Nguruvi3
Labda nikukumbushe tu ya kwamba hata huku Majuu wapo watu wanajitambulisha kwa nchi zao.
Mquebec hajiiti Mcanada na hata Mscotish hajiiti Muingereza wala British, haya ni maswala ya kawaida kabisa ktk miungano ya nchi kuunda Taifa kwa sababu mara nyingi maamuzi ya kuungana nchi hufanywa na watawala kutokana na historia ya nchi hizo. Sisi tulozaliwa baada ya muunganmo ndio tunaokuja na hoja nzito dhidi ya Muungano bila kufahamu ya kwamba historia ndio ilowalazimu wao kuungana kutokana na WATU, ARDHI na USALAMA wa nchi hizo.
Factors hizi haziondoki kirahisi kama jinsi watu wengi wanavyofikiria.
Unaposema tuwe na mambo 7 tu huu ni muungano wa aina gani?
Je, Unawezaje kuwa na serikali ya Tanganyika pasipo kuwa na nchi yake na kama itakuwepo hii tanganyika itakuwa na mihimili mingapi na itachukua muda gani kuiandaa.
Je hiyo Tanganyika itakuwa na bunge lake? halafu ndio tuwe na bunge la Muungano ambalo Wazanzibar pia hawalitaki isipokuwa kujiunga na bunge la EAC walitakalo!.
Je, Unapokubali mambo 7 ya muungano haitakuwa muunganosawa na huo wa jumuiya ya EAC, hivyo unahitaji nini kuwa na mkataba mpya na Zanzibar wakati tunaweza tu kuvunja huu uliopo na tukakutana huko Arusha sijui Nairobi kisha tuanze ya Kagame vs JK!
Pili, Uksha unda serikali ya Tanganyika utahitaji kuwa na bunge la Tanganyika hivyo utaanzisha uchaguzi mpya wa wabunge utakao chukua miezi na kisha utunzi wa katiba ya tanganyika ambayo itapitia changamoto kama hizi tena. YYaani ni mlolongo wa maswali wa mambo ambayo yanaiweka katiba mpya tuitakayo kapuni.
haya nipe majibu ya haraka kuhusu haya:-
1.Bunge la Tanganyika litawakilishwa na vyama gani? maana CUF ni chama cha visiwani na Chadema chama cha bara kama wasemavyo wanasiasa, Je ni sheria ipi itakayo wazuia CUF na vyama vya visiwani kugombea bara au Chadema na vyama vya bara kugombea Visiwani?
2. Hiyo CCM itaruhusiwa kugombea upande gani Zanzibar au bara wakati kina wanachama kila upande au nacho ni chama cha bara? na kama hakitaruhusiwa kugombea Zanzibar, mgombea wa chama hicho atakuwa na mahusiano gani na CCM ya bara? au vitaanzishwa vyama vipya pande zote? nini mipaka ya vyama vilivyopo upande wa pili (ili Znz) wasione wanaingiliwa ktk mambo yao.
Wakuu zangu, hivi kweli haya yote mmeyafikiria au mnasema tu ili mradi mnaitaka Tanganyika! na mkisha ipata Tanganyika kweli bado mtakubali kuwa na hayo mambo 7? au nilichosema mimi ndio rahisi kabisa. Kumbuka tu ya kwamba Mambo yote yakiwa ya Muungano, tunawalazimisha kina Jussa kuufyata. hakuna swala la Uzanzibar wala Utanganyika ila Utanzania hata kama watajiita Wazanzibar nawe unaweza kujiita Mtanganyika na ukaipeperusha bebdera ya tanganyika juu ya paa la nyumba yako.
Hii ni Identity tu ktk mfumo wa Kiutawala na pride ya uzawa, kama tulivyokuwa tukifanya sisi na makabila yetu. Utakapo itumia vibaya hiyo pride against others hapo ndipo utakuwa umevunja sheria, otherwise ni jambo jema tu kaa vile mataifa yatakavyo peperusha bendera zao huko Brazil kuanzia hiyo kesho..
Ni ngumu sana kumwelewa Mkandara anasimamia nini, na kwasababu zipi. Labda kwa wale wenye wasi wasi kuhusu kutomwelewa mkuu naomba niwatoe hofu kwa kuonyesha bandiko lake hapo juu lilivyojichanganya juzi, jana, leo na kesho.
1. Kwazana si kweli, Waquebec wanaojiita hivyo ni wale extremist.
Hata wao wakiwa nje ya nchi yao hujulikana kama Wacanada. Kama wangekuwa wanjivunia Uquebec, wengi wasingevuka Gateneu siku ya referendum, na wengine hawakuwahi kurudi.
Miezi miwili wamemkataa Duccep aliyekuwa kinara wa U-Quebec. Hivyo mkuu, usitudanganye.
2. Mkandara anasema, mambo yote ni ya muungano. Amerudia kauli hiyo zaidi ya mara 10 hadi sasa.
Kwabahati mbaya Mkandara anajisahaulisha historia.
Muungano ulianza na mambo 11 si yote, hivyo kuuliza 7 ya nini ni kutofahamu historia ya muungano.
Katika hayo 11 ya awali yalioasisiwa na Nyerere na Karume, Mkandara hakuona tatizo.
Miaka 40 baadaye mambo yakaongezwa na kufikia 22 ambayo yakinyumbulishwa yatakuwa 47.
Hapo tulikuwa tunaelekea katika mambo yote ni ya muungano kwa mujibu wa Mkandara.
Mkandara yupo katika rekodi akisema kuongezwa mambo hayo kulikuwa 'Unyemela'
Yaani kufanya 'mambo yote' yawe ya muungano kama anavyosema leo, huko nyuma aliita unyemela.
Mambo ya kinyemela yaliingizwa katika katiba na sheria kwa kutumia bunge la S2 analotetea Mkandara.
Wakati huo huo anasema, kuingiza kinyemela kulilenga kupora madaraka na kuionea Zanzibar.
Alichosahau ni kuwa huko nyuma ametetea S2 kama suluhisho, leo anatuambia S2 zilifanya makosa kuingiza mambo Kinyemela.
Mkandara anasema suluhisho ni S2. Amesahau kuwa S2 ndizo zilizoruhusu znz kuandika katiba ya 2010 ambayo imeondoa mambo 22 bila kutumia sheria ya bunge la S2a analotetea.
Miongoni mwa mambo hayo yapo 4 yaliyokuwepo katika yale 11 ya awali.
Kwa maana kuwa baada ya kuondoa 22 sasa wamefikia mahali na kuondoa hata 4 katika 11 na kubaki 7.
Yanapobaki 7 kutoka 11 Mkandara anashangaa huo utakuwa muungano gani.
Kwani yale ya 1964 si yalikuwa 11, je huo ulikuwa muungano wa kitu gani.
Kwamba, alichokifanya Warioba na tume ni kuhalalisha mambo yaliyoondolewa na Zaznibar tena kwa kiburi, jeuri na ufidhuli wa kutoheshimu katiba wala taratibu.
Kama unadhani Mkandara anakuchanga, subiri, hebu endelea hapa chini uone anavyojivuruga na kukuvuruga kimantiki
Mkandara anadai ni muda gani utatumika kufanya uchaguzi na kuandika katiba ya Tanganyika.
Huko nyuma alisema mambo asilimia 95 ya bunge la JMT ni ya Tanganyika.
Akasema hata serikali ni ya Tanganyika. Leo anashindwaje kuelewa kuwa ukiwaondoa wale watalii 81 wasiokuwa na kazi kutoka nchi jirani ya znz, bunge na katiba ni ya Tanganyika.
Katiba ya sasa ni ya Tanganyika kwasababu znz haitambui, na wala haina heshima juu yake.
Kama katiba ya znz ni juu kuliko ya JMT, basi hiyo ya JMT ni ya Tanganyika. Ugumu anaosema unatoka wapi?
Mkandara anadai wagombea wa Tanganyika watatoka vyama gani. Hee ! kwani hilo ni la ajabu?
Kule znz sasa hivi BLW lina wabunge wa vyama gani?
Nani amewazuia Watanganyika wasigombee znz na kwanini Tanganyika ikitumia mwiko ule ule kupakua pilau yake ionekane nongwa. Hili la vyama lipo wazi sana na wala halihitaji kujadili unless mtu amejitoa ufahamu.
Mkandara anasema wazanzibar hawataki bunge la shirikisho. Hana takwimu za aina yoyote bali hisia zake tu kujenga utetezi. Wazanzibar wasingetaka hilo bunge basi wasingekubali S3. Hivyo anawasingizia.
Na mwisho anasema, kama mambo 7 basi tuelekee EAC.
Mbona hili tumelijadili siku nyingi sana. Kwani ni nani anayetaka mamlaka kamili, na kama ni znz nani kawazuia?
Leo wakitaka tukutane EAC hewala, hakuna anayewashikilia.
Wznz wanajishikilia wenyewe kwasababu hawajui wanataka nini.
Mkandara si hawa akina Kificho, Vuai, Borafia na sasa Raza wanaotaka S2. Kama wangekataa si tungekutana Arusha?
Kama Mkandara angekuwa mkweli, kwanza angeanza na kusema katiba ya 2010 ya znz imeshavunja muungano.
Na kuvunjwa muungao maana yake ni kushindwa kazi kwa S2.
Na muungano uliopo ni wa kufaa wznz tu lakini hauna maana ya muungano. Umeshakufa kutokana na S2.
Juzi wamedai passport na Uraia, hivi hapo Mkandara bado unaamini hawa ni wenzetu na wapo kwa ajili ya Tanzania?
Wapi katika republics zako unazozitaja kila siku kuna nchi ina majimbo yenye urai na passport zake.
Je, ndivyo Ontario wanavyofanya? Ndivyo Montana wanavyofanya? Ndivyo Berth wanavyofanya?
Mkandara kama umedhamiria kuichanganya hadhra, basi umefanikiwa.
Inahitaji jiniazi au psychic kukuelewa na kuelewa position yako.
Mkuu wangu, sikujua wewe ni spinning doctor mzuri sana.