkuu Muungano na makamo wa 2 wa Znz.Mpaka sasa bado kutoa hisabu kamili kuwa kila mtu achangia kiasi gani.

Nitakushangaa sana kuona una lalama Znz munaibeba kwa lipi? na ni manufaa gani munayopata kwa kuibeba Znz wakti wananchi wa TGK wana hali mbaya sana kiuchumi. (hakuna huduma nzuri za afya, ilmu, miundombinu ya barabara, maji safi na njaa?

Kumbuka kuwa wachumi tunaamini HAKUNA JAMBO LA BURE DUNIYANI? Na hivyo nahisi kama maneno yako ni sawa basi kuna jambo kubwa mnalolipata katika huo muungano wenu na Znz?

Tuweke wazi basi.


 

Mkandara,

Mimi nitafurahi sana kama utaonyesha wapi katika maandiko yangu kukhusu UFAFANUZI WANGU NAMNA MUUNGANO WA NCHI HIZO MBILI ULIVYOKUWA.

Kumbuka kuwa mimi sijagusia kabisa HISTORIA KABLA MUUNGANO MIMI NIMEANZIA PALE WALIPOSEMA TUUNGANE. Ndio maana katika andiko langu nimeanza kwa kusema

Mzizi asili haswa wa muungano ni kauli, ya Nyerere na Karume.

Nyerere " Sisi ni ndugu, kwa nini tusiungane?".
Karume " Tuungane, wewe rais. mimi makamo".

Shughuli ilianza na kumalizika in a split of a second!.

lakin hii la mikutano mingi kabla uhuru Znz kufanyika Tanganyika ukilichukulia ndio kigezo au chimbuko la muungano HILO SIO SAHIHI. Kwani Tanganyika imesaidia wengi sana katika kujipatia uhuru lakin hazijaweza kuungana nazo. Kumbuka uhuru wa Msumbiji, Frelimo waliweka makambi kule nachingwea, Uhuru wa Africa Kusini , ANC waliweka makambi kule Morogoro, na wengine kama SWAPO n.k

Mbona Tanganyika hakuweza kuungana nazo. Mimi nafikiri historia ya Znz ni pana sana na tuliozaliwa huko kabla huo mvungano tuliona mengi japo mengi yamefichwa.

Kifupi Tanganyika na Znz walikuwa ni nchi jirani na watu wake walikuwa ni ndugu kama ilivyokuwa ujirani na udugu wa watu wa pale Namanga na kenya, au SIRALI n.k.

Hata marhum baba yangu alikuwa a biashara zake huko dar, tanga na tabora kabla ya huo muungano wakt yeye alikuwa Mznz.

Kama unataka hii historia ya Muungano kabla ina mengi na imekorogwa sana ni bora tu tuanzia hapo Nyerere alipokwenda Znz kuzungumza na karume kukhusu kuunganisha nchi hizo na kisha mchakato ulivyoanza.

Ahsantum
 

Ahali yangu Mchambuzi,

Nilipo Underline.

Hapo napenda kukwambia MUUNGANO WENU WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR HAUNA HADHI WALA UHALALI WA KISHARIA. Na hilo NINALIBAINISHA KISHARIA.

Kwa vile hizi ni nchi mbili tofauti zenye uhuru wake na zote ni Jamuhuri huru, kauli pekee haitoshi kuziunganisha, lazima kufuata taratibu, sharia na kanuni ili kuhalalisha nia na kauli hizo, ndipo zikaandaliwa hizo articles of union!.

Articles zile japo zilikosa sifa ya kisharia ya kuutwa mkataba "contract" kutokana na tatizo la kisharia liitwalo "privity of contract", articles zile zilikuwa na sifa zote za kuitwa ' international treaty" kuunganisha nchi mbili, na ili any international treaty kupata uhalali na nguvu ya kisharia, ni lazima treaty hiyo iwe ratified na mabunge ya nchi husika!.

Ratification is a process ambayo hufanywa kwa procedures maalum na kufanywa in writing!.

Bunge la Tanzania lilifuata sheria, taratibu na kanuni zote ku ratify zile articles of union kwa maandishi!.
Zanzibar, walikuwa ndio kwanza wametoka kwenye mapinduzi, hivyo hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa kila kitu!. Lilipaswa kuziridhia zile articles of union kwa ratification ambayo hufanywa kwa maandishi!. Vikao vyote vya BLM vina hansard, lakini hilo halikufanyika na hakuna kumbukumbu yoyote ya maandishi kwamba ratification ilifanyika!.

Kisheria Muungano ni wa bara tuu, ndio maana Dourado alipomtonya Jumbe kuhusu Zanzibar kutouratify muungano na wakataka kuweka mambo sawa, Jumbe alishughulikiwa ipasavyo!.

NDIO MAANA TUNASEMA MVUNGANO HUO NI BATILI NA UMEWEKA KINYUME CHA SHARIA HIVYO HARAMU.

Sasa labda na wewe unidadavulie uhalali unaodai upo wapi?

Ahsantum
 
Nguruvi3,

Ahaa sasa nimemtoa nyoka pangoni maana nilitaka wewe useme ukweli wako moyoni ya kwamba huutaki Muungano. Sasa hizi habari za serikali 3 au 1 ni kufurahisha watu tu maana moyoni mwako umeshajenga uadui na Wazanzibar kwa sababu ya mdomo wao.

Tazama basi ebu waulize hao Wanaojiita Wazanzibar asili ya wapi hawa kina barubaru utakuta ni watu wa msumbiji, Wangazija na waarabu wa Oman ambao ni wahamiaji tena niseme wazi kuwa ni WAKIMBIZI kwa asili leo wana mdomo na uthubutu wa kuuliza uhalali wa Muungano wetu.

Mimi sintokubali kabisa kuvurugwa na kundi la wahuni kwa sababu uya mdomo wao ila nitawasikiliza wale tuloshirikiana ao kufanya MAPINDUZI na kuikomboa Zanzibar toka mikono ya habith yule Sultan alokuwa akiwapaka chokaa dada zetu il waonekane weupe na vinyago wanapomhudumia.

Na ndio maana wanataka sana kujua Artical of Union ilikuwa ratified vipi ili hali hawajui chimbuko la MAPINDUZI yenyewe maana walipigwa wakiwa usingizini. Akili zao bado zimejengwa ktk mfumo wa Zanzibar huru ya Sultan na Shamte akiwa waziri mkuu hivyo hawa ndio walotakiwa kuweka saini mkataba.

Binafsi sipendi kurudia Historia wala siuna sababu ya kuwathibitishia watu uhalali wa ndoa yetu, iwe imefungwa Kikristu au Kiislaam kinyume cha imani zao. Ni wanandoa ndio waloamua kuifunga ndoa ile kwa ridhaa ya wazazi wao. Nyie watoto mlozaliwa ktk ndoa hiyo mkitaka kusepa na kuchukua dini nyingine mlango uko wazi. Ondokeni jikoni mkizidiwa na joto au livueni koti lilowabana ndio maana wengine wamekimbilia Oman na kadhalika. Hata kama Artical ingekuwa haikuwa ratified, Articles siku zote hutoa domestic na international legitimacy kwa nchi iliopo hata kama kuna utawala wa Kidikteta, Kisultan, demokrasia, Kijeshi na kadhalika sii lazima mfumo wa viongozi wake uwe ktk mfumo wa bunge ili ipatikane legitimacy.

Kuna nchi kibao zimefanya Mapinduzi na kesho yake wakatambuliwa UN huku wamevunja Bunge na baraza la mawaziri zima na nchi hizo hadi leo zinatambuliwa kama nchi iwe huu Muungano. Mbona ule wa kuunda Marekani ni nchi 16 tu zilishiriki na leo tuna nchi 50 ndani ya Muungano wao mtasema nao haukuwa halali?. Nchi za Kiarabu UAE walifanyaje. Msiwasikilize wapuuzi hawa ambao akili zao siku zote ni kutafuta nchi yao maana ni wakimbizi wasokuwa na nchi.

Hivyo hizi hadithi za Kisheria ni upuuzi mtupu wa kundi la Jamheed wakitafuta wajinga wajinga, Wamakonde walowezi wasokuwa na elimu kumtukana mwalimu na Karume wakati wanashindwa kuelewa kwamba hata hao viongozi wao wana asili ya bara, Kongo na Msumbiji kutokana na biashara ya utumwa. Leo Mu Oman na Mnazija anathubutu kujiita yeye Mzanzibar kuliko Mnyamwezi?

Hili ni no!! noo! na ndio maana JK kaifufua upya sikukuu ya MAPINDUZI kuwa sikukuu ya Kitaifa ili watie akili. Yadumu Mapinduzi na tutayalinda kwa kila hali na mali maana tunaijua historia kama ilikuwa jana vile. Tunasonga mbele hakuna kurudi nyuma hapa!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara
Tangu miaka nenda rudi, msimamo wangu umekuwa ule ule
1. Serikali 3 ikibidi
2. Vunja jahazi tugawane mbao!
Na ndicho tulikuwa tunajadili hadi hapo alipotokea huyu jamaa yetu kuanza kudhihaki Muungano wenyewe, ati haukuwa halali. Upotoshaji wa namna hii unanikera sana na ndio maana sikupenda hata kumjibu Mchambuzi kwa sababu inatutoa ktk mjadala.

Mimi nitauliza hivi:- hizo serikali 3, zitasuluhisha nini ktk kero zilizopo? na Tukivunja Muungano lengo lake nini haswa? maana nilishasema sana huko nyuma ya kwamba mkeo akipiga kelele na matusi juu kwa sababu ya Ulevi wako, kisha akafikia kuomba taraka. je, hatua nzuri ni kumtarakia, ku seperate au wewe mwenyewe kutambua tatizo hapa sio ndoa, sio mke,wala wewe, tatizo ni hulka yako ya Ulevi!
 
wakuu napenda sana kuwasoma mnavyochambua mambo, natamani ningekuwa na uwezo huo mliojaaliwa na mwenyezi Mungu, ila naendelea kujifunza toka kwenu, haya leo rasimu ya katiba imewasilishwa rasmi Bunge maalumu na mwenyekiti wa Tume, nikisoma hiki kipande na refer mengi mliyoyajadili....


 
zumbemkuu,
Shukran sana na ndicho nachokisemea mimi humu Janvini. Tazama basi rasimu nzima haituonyeshi jinsi gani serikali 3 zitaondoa hizo kero zilizopo.Rasiomu imetumia muda kuonyesha ubaya wa serikali mbili ulozileta kero hizo lakin pia haizungumzii ni kero zipi hizo, hivyo anapozungumzia serikali 3 zioneshe zitaondoa vipi kero hizo badala yake kilichoonekana ni changamoto. Je hizi changamoto ndio kero za muungano ama ni vitu vile vile vilivyomo ktk serikali 2 na sioni unafuu wake kwa kuunda serikali 3 pasipo kugusia kero za Muungano.

Hizi Changamoto, sio sababu ya kuvunja serikali 2 bali ni kukosekana UMOJA wa kudumu ambao sisi wengine tunategemea kusikia hiyo serikali ya 3 ambayo ni kuu (Federal) itaweza vipi ku deal na kero zilizopo. hakuna mahala rasimu umegusia kero zenyewe isipokuwa dhana tu ya kuzaliwa Tanganyika kama vile kutokuwepo Tanganyika ndio kero.

CUF walikuwa na msimamo wa serikali 3 toka zamani lakini kwa maana ya Znz kuwa na mamlaka kamili kama TAIFA na kiti chake UN. Mkataba uwepo wa kuunda federation kama ile ya Ulaya EU ama EAC. Sasa nambieni hiyo serikali ya 3 kazi yake haswa itakuwa nini maana Znz wanataka kiti UN kama Taifa huru. Serikali 3 itatoa mamlaka kamili kwa Znz, Je itaiwezesha Znz kuwa na kiti chake UN au tunababaisha tu maneno.

Nitauliza tena kwa wajumbe wa katiba, ikiwa kweli waasisi wetu wa Muungano waliunganisha NCHI 2 kuwa NCHI 1 (Taifa) yenye serikali 2 (nchi 1 serikali 2)na sio nchi 2 zenye serikali 2. Kwa nini Watanzania bara walikuwa wakienda Znz kwa passport ilihali ni nchi 1?. kama ni nchi 1 kwa nini hadi leo Mtanzania bara haruhusiwi kununua ardhi Znz wakati ni nchi 1?.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…