Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Joint Finance Commission iliundwa kwa lengo la kushauri serikali Mbili za muungano juu ya sharing of revenues and expenditures, na fiscal relations kwa ujumla. Mgogoro mkubwa upo kwenye suala Zima la "shared expenditures", kizingiti kikubwa cha joint finance commission kutekeleza kazi yake ni upande huu wa "shared expenditures" kuliko upande wa "shared revenues". Kwa mtazamo wako, kwanini Hali Ipo hivyo? Kwa maana nyingine - je kwanini kikwazo kikubwa kwa JFC kipo zaidi kwenye suala la matumizi ya muungano (uchangiaji wa gharama za kuendesha muungano) kuliko kwenye suala la Mapato?

Sent from my iPhone using JamiiForums
Samahani mkuu wangu, unapoweza kupata ukusanyaji wa mapato utaweza kupata kirahisi uchangiaji wa matumizi. Kama wewe utakadiria kukusanya ama umekusanya 20 nami nakadiria kukusanya/nimekusanya 10 (mapato) matumizi yatatokana na hizo 30 zilizokadiriwa ama zilizopatikana.

Ni sawa na bajeti yetu ya taifa huwa inakadiriwa mapato kwanza na kutokana na makadirio hayo ndio matumizi ya bajeti hutayarishwa. hauwezi kuanza na kugawana gharama za kuendesha serikali ikiwa hakuna uwezekano mgawano ktk mapato ya serikali..
 
Hapana, pengine hujaelewa au unataka kupindisha. Mapato, matimizi na mgawanyo ni pacha watatu.

Huwezi kupata mapato kwanza ukayagawanya kama hujui gharama.
Unapokuwa katika ushirika au shirika ukanunua hisa, kwanza unapata mapato, unaondoa gharama za uendeshaji, unapanga gharama za maendeleo halafu unatoa dividend.
Nitashangaa kama breweries watapata mapato, na kuanza dividend kabla ya kuangalia running cost.

Hoja yako ni kugawana mapato kwanza halafu tugawane gharama. Ni utamaduni ule ule wa kutumia umeme halafu bill zinatupiwa Mtanganyika. Mkandara, mznz hana utamaduni wa kufikiria gharama, utamaduni wake ni kudai hata kisicho chake.
Tugawane mapato gani ikiwa mapato hayo ni ya mmoja?

FYI ukimsikia mznz anaongelea gharama ujue ni mwendawazimu.
 
Nguruvi3
Labda nikukumbushe tu ya kwamba hata huku Majuu wapo watu wanajitambulisha kwa nchi zao.
Mquebec hajiiti Mcanada na hata Mscotish hajiiti Muingereza wala British, haya ni maswala ya kawaida kabisa ktk miungano ya nchi kuunda Taifa kwa sababu mara nyingi maamuzi ya kuungana nchi hufanywa na watawala kutokana na historia ya nchi hizo. Sisi tulozaliwa baada ya muunganmo ndio tunaokuja na hoja nzito dhidi ya Muungano bila kufahamu ya kwamba historia ndio ilowalazimu wao kuungana kutokana na WATU, ARDHI na USALAMA wa nchi hizo.
Factors hizi haziondoki kirahisi kama jinsi watu wengi wanavyofikiria.

Unaposema tuwe na mambo 7 tu huu ni muungano wa aina gani?
Je, Unawezaje kuwa na serikali ya Tanganyika pasipo kuwa na nchi yake na kama itakuwepo hii tanganyika itakuwa na mihimili mingapi na itachukua muda gani kuiandaa.

Je hiyo Tanganyika itakuwa na bunge lake? halafu ndio tuwe na bunge la Muungano ambalo Wazanzibar pia hawalitaki isipokuwa kujiunga na bunge la EAC walitakalo!.

Je, Unapokubali mambo 7 ya muungano haitakuwa muunganosawa na huo wa jumuiya ya EAC, hivyo unahitaji nini kuwa na mkataba mpya na Zanzibar wakati tunaweza tu kuvunja huu uliopo na tukakutana huko Arusha sijui Nairobi kisha tuanze ya Kagame vs JK!

Pili, Uksha unda serikali ya Tanganyika utahitaji kuwa na bunge la Tanganyika hivyo utaanzisha uchaguzi mpya wa wabunge utakao chukua miezi na kisha utunzi wa katiba ya tanganyika ambayo itapitia changamoto kama hizi tena. YYaani ni mlolongo wa maswali wa mambo ambayo yanaiweka katiba mpya tuitakayo kapuni.

haya nipe majibu ya haraka kuhusu haya:-
1.Bunge la Tanganyika litawakilishwa na vyama gani? maana CUF ni chama cha visiwani na Chadema chama cha bara kama wasemavyo wanasiasa, Je ni sheria ipi itakayo wazuia CUF na vyama vya visiwani kugombea bara au Chadema na vyama vya bara kugombea Visiwani?

2. Hiyo CCM itaruhusiwa kugombea upande gani Zanzibar au bara wakati kina wanachama kila upande au nacho ni chama cha bara? na kama hakitaruhusiwa kugombea Zanzibar, mgombea wa chama hicho atakuwa na mahusiano gani na CCM ya bara? au vitaanzishwa vyama vipya pande zote? nini mipaka ya vyama vilivyopo upande wa pili (ili Znz) wasione wanaingiliwa ktk mambo yao.

Wakuu zangu, hivi kweli haya yote mmeyafikiria au mnasema tu ili mradi mnaitaka Tanganyika! na mkisha ipata Tanganyika kweli bado mtakubali kuwa na hayo mambo 7? au nilichosema mimi ndio rahisi kabisa. Kumbuka tu ya kwamba Mambo yote yakiwa ya Muungano, tunawalazimisha kina Jussa kuufyata. hakuna swala la Uzanzibar wala Utanganyika ila Utanzania hata kama watajiita Wazanzibar nawe unaweza kujiita Mtanganyika na ukaipeperusha bebdera ya tanganyika juu ya paa la nyumba yako.

Hii ni Identity tu ktk mfumo wa Kiutawala na pride ya uzawa, kama tulivyokuwa tukifanya sisi na makabila yetu. Utakapo itumia vibaya hiyo pride against others hapo ndipo utakuwa umevunja sheria, otherwise ni jambo jema tu kaa vile mataifa yatakavyo peperusha bendera zao huko Brazil kuanzia hiyo kesho..
Ni ngumu sana kumwelewa Mkandara anasimamia nini, na kwasababu zipi. Labda kwa wale wenye wasi wasi kuhusu kutomwelewa mkuu naomba niwatoe hofu kwa kuonyesha bandiko lake hapo juu lilivyojichanganya juzi, jana, leo na kesho.

1. Kwazana si kweli, Waquebec wanaojiita hivyo ni wale extremist.
Hata wao wakiwa nje ya nchi yao hujulikana kama Wacanada. Kama wangekuwa wanjivunia Uquebec, wengi wasingevuka Gateneu siku ya referendum, na wengine hawakuwahi kurudi.
Miezi miwili wamemkataa Duccep aliyekuwa kinara wa U-Quebec. Hivyo mkuu, usitudanganye.

2. Mkandara anasema, mambo yote ni ya muungano. Amerudia kauli hiyo zaidi ya mara 10 hadi sasa.
Kwabahati mbaya Mkandara anajisahaulisha historia.
Muungano ulianza na mambo 11 si yote, hivyo kuuliza 7 ya nini ni kutofahamu historia ya muungano.
Katika hayo 11 ya awali yalioasisiwa na Nyerere na Karume, Mkandara hakuona tatizo.

Miaka 40 baadaye mambo yakaongezwa na kufikia 22 ambayo yakinyumbulishwa yatakuwa 47.
Hapo tulikuwa tunaelekea katika mambo yote ni ya muungano kwa mujibu wa Mkandara.

Mkandara yupo katika rekodi akisema kuongezwa mambo hayo kulikuwa 'Unyemela'
Yaani kufanya 'mambo yote' yawe ya muungano kama anavyosema leo, huko nyuma aliita unyemela.

Mambo ya kinyemela yaliingizwa katika katiba na sheria kwa kutumia bunge la S2 analotetea Mkandara.
Wakati huo huo anasema, kuingiza kinyemela kulilenga kupora madaraka na kuionea Zanzibar.
Alichosahau ni kuwa huko nyuma ametetea S2 kama suluhisho, leo anatuambia S2 zilifanya makosa kuingiza mambo Kinyemela.

Mkandara anasema suluhisho ni S2. Amesahau kuwa S2 ndizo zilizoruhusu znz kuandika katiba ya 2010 ambayo imeondoa mambo 22 bila kutumia sheria ya bunge la S2a analotetea.

Miongoni mwa mambo hayo yapo 4 yaliyokuwepo katika yale 11 ya awali.
Kwa maana kuwa baada ya kuondoa 22 sasa wamefikia mahali na kuondoa hata 4 katika 11 na kubaki 7.

Yanapobaki 7 kutoka 11 Mkandara anashangaa huo utakuwa muungano gani.
Kwani yale ya 1964 si yalikuwa 11, je huo ulikuwa muungano wa kitu gani.

Kwamba, alichokifanya Warioba na tume ni kuhalalisha mambo yaliyoondolewa na Zaznibar tena kwa kiburi, jeuri na ufidhuli wa kutoheshimu katiba wala taratibu.

Kama unadhani Mkandara anakuchanga, subiri, hebu endelea hapa chini uone anavyojivuruga na kukuvuruga kimantiki

Mkandara anadai ni muda gani utatumika kufanya uchaguzi na kuandika katiba ya Tanganyika.
Huko nyuma alisema mambo asilimia 95 ya bunge la JMT ni ya Tanganyika.

Akasema hata serikali ni ya Tanganyika. Leo anashindwaje kuelewa kuwa ukiwaondoa wale watalii 81 wasiokuwa na kazi kutoka nchi jirani ya znz, bunge na katiba ni ya Tanganyika.

Katiba ya sasa ni ya Tanganyika kwasababu znz haitambui, na wala haina heshima juu yake.
Kama katiba ya znz ni juu kuliko ya JMT, basi hiyo ya JMT ni ya Tanganyika. Ugumu anaosema unatoka wapi?

Mkandara anadai wagombea wa Tanganyika watatoka vyama gani. Hee ! kwani hilo ni la ajabu?
Kule znz sasa hivi BLW lina wabunge wa vyama gani?

Nani amewazuia Watanganyika wasigombee znz na kwanini Tanganyika ikitumia mwiko ule ule kupakua pilau yake ionekane nongwa. Hili la vyama lipo wazi sana na wala halihitaji kujadili unless mtu amejitoa ufahamu.

Mkandara anasema wazanzibar hawataki bunge la shirikisho. Hana takwimu za aina yoyote bali hisia zake tu kujenga utetezi. Wazanzibar wasingetaka hilo bunge basi wasingekubali S3. Hivyo anawasingizia.

Na mwisho anasema, kama mambo 7 basi tuelekee EAC.
Mbona hili tumelijadili siku nyingi sana. Kwani ni nani anayetaka mamlaka kamili, na kama ni znz nani kawazuia?
Leo wakitaka tukutane EAC hewala, hakuna anayewashikilia.

Wznz wanajishikilia wenyewe kwasababu hawajui wanataka nini.
Mkandara si hawa akina Kificho, Vuai, Borafia na sasa Raza wanaotaka S2. Kama wangekataa si tungekutana Arusha?

Kama Mkandara angekuwa mkweli, kwanza angeanza na kusema katiba ya 2010 ya znz imeshavunja muungano.
Na kuvunjwa muungao maana yake ni kushindwa kazi kwa S2.
Na muungano uliopo ni wa kufaa wznz tu lakini hauna maana ya muungano. Umeshakufa kutokana na S2.

Juzi wamedai passport na Uraia, hivi hapo Mkandara bado unaamini hawa ni wenzetu na wapo kwa ajili ya Tanzania?
Wapi katika republics zako unazozitaja kila siku kuna nchi ina majimbo yenye urai na passport zake.

Je, ndivyo Ontario wanavyofanya? Ndivyo Montana wanavyofanya? Ndivyo Berth wanavyofanya?

Mkandara kama umedhamiria kuichanganya hadhra, basi umefanikiwa.
Inahitaji jiniazi au psychic kukuelewa na kuelewa position yako.

Mkuu wangu, sikujua wewe ni spinning doctor mzuri sana.
 
Joint Finance Commission iliundwa kwa lengo la kushauri serikali Mbili za muungano juu ya sharing of revenues and expenditures, na fiscal relations kwa ujumla. Mgogoro mkubwa upo kwenye suala Zima la "shared expenditures", kizingiti kikubwa cha joint finance commission kutekeleza kazi yake ni upande huu wa "shared expenditures" kuliko upande wa "shared revenues". Kwa mtazamo wako, kwanini Hali Ipo hivyo? Kwa maana nyingine - je kwanini kikwazo kikubwa kwa JFC kipo zaidi kwenye suala la matumizi ya muungano (uchangiaji wa gharama za kuendesha muungano) kuliko kwenye suala la Mapato?

Sent from my iPhone using JamiiForums

Mchambuzi,

Kabla ujibu suala lako ningependa nikuweka sawa jambo fulani hapa.

Kwa mujibu wa Sharia ya JMTz y ibara ya 133 imefafanua wazi kuwa Joint Finance Commission (JFC) ndio yenye mamlaka kisharia kutunza akaunti maalum ya fedhwa za muungano wa Tz.

Na Ibara hiyo ikazidi kuainisha kuwa fedhwa kwa ajili ya shughuli za Muungano zitakuwa zinalindwa na kuhifadhwiwa katika akaunti hiyo matumizi ya mambo ya muungano tu
.

Na ikazidi kusisitiza mapato yote ikiwemo michango au tozo kwa nchi washirika na misaada na mikopo yote kwa taasisi a mambo ya muungano na wizara hizo yataratibiwa na akaunti hiyo chini ya usimamizi wa Tume ya wataalamu wa fedhwa na uchumi wa (JFC) nchi hizo.

Nikija kwenye suala lako na naunganisha na kuanzishwa kwa Tume hii JFC.

Tume hii ya pamoja iliundwa rasmi 1996 ili kuondoa kero za muungano ambazo kwa kiasi kikubwa sana zilichangiwa na manung'uniko na kulalamika kwa nchi wanachama kuhusu mas'ala ya uchumi.
a) Watanganyika walilalamika kuibeba Znz kiuchumi lakin hakukuweza kupatikana takwimu sahihi na za kitaalamu kuonyesha wanawabeba kiasi gani.

b) Watanganyika walisema kuwa Znz haichangii muungano lakin hakuna pahala popote panapoonyesha TGK imechangia kiasi gani na Znz haikuchangia kiasi gani?

c) Upande wa Znz wao wlilalamika TGK wanakopa pesa katika taasisi zaa kimataifa kwa mambo yasiyo ya muungano kwa kutumia nembo ya Tanzania na hivyo deni hilo kulipwa na nchi zote wakti waliokopa ni TGK..

Sasa Serikali ya Mkapa mwaka 1996 iliunda tume hii kwa ajili ya kuondosha manunguniko hayo na kama ingefanya kazi zake kama ilivyokusudiwa na Bunge kwa kuundwa kutekeleza majukumu yake ya kutunza akaunti ya muungano kwa matumizi ya taasisi za muungano na wizara za muungano kwa mujibu wa Katiba yya JMtz basi haya malalamiko ya nguruvi3 yote angebaki kuwa ni historia,

Tunaposema kutunza akaunt ina maana kuangalia na kuratibu kile kinachoingia katika mfuko huo na vile vile kuratibu kile kinachotoka katika mfuko huo na kuhakikisha kinatumika na taasisi za muungano tu na si vinginevyo,,

Sasa ahali yangu Mchambuzi tuache kutabiri jambo bila kulifanya Kinachotakiwa ni kuanza kazi kwa Akaunti ya pamoja chini ya JFC na kupitia ripoti zake za mwaka kuonyesha ni nchi gani haijachangia na kwa kiasi gani kuliko kuweka tuhuma bila kuwa na data sahihi lakin pia kuondosha malalamiko kuwa nchi moja inafuja pesa za muungano ikiwemo mikopo na misaada lakin zogo la deni linadondokea kwa wote.

Ni vizuri Serikali ya JMTz ifanye kila linalowezekana kuanzisha Akaunti hii ili kuondoa kero zote za muungano kwani kuacha kuanzisha KUNATUPA FURSA WACHUMI NA WANANCHI WA KAWAIDA KUJIULIZA JE JMTz KUNANI?

Kwanza, njoo umjibu Mchambuzi hapo juu

Pili, tueleze kwa muundo wa sasa ni zipi wizara na taasisi za muungano tu.
Tatu, tueleze ni zipi rasilimali za pamoja za muungano
Nne, nini chanzo cha mapato cha account hiyo
Tano, kwanini kusimamia mgawanyo na si kusimamia ukusanyaji wa mapato.

Nguruvi3,

Nafikiri mengi ya masuala yako nilikujibu kule kwenye UZI WA KWANINI ZNZ WAPATE 21% YA AJIRA ZA MUUNGANO.

Lakin kwa kukusaidia zaidi Kujuamambo ya Muungano HAYA YAMEAMBATANISHWA MWISHO WA KATIBA YA JMTz. Naomba uyapitia utayaona.

Unaposema Rasilimali hii inakusudiwa wafanyakazi na mali zote za wizara hizo ikiwemo majumba, thamani na magari na vingine vyote.

Vyanzo vya mapato vimeainishwa na Taarifa ya TUME YA PAMOJA YA UCHUMI NA FEDHWA (JFC) KATIKA ripoti na mapendekezo yake ya mwaka 2006 kwa Serikali ya JMTz.na hata ukipitia tovuti ya JFC

La mwisho tusiwe watabiri bali tunatakiwa kutekeleza SHARIA KWA KUANZISHA HII AKAUNTI YA PAMOJA YA FEDHWA ZA MUUNGANO TU Itakayoratibiwa na JFC ili kuthibitisha hayo malalamiko yako na mengine niliyoainisha wakti namjibu Mchambuzi na kutatua kero hizo za Mvungano wenu.

Labda nikuulize kwa mara nyingine KWANINI JMTz INAJIKANYAGA KATIKA KUANZISHWA KWA AKAUNTI HII YA PAMOJA YA MUUNGANO? au ndio yale yale kukopa kwa jina la TZ na kutumia mikopo hiyo kujenga barabara ya Nyamwage- Lindi, Bwanga kupitia kanazi mpaka Biharamuro, Biharamuro - Lusaunga, au Kujenga barabara kutoka Mbezi kupitia maramba mawili mpaka Kinyerezi, Au Tabata kupitia dampo mpaka Kigogo kama inavyojionyesha katika bajeti yenu ya wizara ya Magufuri ya 2014/15
 
Hapana, pengine hujaelewa au unataka kupindisha. Mapato, matimizi na mgawanyo ni pacha watatu.

Huwezi kupata mapato kwanza ukayagawanya kama hujui gharama.
Unapokuwa katika ushirika au shirika ukanunua hisa, kwanza unapata mapato, unaondoa gharama za uendeshaji, unapanga gharama za maendeleo halafu unatoa dividend.
Nitashangaa kama breweries watapata mapato, na kuanza dividend kabla ya kuangalia running cost.

Hoja yako ni kugawana mapato kwanza halafu tugawane gharama. Ni utamaduni ule ule wa kutumia umeme halafu bill zinatupiwa Mtanganyika. Mkandara, mznz hana utamaduni wa kufikiria gharama, utamaduni wake ni kudai hata kisicho chake.
Tugawane mapato gani ikiwa mapato hayo ni ya mmoja?

FYI ukimsikia mznz anaongelea gharama ujue ni mwendawazimu.
Mkuu mbona wewe ndio unajichanganya? serikali haina Ubia wala hisa ktk kuendeshaji mambo yake kama Breweries na kutegemea mwisho wa siku kugawana dividend. dah mkuu wangu ama kweli bado upo ktk dunia nyingine kabisa..Nadhani wewe bado upo ktk mfumo wa serikali kuu kushika njia zote za uchumi, serikali ya CCM ukiendesha miradi yake na kwamba serikali hiyo ndio inayopeleka maendeleo kwa wananchi kwa kuendesha biashara na uchumi wa nchi hivyo mtaji wake ktk uwekezaji na hisa ndio chanzo cha mapato yake. Hapana mkuu wangu hapa umeingia choo cha kike! na ndio maana CCM kila siku wao husisitiza kwamba wao ndio wamepeleka umeme, maji na kujenga barabara kwa sababu wana mtaji mkubwa nanyi mkaamini kwamba sio kodi zenu ndizo zinazojenga.

Mkuu wangu, tupo ktk mfumo wa Ubebari toka mwaka 1993 na ndio maana sisi tumeitaka katiba mpya! usiendelee kufikria Kikomunist ati serikali ndio inayoshikilia njia kuu za muchumi na kufanya biashara, serikali yoyote ndanii ya mfumo huu tulokuwa nao sasa hutegemea vyanzo vyake vya mapato toka kodi za wananchi wake wawekezaji, wajasiriamali, Wakulima na Wafanyakazi. Kila mmoja wetu ndiye mtaji wa serikali na ndio maana tunawataka viongozi wote nao ktk nafasi zote za kiutawala walipe kodi maana jukumu sii letu sisi wananchi bali sote na wao pia ni sehemu ya wananchi. Misamaha ya kodi kwa mashirika ya nje ifutwe isipokuwa kwa maeneo yatakayo wawezesha wananchi kushiriki kikamilifu ktk ujenzi wa nchi hii kama ufunguzi wa viwanda vya ndani kusindika mazao yetu pamoja na zana za Kilimo.

Serikali kazi yake ni kulinda utekelezaji wa sheria na matumizi yalopitishwa, Ukusanyaji wa kodi na kupanga mipango ya maendeleo ilotokana na sera zake wakitegemea kodi zetu. Ni kuwawezezesha wananchi wake ktk mikopo na misaada ambayo upande wa pili serikali hiyo inabashiria kunufaika na kodi za mapato na mzunguko wa fedha. Hivyo tunapozungumzia MAPATO ya serikali ni kutokana na makadirio yake ya ukusanyaji wa hizo kodi na mikopo (grants) toka nje kwa dhamana ya Utaifa. Muungano wa nchi hauna Ubia bali ni kama nilivyoitumia NDOA, ya kwamba hufungi ndoa kwa sababu ya fedha atakazoingiza mwenza wako ktk ndoa yenu! hakuna Ubia ktk ndoa wala sii swala la fedha lilowaunganisha ila ubia wa nafsi ya kujituma, kuji commit na kuwa responsible na maisha ya ndoa. Mkianza na kuulizana wewe unakuja na nini ktk ubia haya ndio matokeo ya ndoa zetu na hata Muungano wetu kufikia hapa tulipo.

Vyanzo vya mapato ya serikali ni WATU wenyewe walowekeza ndani ya nchi hizo hivyo serikali haina mtaji isipokuwa pato lake hutoka kwa WATU wake. Na hivyo matumizi ya serikali hutanguliwa na ukusanyaji wa kodi na sio uwekezaji wake ktk miradi ya kiuchumi kama mnavyoendelea kuubeba Ujamaa na Kujitegemea. Kama serikali ingehitaji mtaji kwanza basi sidhani kama tungekuwa na serikali maana hata hao Sudan ya kusini hawakuwa na ndululu mfukoni zaidi ya nia yao ya kuelewa kwamba kodi zao mapato ya mafuta haiwanufaishi watu wa kusini bali huenda kuijenga North.

Hivyo mkuu wangu vyanzio vya mapato ya serikali hukadiriwa kutokana na ukusanyaji wa kodi, serikali haifanyi biashara bali huandika policies kuwawezesha wananchi kuzalisha na serikali pia huwawezesha wananchi wake mikopo ya ndani ktk ubunifu wao ili wapate kuijenga nchi yao. Gharama za uendeshaji serikali hutokana na kodi za wananchi hivyo kinachotazamwa hapa ni vyanzio vya upatikanaji kodi hizo na sii kwamab serikali inawekeza ubia mahala ili ipate faida kama Benki au mashirika.

Na ndio maana halisi ya hata msemo wa JFK akisema 'My fellow American. ask not what your country can do for you, ask what you can do for your country!' Kwa maana ya kwamba wewe mwananchi ndiye chanzo cha mapato ya serikali, wao kazi yao kubwa ni kusimamia utekelezaji wa sheria zinazowalinda.
 
Ni ngumu sana kumwelewa Mkandara anasimamia nini, na kwasababu zipi. Labda kwa wale wenye wasi wasi kuhusu kutomwelewa mkuu naomba niwatoe hofu kwa kuonyesha bandiko lake hapo juu lilivyojichanganya juzi, jana, leo na kesho.

1. Kwazana si kweli, Waquebec wanaojiita hivyo ni wale extremist.
Hata wao wakiwa nje ya nchi yao hujulikana kama Wacanada. Kama wangekuwa wanjivunia Uquebec, wengi wasingevuka Gateneu siku ya referendum, na wengine hawakuwahi kurudi.
Miezi miwili wamemkataa Duccep aliyekuwa kinara wa U-Quebec. Hivyo mkuu, usitudanganye.

2. Mkandara anasema, mambo yote ni ya muungano. Amerudia kauli hiyo zaidi ya mara 10 hadi sasa.
Kwabahati mbaya Mkandara anajisahaulisha historia.
Muungano ulianza na mambo 11 si yote, hivyo kuuliza 7 ya nini ni kutofahamu historia ya muungano.
Katika hayo 11 ya awali yalioasisiwa na Nyerere na Karume, Mkandara hakuona tatizo.

Miaka 40 baadaye mambo yakaongezwa na kufikia 22 ambayo yakinyumbulishwa yatakuwa 47.
Hapo tulikuwa tunaelekea katika mambo yote ni ya muungano kwa mujibu wa Mkandara.

Mkandara yupo katika rekodi akisema kuongezwa mambo hayo kulikuwa 'Unyemela'
Yaani kufanya 'mambo yote' yawe ya muungano kama anavyosema leo, huko nyuma aliita unyemela.

Mambo ya kinyemela yaliingizwa katika katiba na sheria kwa kutumia bunge la S2 analotetea Mkandara.
Wakati huo huo anasema, kuingiza kinyemela kulilenga kupora madaraka na kuionea Zanzibar.
Alichosahau ni kuwa huko nyuma ametetea S2 kama suluhisho, leo anatuambia S2 zilifanya makosa kuingiza mambo Kinyemela.

Mkandara anasema suluhisho ni S2. Amesahau kuwa S2 ndizo zilizoruhusu znz kuandika katiba ya 2010 ambayo imeondoa mambo 22 bila kutumia sheria ya bunge la S2a analotetea.

Miongoni mwa mambo hayo yapo 4 yaliyokuwepo katika yale 11 ya awali.
Kwa maana kuwa baada ya kuondoa 22 sasa wamefikia mahali na kuondoa hata 4 katika 11 na kubaki 7.

Yanapobaki 7 kutoka 11 Mkandara anashangaa huo utakuwa muungano gani.
Kwani yale ya 1964 si yalikuwa 11, je huo ulikuwa muungano wa kitu gani.

Kwamba, alichokifanya Warioba na tume ni kuhalalisha mambo yaliyoondolewa na Zaznibar tena kwa kiburi, jeuri na ufidhuli wa kutoheshimu katiba wala taratibu.

Kama unadhani Mkandara anakuchanga, subiri, hebu endelea hapa chini uone anavyojivuruga na kukuvuruga kimantiki

Mkandara anadai ni muda gani utatumika kufanya uchaguzi na kuandika katiba ya Tanganyika.
Huko nyuma alisema mambo asilimia 95 ya bunge la JMT ni ya Tanganyika.

Akasema hata serikali ni ya Tanganyika. Leo anashindwaje kuelewa kuwa ukiwaondoa wale watalii 81 wasiokuwa na kazi kutoka nchi jirani ya znz, bunge na katiba ni ya Tanganyika.

Katiba ya sasa ni ya Tanganyika kwasababu znz haitambui, na wala haina heshima juu yake.
Kama katiba ya znz ni juu kuliko ya JMT, basi hiyo ya JMT ni ya Tanganyika. Ugumu anaosema unatoka wapi?

Mkandara anadai wagombea wa Tanganyika watatoka vyama gani. Hee ! kwani hilo ni la ajabu?
Kule znz sasa hivi BLW lina wabunge wa vyama gani?

Nani amewazuia Watanganyika wasigombee znz na kwanini Tanganyika ikitumia mwiko ule ule kupakua pilau yake ionekane nongwa. Hili la vyama lipo wazi sana na wala halihitaji kujadili unless mtu amejitoa ufahamu.

Mkandara anasema wazanzibar hawataki bunge la shirikisho. Hana takwimu za aina yoyote bali hisia zake tu kujenga utetezi. Wazanzibar wasingetaka hilo bunge basi wasingekubali S3. Hivyo anawasingizia.

Na mwisho anasema, kama mambo 7 basi tuelekee EAC.
Mbona hili tumelijadili siku nyingi sana. Kwani ni nani anayetaka mamlaka kamili, na kama ni znz nani kawazuia?
Leo wakitaka tukutane EAC hewala, hakuna anayewashikilia.

Wznz wanajishikilia wenyewe kwasababu hawajui wanataka nini.
Mkandara si hawa akina Kificho, Vuai, Borafia na sasa Raza wanaotaka S2. Kama wangekataa si tungekutana Arusha?

Kama Mkandara angekuwa mkweli, kwanza angeanza na kusema katiba ya 2010 ya znz imeshavunja muungano.
Na kuvunjwa muungao maana yake ni kushindwa kazi kwa S2.
Na muungano uliopo ni wa kufaa wznz tu lakini hauna maana ya muungano. Umeshakufa kutokana na S2.

Juzi wamedai passport na Uraia, hivi hapo Mkandara bado unaamini hawa ni wenzetu na wapo kwa ajili ya Tanzania?
Wapi katika republics zako unazozitaja kila siku kuna nchi ina majimbo yenye urai na passport zake.

Je, ndivyo Ontario wanavyofanya? Ndivyo Montana wanavyofanya? Ndivyo Berth wanavyofanya?

Mkandara kama umedhamiria kuichanganya hadhra, basi umefanikiwa.
Inahitaji jiniazi au psychic kukuelewa na kuelewa position yako.

Mkuu wangu, sikujua wewe ni spinning doctor mzuri sana.
Wee kweli sii muelewa..
1. Nilichosema ni kwamba Wa Quebec hujiita hivyo haina maana wao sio WaCanadian ama wanajulikana kama wao ni WaQubec, hata hao Wazanzibar wanajiita hivyo wakiwa ndani lakini ktk sheria hujulikana kama Watanzania isipokuwa wale wenye siasa kali extremist. Swala linalokukwaza ni kelele zao ambazo hata Quebec wanazo kutokana na hifadhi ya Identity yao. Mimi nikijiita Mkerewe haina maana naupoteza Utanzania wangu bali ni pride fulani inayotokana na Uzawa kama vile mimi pamoja na kuiwa MCanadian bado naamini mimi ni Mtanzania na najitambulisha kama Mtanzania hapa nchini. Kila kabila na kila mtu huku majuu hujitambulisha na asili yake na sii kosa. Ndio maana nikaunganisha hili la Wazanzibar na lile la uraia pacha ili upate kufahamu lakini wapi! - hunielewi! na wala huko peke yako, mpo wengi sana Wadanganyika!

2. Mkuu wangu lazima unisome naandika nini. Huko nyuma nilisema nini madai ya Wazanzibar, hivyo naposema ama kuandika mambo hayo yaliongezwa kinyemela nina maana ya kwamba ndivyo Wazanzibar kina Jussa na Ukawa wanavyodai na ukweli wake nikasema mimi siujui na zipo sehemu kadhaa nimesema hivyo. JK akatuhakikishia kwamba hayakuongezwa kinyemela bali yalitokana na kuvunjika kwa EAC na walikubaliana kuyaweka ktk mambo ya Muungano, wakati huo tulikuwa ktk siasa za Ujamaa na Kujitegemea japo awali ya yote walikubaliana kuwa na mambo 11. Hii imeeleweka.

Pili, Kila napoandika mawazo yangu mkuu wangu, naitazama Tanzania ya leo. Tanzania ambayo sii ya Kijamaa tena ila Tanzania ambayo imepokea mfumo wa demokrasia wa vyama vingi na tupo bado ktk transformation ya kiuchumi toka Ujamaa, hivyo katiba lazima ijengwe ktk misingi ya kuwezesha transformation hiyo japo serikali ya CCM wao wanadai tupo ktk transition ya kiuchumi.. Transition ya watu kuuza utu wao na ardhi yao ambayo haitaweza kuwanufaisha wananchi hata siku moja hata kama tukipewa miaka 200 ya transition ndani ya katiba hi ya CCM (ya mwaka 1977). Wananchi watarudi ktk utumwa na kutawaliwa, na imedhihirisha tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele kila siku ya transition hii.

Swala la serikali 2 au 3.
Mimi nachosema sii kwamba serikali 1,2 wala 3 ndio suluhisho la matatizo yetu. Wewe umekazania serikal 3 na kuniweka mimi ktk kuzipendelea serikali 2 zilizopo! hii sii kweli wala sahihi. Unashadadia hili pasipo kuzingatia kwamba mimi natazama mapungufu yetu (ktk muungano) na sio kero zetu kutokana na muundo wa serikali 2. tuwe na serikali 3 pasipo kutatua mapungufu ya katiba iliyopo hatuwezi kuwa na muungano wa nchi zetu kwa kuwa na mambo 7, 11 wala 22 ndani ya mfumo wa kibepari na demokrasia ambao siasa ya nchi na policies zake zote zinaupa UCHUMI kipaumbele ya Ulinzi ama uzawa hivyo, Ni nani awe na mamlaka ya shughuli za mambo haya ndilo somo kubwa tutoendelea na micromanagement!.

Hii haijalishi wingi/uchache wa mambo ktk JMT bali nani mwenye mamlaka ktk shughuli za uendeshaji wa mambo hayo! tunagawanaje majukumu na kupanga na kuchagua, sheria, uzalishaji na ukusanyaji kodi ili kuinua uchumi wa taifa. Nini mipaka ya mamlaka ya kila wadhifa na nchi, hii inakwenda hadi mamlaka ya Meya kama hana mamlaka ya kusimamia shughuli za halmashauri yake, basi hata yeye anakuwa amemezwa na serikali ya Tanganyika a.k.a CCM, bila kujali ni hesabu ya mambo mangapi yamo ktk serikali yake. CCM wakitaka kujenga ama kuuza uwanja wa Anatoglou au kuvunja, Meya hana sauti wala sii mamlaka yake hlii ndio tatizo na mfumo tulokuwa nao ndani ya utawala wetu. Serikali iliyopo madarakani inakuwa bwana wa wananchi na sii kweli kwamba serikali inawatumikia wananchi kama ilivyotakiwa.

Hofu ya Tanganyika kuimeza Zanzibar ingetokana na sii wingi wa mambo ya Muungano, bali impact imetokana na MAMLAKA YA SERIKALI ya Tanganyika ndani ya shughuli za maendeleo. Unaweza wewe jenga nyumba lakini mamlaka ya uendeshaji nyumba hiyo akawa nayo mkeo, sii lazima wewe uingie jikoni kupanga hata sufuria, mapato/matumizi yake. Mke akilitaka jiko, kupanga matumizi yake mwachie aliendeshe maadam watoto wanakula wewe hutapoteza sahani yako mezani, hivyo kuanza kudai kila mtu awe na jokofu (fridge)yake!. Na ndicho wasichokiona hata hao Wazanzibar kwa sababu wanatazama tu picha iliopo mbele yao na sii undani wa picha hiyo. Na ndio maana nazidi kusisitiza wewe upate kufahamu tofauti baina ya MAMBO YA MUUNGANO na MAMLAKA YA KUENDESHA SHUGHULI ZA SERIKALI ambayo tunajua kwamba serikali ni sehemu tu ya mihimili.

Wazanzibar kina Jussa wanacholalamikia ni haya Mambo ya Muungano kutoka 11 na kuwa 22 pasipo hata kujua kwamba haya mambo mengine yaloongezwa yalitoka EAC na sijui yanainufaisha vipi Tanganyika ama kuimeza vipi Zanzibar kama sii mamlaka yake kuwa chini ya serikali ya Tanganyika. Hawajui kwamba kulikuwepo na makubaliano baina ya viongozi wa serikali 2 kuyaweka ktk mikono ya Muungano maana reli, bandari na Posta ni vitu ambavyo wakati ule ilikuwa mtaji tosha wa nchi ktk ujamaa na muhimu zaidi ktk uchumi wa nchi lakini kosa lipo ktk mamlaka ya usimamizi wake baada ya kuondokana na Ujamaa.

Kina Jussa wao wanatumia tu hili neno - Mambo yalikuwa 11 sasa 22 inatoka wapi na kwa makubaliano gani kisiasa! Hii ndio arguement yao kutafuta sheria iloruhusu hayo na toka wapewe majibu hawaendi huko tena ila bado wanataka mambo haya yaondolewe kutokana na ule mkataba wa kwanza. Ni siasa zinazowavutruga wananchi haswa Wazanzibar ambao hawajui faida wala hasara za mambo hayo kwao ila utengano.

Lakini basi mimi najua fika kwamba sii Mambo ya Muungano ndio yalotufikisha hapa tulipo bali ni mamlaka ya shughuli za serikali ndio chanzo na sababu ya hii kutoelewana baina ya bara na visiwani. Tanganyika inaweza kuimeza Zanzibar kwa kutumia mamlaka ya shughuli za serikali na utunzi wa sheria. Wao kukosa mamlaka kamili ya kusimamia uendeshaji wa shughuli zao za maendeleo ndio kisa mkasa wa kero zote maana ukitazama swala la Zanzibar kujiunga na IOC limepigwa vita kutokana na kwamba hawana mamlaka hayo bali serikali ya JMT ambayo ni Tanganyika hadi leo, hivyo hatuna serikali ya Muungano ila ya Tanganyika kutokana na mfumo wa UJIMA unaoshikiliwa na CCM.

Na hata tukirudisha mambo yawe 7, na katika mfumo huu wa Kibepari basi haitakuwa jawabu kabisa kwani serikali hiyo ya muungano haitaweza kujiendesha. Itakuwa haina vyanzo wala haina nguvu hivyo rais na serikali yake watakuwa ceremonial tu.. sasa huu muungano una faida gani kwetu? haitapita Muda Tanganyika na zanzibar watavunja hata hiyo serikali ya Muungano maana itakuwa mzigo na gharama kwao. hapo muungano hautakuwepo tena. Hivyo swala sii kupinga serikali 3, bali ni mamlaka ya pande mbili yatazamwe upya! Serikali 2 au 3 ni sawa na mgonjwa wa malaria unapompa Panadol 2 au 3 kutuliza maumivu ya kichwa, hujatibu maradhi yenyewe!
 
Wee kweli sii muelewa..
Na hata tukirudisha mambo yawe 7, na katika mfumo huu wa Kibepari basi haitakuwa jabu kabisa kwamba serikali hiyo ya muungano haitaweza kujiendesha. haina vyanzo wala haina nguvu hivyo rais wake ntakuwa ceremonial tu.. sasa huu muungano una faida gani kwetu? haitapita Muda Tanganyika na zanzibar watavunja hata hiyo serikali ya Muungano maana itakuwa gharama kwao. hapo muungano hautakuwepo tena.

Hivyo swala sii kupinga serikali 3, bali ni mamlaka ya pande mbili yatazamwe upya! Serikali 2 au 3 ni sawa na mgonjwa wa malaria unapompa Panadol kutuliza maumivu ya kichwa hujatibu maradhi yenyewe!
Mamlaka ya pande mbili zipi Mkandara?

Kuna ZNZ na JMT ambayo ZNZ imo, sasa pande mbili ni zipi.
Hapa sema mamlaka ya pande moja na nusu umma utakuelewa.

Huwezi kutuweka katika JMT ambayo wznz wapo ukasema sisi ni Watanganyika.
Namna hii ya kufikiri ni hatari sana, ndio imetufikisha hapa kwasababu CCM kama Mkandara hawa appreciate tatizo, wanadhani kufariji wznz ndio suluhu.

Na sisi wengine tupo jamvini kupiga vita hii mentality ili kizazi kijacho kisirithi kupitia simulizi danganyifu unless kuna genes katika DNA za namna hiyo, we can't help.

Pili, Mkandara kama Mwigulu na zaidi ya Nape, wanasema kuendesha serikali 3 ni tatizo kwasababu itakuwa haina chanzo cha uhakika cha mapato.
Wasichosema ni kuwa S2 chanzo chake cha mapato ni kipi.
Hawasemi hilo kabisa ili kutowaudhi Wazanzibar.

Tatu, Mkandara kama Pandu Kificho, anasema, rais atakuwa ceremonial.
Hivi unaweza kuwa na rais mwenye jeshi akawa ceremonial.

Lakini pia wamegoma kabisa kushughulisha fikra zao.
Wapo Kunji ya kufikiri! state of denial

Hivi huyu Rais wa sasa si ceremonial tuu! Unawezaje kuwa COMMANDER IN CHIEF, ukawa pembeni wakati jeshi lake linakula kiapo kwa Rais wa nchi jirani ya znz.

Na mwisho Mkandara kwa kutumia fikra za Kingunge anasema S3 itakuwa gharama.
Kwamba S2 zinajiendesha kwa solar energy. Bila kuwaeleza hawa CCM na kina Mkandara, upotoshaji utaendelea.

Leo ukimsoma hapo juu kachukua position nyingine kabisa.
Mkuu you can't be everywhere! flip flop day in day out is cantankerous, where do you stand on issues.
 
Unajua unashangaza sana wee.. Ni wewe mwenyewe ulosema bunge la JMT linajadili mambo asilimia 95 ya Tanganyika, sasa unazitaka nchi 2 zipi kama sio Tanganyika na Zanzibar. Majibu yangu toka mwanzo ni kwamba Kiuhalisia hatuna serikali ya 3 ambayo ni serikali ya Muungano. Ukisema unaomba serikali 3 ili tuwe na serikali ya Muungano nitakuelewa vizuri maana hiyo haipo na ndio maana nikasema serikali hiyo iwe na mambo yote ya Muungano.

Hivyo tunaweza kuwa na serikali 3 lakini kazi kubwa ya kuunda serikali hiyo imetanguliwa na maswali mengi mazito nilokupa hapo nyuma lakini umeyakwepa kijanja japo ktk real life yatahitaji majibu. Lakini ktk hizi serikali 2 tunaweza kuyaweka mambo yote yawe ya Muungano na tukaweza kuiendesha serikali ya tanganyika ndani yake kama tulivyoweza kwa miaka 50 toka mambo 11 hadi 22 na hata yakiwa yote haitabadilisha kitu isipokuwa ni mamlaka ya uendeshaji wa shughuli zake ndio muhimu tugawane majukumu.

Sasa kama hunielewi na bado unatazama picha ilowekwa ubaoni ya serikali 2 badala ya kutazama mamlaka ya serikali hizi yanatumikaje basi hutanielewa kamwe! natanguliza shukran kwa mjadala maana hata akija Yesu bado hutanielewa.

Haya tena unazungumzia rais ceremonial kuwa na Jeshi haiwezekani!, hivi unaelewa nini maana ya na matumizi ya neno hili maana wapo marais kibao. Ni nani commander in cheif wa majeshi ya Uingereza? Huko Singapore na hata Ma sultan wote hawa ni ceremonial ila serikali zao zinaendeshwa na Mawaziri wakuu ambao sii amiri jeshi wakuu i wee vipi? tunazungumzia shughuli na sii mambo ya muungano.Hata mambo yote ya Utawala wa Uingereza na makoloni yake yapo chini ya Malkia. Shughuli zake ndio hutekelezwa na vyombo vya mihimili ya nchi hizo, serikali ikiongozwa na waziri mkuu.

Ama kweli wee kazi kweli kweli kuelewa wala kukubali hujui!
 
Unajua unashangaza sana wee.. Ni wewe mwenyewe ulosema bunge la JMT linajadili mambo asilimia 95 ya Tanganyika, sasa unazitaka nchi 2 zipi kama sio Tanganyika na Zanzibar. Majibu yangu toka mwanzo ni kwamba Kiuhalisia hatuna serikali ya 3 ambayo ni serikali ya Muungano. Ukisema unaomba serikali 3 ili tuwe na serikali ya Muungano nitakuelewa vizuri maana hiyo haipo na ndio maana nikasema serikali hiyo iwe na mambo yote ya Muungano.

Hivyo tunaweza kuwa na serikali 3 lakini kazi kubwa ya kuunda serikali hiyo imetanguliwa na maswali mengi mazito nilokupa hapo nyuma lakini umeyakwepa kijanja japo ktk real life yatahitaji majibu.

Lakini ktk hizi serikali 2 tunaweza kuyaweka mambo yote yawe ya Muungano na tukaweza kuiendesha serikali ya tanganyika ndani yake kama tulivyoweza kwa miaka 50 toka mambo 11 hadi 22 na hata yakiwa yote haitabadilisha kitu isipokuwa ni mamlaka ya uendeshaji wa shughuli zake ndio muhimu tugawane majukumu.

Sasa kama hunielewi na bado unatazama picha ilowekwa ubaoni ya serikali 2 badala ya kutazama mamlaka ya serikali hizi
yanatumikaje basi hutanielewa kamwe! natanguliza shukran kwa mjadala maana hata akija Yesu bado hutanielewa.

Haya tena unazungumzia rais ceremonial kuwa na Jeshi haiwezekani!, hivi unaelewa nini maana ya na matumizi ya neno hili maana wapo marais kibao. Ni nani commander in cheif wa majeshi ya Uingereza? Huko Singapore na hata Ma sultan wote hawa ni ceremonial ila serikali zao zinaendeshwa na Mawaziri wakuu ambao sii amiri jeshi wakuu i wee vipi? tunazungumzia shughuli na sii mambo ya muungano.Hata mambo yote ya Utawala wa Uingereza na makoloni yake yapo chini ya Malkia. Shughuli zake ndio hutekelezwa na vyombo vya mihimili ya nchi hizo, serikali ikiongozwa na waziri mkuu.
Ama kweli wee kazi kweli kweli kuelewa wala kukubali hujui!
Kutokujua si jambo baya, hatari ni kudhani mtu anajua kwakukubali tu.

Nimekuuliza swali la muhimu sana, unawezaje kutenganisha mamlaka ya serikali mbili? ZNZ na JMT?
Nani atakayesimamia mambo yasiyo ya muungano?
Kwasasa ndivyo ilivyo, Mkandara amesahau kuwa kufanya hivyo ni kuvaa koti la muungano.

Mfano, nani atasimamia mambo yasiyo ya muungano ikiwa Rais, makamu na waziri mkuu ni watu wa muungano. Hiyo si ndio sintofahamu iloyopo sasa hivi? Bado mkuu anasema tubaki hapo hapo ili tutenganishe shughuli.

Halafu anasema tunaweza kuendelea na S2 kama ilivyokuwa miaka 50. Nasikitika kukutaarifu kuwa miaka 50 ya muungano ni failure kwasababu muungano haupo kwasasa. Unachosema ni kupongeza failure.
ZNZ wameshajitoa katika muungano kupitia 2010, Mkandara unaongelea muungano upi.

Na anapo ji contradict ni pale anaposema shughuli zitenganishwe, wakati huo huo anasema Tanganyika imevaa koti la muungano, halafu anaseama lazima yawepo mambo ya muungano na yasiyo ya muungano na anamalizia kwa kusema kila jambo ni la muungano. Mkuu, kwanini umeamua kwa makusudi kabisa kukiumiza kizazi hiki kwa kukichanganya?

Mkandara unaheshima kubwa sana jamvini, hofu yangu ni uwezekano wa kutuzalishia vijana waliochanganyikiwa. Why mkuu! let us be fair, kuna vijana wanatusoma na sasa wameshika vichwa jinsi unavyowapeleka left right
 
Mkuu Barubaru:

Huwa tunasahau kutazama Hali ilivyokuwa Kabla ya muungano. Katika kipindi cha 1961-1964, Tanganyika ilikuwa na Mapato yake, na vile vile znZ. Kwa upande wa Tanganyika, vyanzo Vikuu (75%) villi kuwa ni Kama ifuatavyo:

1. Kodi ya makampuni na Watu binafsi (corporate and personal income taxes).
2. Ushuru wa forodha.
3. Ushuru wa bidhaa zilizouzwa nje (katani, kahawa, pamba, chai n.k).

Property tax na other sources zikabeba the remaining 25%.

Upande wa znZ, revenues zilitegemea zaidi ushuru wa bidhaa zilizouzwa nje, hasa karafuu.

Muungano ulipokuja, kwa vile znZ haikuwa na Mapato ya kuweza changia Sawa kutokana na udogo wake, zile kodi hapo juu yani 75% ya Mapato ya Tanganyika yakageuzwa kuwa Ndio Mapato ya muungano kuhudumia masuala 11 ya muungano. Leo hii, Mapato haya yanaitwa Mapato ya serikali ya muungano Wakati kimsingi ni Mapato ya Tanganyika. Leo, forodha inaingiza sh bilioni 500, ushuru wa bidhaa sh trillioni 1.1, na kodi ya makampuni na personal taxes sh trillioni Kama 2.5.

Baada ya muungano, Kama una kumbuka, suala la kumi la muungano likawa:

1. Kodi ya Mapato - Watu na mashirika.
2.ushuru wa forodha.
3.ushuru wa bidhaa zinazozalishwa nchini.

Ukitazama activities zinazozalishwa kodi husika, ni Kama Zipo Tanganyika tu. Hapa Tanganyika ilaumiwe kwa lipi badala ya kupewa shukrani kwa kufanya yake ni ya wote huku ya znZ yakibakia kuwa ya znZ? Kumbuka, Structural weakness ya znZ ilikuwepo hata Kabla ya muungano, karafuu lilikuwa Ndio zao kuu Kama ilivyokuwa kwa Tanganyika na Mazao yake ya katani, pamba n.k.

Nikija kwenye hoja yako ya msingi sasa kuhusu akaunti ya pamoja - ni kweli Ipo kikatiba (ibara ya 133). Lakini Kama ulivyojadili, akaunti hii haipo. Lakini haujasema kitu kimoja - kwa kipindi chote ambacho hakuna akaunti ya pamoja kugharamia mambo ya muungano, mambo ya muungano yanagharamiwa na Mapato ya serikali ya jmt ambayo ndiyo Ile iliyoamua 1964 kutoa 75% ya Mapato yake kuendesha muungano kwa vile znZ haikuwa na uwezo wa kuchangia kwa usawa, kwahiyo kwa maana nyingine, anategharamia muungano, ni mtanganyika. Ndio maana nikakuiza, kwanini suala la uchangiaji ni kikwazo kwa JFC kuliko Mapato?

Suala lingine ambalo haulisemi Katika muktadha wa JFC ni Kwamba kwa miaka 50, bajeti ya muungano haitenganishi Vyanzo vya Mapato na matumizi kwa utaratibu wa mambo ya muungano na mambo ya Tanganyika. Mwisho wake ni Kwamba kila mwaka tunaposema ni bajeti ya muungano, maana yake ni bajeti ya serikali moja inayosimamia
mambo ya muungano na mambo ya Tanganyika. Bajeti ya aina hii inaathiri sana mipango, utekelezaji na vipaumbele vya Tanganyika, at the expense of treating wazanzibari Kama watanzania wenzetu. Lakini for some reasons, wazanzibari walio wengi hawauthamini utanzania kama wanavyouthamini uzanzibari.

Katika muktadha huu, hauoni Kwamba kikwazo cha JFC kinatokana zaidi na tatizo la uchangiaji wa znZ? Kwani znZ hawatumii muda wao zaidi kubuni vyanzo vyao vya ndani na kupigania reforms Za Mfumo wa kodi na badala yake wanapigania Haki ya kujipatia mikopo na misaada ya nje? Wakati Wengine barani afrika wanapigania kuondokana na fedha Za nje Katika bajeti, wao wanapiganiaa Haki za kukopa;

Kwa akili ya kawaida, znZ ilitakiwa ishukuru Kwamba imekwepa the aid curse, hiyo kaibeba mtanganyika kwa niaba yake.

Barubaru, lipi ni ukoloni zaidi kwa mzanzibari Kati ya foreign aid iliyojaa imperialistic elements na suala la mtanganyika Kudhamini 88% ya mikopo ya znZ - mikopo ya nje? 88% ya mikopo inadhaminiwa na mtanganyika, over 75% za kodi ya mtanganyika zinahudumia utanzania, utaifa ambao mzanzibari hauthamini, hauoni tatizo hapo?

hauoni kikwazo kikubwa kwa JFC kutekeleza kazi zake chanzo ni znZ?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi;9792499]Muungano ulipokuja, kwa vile znZ haikuwa na Mapato ya kuweza changia Sawa kutokana na udogo wake, zile kodi hapo juu yani 75% ya Mapato ya Tanganyika yakageuzwa kuwa Ndio Mapato ya muungano kuhudumia masuala 11 ya muungano. Leo hii, Mapato haya yanaitwa Mapato ya serikali ya muungano Wakati kimsingi ni Mapato ya Tanganyika. Leo, forodha inaingiza sh bilioni 500, ushuru wa bidhaa sh trillioni 1.1, na kodi ya makampuni na personal taxes sh trillioni Kama 2.5.
Mchambuzi, naona ume mu address Barubaru, nadhani ujumbe huu ni muhimu sana kwa Mkandara.
Mkandara anasema tuna muungano na kinachotakiwa ni kugawana mapato.
Kwa maneno mengine tugawane vya Tanganyika kwa vile kuna pande mbili, ZNZ na ya pili ni JMT.

Upande wa JMT ndio Tanganyika, kwavile anataka znz inufaike anauita Tanganyika.
Wakati wa kugawana anasema ni mali za Tanzania, znz ni mshiriki. Umeona eh!
Ukitazama activities zinazozalishwa kodi husika, ni Kama Zipo Tanganyika tu. Hapa Tanganyika ilaumiwe kwa lipi badala ya kupewa shukrani kwa kufanya yake ni ya wote huku ya znZ yakibakia kuwa ya znZ? Kumbuka, Structural weakness ya znZ ilikuwepo hata Kabla ya muungano, karafuu lilikuwa Ndio zao kuu Kama ilivyokuwa kwa Tanganyika na Mazao yake ya katani, pamba n.k.
Barubaru na Mkandara(yupo katika rekodi) wanasema muungano ndio umeua znz kiuchumi, wakikufumbia macho suala la karafuu.

Hawakubali ukweli kuwa kifo cha karafuu iliporomosha uchumi wa znz.
Ndivyo ilivyokuwa kwa katani, Pamba na Korosho kwa upande wa Tanganyika.

Tanganyika pamoja na kubeba muungano kama ulivyoeleza hawajalalamika kuhusu uchumi wao kuharibiwa na zigo la znz , wanalaumiwa kubeba mzigo
Nikija kwenye hoja yako ya msingi sasa kuhusu akaunti ya pamoja - ni kweli Ipo kikatiba (ibara ya 133)Lakini Kama ulivyojadili, akaunti hii haipo. Lakini haujasema kitu kimoja - kwa kipindi chote ambacho hakuna akaunti ya pamoja kugharamia mambo ya muungano, mambo ya muungano yanagharamiwa na Mapato ya serikali ya jmt ambayo ndiyo Ile iliyoamua 1964 kutoa 75% ya Mapato yake kuendesha muungano kwa vile znZ haikuwa na uwezo wa kuchangia kwa usawa, kwahiyo kwa maana nyingine, anategharamia muungano, ni mtanganyika. Ndio maana nikakuiza, kwanini suala la uchangiaji ni kikwazo kwa JFC kuliko Mapato?
Hakuna mznz mwenye akili timamu anayejua suala la kuchangia.Kilichopo mbele ni nataka,nipe, namimi.

Ndio utamaduni na barubaru yupo within the cultural parameters, hatuwezi kumlaumu.
Mkandara anashangaza maana hayupo katika 'parameters'
Suala lingine ambalo haulisemi Katika muktadha wa JFC ni Kwamba kwa miaka 50, bajeti ya muungano haitenganishi Vyanzo vya Mapato na matumizi kwa utaratibu wa mambo ya muungano na mambo ya Tanganyika. Mwisho wake ni Kwamba kila mwaka tunaposema ni bajeti ya muungano, maana yake ni bajeti ya serikali moja inayosimamia
mambo ya muungano na mambo ya Tanganyika. Bajeti ya aina hii inaathiri sana mipango, utekelezaji na vipaumbele vya Tanganyika, at the expense of treating wazanzibari Kama watanzania wenzetu. Lakini for some reasons, wazanzibari walio wengi hawauthamini utanzania kama wanavyouthamini uzanzibari
Mkandara anasema zitengwe shughuli za muungano, Tanganyika na znz.
Halafu anasema mambo yote yawe ya muungano. Anarudi na kusema tugawane mapato, sijui mambo yote ya muungano ni yapi?

Haangalii ukweli kuwa Tanganyika ndiyo inayobeba muungano na kwamba huwezi kuwa na JMT na ZNZ ukafanya shughuli bila matatizo.

Mkuu Mkandara anasema yapo mafanikio sana kwa miaka 50! real! serious!
Unaweza kuwa na mgonjwa mahututi ICU ukasema hali ya familia ni nzuri sana.!
Katika muktadha huu, hauoni Kwamba kikwazo cha JFC kinatokana zaidi na tatizo la uchangiaji wa znZ? Kwani znZ hawatumii muda wao zaidi kubuni vyanzo vyao vya ndani na kupigania reforms Za Mfumo wa kodi na badala yake wanapigania Haki ya kujipatia mikopo na misaada ya nje? Wakati Wengine barani afrika wanapigania kuondokana na fedha za nje Katika bajeti, wao wanapiganiaa Haki za kukopa;
Hii akili mbovu sana na inapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote.

Nilidhani nchi zinapaswa kujitegemea kwanza. Hoja kubwa sana ya Mkandara ni kuwa misaada na mikopo ni sehemu ya bajeti yetu. Ndiyo, hata Tanganyika tunalaani kuishi kwa misaada na mikopo.

Lakini basi mikopo ikiwa 40% na mapato mengine ya ndani ni 60% ukiuliza katika 60% znz inachangia nini, hakuna mwenye jibu.
Kwa akili ya kawaida, znZ ilitakiwa ishukuru Kwamba imekwepa the aid curse, hiyo kaibeba mtanganyika kwa niaba yake.
Na Mkandara pia alitakiwa awasaidie kuelewa hili.
Barubaru, lipi ni ukoloni zaidi kwa mzanzibari Kati ya foreign aid iliyojaa imperialistic elements na suala la mtanganyika Kudhamini 88% ya mikopo ya znZ - mikopo ya nje? 88% ya mikopo inadhaminiwa na mtanganyika, over 75% za kodi ya mtanganyika zinahudumia utanzania, utaifa ambao mzanzibari hauthamini, hauoni tatizo hapo?hauoni kikwazo kikubwa kwa JFC kutekeleza kazi zake chanzo ni znZ?
WZN wanaamini ila mikopo na misaada hakuna muungano, hawana cha kuchangia.

Akili ya misaada na mikopo ni ya ajabu na inatia kinyaa. Hivi kweli muungano wetu umejengwa katika misingi ya misaada na mikopo na kwamba nje ya hapo hakuna muungano. Kwamba wafadhili wakikataa kama walivyokataa mwaka huu basi hakuna muungano.

Hivi kuna ukoloni uliozidi huu ujinga wa kudai misaada na mikopo badala ya kujiendeleza.
Hiyo znz nje ya Tanganyika inayochukua 88% dhamana haiwezi kukopesheka.

Haina assets za kukopesheka, itaishia kupewa karanga na biscuit.
Kukopesheka kwa znz ni kutokana na dhamana ya Tanganyika.

Ndio maana Tanesco wanakopesha umeme wakijua znz ikikataa kama wanavyokataa,JMT , atalipa.
Ukiuliza JMT ni nani unaambiwa na znz imo.

Ukiuliza inachangia nini unapewa jibu la misaada na mikopo.
Ukiuliza kile kisicho misaada inachangia nini unaambiwa si mambo ya muungano.

Ukiuliza ya muungano ni yapi unaambiwa ni 11. Ukiuliza kwanini znz inayapunguza unaambiwa ni mamlaka kamili. Ili mradi tu kuchanganya Watanganyika, waendelee kubeba zigo

Huko Paris na Washngton nao wanaelewa hivyo, bila asset za Tanganyika,kumkopesha mznz ni risk

Mkuu Barubaru:

Huwa tunasahau kutazama Hali ilivyokuwa Kabla ya muungano. Katika kipindi cha 1961-1964, Tanganyika ilikuwa na Mapato yake, na vile vile znZ. Kwa upande wa Tanganyika, vyanzo Vikuu (75%) villi kuwa ni Kama ifuatavyo:

1. Kodi ya makampuni na Watu binafsi (corporate and personal income taxes).
2. Ushuru wa forodha.
3. Ushuru wa bidhaa zilizouzwa nje (katani, kahawa, pamba, chai n.k).

Property tax na other sources zikabeba the remaining 25%.

Upande wa znZ, revenues zilitegemea zaidi ushuru wa bidhaa zilizouzwa nje, hasa karafuu.

Muungano ulipokuja, kwa vile znZ haikuwa na Mapato ya kuweza changia Sawa kutokana na udogo wake, zile kodi hapo juu yani 75% ya Mapato ya Tanganyika yakageuzwa kuwa Ndio Mapato ya muungano kuhudumia masuala 11 ya muungano. Leo hii, Mapato haya yanaitwa Mapato ya serikali ya muungano Wakati kimsingi ni Mapato ya Tanganyika. Leo, forodha inaingiza sh bilioni 500, ushuru wa bidhaa sh trillioni 1.1, na kodi ya makampuni na personal taxes sh trillioni Kama 2.5.

Baada ya muungano, Kama una kumbuka, suala la kumi la muungano likawa:

1. Kodi ya Mapato - Watu na mashirika.
2.ushuru wa forodha.
3.ushuru wa bidhaa zinazozalishwa nchini.

Ukitazama activities zinazozalishwa kodi husika, ni Kama Zipo Tanganyika tu. Hapa Tanganyika ilaumiwe kwa lipi badala ya kupewa shukrani kwa kufanya yake ni ya wote huku ya znZ yakibakia kuwa ya znZ? Kumbuka, Structural weakness ya znZ ilikuwepo hata Kabla ya muungano, karafuu lilikuwa Ndio zao kuu Kama ilivyokuwa kwa Tanganyika na Mazao yake ya katani, pamba n.k.

Nikija kwenye hoja yako ya msingi sasa kuhusu akaunti ya pamoja - ni kweli Ipo kikatiba (ibara ya 133). Lakini Kama ulivyojadili, akaunti hii haipo. Lakini haujasema kitu kimoja - kwa kipindi chote ambacho hakuna akaunti ya pamoja kugharamia mambo ya muungano, mambo ya muungano yanagharamiwa na Mapato ya serikali ya jmt ambayo ndiyo Ile iliyoamua 1964 kutoa 75% ya Mapato yake kuendesha muungano kwa vile znZ haikuwa na uwezo wa kuchangia kwa usawa, kwahiyo kwa maana nyingine, anategharamia muungano, ni mtanganyika. Ndio maana nikakuiza, kwanini suala la uchangiaji ni kikwazo kwa JFC kuliko Mapato?

Suala lingine ambalo haulisemi Katika muktadha wa JFC ni Kwamba kwa miaka 50, bajeti ya muungano haitenganishi Vyanzo vya Mapato na matumizi kwa utaratibu wa mambo ya muungano na mambo ya Tanganyika. Mwisho wake ni Kwamba kila mwaka tunaposema ni bajeti ya muungano, maana yake ni bajeti ya serikali moja inayosimamia
mambo ya muungano na mambo ya Tanganyika. Bajeti ya aina hii inaathiri sana mipango, utekelezaji na vipaumbele vya Tanganyika, at the expense of treating wazanzibari Kama watanzania wenzetu. Lakini for some reasons, wazanzibari walio wengi hawauthamini utanzania kama wanavyouthamini uzanzibari.

Katika muktadha huu, hauoni Kwamba kikwazo cha JFC kinatokana zaidi na tatizo la uchangiaji wa znZ? Kwani znZ hawatumii muda wao zaidi kubuni vyanzo vyao vya ndani na kupigania reforms Za Mfumo wa kodi na badala yake wanapigania Haki ya kujipatia mikopo na misaada ya nje? Wakati Wengine barani afrika wanapigania kuondokana na fedha Za nje Katika bajeti, wao wanapiganiaa Haki za kukopa;

Kwa akili ya kawaida, znZ ilitakiwa ishukuru Kwamba imekwepa the aid curse, hiyo kaibeba mtanganyika kwa niaba yake.

Barubaru, lipi ni ukoloni zaidi kwa mzanzibari Kati ya foreign aid iliyojaa imperialistic elements na suala la mtanganyika Kudhamini 88% ya mikopo ya znZ - mikopo ya nje? 88% ya mikopo inadhaminiwa na mtanganyika, over 75% za kodi ya mtanganyika zinahudumia utanzania, utaifa ambao mzanzibari hauthamini, hauoni tatizo hapo?

hauoni kikwazo kikubwa kwa JFC kutekeleza kazi zake chanzo ni znZ?

Sent from my iPhone using JamiiForums

Mchambuzi,

Awali ya yote tuliza munkar na jazba katika kutaka kujua mambo lakin pia ni vizuri unisome kwa uzuri sana utaelewa kile nilichobainisha kuhusu NINI NIA YA KUANZISHWA KWA AKAUNTI ya Pamoja ya uchumi na fedhwa. Nilibainisha kuwa hivi
Sasa Serikali ya Mkapa mwaka 1996 iliunda tume hii kwa ajili ya kuondosha manunguniko hayo na kama ingefanya kazi zake kama ilivyokusudiwa na Bunge kwa kuundwa kutekeleza majukumu yake ya kutunza akaunti ya muungano kwa matumizi ya taasisi za muungano na wizara za muungano kwa mujibu wa Katiba yya JMtz basi haya malalamiko ya nguruvi3 yote angebaki kuwa ni historia,

Tunaposema kutunza akaunt ina maana kuangalia na kuratibu kile kinachoingia katika mfuko huo na vile vile kuratibu kile kinachotoka katika mfuko huo na kuhakikisha kinatumika na taasisi za muungano tu na si vinginevyo,,

Sasa ahali yangu Mchambuzi tuache kutabiri jambo bila kulifanya Kinachotakiwa ni kuanza kazi kwa Akaunti ya pamoja chini ya JFC na kupitia ripoti zake za mwaka kuonyesha ni nchi gani haijachangia na kwa kiasi gani kuliko kuweka tuhuma bila kuwa na data sahihi lakin pia kuondosha malalamiko kuwa nchi moja inafuja pesa za muungano ikiwemo mikopo na misaada lakin zogo la deni linadondokea kwa wote.

lakin pia mimi nimefanyakazi wizara ya fedhwa muungano hizo Takwimu za TGK kuisaidia gharama kama nilivyo BOLD umezitoa wapi. Kwani kwa kifupi hakuna takwimu zozote sahihi zinazoweza kuthibitisha hayo na kama utapitia bajeti za miaka yote kuanzia 1970 mpaka ya 2014/15 ambazo mimi nazifahamu unaona wazi bajeti ya Muungano kwa makusanyo yenu yanakuwa hayazidi 50% ya matumizi yenu na hivyo kwa more than 40% ya bajeti kutegemea wahisani..

Mchambuzi unatakiwa ujue uchumi ni taaluma. sasa labda nikupa mfano mdogo tu. Chukulia mfano mdogo tu wa Jeshi la Polisi ambalo ni taasisi ya muungano. Ukitazama kimataifa kwa nchi maskini polisi mmoja anatakiwa kulinda watu 300. Sasa chukulia Znz kuna watu wasiozidi 1.5 milioni na Tanganyika wana watu zaidi ya 45 milioni.. utaona wazi TGK watahitaji polisi zaidi ya 150000 na Znz watahitaji polisi wasiozidi 5000. Tujaalie matumizi kwa kila polisi ukijumlisha na mishahara na stahili nyingi na vitendea kazi kwa kila polisi labda tuseme ni 1 milion kwa mwaka. Je hapa inawezekana Znz kulipa sawa na TGK?.

Nilichotaka kukusaidia hapo Mchambuzi ni kuwa kulipia muungano ni laazima wataalamu wa uchumi wakae na kuweka formula ili kila mtu ajue analipia kiasi gani bila kudhulumiana. NA NDIPO HAPO IKAUNDWA TUME HII YA JFC KUWEKA SAWA HISABU HIZO.

Sasa siku zote mkanganyiko mkubwa unatokea pale ambapo TGK inakataa kutenganisha fedhwa za mambo ya muungano na fedhwa za mambo yasiyo ya muungano na hivyo wanapokopa hata kwa mambo yasiyo ya muungano pasa hizo zinaingia katika deni la muungano ambapo Znz ni mdau mkubwa.

Tukumbuke kuwa Akaunti maalum ya fedhwa za mambo ya muungano itakayosimamiwa na JFC itaondoa kero hii na kuonyesha wazi stahili za kila mtu. Na kuhusu huo uchangiaji so long as pesa zote za mikopo na misaada zitapitia katika akaunti hiyo basi JFC itakata pesa hizo kulipia gharama za nchi husika katika kuchangia muungano. Kumbuka kuwa zaidi ya 42% a bajeti zenu zote zinategemea mikopo na misaada kutoka kwa wahisani na taasisi za kimataifa...

Sasa nitakushangaa sana unaposema uchangiaji wa muungano wakti hata bajeti yenyewe ya JMTz inategemea kuchangiwa kwa zaidi ya 43% na wahisani kwa njia ya mikopo na misaada..
Kumbuka kuwa kufanyakazi kwa akaunti ya pamoja ya fedhwa chini ya JFC kungepunguza kazi kwa Single Tressure Account (STA) ambayo ni akaunti kuu ya Serikali ndani ya BOT.. kwani hii Account angejikita kwa masuala yasiyo ya muungano na yale ya muungano yangeratibiwa na JFC

Sasa sijui wasi wasi wako au uwoga wako upo wapi katika kuunda hii akaunti ya pamoja ya mambo ya muungano chini ya JFC kama ilivyoelekezwa na sharia za JMTz ibara ya 133?

Kuhoji kwa hoja imekuwa ni jazba, munkari, woga na wasiwasi tangia lini? Takwimu za Tanganyika Kudhamini 88pct ya deni la nje la znZ Zipo kwenye hotuba ya bajeti ya waziri wa fedha wa znZ bwana mzee, na takwimu za 75%ya kodi za Tanganyika kufanywa kuwa ni Mapato ya muungano 1964 na kuendelea ni study moja ya Lipumba.

Umejitahidi kujadili changamoto za JFC lakini bado unakwepa Ukweli juu ya mchango wa znZ Katika changamoto husika. Fanya utafiti utaona jinsi gani SMZ inachangia Katika Hilo.

Study hiyo unasema pia znZ ilikuwa inachangia moja kwa moja kwa wastani wa sh milioni 12 kwa mwaka kwa kipindi cha 1964-1977, Kabla ya mabadiliko yaliyofuata ambapo muungano sasa ukaanza kugharamiwa na Mapato ya serikali ya muungano, ambayo nimeyaelezea Katika Ile 75% kuhudumia mambo 11. Je kwa mambo 22 na ushee Leo kodi za Tanganyika zinazohudumia muungano zitakuwa ni kiasi gani?

Ningependa pia kusikia maoni yako juu ya hoja yangu ya misaada na mikopo ambayo Nguruvi3 pia kaijadili hapo juu. Pia hoja ya utaifa wa Zanzibar na utanzania.

Lengo Hapa ni kuelimishana, sio kurushiana lawama. Jaribu kuitazama JFC with a bird's view, not a fish view.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Barubaru;9795909]Mchambuzi,Mchambuzi unatakiwa ujue uchumi ni taaluma. sasa labda nikupa mfano mdogo tu. Chukulia mfano mdogo tu wa Jeshi la Polisi ambalo ni taasisi ya muungano. Ukitazama kimataifa kwa nchi maskini polisi mmoja anatakiwa kulinda watu 300. Sasa chukulia Znz kuna watu wasiozidi 1.5 milioni na Tanganyika wana watu zaidi ya 45 milioni.. utaona wazi TGK watahitaji polisi zaidi ya 150000 na Znz watahitaji polisi wasiozidi 5000. Tujaalie matumizi kwa kila polisi ukijumlisha na mishahara na stahili nyingi na vitendea kazi kwa kila polisi labda tuseme ni 1 milion kwa mwaka. Je hapa inawezekana Znz kulipa sawa na TGK?.
Ohh la la la, OK. Umekimbia hoja za mchambuzi za awali. Hata hivyo tutakueleza kutokana na mifano yako.

Kwa mfano huo wa Polisi, hujaeleza hao askari 5000 wa znz wanalipwa kwa utaratibu gani ikiwa SMZ haichangii muungano kwa data za Malyamokono na wachumi wengine ambazo hazipingwa na msomi mwingine.
Pili, katika askari 150,000 hujaeleza wznz wangapi wameajiriwa. Najua huwezi kufahamu kuwa employment ni sehemu ya uchumi. Jeshi la 150,000 ni fursa ya wznz kuajiriwa ambao otherwise wangekuwa unemployed. Mchumi hili hulioni kweli.

Tatu, kwa minajili ya mjadala huu, tu assume kuwa misaada ni 60% ya bajeti.
Swali usliojibu na ambalo hutajibu ni hili. Katika 40% iliyobaki znz inachangia nini.

Nne, tu assume kuwa wafadhili wamegoma kutoa pesa kama walivyowahi kufanya kwa Mwinyi huko nyuma na mwaka huu wa fedha.
Je, JFC itaendelea kuwepo au ndio itakuwa umefikia ukomo, tukizingatia kuwa chanzo chake ni mapato ni misaada.
Je, muungano nao utakuwa umefikia mwisho kwasababu znz haitaweza kuchangia chochote kwa kukosa misaada?

Kuhoji kwa hoja imekuwa ni jazba, munkari, woga na wasiwasi tangia lini? Takwimu za Tanganyika Kudhamini 88pct ya deni la nje la znZ Zipo kwenye hotuba ya bajeti ya waziri wa fedha wa znZ bwana mzee, na takwimu za 75%ya kodi za Tanganyika kufanywa kuwa ni Mapato ya muungano 1964 na kuendelea ni study moja ya Lipumba.

Umejitahidi kujadili changamoto za JFC lakini bado unakwepa Ukweli juu ya mchango wa znZ Katika changamoto husika. Fanya utafiti utaona jinsi gani SMZ inachangia Katika Hilo.

Study hiyo unasema pia znZ ilikuwa inachangia moja kwa moja kwa wastani wa sh milioni 12 kwa mwaka kwa kipindi cha 1964-1977, Kabla ya mabadiliko yaliyofuata ambapo muungano sasa ukaanza kugharamiwa na Mapato ya serikali ya muungano, ambayo nimeyaelezea Katika Ile 75% kuhudumia mambo 11. Je kwa mambo 22 na ushee Leo kodi za Tanganyika zinazohudumia muungano zitakuwa ni kiasi gani?

Ningependa pia kusikia maoni yako juu ya hoja yangu ya misaada na mikopo ambayo Nguruvi3 pia kaijadili hapo juu. Pia hoja ya utaifa wa Zanzibar na utanzania.

Lengo Hapa ni kuelimishana, sio kurushiana lawama. Jaribu kuitazama JFC with a bird's view, not a fish view.

Sent from my iPhone using JamiiForums

Mchambuzi,

Kwanza kabisa naomba uniambie ni study gani hiyo iliyosema Znz ilikuwa inachangia 12 Milioni katika muungano bila kutaje TGK inachangia kiasi gani na vile vile Ni kiasi gani kilichokuw kinahitajika? Naomba nieleze nitafatilia kwani uchumi ni kazi zangu na kwa bahti kubwa nilikuwa Wizara ya Fedhwa Muungano kitengo cha bajeti kwa miaka 6.nitaomba unibainishie study hiyo ilifanywa na nani ili niweze itafuta.

Kuhusu alilosema Nguruvi3 la mikopo na misaada. Mimi naomba nikupe kitu live kutoka katika bajeti yenu ya Muungano ya 2014/2015. kama Ulimsikiliza na kuipitia vizuri bajeti yenu iliyosomwa jana na Bi Saada bint Salum ameweka wazi kuwa bajeti yenu ni zaidi ya 19 Trilion na makusanyo yenu yote pamoja na maduhuli yanakadiriwa kufikia chini ya 11 Trillion. Sasa hapo utaona kuna upungufu wa zaidi ya 8 Trikllion.

Na kama utazidi kuichambua zaidi utaona pasa zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ni chini ya 17% , hivyo mnategemea MIKOPO PAMOJA NA MISAADA KWA AJILI YA FEDHWA ZA MAENDELEO KWA ZAIDI YA 80%. au ujaliona hilo?

Sasa kama unajitambua au ukiwa na ilmu kidogo ya uchumi TUNASEMA BAJETI YENU NI TEGEMEZI KWA TAKRIBAN NUSU YA BAJETI MNATEGEMEA IHSAN ZA WAHISANI KWA KUWAPA MISAADA NA MIKOPO NAFUU. Sasa sijui unalielezaje hilo.

Nikirudi kwenye mada napenda nikuulize kama umepitia bajeti ya wizara ya miundombinu ya Mh Magufuri ya 2014/2015 umeona kuwa wamekopa pasa kutoka nje kwa ajili ya barabara ya Tunduru - namtumbo na nyingine kutoka Tunduru kwenda mangaka. lakin vile wanatafuta fedhwa za kukopa kukamilisha barabara ya Mbezi kupitia maramba mawili mpaka kinyerezi. sasa jiulize je barabara hizi zinahusu nini na Znz? kwanini wasikope kwa jina la TGK ili wadaiwe TGK bali wanakimbilia kukopa kwa jina la Tanzania ili Znz nao wahusike na huo mkopo? Je hii uoni kuwa ni dhulma kwa Znz?

Na uoni kuwa ujanja huu ndio unaosababisha JMTz kupata kigugumizi kutekeleza sharia zake ikiwemo hii ya Akaunti ya pamoja chini ya JFC ambayo itahusika tu na mambo ya muungano kama mambo ya ndani, Ulinzi, mambo ya nje na taasisi zake?

Kubwa la mwisho nilitaka nikupe taarifa kuwa Wizara ya fedhwa Si katika wizara za Muungano lakin ndani yake kuna BOT na TRA ambayo ni mambo ya muungano? Je uoni kuwa kuna ukakasi hapo?Lakin hata wizara ya Mao ya ndani ambayo ni ya muungano lakin ndani yake kuna magereza ambacho si kitu cha muungano? Je ukakasi huu mpaka lini?

Kuhusu hii la Utaifa nafikiri hili lipo wazi kabisa kuwa Znz ni nchi na limewekwa kabisa kisharia katika katiba ya Znz.

Nafikiri nimekukidhi kwa majibu yangu lakin kama una zaidi Bismillah

Ohh la la la, OK. Umekimbia hoja za mchambuzi za awali. Hata hivyo tutakueleza kutokana na mifano yako.

Kwa mfano huo wa Polisi, hujaeleza hao askari 5000 wa znz wanalipwa kwa utaratibu gani ikiwa SMZ haichangii muungano kwa data za Malyamokono na wachumi wengine ambazo hazipingwa na msomi mwingine.
Pili, katika askari 150,000 hujaeleza wznz wangapi wameajiriwa. Najua huwezi kufahamu kuwa employment ni sehemu ya uchumi. Jeshi la 150,000 ni fursa ya wznz kuajiriwa ambao otherwise wangekuwa unemployed. Mchumi hili hulioni kweli.

Tatu, kwa minajili ya mjadala huu, tu assume kuwa misaada ni 60% ya bajeti.
Swali usliojibu na ambalo hutajibu ni hili. Katika 40% iliyobaki znz inachangia nini.

Nne, tu assume kuwa wafadhili wamegoma kutoa pesa kama walivyowahi kufanya kwa Mwinyi huko nyuma na mwaka huu wa fedha.
Je, JFC itaendelea kuwepo au ndio itakuwa umefikia ukomo, tukizingatia kuwa chanzo chake ni mapato ni misaada.
Je, muungano nao utakuwa umefikia mwisho kwasababu znz haitaweza kuchangia chochote kwa kukosa misaada?

Nguruvi3,

Ahali yangu naona tunarudi kule kule nilikokubainishia toka awali.

Huo mfano nilikuwekea ujue kuwa hata siku moja hamuwezi kuchangia 50/50 % kwenye muungano wenu kwa kila nchi kwani huo ndio uhalisia kutokana na eneo la nchi na idadi ya watu. Ndio maana wachumi wa nchi hizo wakaja na mapendekezo hayo.

Kumbuka kuwa JFC wamechambua kwa kina na kuja formula mbayo ndio hiyo ikiwemo 21% ya ajira katika vyombo vya muungano laazima wapewe wa Znz lakin TUNALOJADILI HAPA NI KUWEPO NA AKAUNTI YA PAMOJA YA FEDHWA ZA MUUNGANO AMBAZO ZITARATIBIWA NA KUSIMAMIWA NA JFC. Hii account itaondoa hayo malalamiko na manung'uniko yako. Kwani kwa sasa kutokana na TGK kujivika Joho la Tanzania wanawadhulumu sana wa Znz.
Mfano tunaposema mambo ya Ulinzi ni ya Muungano, ni vipi katika wizara hiyyo IWEMO JKT ambacho si chombo cha muungano. Kumbuka Znz kuna JKU. Au wizara mambo ya ndani ambacho ni chombo cha Mungano iweje kuwe na Magareza au Zimamoto ambavyo si vyombo vya muungano?. Kumbuka Znz kuna Chuo cha mafunzo na jeshi la Zimamoto.

Sasa unapopitisha Bajeti hii na kuita ya muungano huoni kuwa ukakasi umezidi hapo. Kwanini vyombo hivi vya Muungano na taasisi zake wasifate mgawo wao wa bajeti zao kupitia JFC na kutoka fedhwa zao katika Akaunti maalum ya pamoja na kuwaacha Pesa za mambo yasiyo ya muungano ziendelee kupitia katika Single Tressure Account iliyopo BOT?

sasa wasi wasi wenu ni nini?

Kumbuka mzowea vya kunyonga ...

Hakuna marefu yasiyo na ncha. Znz huru ileeeeeeeeeeeeeeeeeee

waachwe Znz wapumue

Mchambuzi, naona ume mu address Barubaru, nadhani ujumbe huu ni muhimu sana kwa Mkandara.
Mkandara anasema tuna muungano na kinachotakiwa ni kugawana mapato.
Kwa maneno mengine tugawane vya Tanganyika kwa vile kuna pande mbili, ZNZ na ya pili ni JMT.

Upande wa JMT ndio Tanganyika, kwavile anataka znz inufaike anauita Tanganyika.
Wakati wa kugawana anasema ni mali za Tanzania, znz ni mshiriki. Umeona eh! Barubaru na Mkandara(yupo katika rekodi) wanasema muungano ndio umeua znz kiuchumi, wakikufumbia macho suala la karafuu.

Hawakubali ukweli kuwa kifo cha karafuu iliporomosha uchumi wa znz.
Ndivyo ilivyokuwa kwa katani, Pamba na Korosho kwa upande wa Tanganyika.

Tanganyika pamoja na kubeba muungano kama ulivyoeleza hawajalalamika kuhusu uchumi wao kuharibiwa na zigo la znz , wanalaumiwa kubeba mzigo Hakuna mznz mwenye akili timamu anayejua suala la kuchangia.Kilichopo mbele ni nataka,nipe, namimi.

Ndio utamaduni na barubaru yupo within the cultural parameters, hatuwezi kumlaumu.
Mkandara anashangaza maana hayupo katika 'parameters' Mkandara anasema zitengwe shughuli za muungano, Tanganyika na znz.
Halafu anasema mambo yote yawe ya muungano. Anarudi na kusema tugawane mapato, sijui mambo yote ya muungano ni yapi?

Haangalii ukweli kuwa Tanganyika ndiyo inayobeba muungano na kwamba huwezi kuwa na JMT na ZNZ ukafanya shughuli bila matatizo.

Mkuu Mkandara anasema yapo mafanikio sana kwa miaka 50! real! serious!
Unaweza kuwa na mgonjwa mahututi ICU ukasema hali ya familia ni nzuri sana.! Hii akili mbovu sana na inapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote.

Nilidhani nchi zinapaswa kujitegemea kwanza. Hoja kubwa sana ya Mkandara ni kuwa misaada na mikopo ni sehemu ya bajeti yetu. Ndiyo, hata Tanganyika tunalaani kuishi kwa misaada na mikopo.

Lakini basi mikopo ikiwa 40% na mapato mengine ya ndani ni 60% ukiuliza katika 60% znz inachangia nini, hakuna mwenye jibu. Na Mkandara pia alitakiwa awasaidie kuelewa hili.WZN wanaamini ila mikopo na misaada hakuna muungano, hawana cha kuchangia.

Akili ya misaada na mikopo ni ya ajabu na inatia kinyaa. Hivi kweli muungano wetu umejengwa katika misingi ya misaada na mikopo na kwamba nje ya hapo hakuna muungano. Kwamba wafadhili wakikataa kama walivyokataa mwaka huu basi hakuna muungano.

Hivi kuna ukoloni uliozidi huu ujinga wa kudai misaada na mikopo badala ya kujiendeleza.
Hiyo znz nje ya Tanganyika inayochukua 88% dhamana haiwezi kukopesheka.

Haina assets za kukopesheka, itaishia kupewa karanga na biscuit.
Kukopesheka kwa znz ni kutokana na dhamana ya Tanganyika.

Ndio maana Tanesco wanakopesha umeme wakijua znz ikikataa kama wanavyokataa,JMT , atalipa.
Ukiuliza JMT ni nani unaambiwa na znz imo.

Ukiuliza inachangia nini unapewa jibu la misaada na mikopo.
Ukiuliza kile kisicho misaada inachangia nini unaambiwa si mambo ya muungano.

Ukiuliza ya muungano ni yapi unaambiwa ni 11. Ukiuliza kwanini znz inayapunguza unaambiwa ni mamlaka kamili. Ili mradi tu kuchanganya Watanganyika, waendelee kubeba zigo

Huko Paris na Washngton nao wanaelewa hivyo, bila asset za Tanganyika,kumkopesha mznz ni risk

Nguruvi3,

Naona unajiviringisha bila kujua mwelekeo wako.

Ngoja nikurudisha katika uhalisia KWANI MARA ZOTE NAKWAMBIA UCHUMI NI TAALUMA NA WALA SIO BLA BLA. Rejea katika Bajeti ya JMTz ya mwaka huu 2014/2015. jaribu kuangalia taratibu uone ni kiasi gani Bajeti hiyo inategemea ihsan za misaada kutoka kwa wahisani na wafadhwili lakin pia Mikopo kutoka taasisi za kimataifa na mabenk na nchi wahisani?

Je nikikwambia kuwa Bajeti yenu haiwezi kutekelezeka kabisa bila wahisani kutoa misaada na kuwapa mikopo?je utabisha hata hilo. ichambue kwa kina bajeti yenu utaona hayo na kuweka majibu yako hapa.

Je unajuwa Deni lenu la Taifa mpaka kufikia April 2014?

Pole sana.

Back
Top Bottom