Mkandara,
Waberoya,
Zakumi,
Ritz,
Adharusi. Nawaombeni tuache siasa za kinafiki na kishabiki, nawaombeni msuze nyuso zenu zilizojaa masizi hivyo kutoweza kuona jinsi gani
Zitto ni tapeli na mlaghai mkubwa kwa wananchi. Tutafafanua hoja kwa hoja:
Katika uzinduzi wa ACT Wazalendo kufuatia ZItto na akina kitila mkumbo kuwapora watanzania wengine chama chao cha ACT Tanzania, Zitto alitamka kwamba amejiunga na chama cha ACT Wazalendo kwa kuwa chama hicho ndiyo chama pekee nchini kinachokubaliana na itikadi ya ujamaa na kinaamini katika falsafa ya Nyerere. Ndugu zangu, sijui kwanini hamtaki kukubali kwamba hakuna ukweli wowote katika kauli hizi za supreme leader zitto. Zitto analenga kutapeli na kudanganya umma kwa maslahi binafsi. Kwanza, Zitto sio mjamaa, na pili, hakuna jambo hata moja ambalo tunaweza kumfananisha Zitto na Mwalimu Nyerere. Hakuna! Kwa mfano:
· Tofauti na zitto, nyerere alikuwa na maono; zitto hana maono.
· Tofauti na zitto, nyerere hakuwa msaliti; zitto ni msaliti,
· Tofauti na zitto, nyerere alitenganisha maisha yake binafsi na uongozi; zitto anatumia uongozi wake kujikweza na kujinufaisha kibinafsi.
· Tofauti na zitto, kwa Mwalimu uongozi ulikuwa ni utumishi kwa wananchi, uongozi haukuwa ni kujikweza, kujinufaisha binafsi, na kujitafutia sifa kwa nguvu;
· Tofauti na zitto, Mwalimu hakuwa kujiingiza katika mgongano wa maslahi;
· Tofauti na Zitto, Mwalimu, aliweka taifa lake mbele kwanza;
· Tofauti na zitto, mwalimu hakuwahi kugonganisha wanachama wa chama chake cha CCM kwa maslahi ya watu wengine waliopo nje ya chama.
Tukiangalia hata kwa macho ya usingizi, ni rahisi sana kubaini kwamba hakuna ujamaa katika Zitto, na hakuna Azimio la Arusha katika ACT. Zitto ni tapeli na mlaghai mkubwa kwa wananchi. Cha ajabu ni kwamba hata nyinyi mmeamua kwa akili zenu timamu kabisa kujiunga na utapeli huu na ulaghai huu. Mnautetea usiku na mchana.
Tulitazame kwa undani kidogo Azimio la Arusha. Azimio la Arusha katika sehemu inayozungumzia viongozi linasema yafuatayo:
1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima aumfanyakazi na asishiriki katika jambo lo lote la kibepari au kikabaila.
· Je Zitto anatosha hapa? Kati ya ubepari na ujamaa, Zitto anaishi maisha ya namna gani zaidi?
2. Asiwe na hisa katika makampuni yo yote.
Je, zitto anatosha katika hili? Tusisahau sakata la Leka Tukige Limited na Gombe Advisors Limited.
3. Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au kibepari.
Rejea hoja ya hapo juu.
4. Asiwe na mishahara miwili au zaidi.
Je, zitto anatosha katika hili? Tusisahau ulaghai wake katika sakata la posho za wabunge. Vile vile, tusisahau jinsi gani ametuhumiwa kujinufaisha mara kwa mara na fedha za walipa kodi kupitia taasisi zilizokuwa chini ya kamati yake ya PAC, Tanapa na NSSF.
5. Asiwe na nyumba ya kupangisha.
Je anatosha katika hili?
6. Viongozi tunaofikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu
ya Taifa, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Vyama vilivyoshirikishwa na TANU, Wakuu wa Mashirika ya Kiserikali.
Je si yumo humu kama mbunge (aliyejiuzulu)?
Katika madhumuni, Azimio la Arusha linasema hivi:
·
Kuona kwamba Serikali inatoa nafasi zilizo sawa kwa wote,
wake kwa waume, bila kujali rangi, kabila, dini au hali.
·
Kuona kwamba Serikali inaondoa kila namna ya dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa na upotofu.
Katika haya, zitto hatoshi kwani akiwa ACT amekuwa mstari wa mbele kuwagawa watanzania kwa makabila yao na hali zao za maisha.
Kwanini tumuamini tapeli, laghai na mchonganishi Zitto kwa kumpa dhamana ya uongozi?
Tumeshuhudia jinsi gani Zitto amekuwa mstari wa mbele akihubiri siasa za kibaguzi.
Kwanini tufanye kosa la kumpa mtu hatari kama huyu dhamana ya uongozi?
Pia zitto ametuhumiwa kujipatia fedha kutoka TANAPA na NSSF kwa njia za rushwa na ujanja ujanja. Hajawahi kukanusha tuhuma hii kwa hoja,
Azimio la Arusha pia linasema haya kuhusiana na
Siasa ya Ujamaa, siasa ambayo Zitto analaghai wananchi kwamba yeye na ACT ndio inafuata misingi yake:
Katika nchi ya Ujamaa kamili mtu hamnyonyi mtu, bali kila awezaye kufanya kazi hufanya kazi, na kila mfanya kazi hupata pato la haki kwa kazi aifanyayo na wala mapato ya wafanyakazi mbali mbali hayapitani mno.
Hii ndio Tanzania ambayo tuliiona kupitia Azimio la Arusha, Tanzania ambayo Mwalimu alipigana usiku na mchana kuijenga kwa maslahi ya watanzania wote. Tofauti na hayo, tumeona jinsi gani Zitto amekuwa akilaghai watanzania kwa kuleta takwimu zilizojaa upotoshaji kwamba ipo baadhi ya mikoa ambayo inanyonya mikoa mingine. Kupitia takwimu za kodi ya mapato nchini, tumeona kwamba mikoa ambayo zitto amekuwa akiichonganisha na mikoa mingine kwa viel tu imepiga hatua kimaendeleo, kumbe ni mikoa ambayo imekuwa inapata mgao kutokana na jasho la wananchi wa mikoa hiyo (Makusanyo ya Kodi).
Azimio la arusha linazidi kulinda wananchi wa mikoa ya Kilimanjao na Arusha inayobaguliwa na ZItto pale linaposema kwamba:
MASHARTI YA MAENDELEO:
1. Juhudi:
Kila mwananchi anataka maendeleo, lakini si kila mwananchi
anaelewa na kukubali masharti ya maendeleo. Sharti moja
kubwa ni JUHUDI.
2. Maarifa:
Sharti la pili la maendeleo ni MAARIFA. Juhudi bila maarifa haiwezi
kutoa matunda bora kama juhudi na maarifa.
Nguruvi3 na wengine wamejadili suala hili kwa kina pale walipokuwa wanapingana na hoja za zitto za kuwabagua wananchi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro. Hoja ya msingi ya
Nguruvi3 katiak suala hili imekuwa kwamba maendeleo ya wananchi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ni matokeo ya juhudi na maarifa yao, kama jinsi azimio la arusha linavyoelekeza.
Tutazidi kuonyesha kwa hoja jinsi gani supreme leader Zitto ni tapeli na laghai wa kisiasa na kwamba, kama hatajirekebisha, basi huu ni wakati kwa watanzania kukaa mbali nae kama ukoma.