ni ukweli usiopingika kwamba tunahitaji siasa za kisasa zaidi na demokrasia ya ukweli na haki isiyoshawish juu ya mtu ama kundi ila inashawish kwa sera, na mwongozo wa chama huku ikilinda na kutetea katiba na maslahi ya raia wa nchi hii....
nguruvi 3 umechambua kwa umakini sana lakin naona umejikita zaid katika kukosoa sio jambo baya lakin ukasahau kutuonyesha aina za siasa tuzitakazo kwa unyumbulifu..
nafkiri mimi sio mtanzania pekee niliyechoshwa na utitiri wa wanasiasa ambao hawana tija kwa taifa zaid ya kujenga majina yao, kujineemesha na hata kutunyang'anya rasilimali zetu zikiwemo pesa zetu za michango mifukoni mwetu.
labda nafkiri kwa muda mrefu tumekuwa na amzoea ya kuona mmtu fulan ama kundi fulan can do something lkn sasa yatupasa kubadilika hasa pale ambapo mtu huyu ama kundi hilo tulilipa nafasi na likashindwa kutuonyesha ufanisi. umefika wakati ambao kwa sasa tunataka sera ambazo kiuhalisia zinatekelezeka na zinaboresha maisha na ustawi wa watu na nchi kwa ujumla.
hakuna haja ya kusema eti lazima ZZK awe mwenyekiti ama sijui nani hapana kwani kama kuna demokrasia ya kweli atagombea kwa kunadi sera zake na hapo ndipo tutakapojua nani anayetufaa na wanachama wataamua nani anafaa zaid basing on sera na experience yake.
kuna jambo ambalo mimi naliona kila siku kama tatizo kwa wanasiasa wetu nalo ni ni wazuri sana kwa kusema majukwaani lkn wazito sana kwa kutenda kivitendo, na hili halina mtu ambaye halimgusi anzia kwa serikali yenyewe hadi vyama vya upinzani.
kwa mfano kama kitila anaweza kuikosoa CCM kwa kutokuwa na demokrasia ya kweli, akasema chaguzi za NEC zimejaa rushwa na majina fulan kwanini leo hii naye atuletee chaguzi zilizojaa majina na pengine rushwa itatumiaka??
kw akufuata mifano ya wapinzani wetu sio CUF, ama NCCR-mageuzi, ama TLP ama CDM, kote utaona demokrasia hakuna wanachama wanalazimika kumchagua mwenyekiti kwa kufuata jina na kuna wengine wanaamin kwamba mtu fulan pekee ndiye anayefaa kuwa mwenyekiti hapa, sasa kwa makosa haya bado CCM anajiona mshindi kwamba bora hata mimi chaguzi zangu zinaanziaga ngazi ya mjumbe wa nyumba kumi na hata kwenye NEC huwa zinaonekana wazi kuliko wenzangu ambao wao chaguzi hufanywa chumban na watu wachache,,,,,,,,(nafkiri nitaeleweka vizuri hapa)
kama kweli tunataka vyama vya siasa vyenye upinzani wa kweli basi ni lazima vihakikishe kwanza
1) vina sera nzuri kuliko zilivyo za chama tawala
2) wanapractice demokrasia ya kweli na
3) sera zao zina uhalisia ndani yake kwamba zinatekelezeka na si kuwa maneno matamu yasiyotekelezeka milele mf. kusema chama kitafanya elimu ya msingi kuwa bure lazima wasema bure ipi manake kusema bure tu haitoshi na bure ziko nyingi inaweza ikamaanisha bure ya kutolipa ada lkn michango mingine ikawepo pale pale hivyo bure hapo haipo.