Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Chama kinawezaje kushusha bendera ya chama kingine?
Sema wazi kwamba waliokuwa wanachama wa Chadema wameswitch sides!! na hiyo ni haki yao
WanaChadema wanachoweza kukifanya ni kwenda mahakamani ili kudai ofisi zao(kama walizijenga though)
Asante kwa Jibu lako. "Wanachadema wanahamia ACT" Kama first bunch la wanachama wapya wa ACT.That's the bottom line.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Dr Kitila Mkumbo , ningeshauri ufuate nyao za Nyakarungu. Yeye kasema wazi kama chama cha 'uwazi' kilivyo. Nyakarungu hakuficha hisia na fikra zake. Kaweka wazi kabisa lazima wapambane na wapinzani wenzao. kumbuka, hayo si maneno ya duru za siasa, ni maneno ya mwanachama mwandamizi.

Nyakarungu kaiba kauli ya sera tofauti na ya Dr aliyeamua kukimbilia uteuzi wa mwenyekiti.
Hakuna shaka Nyakarungu anajibu hoja ingawa amekimbia kujumika nasi.

Dr Kitila, Political science na public relation ni muhimu kwa sasa kuliko uteuzi wa mwenyekiti.
Nyakarungu analeta damage uliyoanzisha akijua anafanya damage control wakati akifanya damage zaidi

cc Ng'wamapalala Mkandara JingalaFalsafa Mchambuzi

Mkuu ndio maana nilikuambia huu si wakati muafaka wa kutoa hukumu uliyotoa kwa ACT! Hivi kweli unataka kutuaminisha hoja zako kwa ushahidi wa porojo za MwanaJF ambaye hata hatumjui? Kwanini ujenge hoja kwa kulazimisha mno? Unachofanya kinakaribia kutuaminisha alichosema Gamba la Nyoka kuwa huko ni kupambana na act kwa malengo ya kuinusuru Chadema.

Bado nasisitiza kuwa huu si wakati muaafaka wa hoja zako!

Mkuu Mchambuzi, Je anachofanya Nguruvi3 ndio misingi ya demokrasia ambayo anaona haipo ACT kufikia kuwaita mamluki! Misingi hiyo ndio iliyomsukuma kusema kuwa ACT kama chama kina wenyewe hivyo watakaokaribishwa wakae kando katika uongozi? Misingi hiyo ndio inayosema kauli ya mwanachama au shabiki mmoja inatosha kukiona chama ni mamluki?

Kwa kauli ya kudai ACT inawenyewe aliyotoa Nguruvi3 je inatosha kwa sisi kuanza kumponda na kupuuza kila alichoandika humu Jf na kwingineko?

Mwisho wa siku huu ni ushahidi kuwa Demokrasia si kitu kinachowezekana kwa sasa Afrika. Nakumbuka nimewahi kusikia kitu hiki toka kwa Nyerere kuwa watu tuko bankrupt kabisa kisiasa, ukizungumzia siasa watu tutaingizia ukabila, viudinidini, na sasa ni uchamachama, n.k. TUAMKE!

Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:

Mkuu @JLF,

Nadhani maoni yangu kwa hili yapo bayana #44 .

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, Nguruvi3

Huyo Nyakarungu ndiyo nani?.

Mwanachama Mwandamizi ndiyo nini?.

ACT ina verified name hapa JF na kupitia Verified name ndiyo tunaweza kujadili content zake kwa sababu haya aliyoleta ni mawazo yake binafsi kama yalivyo mawazo yako.
Nyakarungu ni verified member FYI.
Alihusika na kesi ya CDM Tarime kama sijakosea. I stand to be correct though
 
nimeupitia huu uzi kwa makini sana na hapa nimejikuta nina swali la msingi sana ambalo sijaona jibu lake kwenye hoja zilizojadiliwa humu ndani swali langu ni

je! bado wananchi tunaamini mtu/ kikundi fulan kinaweza kutupa msaada tuutakao ili tupige hatua katika kuijenga tanzania yetu??

na je ndani ya Tanzania hakuna watu wanaofaa kuwa viongozi zaid ya hawa ambao kila siku tunawaona na hawana jipya kwetu??
 
Mkuu ndio maana nilikuambia huu si wakati muafaka wa kutoa hukumu uliyotoa kwa ACT! Hivi kweli unataka kutuaminisha hoja zako kwa ushahidi wa porojo za MwanaJF ambaye hata hatumjui? Kwanini ujenge hoja kwa kulazimisha mno? Unachofanya kinakaribia kutuaminisha alichosema Gamba la Nyoka kuwa huko ni kupambana na act kwa malengo ya kuinusuru Chadema.

Bado nasisitiza kuwa huu si wakati muaafaka wa hoja zako!

Mkuu Mchambuzi, Je anachofanya Nguruvi3 ndio misingi ya demokrasia ambayo anaona haipo ACT kufikia kuwaita mamluki! Misingi hiyo ndio iliyomsukuma kusema kuwa ACT kama chama kina wenyewe hivyo watakaokaribishwa wakae kando katika uongozi? Misingi hiyo ndio inayosema kauli ya mwanachama au shabiki mmoja inatosha kukiona chama ni mamluki?

Kwa kauli ya kudai ACT inawenyewe aliyotoa Nguruvi3 je inatosha kwa sisi kuanza kumponda na kupuuza kila alichoandika humu Jf na kwingineko?

Mwisho wa siku huu ni ushahidi kuwa Demokrasia si kitu kinachowezekana kwa sasa Afrika. Nakumbuka nimewahi kusikia kitu hiki toka kwa Nyerere kuwa watu tuko bankrupt kabisa kisiasa, ukizungumzia siasa watu tutaingizia ukabila, viudinidini, na sasa ni uchamachama, n.k. TUAMKE!

Anaita sasa!
Mkuu JingalaFasala , naona umekuja na hamaki kidogo, ningekuomba utulie.
1. Katika bandiko la mwanzo kabisa nimeonyesha scenario zote za Kitila Mkumbo na wapi anataka kututelekeza kana kwamba ni mazuzu wa mitaani. Nikaendelea kufafanua hoja hizo katika mabandiko yaliyofuata.

Ninashangaa sana watu hawapingi kile nilichosema, wanaleta hisia ambazo hazipo.
Hoja za bandiko langu zinabaki kusimama bila kupingwa, ila zinapingwa kwa hisia

2. Huyo Nyakarungu ni mwanachama wa zamani wa CDM anayejulikana kwa kiasi ninachofahamu unless kuna Nyakarungu mwingine wanayetumia naye ID moja. Nakumbuka ID hiyo ameitumia si mara moja.
Nitajiridhisha zaidi na kama si kweli nitaondoa hilo bandiko.

3. Hoja ya Kitila kuteua mwenyekiti inapewa pass kana kwamba ni suala la kawaida na jema tu

4. Hoja ya kutanguliza sera na si majina inaonekana kutowaingia masikioni wengi, pengine kwa hasira vinatafutwa vitu visivyohusiana na mada na kukuzwa

5. Hapo niliposema 'ACT ina wenyewe' nadhani unge quote sentensi ili nieleze nilichokusudia.
Ukisema Rais kafumaniwa, haitoshi, kwasababu Rais anaweza kuwa wa TFA au DARUSO n.k.
Ningeomba unitendee haki kwa kuni quote ili nami nipate nafasi ya kueleza nilikusudia nini.

6. Kuhusu kuponda maandishi yangu, hilo wala lisikutie shaka. Ninapoandika sitegemei kuwa kila mmoja anatakubaliana na hoja zangu na kama nisivyokubaliana na za baadhi ya wenzangu.
Kutofautiana kimawazo hakuna maana ya upungufu, kuna maana ya kuangalia mambo kwa mtazamo mpana zaidi.

7. Hoja yangu kuu ni kuwa demokrasia lazima istawi katika ukweli. Wakati tulio nao si nyakati za kufanya siasa za ulaghai.
Huko nyuma tuliaminisha ZZK anataka kufundisha na ataachana na siasa. Waraka ukatuonyesha ilikuwa ni mbinu tu lengo lilikuwa kuwa mwanasiasa zaidi kama mwenyekiti na si mwwalimu wa chuo.

Haionekani kwamba waliotenda kosa hilo wamejifunza. Kutokana na scenario 1-5 hapo juu, duru inasimama na kupinga ulaghai wa kisiasa unaofanywa na watu ambao kimsingi nafasi yao katika jamii ni kubwa kwa namna nyingi.
Leo huwezi kutushaiwshi kuwa Kitila anamshauri ZZK ajiunge wakati tunajua anataka kumuondoa mahakamani.

Leo hutushawishi kuwa kumteua ZZK ni sehemu ya demokrasia iliyoliliwa kwa waraka.
Leo hakuna tuamini Kitila kajiunga na ACT juzi wakati kulikuwa na preamble za mtu mwenye akili kutambua.

Na mwisho, hoja hii inaweza kuudhi watu wengi sana kwasababu kadhaa, lakini tukubaliane kuwa kama tunavyowasema CCM na ufisadi, kama tulnamvyomsema Mbowe na togwa, au Dr Slaa kwa suala la Kgame, akina Nape na wengine, Zitto au Kitila hawana immunity ya aina nyingine tofauti.
 
nimeupitia huu uzi kwa makini sana na hapa nimejikuta nina swali la msingi sana ambalo sijaona jibu lake kwenye hoja zilizojadiliwa humu ndani swali langu ni

je! bado wananchi tunaamini mtu/ kikundi fulan kinaweza kutupa msaada tuutakao ili tupige hatua katika kuijenga tanzania yetu??

na je ndani ya Tanzania hakuna watu wanaofaa kuwa viongozi zaid ya hawa ambao kila siku tunawaona na hawana jipya kwetu??
Hoja za msingi sana.
Ukisoma kwa makini, tofauti na wengi wanavyoligeuza suala hili kama la ACT, maana ya mada ni kuonyesha kuwa tuna tatizo katika siasa za nchi hii. Tatizo si wanasiasa ambao kimsingi ni walaghai, tatizo ni sisi wananchi kukubali kulaghaiwa kila mara tukipiga makofi, nderemo na vifijo.

Ukisoma bandiko la I tumeonyesha mazingira yote ya 'udanganyifu'. Hakukuwa na sababu za Kitila kuzunguka zunguka, angeweza kuwa muwazi tu na wala lisingeleta tatizo.
Tunachokipinga ni siasa za kina mzee Mustafa Songambele za November 1957 kufanyika May 2014.

Tunachoonyesha hapa ni kuwa wasomi kama Dr Kitila bado wanaamini katika demokrasia ya uteuzi wa watu na wala si uchguzi. Wakati wanaamini hivyo, wanarudi upande mwingine kupinga CCM na CDM kwa kile kile wanachokitenda mchana huu.

Wasomi kama Dr Kitila bado wanaamini katika mtu na wala sii sera za chama.
Kitu cha kwanza cha kuitangaza ACT ni 'kumtambulisha Zitto' na wala si kueleza sera za chama hicho.
Katika mazingira haya tunatakiwa tukae kimya kwasababu wenzetu kama Mkandara wanaamini kabisa kuwa kuwasema hawa watu ni dhambi kuu na uongo.

Ni uongo gani wakati Mchambuzi kaonyesha pande mbili za Kitila kwa kutumia maneno ya Kitila.

Tunachotaka ni kuwa na siasa za kileo na si za kusubiri mtu abebe wanachama kwa jina.
Ujenzi huu wa chama katika njia potofu, dhaifu na dhalili unapaswa kukemewa.
Kitila kapata wapi nguvu za kumteua mwenyekiti ZZK tena bila kueleza sera, au huyo mwenyekiti kujua sera achilia mbali katiba.

Kitila alipaswa afanye 'nurturing' ya vijana kwa kutumia uwezo wake.
Taifa haliwezi kuishi kwa kumtegemea Zitto.
ANC ilikuwepo bila Mandela na inaendelea bila Mandela, akina Kitila wanaamini mworabaini wa siasa na demokrasia za nhi hii hahukamiliki isipokuwa tu pale ZZK atakapokuwa mwenyekiti.

Kuendelea kukaa kimya bila kuwaonyesha kuwa tunafahamu, tunajua na tunaweza ni kuwapa uhalali wa kuendelea kupaza sauti katika vyombo vya habari bila second thought. Kuwapa uhalali wa kutuona mazuzu. Ney, hapana!

Na kwa bahati mbaya waretezi na waumini wa Kitila/Zitto hawapingi hoja zilizo mezani. Wanachokifanya ni spinning ili kwenda nje ya mada. Tunasema hapana, tumechoka na udanganyifu wa akina Nape na maisha bora na hatupo tayari kusikia demokrasia ya uteuzi wa mtu upande mwingine.

Watu wanaaminishwa kwa majina na sera ndilo hasa tatizo. Tunataka mabadiliko.
 
Kumradhi Mkuu wangu Nguruvi3 kwa hamaki!

Niseme hivi tu, Chama kimekaribisha watu kukikosoa na kukishauri katika harakati zake za kujiimarisha. Heading na maudhui ya uzi huu hayakukaa kukosoa tu ila kuponda kwa kosa la mtu mmoja, hata awe muasisi au kiongozi, haikutosha kukiponda chama ila tu kukikosoa, kukionya, kukitahadharisha na kukionesha njia! Ingesaidia zaidi! Ila hapa umeonesha ACT ni Mamluki tu, NO REMARKS!

Mkuu , kuna uhusiano kati ya Kitila na ACT. Ukisoma maudhui kwa undani unaona ACT kama chama hakijatajwa kama mhusika mkuu Kitila.

Tutaendelea kukosoa, kuelimisha na kutahadharisha na bandiko linalofuata litakuwa na haya yote uliyosema.
Shukran
 
HOJA ZA KITILA
NI MAKUSUDI AU BAHATI MBAYA?

Tangu mjadala uanze hakuna anayepinga kuwa Kitila hakupaswa kuteua mwenyekiti wa chama cha siasa bali kupitia mamlaka ya wanachama

Kwamba, Kitila hakuitendea haki demokrasia. Na kwamba, hakufuata misingi ya uenezi na utangazaji wa chama.Ni hoja muhimu ambazo zimekwepa.
Kinachozungumziwa ni ima nje ya mada au kutafuta sababu za kuficha tatizo

Tunakwenda mbali na kwa kuonyesha kwanini kitila amekosea ili kutoa funzo kwa wanasiasa na kuwaamsha wananchi waache kuamini siasa za watu, bali za sera.

Sehemu I
Kitila hakufanya aliyoyafanya kwa bahati bali kwa makusudi yenye nia njema kwake, wala halikuwa tatizo. Ni sehemu ya mikakati ya kisiasa.

Tatizo ni kufanya njia mbaya aliyotumia, na zoezi zima kuonekana hata kuhoji kuhusu uwezo wake kisiasa siku za karibuni.
Kitila alikusudia kukitangaza ACT, nia njema kabisa isiyo na tatizo

Hisoria ya Kitila ndani ya Chadema kama mshauri wa ufundi, na matukio ya Waraka, na hili la uteuzi wa mwenyekiti lipo jambo watu hawalifahamu

Kitila yupo katika nafasi ya kazi tofauti na uwezo wake (talent)
Kimsingi ni mtaalamu na hauna shaka ana mchango mkubwa katika Chadema ya Leo.
Ni mtaalamu wa mikakati ‘strategist' na apewe credit kwa hilo

Katika siasa kuna makundi ya watu wenye kazi tofauti.
Kuna wanasiasa (Politicians) ambao kazi yao ni kueleza vyama , sera zao n.k.
Sifa kuu ya politician ni uwezo wa kufafanua, kupambua, kuzua hata kufanya spinning kwa njia zinazojenga au kubomoa hoja. Wanasiasa huambatana na mvuto wao (Charisma)

Kundi la pili ni watu wa mikakati (Strtegist). Hawa hawaonekani majukwaani lakini ndio wanaopanga, wanaoamua, kupima na kungalia mwelekeo wa kisiasa.
Moja ya kazi zao ni kushauri politicians katika kutenda kazi zao.
Ni nadra sana kuwajua na ndivyo alivyokuwa Kitila Chadema

Kundi la tatu ni wapiga debe (Pundits). Kazi kubwa ni kueneza chama, kuzuia uharibifu(damage control) kupambua hoja na kueneza chama katika hali ya kuwapamba wanasiasa wakiunganisha sera, mikakati n.k.
Sifa ya pundits ni uwezo wa kujenga hoja, kubomoa, kuangalia uelekeon.k
Hawana hamaki wala hasira na huwa na lugha nzuri ya kuvutia.

Kwa ufupi haya ni makundi matatu lakini yapo zaidi ya hapo.
Kwa muktadha wa mjadala nimeyaweka kuonyesha kwanini kuna tatizo.
Inaendelea sehemu ya II
 
Sehemu ya II
Kwa vile Kitila si mwanasiasa(Politician) bali mtu wa mikakati (Stretegist), alichokifanya hadharani ni mkakati akisahau mkakati hufanywa nyuma ya pazia.

Kwa vile ni mtu wa mikakati aliyejivika haiba ya uanasiasa asiyokuwa nayo, Kitila amejikuta akiteua mwenyekiti(mkakati), akiacha kutangaza sera za chama( kazi ya politician) na akilenga kuvuruga uungwaji mkono (kazi ya pundits)

Mkakati wake ulikuwa mzuri nyuma ya pazia na kwa malengo aliyokusudia.
Kwa kujivika uanasisasa akajikuta anatangaza uteuzi wa mwenyekiti.
Na kwa kuwa ‘pundits' akajikuta anamtangaza mtu na si sera

KITILA ALIPASWA KUFANYA NINI?
Alipaswa kuelewa makala zake za magazetini zinaweza kutumika kumhukumu,kila aliloandika alitakiwa awe mwangalifu.

Mfano, hakutakiwa aandike mbadala wa CCM na CDM, akifahamu alikuwa na mzigo wa Waraka na ingekuwa rahisi kuhusishwa nao. Angeweza kuandika kushindwa kwa sera za vyama vya siasa kwa ujumla bila kutaja vyama, na mbadala unaoweza kuhitajika.

Kwa kuelewa ameelemewa na zigo la waraka, Kitila alitakiwa ajiepushe na ‘tete a tete' na Chadema. Hilo lingemfanya aonekane mvumilivu na mwenye busara.

Kujiunga kwake ACT hakukutakiwa kuwe na matangazo, yeye ni public figure kupitia waraka hata kama kuna mazuri ameyafanya.
Umma ungetafuta (curiosity) wapi alipo ,ingekuwa habari ya uenezi wa chama bila neno hata moja

Kitila hakutakiwa kwenda kwenye radio kumnadi Zitto.
Zitto ni public figure ambayo ni ‘brand'isyohitaji nakshi.
Kwa kuzingatia tatizo la waraka Kitila alipaswa kuelewa chochote anachokifanya kitakuwa extrapolated na kutoa siri za mikakati

Na kama ingebidi kumtangaza ZZK, Kitila asingeanzia na ueneyekiti ambao ni tatizo walililobeba katika waraka linalowaandama

Kitila ngemshauri ZZK kimya kimya(kama hajamshauri hadi sasa) aondoe kesi mahakamani na siku ya kuondoa kesi ndio iwe siku ya kutanganza kujiunga na ACT.

Hapo angekuwa anarejesha haiba ya ‘brand' yake kwa political stunt kubwa.
Definite wafuasi wangeunga ‘tela' bila neno hata moja la Kitila.

Kwa muda walitakiwa wakijenge ‘chama'wakisubiri uchaguzi ili kujenga uhalali wa kisiasa. Wangejiepusha na sintofahamu alizozua Kitila kiu ya uenyekiti wa ZZK bado inzunguka vichwani mwa watu na kuliongelea hilo ni kufumua vidonda upya

Inaendelea sehemu ya III
 
Sehemu III
Tumeona Kitila si mwanasiasa au mwenezaji kiuhalisia(natural) ni mtu wa mikakati.
Kitendo cha kujivika majukumu yasiwiana na haiba au wasifu yake ndicho chanzo cha timbwili linalofuka kuhusiana na ujio wa ACT

JE, MWANAMKAKATI ALIKUWA NA MKAKATI?
Pamoja na kuwa mtu wa mikakati, Kitila amezidiwa na hamasa kiasi cha kufanya mikakati iswe timilifu.

Kwa mfano, kitendo cha kushindwa kutangaza sera ni kosa la kisiasa. Siasa za sasa ni za sera na si mtu au watu. Kitila kumtangaza ZZK kama mwenyekiti mtarajiwa kumeondoa sehemu kubwa ya uungwaji mkono wa ACT.

Kwa mkakati wake wa sasa atapata ‘zoa zoa' tu wanaorudisha na kuchukua kadi, watu wenye akili zao watajiuliza, je kuna demokrasia ya kweli ndani ya chama? Wapi sera za chama? Na je wanajiunga na ACT kumfuata Zitto au kutafuta mwelekeo mpya wa kisiasa.

Majibu ya maswali hayo yatawanyima ACT wanachama, kosa la kimkakati la Kitila.
Mfano wa pili, kitendo cha kuanza kuwataja mahasimu wake kisiasa(Chadema) kama makala inavyosema kinajenga uhasama wa kisiasa.

Kama lengo ni kupata wanachama wa CDM watakaoondoka na ZZK, wapo watakaosita wakiamini katika demokrasia.Kitila atakuwa ameiumiza ACT kama individual.

Mfano wa 3, Kitendo cha kumtanguliza mtu na si sera kinajenga mazingira ya kuvunja moyo. Leo wapo vijana ndani ya ACT(tuamini wapo kwasababu kina usajili) wenye malengo mbali mbali.

Kwasasa wanajua nafasi zao katika chama ni nyingine kwasababu mwenyekiti keshateuliwa na hawana nafasi. Kitila anazidi kupoteza uungwaji mkono.

Mfano wa 4, Ni vema Kitila akafahamu hadhira anayowasiliana nayo (audience). Mbinu za kudanganya kuhusu kumshauri ZZK hadhira ikijua ni ulaghai kunampunguzia uaminifu wa kisiasa (honesty) na hilo linatosha kumjumuisha yeye na ACT, amekiumiza chama.

Mfano wa mwisho, kama mkakati wa Kitila akiwa nyuma ya pazia ni kudhoofisha upinzani ili kujenga upinzani mpya,mkakati huo una matatizo

  1. Imechukua miaka 20 kwa upinzani kuwa tishio kwa CCM. Mkakati wa Kitila unalenga kuchukua miaka 10 ya kubomoa upinzani na miaka 10 kujenga mbadala.
  2. Ndani ya miaka 10 ya kujenga mbadala kutatokea wengine wanaohitaji mbadala zaidi na kutaka miaka 10 ya kubomoa mbadala mpya kujenga mbadala mpya zaidi. Vicious circle ya kuunda upinzani
  3. Mbinu ya kudhoofisha upinzani inalenga kuimarisha CCM kwa kuipa muda wa kupumua na kujisahihisha kwa muda kutegemeana na mazingira.

Inaendelea sehemu ya mwisho
 
SEHEMU YA MWISHO

Katila ashauriwe kuhusu makosa anayoyafanya. Asaidiwe kujifunza makosa ya nyuma na sasa.
Ni vema angerudi katika nafasi yake ya mikakati'strategist'.
Nafasi ya uanasiasa(politician) na upiga debe(Pundits) zinampwaya.

Kauli zake za karibuni sit u zimemuumiza bali pia zimegusa maeneno mengine.
Kwanza, anazidi kujenga udadisi ( intriguing questions) dhidi ya swahiba Zitto.

Pili,Kitila amekiweka chama cha ACT katika mazingira magumu.
Kutakuwa na ufukunyuku (curiosity) kwa kila linalofanywa nap engine kudumuza jitihada za kujieneza.

Kwa mwendo wa Kitila ACT imeanza kwa mguu mbovu kwa hoja za mwanachama mmoja Kitila.

Wananchi waache kushabikia siasa za watu, wajikite katika siasa za sera na demokrasia.

Kuficha mapungufu ni kule uozo. Tumeyaona kwa NCCR, TLP, CUF n.k Huko kote matokeo yake ni kupungua kwa nguvu badala ya kuongezeka

Kumuonea aibu Kitila ni kudumuza demokrasia, kupalilia udhaifu na kuendeleza miaka 50 iliyotufikisha hapa. Ni wakati wa modern politics, siasa za ulaghai zikataliwe.

Tufike mahali tunamuuliza mtu kwanini anataka uongozi, atafanya nini na kwa mikakati ipi kwa namba na hesabu na si kuamini jina.

Tufike mahali tunajenga utamaduni wa kuwawajibisha viongozi bila kujali ukubwa wa vichwa au akili zao.

Na ifike mahali viongozi waogope kutudanganya kwa kujua tunajua wanatudanganya na wajue we will hold them accountable perfect and square without fear or favor.

Tusemezane
 
Kwa muda mrefu sasa hofu ya Chadema imekuwa ndani ya chama. Wadhungu wanasema - Young chicken wil always come home to roost!

Mimi nawashangaa sana hawa vijana wetu ambao wanataka sana kutuaminisha kwamba Chama kinaweza kushinda uchaguzi kwa kuandikisha wananchama wengi. Hii watu mliitoa wapi? Je imani hii inatokana na kwamba CCM inawanachama wengi hivyo kuna uwezekano mkubwa kuwa hii ndio sababu ya ushindi wao?

Jamani jamani, sasa ACT ikichukua wanachama wa Chadema ndio itawafanyia nini? hawa watakiwezeshaje chama kiweze kushinda uchaguzi? na lini wanachama ndio wanahesabiwa ili kupata ushindi. Basi kama ingekuwa hivyo Arsenal na ManU wangechukua ubingwa wa kandanda miaka yote maana nijuavyo mimi wanachama au wapenzi hujiunga tu ikiwa chama chenyewe kimeonyesha ari, nia na uwezo mkubwa wa kukidhi matumaini yao wananchi.

Hata kama ACT itachukue wanachama wote wa CDM, ifahamike ni kwa sababu wananchi hao wamekosa imani ya chama hicho kama ilivyotokea kwa CCM ktk mikoa ya Mwanza na Arusha. Ni kazi ya CDM kuacha hizi za mipasho, kulaumu watu wengine mahala ambapo wao wenyewe wanalikoroga. CDM ya leo ni sawa na gazeti la NIpashe! na inasikitisha sana hata Ukumbi huu umekuwa wa mipasho na tunzi za kuuza magazeti. Hivi kweli mnataka tuamini kwamba vyama vya Upinzania vinagombania wananchama badala ya kuwajaza wananchi wapiga kura matumainiya maisha bora.

Hivi kweli nyie wanaChadema mnaamini Ushindi dhidi ya CCM utapatikana kutokana na kuandikisha wanachama wengi kutoka CCM na ndio maana mnaweka nguvu kubwa majukwaani kuongeza wananchama? Halafu mkikosolewa mnaanza kutukana na kuita watu wengine wasaliti! Basi chama hiki kweli hakijajiandaa kuingia IKULU maana unapopanda Mahindi usitegemee kuvuna Mchele! kosa kubwa la Chadema ni kutojiandaa kushinda uchaguzi mkuu bali inashindana kupata wanachama wengi zaidi ya CCM.

Nachoweza kusema ni kwamba hata siku moja wanachama sii sehemu ya kuimarisha chama bali ni matunda ya nguvu kubwa ilotumika kuwaonyesha wananchi njia. Uongozi wa chama ni sawa na watu naloshika kandili ktk giza nene, hivyo sii maelekezo tu ya njia kwa sera na ilani bali unawapa wananchi mwanga wa kuona waendako.

Hao ACT watakuwa wajinga sana ikiwa watalenga kuwavuta wananchi kwa domo tindi na kukashifu vyama vingine maana watakuwa wamerudia makosa ya CDM ambao kwa fikra zao wanafikiri kuwa na wanachama wengi ndio mwanzo wa Ushindi. Wanachama ni sehemu ndogo sana ya wapiga kura a ushindi haupatikani ktk mikutano ya baraza kuu ama majukwaani bali ktk sanduku la KURA.

Binafsi yangu nina hakika ya kwamba maadam ushindi wa kura nchini hutokana na vote ya Popular, basi ni yule alokuwa Popular zaidi ya washindani wengine ndiye atakaye kuwa na nafasi zaidi ya ushindi ktk sanduku la kura. Na hili neno Maarufu halina uhusiano kabisa na wingi wa wanachama bali idadi ya watu wale waloshwishika kuwapa kura zao, hivyo sioni sababu yoyote nje ya siasa za majitaka ambazo inaweza kuniaminisha kwamba ACT ktk mikakati yao wanalenga kuchukua wanachama wa CDM, sasa wakisha wachukua ndio watakuwa wameshinda waani malengo yao ni kuwafilisi mtaji CDM!

Na kwa nini CDM wawe na wasiwasi ya kupoteza wanachama ikiwa chama hiki hakifanyi biashara maana wanachama ni kama mateja, wapo pale kukisaidia chama ktk michango ya fedha na nguvukazi, laa sivyo kama hawatumiwi vizuri basi chama hicho kitafilisika toka ndani kifedha na hata kikiwa na wanachama millioni 3 bado haitawasaidia kitu ktk sanduku la kura 2015.

Chadema, Chadema na uongozi wake acheni hizi habari za udaku na mipasho. Sisi wengine hatutakoma kutoa ushauri wetu japo siku hizi hatusikilizwi maana hatuko class moja, hatuna elimu kama nyie na wala sii kizazi kipya hivyo hatufai tena kushauri. Mnawatafuta wa hadhi sawa nanyi, sisi walalahoi tuko chini hatuyaoni ya juu lakini tu kumbukeni - Unapokwea mti, ni yule waliyeko chini ndiye huyaona mengi zaidi yaliyoko juu yako!. Na usiposikia yao watakusubiri chini maana mpanda mti lazima atashuka!

Asalaam Aleikum..
 
ni ukweli usiopingika kwamba tunahitaji siasa za kisasa zaidi na demokrasia ya ukweli na haki isiyoshawish juu ya mtu ama kundi ila inashawish kwa sera, na mwongozo wa chama huku ikilinda na kutetea katiba na maslahi ya raia wa nchi hii....
nguruvi 3 umechambua kwa umakini sana lakin naona umejikita zaid katika kukosoa sio jambo baya lakin ukasahau kutuonyesha aina za siasa tuzitakazo kwa unyumbulifu..

nafkiri mimi sio mtanzania pekee niliyechoshwa na utitiri wa wanasiasa ambao hawana tija kwa taifa zaid ya kujenga majina yao, kujineemesha na hata kutunyang'anya rasilimali zetu zikiwemo pesa zetu za michango mifukoni mwetu.

labda nafkiri kwa muda mrefu tumekuwa na amzoea ya kuona mmtu fulan ama kundi fulan can do something lkn sasa yatupasa kubadilika hasa pale ambapo mtu huyu ama kundi hilo tulilipa nafasi na likashindwa kutuonyesha ufanisi. umefika wakati ambao kwa sasa tunataka sera ambazo kiuhalisia zinatekelezeka na zinaboresha maisha na ustawi wa watu na nchi kwa ujumla.

hakuna haja ya kusema eti lazima ZZK awe mwenyekiti ama sijui nani hapana kwani kama kuna demokrasia ya kweli atagombea kwa kunadi sera zake na hapo ndipo tutakapojua nani anayetufaa na wanachama wataamua nani anafaa zaid basing on sera na experience yake.

kuna jambo ambalo mimi naliona kila siku kama tatizo kwa wanasiasa wetu nalo ni ni wazuri sana kwa kusema majukwaani lkn wazito sana kwa kutenda kivitendo, na hili halina mtu ambaye halimgusi anzia kwa serikali yenyewe hadi vyama vya upinzani.

kwa mfano kama kitila anaweza kuikosoa CCM kwa kutokuwa na demokrasia ya kweli, akasema chaguzi za NEC zimejaa rushwa na majina fulan kwanini leo hii naye atuletee chaguzi zilizojaa majina na pengine rushwa itatumiaka??

kw akufuata mifano ya wapinzani wetu sio CUF, ama NCCR-mageuzi, ama TLP ama CDM, kote utaona demokrasia hakuna wanachama wanalazimika kumchagua mwenyekiti kwa kufuata jina na kuna wengine wanaamin kwamba mtu fulan pekee ndiye anayefaa kuwa mwenyekiti hapa, sasa kwa makosa haya bado CCM anajiona mshindi kwamba bora hata mimi chaguzi zangu zinaanziaga ngazi ya mjumbe wa nyumba kumi na hata kwenye NEC huwa zinaonekana wazi kuliko wenzangu ambao wao chaguzi hufanywa chumban na watu wachache,,,,,,,,(nafkiri nitaeleweka vizuri hapa)

kama kweli tunataka vyama vya siasa vyenye upinzani wa kweli basi ni lazima vihakikishe kwanza
1) vina sera nzuri kuliko zilivyo za chama tawala

2) wanapractice demokrasia ya kweli na

3) sera zao zina uhalisia ndani yake kwamba zinatekelezeka na si kuwa maneno matamu yasiyotekelezeka milele mf. kusema chama kitafanya elimu ya msingi kuwa bure lazima wasema bure ipi manake kusema bure tu haitoshi na bure ziko nyingi inaweza ikamaanisha bure ya kutolipa ada lkn michango mingine ikawepo pale pale hivyo bure hapo haipo.
 
Chama chochote kinapoanzishwa waasisi wake wana fursa na uwezo wa kumchagua Mwenyekiti wao wa muda hadi hapo Uchaguzi mkuu utakapo fanyika. Chama kilipozaliwa nani alikuwa mwenyekiti wa muda? Mzee Mtei alipata kura za kina nani kuwa mwenyekiti! kabla ya Uchaguzi mkuu au kwa sababu yeye ndiye muasisi ana haki zote za kushika nyadhifa yoyote aitakayo!.. Mbona hatuanzi kujiuliza maswali haya sisi wenyewe tena kibaya zaidi hatuijui historia ya chama kwa undani wake ila kusema ya watu. Mbona CDM haiweki wazi historia ya chama mahala popote tukajua mzee Mtei na wanziwe walianzaje! Na je Inahusu kweli nikijua kwamba Mzee Mtei alijipachika cheo cha Uenyekiti basi chama hiki hakifai!.
 
Kwa muda mrefu sasa hofu ya Chadema imekuwa ndani ya chama. Wadhungu wanasema - Young chicken wil always come home to roost!

Mimi nawashangaa sana hawa vijana wetu ambao wanataka sana kutuaminisha kwamba Chama kinaweza kushinda uchaguzi kwa kuandikisha wananchama wengi. Hii watu mliitoa wapi? Je imani hii inatokana na kwamba CCM inawanachama wengi hivyo kuna uwezekano mkubwa kuwa hii ndio sababu ya ushindi wao?

Jamani jamani, sasa ACT ikichukua wanachama wa Chadema ndio itawafanyia nini? hawa watakiwezeshaje chama kiweze kushinda uchaguzi? na lini wanachama ndio wanahesabiwa ili kupata ushindi. Basi kama ingekuwa hivyo Arsenal na ManU wangechukua ubingwa wa kandanda miaka yote maana nijuavyo mimi wanachama au wapenzi hujiunga tu ikiwa chama chenyewe kimeonyesha ari, nia na uwezo mkubwa wa kukidhi matumaini yao wananchi.

Hata kama ACT itachukue wanachama wote wa CDM, ifahamike ni kwa sababu wananchi hao wamekosa imani ya chama hicho kama ilivyotokea kwa CCM ktk mikoa ya Mwanza na Arusha. Ni kazi ya CDM kuacha hizi za mipasho, kulaumu watu wengine mahala ambapo wao wenyewe wanalikoroga. CDM ya leo ni sawa na gazeti la NIpashe! na inasikitisha sana hata Ukumbi huu umekuwa wa mipasho na tunzi za kuuza magazeti. Hivi kweli mnataka tuamini kwamba vyama vya Upinzania vinagombania wananchama badala ya kuwajaza wananchi wapiga kura matumainiya maisha bora.

..
duh! mkuu wangu unanitia mashaka na ulinganisho wako wa team za mpira na wanachama wa vyama vya siasa, hapo ni kama maji na mafuta, mkuu wanachama wana mchango mkubwa sana kwenye vyama vya siasa, ndo hao mawakala, na ndo waeneza sera za chama,team za mpira ni burudani haifanani kamwe na maisha ya watu kwenye vyama vya siasa, ukisema ACT ikichukua wanachama wa chadema itawafanya nini jibu ni rahisi sana, hoja ya mkuu Nguruvi3 hapo juu kafafanua namna Mkumbo anavyoeleza mbadala wa CCM na CHADEMA, kwa maana miaka kumi kubomoa upinzani na miaka mingine kumi kujenga tena upinzani, mkuu binafsi naona kama umejivika makengeza kuhusu yale yanayojadiliwa hapa kuhusu ACT na badala yake umeamua kui'attack chadema, imekuaje tena mkuu?
 
Last edited by a moderator:
Chama chochote kinapoanzishwa waasisi wake wana fursa na uwezo wa kumchagua Mwenyekiti wao wa muda hadi hapo Uchaguzi mkuu utakapo fanyika. Chama kilipozaliwa nani alikuwa mwenyekiti wa muda? Mzee Mtei alipata kura za kina nani kuwa mwenyekiti! kabla ya Uchaguzi mkuu au kwa sababu yeye ndiye muasisi ana haki zote za kushika nyadhifa yoyote aitakayo!.. Mbona hatuanzi kujiuliza maswali haya sisi wenyewe tena kibaya zaidi hatuijui historia ya chama kwa undani wake ila kusema ya watu. Mbona CDM haiweki wazi historia ya chama mahala popote tukajua mzee Mtei na wanziwe walianzaje! Na je Inahusu kweli nikijua kwamba Mzee Mtei alijipachika cheo cha Uenyekiti basi chama hiki hakifai!.

mkuu Mkandara hapo ndipo mimi ninapopapinga hivi unaweza kufananisha pale CCM ilipoanzia na ilipoanzia CDM??

N i wazi kwamba huwez kulinganisha na likewise huwez kulinganisha pale CDM ilipoanzia na ilipoanzia ACT. kwanini nasema hivyo??

1) ufaham wa walio wengi kuhusu demokrasia haukuwa mkubwa kama ulivyo sasa.

2) uwazi na wenyewe haukuwepo kama ilivyo sasa

3) uhuru wa kushiriki siasa haukuwa mkubwa kama ulivyo sasa

kwasababu hizo hapo juu ni wazi kwamba kwa sasa tulitegema ACT iliyobora zaid kuliko chama chochote cha siasa nchini hapa akwasababu

1) wameshajifunza mengi kuhusu siasa za kileo

2) wanauelewa mpana zaid juu ya elimu ya demokrasia

3) wanayoexperience yakutosha kuhusu makosa ambayo yametendwa na vyama vingine vya siasa na hivyo kujitahd kuyakwepa kama sio kuyapunguza.

sina chuki na ACT wala mimi sina nia ya kuitetea CDM ila nataka kuonyesha tu kwamba lazima tukue kidemokrasia tuache kutenda mambo kwa mazoea. ACT naamini ingetoa upinzani mzuri zaid kama wangeyaelewa haya na kuyafanyia kazi ila wao wamekimbilia kwenye kutafuta uongozi kabla hata ya kuweka sera zao sawa.
 
Last edited by a moderator:
mkuu mkandala chama chochote cha siasa ni wanachama, na wanachama hufuata sera, (japo kwa hapa kwetu Tanzania wanachama ukiwauliza sera za vyama vyao, katika kumi mmoja ndo anaweza akakujibu, wengi hawajui, wengi hufuata mkumbo, wengi hufuata majina ya watu,wanasiasa wanatumia advantage hiyo ya wanaowaongoza kwa maslahi binafsi, ACT kuchukua wanachama wa CHADEMA sio dhambi, je walichokuwa wanakipigia makelele wakiwa chadema mbona ndicho wafanyacho wakiwa ACT? kama tatizo sio uenyekiti ni nini?
 
Last edited by a moderator:
duh! mkuu wangu unanitia mashaka na ulinganisho wako wa team za mpira na wanachama wa vyama vya siasa, hapo ni kama maji na mafuta, mkuu wanachama wana mchango mkubwa sana kwenye vyama vya siasa, ndo hao mawakala, na ndo waeneza sera za chama,team za mpira ni burudani haifanani kamwe na maisha ya watu kwenye vyama vya siasa, ukisema ACT ikichukua wanachama wa chadema itawafanya nini jibu ni rahisi sana, hoja ya mkuu Nguruvi3 hapo juu kafafanua namna Mkumbo anavyoeleza mbadala wa CCM na CHADEMA, kwa maana miaka kumi kubomoa upinzani na miaka mingine kumi kujenga tena upinzani, mkuu binafsi naona kama umejivika makengeza kuhusu yale yanayojadiliwa hapa kuhusu ACT na badala yake umeamua kui'attack chadema, imekuaje tena mkuu?
Sawa mkuu labda unifahamishe Yanga inaendeshwa na kina nani? ama hayo yoote ulosema kama ni mchango wa wanachama wa chama cha siasa huwezi kuyaona kwenye chama cha Mpira!
 
Back
Top Bottom