Katika hili siwezi kupinga kwamba chama hiki cha ACT chaweza kuwa ni Kitila na co. maana sina nilijualo wala ushahidi zaidi ya kkuelewa kilichotokea CDM na sasa ni yaleyale ya miaka yote toka kwa wanasiasa wetu. Hakuna jipya alofanya Kitila tofauti na alivyofanya Mtei, Mtrema ama Maalim Seif wote hawa walikuwa na sababu zao za kisiasa ndani ya chama walichokuwa mwanzo. Na hkuna demokrasia changa ikiwa muasisi anaelewa anatumia demokrasia kama kigezo cha kuanzisha chama na haijalishi umeanzisha mwaka gani kwani maana ya demokrasia haibadilki wala haitabadilika.Kaka yangu @Mkandara,
Kwa maelezo ya kaka yangu @Mchambuzi, kutoka kwa Katibu wa ACT ni dhahiri ya kuwa hiki ni chama cha Kitilya and Co. kwani kingekuwa chama wa wananchi basi kingepingania matatizo ya wananchi walao wapate haki zao ya msingi kama elimu,afya bora na nk. lakini hiki chama kimeanzishwa ili kueleza uchafu wa viongozi wa Chadema. Sasa kweli utasema hiki ni chama cha wananchi?
Binafsi yangu sioni chama chochote cjha Upinzani kilichioanzishwa kwa sababu hiyo zaidi ya viongozi wake kugombana na viongozi wa vyama walivyotoka hivyo basi Kitila hana tofauti na hao wengine zaidi ya kwamba hawachukii itikadi na sera za chama bali wana chuki na uongozi uliopo. Na hata Chadema kipo pale kueleza uchafu wa CCM na CUF kama tungekuwa wakweli ile vita ya CDM na CUF ingekuwa tofauti..Ni vita ile ilowapa CCM mtaji wa mwaka 2010 laa sivyo CCM ingeondoka madarakani toka mwaka huo. Laa jabu nini leo hii?
Maana yangu ni kwamba NCCR Mageuzi ni chama kilichoanzishwa na wanaharakati ambao kwa pamoja walikubaliana kuunda chama hiki na hata matatizo yake mara zote viongozi wamekubali kujitoa ama kustaafu baada ya kushindwa kutawala chama. Ni huko tu ambako sioni kiongozi anawatawala wanachama wake ama yuko juu ya kanuni za chama japokuwa leo hii chama hakina nguvu tena ya ushindani.Hapo kwenye blue sijakuelewa vizuri yaani demokrasia ya kweli ni kujitoa katika chama na kuanzisha chama kipya?
Mwanachama yeyote anapotoka katika chama chake cha awali na kuunda chama kipya kwa vyovyote vile kuna vitu hasivyokubaliana navyo ndani ya chama kile inawezekana hakubaliani na sera za chama chake au hakubaliani na viongozi wake wanavyotekeleza zile sera.. na kwa hilo mimi sina tatizo maana sio lazima sera za chama fulani zikubaliwe na kila mtu yule ambaye anaona kuna anaweza kufanya vizuri zaidi basi ni kujiondoa katika hicho chama na kuanzisha chama kingine.. hilo halina tatizo.. tatizo linakuja unapoanzisha chama kwa madhumuni ya kuua chama chako cha awali hapo lilipo tatizo...
Dada yangu unategemea kisichowezekana kabisa. Kama nilivyosema awali ya yote, kuwa hakuna chama cha Upinzani kilichoanzishwa kwa kutokubaliana na itikadi ama sera za chama tawala, hivyo sii rahisi kufikiria Usomi ndio muarobaini wa kuleta demokrasia nchini bali ni kukubali kutokubaliana kwa viongozi wetu. Huu ndio msingi wa demokrasia ya Tanzania na pengione nchi zote za kiafrika.Hapo ndugu yangu ninakipangana na wewe yaani kwa vile Mzee Mtei alianzisha chama kwenye miaka ya 90 na hakuitisha uchanguzi wa ndani basi kila chama kinachoanzishwa kifanya alivyofanya Mzee Mtei? Kwanini hawa viongozi wanaoanzisha vyama vipya wasije na mkakati mzuri zaidi na bora zaidi kwa kujifunza uanzishwaji wa vya vyama vipya kutoka ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania? Nini maana ya kuwa na wasomi katika vyama? Yaani hiki chama kimeanzishwa na wasomi tena ni wasomi haswa badala ya kuja na kitu kipya basi wanaendeleza vitu vile vile alivyofanya Mzee Mtei? kweli?..
Ninategemea wasomi kuwa wabunifu, kuja na mbinu mpya, mikakati mpya na huu ndio maana ya usomi, usomi sio cheti tu usomi ni pamoja na kuonyesha kwa vitendo ni jinsi gani unaweza kutumia elimu yako kujisaidia wewe mwenyewe na jamii iliyokuzunguka..
Jamani watanzania yatupasa kuwa wabunifu (nitoke nje ya mada kidogo) Mfn Sisi watanzania ubunifu ni msamiati mkubwa sana kwetu, yaani unakuta vitu vilivyobuniwa na mababu yetu ndio tulivyanavyo mpaka leo mfn Mkoani Mwanza ni wakulima wa mahindi, katika mahindi unaweza kupika ugali au kukoroga uji, tangu enzi ya mababu zetu process ni zile zile, kupanda, kuvuna , kusanga mahindi, kupika ugali au kukoroga uji hakuna zaidi ya hapo.. hakuna msomi anaye take risk kusema let us try this labda kutengeneza mkate wa mahindi,au kutengeza spharghetti za mahidi na nk.. Hakuna, wasomi wetu wako kurundika na maisha yanaendelea......
Tena niseme hivi, hao wasomi ndio wabaya zaidi maana ubishi wao sii wa kiitikadi bali hutokana na nafasi zao ktk uongozi hutokana na elimu zao kuwa zaidi ya wale walokuwa juu yao ama umaarufu wao. Kama kina Mtei, Mrema na Maalim Seif walianza hivyo unategemea nini kutoka kwa vijana wake, kama leo vyama vyote vinaikubali itikadi ya CCM, wanakubali mrengo wa CCM na hata katiba yao ila wanapingana na CCM ktk utekelezaji wake, uongozi wake, fitna zao, Ufisadi na mabaya yote ya mtumwa kupewa Unyapala unategemea kweli tutapata chama kinachosimamia itikadi tofauti?. Hivi kweli huoni kuwa uongozi Tanzania sio dhamana ila ni Ubwana nasi ni waja wake! ni sawa na mfungwa mmoja alopewa Unyapala kulinda wafungwa wenzake!Siasa zetu ni za Kiimla tupende tusipende toka majumbani, makanisani, misikitini hadi ktk siasa.
Sisi wenyewe hatuna tofauti sana za kiitikad, asilimia 90 ni wajamaa hadi leo ila hatujui mfumo mzima wa itikadi zaidi ya kwamba Conservative ni wahafidhina wasiotaka mabadiliko.. Je, ni manadiliko gani ya Kiitikadi ambayo ndio chanzo cha Utanzania? bila shaka tutasema ni UJamaa wa mwafirka (tafsiri ya Mwalimu), je kweli kuna chama kinachoshikilia Uhafidhina huo nchini wasitake mabadiliko ya Ujamaa wa mwafrika? sidhani kama kipo! na ajabu ni kwamba Uhafidhina wetu ni viongozxi wasiotaka kuachia madaraka,
Uhafidhina wetu ni kutazama mfumo wa nchi za magharibi ambao ulitokana na Ukristu hivyo hawakubali kubadilika na kuacha imani ya dini zao nje ya siasa lakini kweru kila chama hakina dini, mila wala utamaduni,vyama vyote vinapinga Ushoga ama mabadiliko ya tamaduni zetu japo utamaduni huio hawana. Kwa mtazamo huo CUF wanaweza kuwa Wahafidhina kwa maana ya kusimamia Uzawa na Uislaam huko visiwani lakini wao wanajiita Leberali sasa ni liberali wa itikadi gani? Je, wanaukubali ushoga ama mabadiliko gani ya tamaduni zetu - haijulikani, ila ni kwa uhakika CUF ni wapinzani wa CCM kutokana na historia ya Mwalimu sii siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.
Na kuhusu wasomi wetu hakika walisoma ii wapate AJILA na wanaendelea kusoma kwa malengo hayo hayo hivyo msomi kwetu ni yule alosoma University (Academic) na sii Chuoni (Practical) kwa sababu hatuelewi kuwa ELIMU ni mwanga wa kutuonyesha tunapokwenda maana ktk dunia hii pasipo elimu basi upo kizani. Hivyo elimu ni sawa na mtu alobeba tochi kizani, hii haina maana ndiye huijua njia! tuna safari ndefu sana kama tutategemea wasomi wetu badala ya kutazama mahitaji yetu na jinsi gani tunaweza kuwa wabunifu ili kutosheleza mahitaji hayo.
Majuzi tu nilikuwa nazungfumzia swala la vyoo vya kuchuchumaa maana sisi wengine magoti kwisheni, napokuta choo cha shimo ama kihindi mahala popote kila kitu hufunga!...lakini ajabu ni kwamba Udongo wa mfinyanzi ukichanganywa na Nilu (special material ya kuparaza kuta) tunaweza jenga vyoo vya kisasa kabisa vya kukaa pasipo kuagiza toka China. Hata iwe udongo wa mfinyanzi tu tunaweza jenga vyoo vyetu maana tunaweza kujenga vyungu na mutungi ya maji ambayo haina soko tena. Sasa habari hii kweli nayo inahitajki msomi wa Chuo kikuu kutambua kwamba vyoo vya kisasa vinaweza kuwapata soko kubwa hapa nchini?