Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

mkuu mkandala labda kwa kuongezea tatizo kubwa ninaloliona kwenye matatizo ya muungano ni UMIMI (ubinafsi) kwa maana ya upande mmoja wa Muungano, matatizo ya Muungano yatatatuliwa tu iwapo neno UMIMI litageuka na kuwa UMOJA kama ulivyolitaja hapo, ni namna gani tunaweza kuleta huo UMOJA hapo sijui nawaachia nyinyi magwiji msaidie hili....
 
Last edited by a moderator:
mkuu Nguruvi3 na Mchambuzi hili swali linawahusu maana ingefaa mtoa hoja warioba alijibu ila sidhani kama yupo humu,
 
Last edited by a moderator:
Zumbemkuu
Ukisoma maoni ya tume utaona mambo mengi tuliyajadili tena kwa kina na wale wa serikali 2 hawakuweza kujibu hoja.
Lipo bandiko hapa linaloonyesha gharama kupungua hasa upande wa bunge.

Shukrani kwa kuleta hili tutalijadili kipengele kimoja hadi kingine.
 
Haswaa mkuu umemaliza mjadala na nawaomba sana hao wajumbe wa katiba walitazame hili neno UMOJA kwa makini sana.

Swali la muhimu liwe tutaweza vipi kuondoa hizi kero na kujenga UMOJA? Je serikali 3, 2, 1 ndio kiini cha kero za Muungano? Na bila shaka watagundua tu kwamba kero zote zinatoka Wapinzani wa Muungano. Tutazunguka wee tukiepa ukweli kuwa Wapinzani hasa kutoka Znz hawautaki muungano, hivyo kama tunaitafuta haki na ukweli basi ni haki ya wananchi wa Znz kupiga kura aidha waendelee na Muungano ama wajikate.

Kuwe na mihadhara sambamba yenye kupendekeza kura za NDIO ama HAPANA ili wananchi wa Zenji wajue faida na hasara za Muungano, kisha wapige kura zao maana hili sio tatizo la bara hata kidogo. Ila tu ifahamike tu ya kwamba hao wote waliokaa ktk viti vya uongozi na hata hilo bunge la katiba walipa KUULINDA MUUNGANO.
 
Last edited by a moderator:
mkuu wakati namsikiliza Warioba niliona kama naota ikabidi nirudie kwa kusoma hotuba yake nzima, ni kama kahamisha mjadala wote wa duru za siasa na kuweka kwenye hotuba yake,, wakati namsikiliza ilikuwa kama narudia kusoma mijadala ya humu ndani, sasa tusubiri mipasho siku ya ijumaa kama itabadilisha upepo wa leo au lah
 
What? - ebu rudisha hilo swali pengine sikuliona maana uliuliza maswala 100 kwa wakati mmoja. Twende kwa hatua nitakupa picha nzima maana hujui kwamba tuna deal na viongozi vichaa wenye tamaa na Umimi. Ikiwa tulianza na mikoa 16 leo tuna jalala, tulikuwa na wizara chache leo ni Mbagala, kuna nafuuu gani ya kuita changamoto na sii kero mpya. Hivi unadhani wanaounda serikali ni wananchi ama utawala?
 
Mkandara , ukisoma hotuba ya Warioba vizuri kuna mahali ameuliza swali muhimu sana la Mchambuzi linalohusu legal foundation ya muungano. Mchambuzi ana point kubwa sana kwasababu kila tunachokifanya sasa kipo katika principles zilizoanzisha muungano.

Warioba kasema kuhusu article of union ambayo pamoja na mchambuzi tumekuwa tunaongelea kila siku.
Kaongelea uwepo wa Tanganyika ambao unaupinga na kudai nchi hiyo haipo.
Kaongelea upande wa uchumi tunaoongelea kila siku.

Nampa big up Mchambuzi hasa katika kueleza tulipokuwa, tulipopita, tunapokwenda na tutakapo kwama.
Nakumbuka Mchambuzi alizungumzia sana kuvunjwa katiba kwa kutumia vielelezo ndipo watu wengi wakafahamu kuwa kumbe SMZ ni zaidi ya JMT. Leo Warioba kaonyesha wazi.

Warioba kaeleza vizuri sana kuhusu kero, kaeleza na ufumbuzi wake. Sijui ulitaka aseme nini lakini mjadala wetu wote upo katika hotuba yake. Amesema serikali 1 ambayo ndiyo ilikuwa lengo haiwezekani. Kasema changamoto za serikali 2 ni kubwa sana. Kwa ugumu sana kasema muungano udumu suluhu ni serikali 3.

Kwanini 3
Kila mtu atashughulikia yasiyomhusu bila kumuathiri mwenzake
Itaondoa utegemezi wa upande mmoja, haitamaliza lakini itapunguza
Itajenga nidhamu katika katiba.
Itajenga uzalendo wa nchi kila mmoja akiwa mshiriki na si mmoja kuwa mkokoteni mwingine mzigo.
 
Mkuu mafisadi waliapa kutimiza wajibu wao. Leo tunajua uchafu juu ya viapo vyao.
Rais aliapa kulinda haki za kila raia, leo mabwepande ndicho kituo kikuu cha kung'oa meno(dental unit)
Kuapa kulinda muungano hakuzuii kuvunja muungano. Nyerere alisema 'wznz wakikataa muungano hatawapiga mabomu'
Nyerere aliapa, nao hao watakaokataa waliapa. Kwahiyo kuapa ukuangalie zaidi ya kutamka.

Kuhusu umoja, sijui kama mnao tatizo lilipo.
Umoja hauji kwa maneno ni maridhiano. Umoja unajengwa kwa kuaminiana na kutahaminiana.
Kunapokuwa na ubora na kujiona (Narcississm) utajenga vipi umoja?
 
Maelezo ya wariba hayaonyeshi kero zozote, na sijasikia mjadala wowote unaozitazama kero ila maoni ya kugawana umaskini na jinsi gani tutaweza kugawana vema. Ukiwa mshabiki wa Ubara dhidi ya Zanzibar utamkubali pasipo kujua alichokifanya Warioba ni jibu la jeuri ya Wazanzibar. Udhaifu wa JK ndio umetufikisha hapa tulipo, kina Jussa wakadakia na kuunda UMOJA wao, maana ile katiba isingeandikwa kabisa kama angemchukulia hatua Pinda kwa usemi ule lakini yaonyesha wazi sisi wenyewe Watanganyika tunataka kujitenga na kuunda UMOJA wetu, huo muungano uko wapi?.

Artical of Union inajulikana wazi kuwa ndio legal foundation isipokuwa inapigwa vita na wale walokuwa Hizbu maana wao bado wanautambua utawala wa Sultan chini wa waziri mkuu Shamte kuwa ndio halali. sasa unapoendekeza fikra hizo na kukubali turudi nyuma ili kuwafurahisha CUF ndipo tutakapo ipoteza Tanzania. Kwa sababu hatuwakomeshi CUF bali tunawawezesha kuuvunja muungano.

Hii haihitaji mwana sayansi kuona jinsi anavyopigia debe serikali 3 wakati haya ni mapendekezo ya wananchi. yeye kama jaji inaonyesha kisha chagua upande, hivyo hii kesi itakavyokwenda ina maana Warioba alikuwa upande gani na sii mkusanyaji wa maoni ya wananchi.
 
Last edited by a moderator:
Naam! ni kweli.
 
1.Mkuu nadhani wewe huelewi umuhimu na maana ya kiapo. Hivi kweli unaamini unaweza kuapa jambo halafu ukalifanya kinyume ndani ya kiapo na ikakubalika?. Unaapa kuwa mwanandoa kesho ukaivunja halafu bado ukasema kuna ndoa! basi hiyo KATIBA ya nini ikiwa mtu unaweza kuivunja upendapo. Kwenda kinyume cha Katiba ni Uhaini na nasema tena wanaozungumzia muundo wa Muungano wetu waloapa kuulinda ni wahaini na hawatakiwi kuachwa huru.

2. Kwa hiyo unataka kusema jino kwa jino ndio jibu la UMOJA!
 
0. Nini legal foundation ya muungano wetu
1. Serikali 2 zinapunguzaje gharama
2. Yale yasiyo ya muungano yashughulikiwe na serikali ipi
3. Serikali ya Tanganyika itakayoshughulikia mambo ya Tanganyika yasiyo ya muungano ipo wapi
4. Kwanini katiba ya Zanzibar inakuwa juu ya katiba ya JMT. Ipi ni kubwa katiba ya znz au JMT
5. Tuliungana kama nchi mbili, moja ipo nyingine ipo wapi
6. Gharama za muungano zinachangiwa kwa utaratibu gani.

Twende taratibu
 
Kiapo kina nchi si Tanzania in short.
Nimekuuliza vipi Rais aliyeapa kulinda raia na mali zao, wanapopelekwa dental unit mabwepande, Rais amewalinda vipi.
Kiapo chake kimetumika vipi kumwajibisha kwa kukiuka.

Kiapo kina maana, lakini si rahisi kama unavyosema. Kuapa kulinda muungano hakuna maana ya kutofanyia mabadiliko au kuzamisha jahazi kabisa. Nasema tena Nyerere aliposema hatawapiga mabomu wznz alimaanisha nini?
 
Mkandara, jino kwa jino lipi?
Tanganyika haina meno ndiyo maana inaona imuachie mwenye meno tafune mbuyu.

Tanganyika inataka amani na salama. Haitaki kuwa mzigo kwa mwingine
 
Maswali yako yote hayahusu kuwepo kwa serikali 2 kwa sababu yanaweza kufanyiwa marekebisho kama changamoto. Hizi sio kero zilizotufikisha ktk kuijadili katinba Mpya.
Swali la 1. Serikali 2, 1 au 3 saio kiini cha gharama bali ni utawla uliopo madarakani. maswala ya gharama sii ya kikatiba bali ni ya kisera hivyo ni chama tawala pekee ndicho kinaweza kupunguza gharama. Ila serikali 3 zitaiongeza gharama bila kuondoa kero zilizopo.
3. Kwani miaka yote 50 shughuli za Tanganyika zilishugulikiwa na serikali gani. Ni wapi serikali ya JMT imeonyesha kushindwa kutekeleza shughuli za Tanganyika.
4. Nishasema katiba ya Zanzibar ni makosa makubwa na Uhaini ambao hayakutakiwa kuachwa yakaota mizizi na pia kauli ya Pinda haikutakiwa kusema Zanzibar sio nchi. Zanzibar ni nchi kama mnavyodai nyie Tanganyika ni nchi na ipo.

Unajua mnachekesha sana napowasoma mkisema Tanganyika ni nchi na Warioba anasema Tanganyika ipo, lakini ajabu ya Mussa Warioba huyo huyo anasema Zanzibar sio nchi na wote wanaunga mkono serikali 3 wanadai Zanzibar sio nchi. Sasa iweje iwepo ya Tanganyika lakini sio ya Zanzibar? wakati sisi tunasema Zanzibar ni nchi na Tanganyika sio nchi tena baada ya kuchukua Tanzania kama utambulisho wake ( mama Mzazi).

5. Tuliunganisha nchi 2 sawa, moja ni mtoto aliye tumboni (znZ) na mwingine ni Mama alobeba mimba na kuitwa Tanzania. Kusema mtoto sio binadamu kamili kwa sababu yupo ktk tumbo la mama hivyo mtoto hana uhai wake ni makosa. na mama unapochukua jina la uana ndoa kama Mrs. Nguruvi3 haina maana kapoteza uke wake kwa sababu ati alitakiwa kuitwa Maria (Tanganyika).

6. Kwani sasa hivi gharama za muungano zinachangiwa kwa utaratibu gani. Mkuu kero zipo ktk mfumo mzima wa uongozi ule wa kijamaa na umimi tukiondoa hilo haijalishi ni serikali ngapi tunazo. Leo tunapoteza mabillioni kwa ujinga ujinga kujadili muungano ilihali wananchi hawana hata maji safi, kina mama wanakufa Muhimbili kwa uzazi na kadhalika. Upuuzi mtupu kuwa na akili ya kimaskini kushambulia sinia la pilau ati kula sana ndio afya.

je, katika haya yote ni lipi ambalo ni KERO za muungano toka awali na ndilo lizotufikisha hapa tulipo?
 
Last edited by a moderator:
Swali hili kamuuulize Jumbe? mkuu Nyerere aliyasema aloyasema sio ktk kiapo lakini aliulinda muungano kwa muda wote alokuwa madarakani. Huyo alopelekwa Mabwepande mwenyewe ana historia yake maana yasemekamna alikuwa shushushu mwenyewe na akauza siri. Kifupi alikiuka kiapo chake na wakamfanyia kweli, hiyo ndio habari ya mujini.
 

Mkandara,


Siku zote watu wanapokaa kitako kuanza kuujadili MUUNGANO wengi sana kutoka upande wa Tanganyika wanakuwa wa kwanza kabisa kuionea huruma ZNZ ikiwa pamoja na kuipitia historia yake wakti munasahau kuwa HISTORIA YENU ni khatari sana.


Nafikiri suala la kwanza mlitakiwa mjiulize KWANINI NYERERE ALIFUNGA SAFARI KWENDA ZNZ KUMUOMBA KARUME WAUNGANISHE NCHI HIZO?


Hapa pana siri kubwa sana kwa Nyerere kwani aliona nchi yake ina matatizo kiasi kikubwa sana na suluhisho ilikuwa ni kuungana na ZNZ. Na ndio maana alikubali kwa nia moja nchi yake wakti ule ikiwa na watu zaidi ya milioni 18 kuungana PASU KWA PASU na nchi yenye watu chini ya laki tatu.

Lakin kubwa zaidi bila kusema uwongo na kuwa wanafiki LAAZIMA MUKUBALI KUWA MUUNGANO WENU NI WA MATAKWA YA VIONGOZI NA SIO WANANCHI NA UNALINDWA KWA GHARAMA KUBWA SANA KWA FAIDA YA VIONGOZI, KIASI CHA KULETA KHOFU NA KUTO KUAMINIANA MIONGONI MWA WANANCHI WA NCHI HIZO.


Waarabu tuna usemi " IN ORDER TO BUILD SOMETHING STRONG IT HELPS TO START WITH BEST AND POSSIBLE MATERIALS"

Sasa nilibainisha hapo awali kuwa MUUNGANO ULIKUWA WA MAGUMASHI NA HAUKUFUATA SHARIA ZA KIMATAIFA. HIVYO lazima mpate shida kwani NYUMBA NI MSINGI. Ndio maana hata katika bunge lenu la KATIBA unaona wazi limetawaliwa na KHOFU NA UWOGA MKUBWA kuhusu MUUNGANO.



SASA msingi mkubwa hapo NI KUUVUNJA KISHA KUREJESHA KWA WANANCHI WAAMUE KAMA WANAUTAKA AU LAA. NA WA AINA GANI KAMA WATAUTAKA. Hakuna jinsi hapo lazima maamuzi ya wananchi yahishimiwe.


Enzi za kuogopa kuujadili muungano zimepitwa na wakti. NI VIZURI MUKANDARA UBADILIKE NA ACHA UWOGA KWANI HUO MUUNGANO UMEUNDWA NA WATU.
 
 
Last edited by a moderator:
QUOTE]Mkandara;8991399]What? - ebu rudisha hilo swali pengine sikuliona maana uliuliza maswala 100 kwa wakati mmoja. Twende kwa hatua nitakupa picha nzima maana hujui kwamba tuna deal [/QUOTE] Haya ndiyo maswali niliyokuuliza kama ulivyojibu Na haya ndiyo majibu yako. Hoja zangu zinafuata...
 
Unasema gharama ni suala la kisera na si kikatiba.
Unatuambia nchi inaongozwa kwa sera na si katiba kama sheria mama ambayo sera zinatakiwa zifuate.
Mkandara suala la muungano ni la kikatiba hivyo gharama za muungano ni suala la kikatiba.
Unachoshauri ni kuwa Chadema, CUF wakiingia madarakani katiba iandikwe upya kuhusu muungano!!!!

Lakini usichojibu ni kuwa legal foundation ya muungano ilikuwa nini?
Masuala yasiyo ya muungano ambayo huko nyuma umedai Tanganyika imejilimbikizia yashughulikiwe na nani, na ni jinsi gani kuna mambo ya muungano na yasiyo ya muungano ukiwa na Zanzibar na Tanzania?

Kama unakubali mambo ya Tanganyika yatashughulikiwa na Tanzania ambayo huko nyuma umesema Tanzania ni sawa na Tanganyika kwa mipaka, malalamiko kuwa Tanganyika inanufaika zaidi na yasiyo ya muungano unayatoa wapi.
Kumbuka unasema yasiyo ya muungano, lakini huelezi yawekwe wapi.

Unasema ni wapi serikali ya muungano imeshindwa kutekeleza mambo ya Tanganyika.
Tayari unakubali yapo ya Tanganyika. Huko nyuma umesema Tanganyika inachukua mambo yasiyo ya muungano.
Nashindwa kuelewa wapi unasimamia kuhusu hili.

Unawezaje kuwa na Tanganyika yenye mambo yake halafu yakashughulikiwa na Tanzania?
Zanzibar ina mambo yasiyo ya muungano na inashughulikia, vipi isiyachanganye yakawa ya Tanzania ile Tanganyika iliyochangia.
Kwanini kuna double standards. Hilo hujaeleza.

Kwa mujibu wa katiba ya znz ya 1984 na marekebisho ya 2010 Zanzibar ni nchi.
Kama ni nchi imeungana na kitu gani kuzaa Tanzania. Huko nyuma umesema muungano ni wa zanzibar na Tanzania, nikakuuliza hiyo Tanzania ilizaliwa lini na kupata uhuru lini hadi ikaungana na Znz?

Kama unakubali tuliunganisha nchi 2, moja ikiwa ni znz ingine iliyoungana na znz ni ipi mkuu?
Ukishasema nchi 2 lazima uzitaje. Article of union imezitaja kuwa ni Tanganyika na Zanzibar.

Kinachokukwaza ni kugoma kuzungumzia legal foundation ya union ambapo article of union ingekusaidia sana kuelewa.
Hivyo nakusihi, kwanza kabla ya kujadili muungano pitia na uwe na ufahamu wa legal foundation ya union.

Kwa taarifa yako Tanganyika haikufa mwaka 1964 kama unavyodai. Sheria iliyoiua Tanganyika ni namba 24 ya mwaka 1967.
Tanganyika ilikuwepo hadi mwaka 1967, ilipotezwa ndani ya Tanzania na kuwa recessive.
Serikali ya Tanganyika tunamaanisha izinduke si kurudisha, ipewe legal authority ya kushulikia mambo ya Tanzania.

unaposema serikali 3 zitaongeza gharama huku ukishindwa kuandika mstari mmoja tu wa kuonyesha serikali 2 zinavyopunguza gharama sikuelewi. Ni sawa na kumsumanga tajiri kwa unyonyaji bila kuonyesha masikini amenyonywa wapi.

Watu wote wanaosema serikali 2 hawana takwimu za kuonyesha kwanini serikali 2.
Hawana msingi wa kisheria wa kuonyesha kwanini serikali 2 na hawana msingi wa kichumi wa kuonyesha kwanini 2.
Kitu kibaya hawakubali hoja za wale wa serikali 3.

Hawawezi kueleza kama alivyoshindwa mkandara kutuonyesha wana dawa gani kutoka Appolo hospital zaidi ya ile iliyotumika miaka 50 bila matoke mazuri

Mkuu Mimi nakuelewa unatetea serikali 2 si kwasababu zina manufaa bali kuiweka znz katika nafasi nzuri ya kuendelea kunyonya bila kuchangia.Tanganyika haiepukiki, kwa miaka 50 muungano huu upo na njia ya kuendelea nao ni serikali 3.

Kinyume chake ni kuua. Wznz wenyewe hawataki Mkandara, Watanganyika wamechoka utawaleta vipi katikati?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…