Asante kwa Jibu lako. "Wanachadema wanahamia ACT" Kama first bunch la wanachama wapya wa ACT.That's the bottom line.Chama kinawezaje kushusha bendera ya chama kingine?
Sema wazi kwamba waliokuwa wanachama wa Chadema wameswitch sides!! na hiyo ni haki yao
WanaChadema wanachoweza kukifanya ni kwenda mahakamani ili kudai ofisi zao(kama walizijenga though)
Dr Kitila Mkumbo , ningeshauri ufuate nyao za Nyakarungu. Yeye kasema wazi kama chama cha 'uwazi' kilivyo. Nyakarungu hakuficha hisia na fikra zake. Kaweka wazi kabisa lazima wapambane na wapinzani wenzao. kumbuka, hayo si maneno ya duru za siasa, ni maneno ya mwanachama mwandamizi.
Nyakarungu kaiba kauli ya sera tofauti na ya Dr aliyeamua kukimbilia uteuzi wa mwenyekiti.
Hakuna shaka Nyakarungu anajibu hoja ingawa amekimbia kujumika nasi.
Dr Kitila, Political science na public relation ni muhimu kwa sasa kuliko uteuzi wa mwenyekiti.
Nyakarungu analeta damage uliyoanzisha akijua anafanya damage control wakati akifanya damage zaidi
cc Ng'wamapalala Mkandara JingalaFalsafa Mchambuzi
Mkuu Mchambuzi, Je anachofanya Nguruvi3 ndio misingi ya demokrasia ambayo anaona haipo ACT kufikia kuwaita mamluki! Misingi hiyo ndio iliyomsukuma kusema kuwa ACT kama chama kina wenyewe hivyo watakaokaribishwa wakae kando katika uongozi? Misingi hiyo ndio inayosema kauli ya mwanachama au shabiki mmoja inatosha kukiona chama ni mamluki?
Nyakarungu ni verified member FYI.Mkuu, Nguruvi3
Huyo Nyakarungu ndiyo nani?.
Mwanachama Mwandamizi ndiyo nini?.
ACT ina verified name hapa JF na kupitia Verified name ndiyo tunaweza kujadili content zake kwa sababu haya aliyoleta ni mawazo yake binafsi kama yalivyo mawazo yako.
Mkuu JingalaFasala , naona umekuja na hamaki kidogo, ningekuomba utulie.Mkuu ndio maana nilikuambia huu si wakati muafaka wa kutoa hukumu uliyotoa kwa ACT! Hivi kweli unataka kutuaminisha hoja zako kwa ushahidi wa porojo za MwanaJF ambaye hata hatumjui? Kwanini ujenge hoja kwa kulazimisha mno? Unachofanya kinakaribia kutuaminisha alichosema Gamba la Nyoka kuwa huko ni kupambana na act kwa malengo ya kuinusuru Chadema.
Bado nasisitiza kuwa huu si wakati muaafaka wa hoja zako!
Mkuu Mchambuzi, Je anachofanya Nguruvi3 ndio misingi ya demokrasia ambayo anaona haipo ACT kufikia kuwaita mamluki! Misingi hiyo ndio iliyomsukuma kusema kuwa ACT kama chama kina wenyewe hivyo watakaokaribishwa wakae kando katika uongozi? Misingi hiyo ndio inayosema kauli ya mwanachama au shabiki mmoja inatosha kukiona chama ni mamluki?
Kwa kauli ya kudai ACT inawenyewe aliyotoa Nguruvi3 je inatosha kwa sisi kuanza kumponda na kupuuza kila alichoandika humu Jf na kwingineko?
Mwisho wa siku huu ni ushahidi kuwa Demokrasia si kitu kinachowezekana kwa sasa Afrika. Nakumbuka nimewahi kusikia kitu hiki toka kwa Nyerere kuwa watu tuko bankrupt kabisa kisiasa, ukizungumzia siasa watu tutaingizia ukabila, viudinidini, na sasa ni uchamachama, n.k. TUAMKE!
Anaita sasa!
Hoja za msingi sana.nimeupitia huu uzi kwa makini sana na hapa nimejikuta nina swali la msingi sana ambalo sijaona jibu lake kwenye hoja zilizojadiliwa humu ndani swali langu ni
je! bado wananchi tunaamini mtu/ kikundi fulan kinaweza kutupa msaada tuutakao ili tupige hatua katika kuijenga tanzania yetu??
na je ndani ya Tanzania hakuna watu wanaofaa kuwa viongozi zaid ya hawa ambao kila siku tunawaona na hawana jipya kwetu??
Mkuu , kuna uhusiano kati ya Kitila na ACT. Ukisoma maudhui kwa undani unaona ACT kama chama hakijatajwa kama mhusika mkuu Kitila.Kumradhi Mkuu wangu Nguruvi3 kwa hamaki!
Niseme hivi tu, Chama kimekaribisha watu kukikosoa na kukishauri katika harakati zake za kujiimarisha. Heading na maudhui ya uzi huu hayakukaa kukosoa tu ila kuponda kwa kosa la mtu mmoja, hata awe muasisi au kiongozi, haikutosha kukiponda chama ila tu kukikosoa, kukionya, kukitahadharisha na kukionesha njia! Ingesaidia zaidi! Ila hapa umeonesha ACT ni Mamluki tu, NO REMARKS!
Anaita sasa!
Chama chochote kinapoanzishwa waasisi wake wana fursa na uwezo wa kumchagua Mwenyekiti wao wa muda hadi hapo Uchaguzi mkuu utakapo fanyika. Chama kilipozaliwa nani alikuwa mwenyekiti wa muda? Mzee Mtei alipata kura za kina nani kuwa mwenyekiti! kabla ya Uchaguzi mkuu au kwa sababu yeye ndiye muasisi ana haki zote za kushika nyadhifa yoyote aitakayo!.. Mbona hatuanzi kujiuliza maswali haya sisi wenyewe tena kibaya zaidi hatuijui historia ya chama kwa undani wake ila kusema ya watu. Mbona CDM haiweki wazi historia ya chama mahala popote tukajua mzee Mtei na wanziwe walianzaje! Na je Inahusu kweli nikijua kwamba Mzee Mtei alijipachika cheo cha Uenyekiti basi chama hiki hakifai!.ni ukweli usiopingika kwamba tunahitaji siasa za kisasa zaidi na demokrasia ya ukweli na haki isiyoshawish juu ya mtu ama kundi ila inashawish kwa sera, na mwongozo wa chama huku ikilinda na kutetea katiba na maslahi ya raia wa nchi hii....
nguruvi 3 umechambua kwa umakini sana lakin naona umejikita zaid katika kukosoa sio jambo baya lakin ukasahau kutuonyesha aina za siasa tuzitakazo kwa unyumbulifu..
nafkiri mimi sio mtanzania pekee niliyechoshwa na utitiri wa wanasiasa ambao hawana tija kwa taifa zaid ya kujenga majina yao, kujineemesha na hata kutunyang'anya rasilimali zetu zikiwemo pesa zetu za michango mifukoni mwetu.
labda nafkiri kwa muda mrefu tumekuwa na amzoea ya kuona mmtu fulan ama kundi fulan can do something lkn sasa yatupasa kubadilika hasa pale ambapo mtu huyu ama kundi hilo tulilipa nafasi na likashindwa kutuonyesha ufanisi. umefika wakati ambao kwa sasa tunataka sera ambazo kiuhalisia zinatekelezeka na zinaboresha maisha na ustawi wa watu na nchi kwa ujumla.
hakuna haja ya kusema eti lazima ZZK awe mwenyekiti ama sijui nani hapana kwani kama kuna demokrasia ya kweli atagombea kwa kunadi sera zake na hapo ndipo tutakapojua nani anayetufaa na wanachama wataamua nani anafaa zaid basing on sera na experience yake.
kuna jambo ambalo mimi naliona kila siku kama tatizo kwa wanasiasa wetu nalo ni ni wazuri sana kwa kusema majukwaani lkn wazito sana kwa kutenda kivitendo, na hili halina mtu ambaye halimgusi anzia kwa serikali yenyewe hadi vyama vya upinzani.
kwa mfano kama kitila anaweza kuikosoa CCM kwa kutokuwa na demokrasia ya kweli, akasema chaguzi za NEC zimejaa rushwa na majina fulan kwanini leo hii naye atuletee chaguzi zilizojaa majina na pengine rushwa itatumiaka??
kw akufuata mifano ya wapinzani wetu sio CUF, ama NCCR-mageuzi, ama TLP ama CDM, kote utaona demokrasia hakuna wanachama wanalazimika kumchagua mwenyekiti kwa kufuata jina na kuna wengine wanaamin kwamba mtu fulan pekee ndiye anayefaa kuwa mwenyekiti hapa, sasa kwa makosa haya bado CCM anajiona mshindi kwamba bora hata mimi chaguzi zangu zinaanziaga ngazi ya mjumbe wa nyumba kumi na hata kwenye NEC huwa zinaonekana wazi kuliko wenzangu ambao wao chaguzi hufanywa chumban na watu wachache,,,,,,,,(nafkiri nitaeleweka vizuri hapa)
kama kweli tunataka vyama vya siasa vyenye upinzani wa kweli basi ni lazima vihakikishe kwanza
1) vina sera nzuri kuliko zilivyo za chama tawala
2) wanapractice demokrasia ya kweli na
3) sera zao zina uhalisia ndani yake kwamba zinatekelezeka na si kuwa maneno matamu yasiyotekelezeka milele mf. kusema chama kitafanya elimu ya msingi kuwa bure lazima wasema bure ipi manake kusema bure tu haitoshi na bure ziko nyingi inaweza ikamaanisha bure ya kutolipa ada lkn michango mingine ikawepo pale pale hivyo bure hapo haipo.
duh! mkuu wangu unanitia mashaka na ulinganisho wako wa team za mpira na wanachama wa vyama vya siasa, hapo ni kama maji na mafuta, mkuu wanachama wana mchango mkubwa sana kwenye vyama vya siasa, ndo hao mawakala, na ndo waeneza sera za chama,team za mpira ni burudani haifanani kamwe na maisha ya watu kwenye vyama vya siasa, ukisema ACT ikichukua wanachama wa chadema itawafanya nini jibu ni rahisi sana, hoja ya mkuu Nguruvi3 hapo juu kafafanua namna Mkumbo anavyoeleza mbadala wa CCM na CHADEMA, kwa maana miaka kumi kubomoa upinzani na miaka mingine kumi kujenga tena upinzani, mkuu binafsi naona kama umejivika makengeza kuhusu yale yanayojadiliwa hapa kuhusu ACT na badala yake umeamua kui'attack chadema, imekuaje tena mkuu?Kwa muda mrefu sasa hofu ya Chadema imekuwa ndani ya chama. Wadhungu wanasema - Young chicken wil always come home to roost!
Mimi nawashangaa sana hawa vijana wetu ambao wanataka sana kutuaminisha kwamba Chama kinaweza kushinda uchaguzi kwa kuandikisha wananchama wengi. Hii watu mliitoa wapi? Je imani hii inatokana na kwamba CCM inawanachama wengi hivyo kuna uwezekano mkubwa kuwa hii ndio sababu ya ushindi wao?
Jamani jamani, sasa ACT ikichukua wanachama wa Chadema ndio itawafanyia nini? hawa watakiwezeshaje chama kiweze kushinda uchaguzi? na lini wanachama ndio wanahesabiwa ili kupata ushindi. Basi kama ingekuwa hivyo Arsenal na ManU wangechukua ubingwa wa kandanda miaka yote maana nijuavyo mimi wanachama au wapenzi hujiunga tu ikiwa chama chenyewe kimeonyesha ari, nia na uwezo mkubwa wa kukidhi matumaini yao wananchi.
Hata kama ACT itachukue wanachama wote wa CDM, ifahamike ni kwa sababu wananchi hao wamekosa imani ya chama hicho kama ilivyotokea kwa CCM ktk mikoa ya Mwanza na Arusha. Ni kazi ya CDM kuacha hizi za mipasho, kulaumu watu wengine mahala ambapo wao wenyewe wanalikoroga. CDM ya leo ni sawa na gazeti la NIpashe! na inasikitisha sana hata Ukumbi huu umekuwa wa mipasho na tunzi za kuuza magazeti. Hivi kweli mnataka tuamini kwamba vyama vya Upinzania vinagombania wananchama badala ya kuwajaza wananchi wapiga kura matumainiya maisha bora.
..
Chama chochote kinapoanzishwa waasisi wake wana fursa na uwezo wa kumchagua Mwenyekiti wao wa muda hadi hapo Uchaguzi mkuu utakapo fanyika. Chama kilipozaliwa nani alikuwa mwenyekiti wa muda? Mzee Mtei alipata kura za kina nani kuwa mwenyekiti! kabla ya Uchaguzi mkuu au kwa sababu yeye ndiye muasisi ana haki zote za kushika nyadhifa yoyote aitakayo!.. Mbona hatuanzi kujiuliza maswali haya sisi wenyewe tena kibaya zaidi hatuijui historia ya chama kwa undani wake ila kusema ya watu. Mbona CDM haiweki wazi historia ya chama mahala popote tukajua mzee Mtei na wanziwe walianzaje! Na je Inahusu kweli nikijua kwamba Mzee Mtei alijipachika cheo cha Uenyekiti basi chama hiki hakifai!.
Sawa mkuu labda unifahamishe Yanga inaendeshwa na kina nani? ama hayo yoote ulosema kama ni mchango wa wanachama wa chama cha siasa huwezi kuyaona kwenye chama cha Mpira!duh! mkuu wangu unanitia mashaka na ulinganisho wako wa team za mpira na wanachama wa vyama vya siasa, hapo ni kama maji na mafuta, mkuu wanachama wana mchango mkubwa sana kwenye vyama vya siasa, ndo hao mawakala, na ndo waeneza sera za chama,team za mpira ni burudani haifanani kamwe na maisha ya watu kwenye vyama vya siasa, ukisema ACT ikichukua wanachama wa chadema itawafanya nini jibu ni rahisi sana, hoja ya mkuu Nguruvi3 hapo juu kafafanua namna Mkumbo anavyoeleza mbadala wa CCM na CHADEMA, kwa maana miaka kumi kubomoa upinzani na miaka mingine kumi kujenga tena upinzani, mkuu binafsi naona kama umejivika makengeza kuhusu yale yanayojadiliwa hapa kuhusu ACT na badala yake umeamua kui'attack chadema, imekuaje tena mkuu?