Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Kaka yangu @Mkandara,
Kwa maelezo ya kaka yangu @Mchambuzi, kutoka kwa Katibu wa ACT ni dhahiri ya kuwa hiki ni chama cha Kitilya and Co. kwani kingekuwa chama wa wananchi basi kingepingania matatizo ya wananchi walao wapate haki zao ya msingi kama elimu,afya bora na nk. lakini hiki chama kimeanzishwa ili kueleza uchafu wa viongozi wa Chadema. Sasa kweli utasema hiki ni chama cha wananchi?
Katika hili siwezi kupinga kwamba chama hiki cha ACT chaweza kuwa ni Kitila na co. maana sina nilijualo wala ushahidi zaidi ya kkuelewa kilichotokea CDM na sasa ni yaleyale ya miaka yote toka kwa wanasiasa wetu. Hakuna jipya alofanya Kitila tofauti na alivyofanya Mtei, Mtrema ama Maalim Seif wote hawa walikuwa na sababu zao za kisiasa ndani ya chama walichokuwa mwanzo. Na hkuna demokrasia changa ikiwa muasisi anaelewa anatumia demokrasia kama kigezo cha kuanzisha chama na haijalishi umeanzisha mwaka gani kwani maana ya demokrasia haibadilki wala haitabadilika.

Binafsi yangu sioni chama chochote cjha Upinzani kilichioanzishwa kwa sababu hiyo zaidi ya viongozi wake kugombana na viongozi wa vyama walivyotoka hivyo basi Kitila hana tofauti na hao wengine zaidi ya kwamba hawachukii itikadi na sera za chama bali wana chuki na uongozi uliopo. Na hata Chadema kipo pale kueleza uchafu wa CCM na CUF kama tungekuwa wakweli ile vita ya CDM na CUF ingekuwa tofauti..Ni vita ile ilowapa CCM mtaji wa mwaka 2010 laa sivyo CCM ingeondoka madarakani toka mwaka huo. Laa jabu nini leo hii?

Hapo kwenye blue sijakuelewa vizuri yaani demokrasia ya kweli ni kujitoa katika chama na kuanzisha chama kipya?
Mwanachama yeyote anapotoka katika chama chake cha awali na kuunda chama kipya kwa vyovyote vile kuna vitu hasivyokubaliana navyo ndani ya chama kile inawezekana hakubaliani na sera za chama chake au hakubaliani na viongozi wake wanavyotekeleza zile sera.. na kwa hilo mimi sina tatizo maana sio lazima sera za chama fulani zikubaliwe na kila mtu yule ambaye anaona kuna anaweza kufanya vizuri zaidi basi ni kujiondoa katika hicho chama na kuanzisha chama kingine.. hilo halina tatizo.. tatizo linakuja unapoanzisha chama kwa madhumuni ya kuua chama chako cha awali hapo lilipo tatizo...
Maana yangu ni kwamba NCCR Mageuzi ni chama kilichoanzishwa na wanaharakati ambao kwa pamoja walikubaliana kuunda chama hiki na hata matatizo yake mara zote viongozi wamekubali kujitoa ama kustaafu baada ya kushindwa kutawala chama. Ni huko tu ambako sioni kiongozi anawatawala wanachama wake ama yuko juu ya kanuni za chama japokuwa leo hii chama hakina nguvu tena ya ushindani.
Hapo ndugu yangu ninakipangana na wewe yaani kwa vile Mzee Mtei alianzisha chama kwenye miaka ya 90 na hakuitisha uchanguzi wa ndani basi kila chama kinachoanzishwa kifanya alivyofanya Mzee Mtei? Kwanini hawa viongozi wanaoanzisha vyama vipya wasije na mkakati mzuri zaidi na bora zaidi kwa kujifunza uanzishwaji wa vya vyama vipya kutoka ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania? Nini maana ya kuwa na wasomi katika vyama? Yaani hiki chama kimeanzishwa na wasomi tena ni wasomi haswa badala ya kuja na kitu kipya basi wanaendeleza vitu vile vile alivyofanya Mzee Mtei? kweli?..

Ninategemea wasomi kuwa wabunifu, kuja na mbinu mpya, mikakati mpya na huu ndio maana ya usomi, usomi sio cheti tu usomi ni pamoja na kuonyesha kwa vitendo ni jinsi gani unaweza kutumia elimu yako kujisaidia wewe mwenyewe na jamii iliyokuzunguka..

Jamani watanzania yatupasa kuwa wabunifu (nitoke nje ya mada kidogo) Mfn Sisi watanzania ubunifu ni msamiati mkubwa sana kwetu, yaani unakuta vitu vilivyobuniwa na mababu yetu ndio tulivyanavyo mpaka leo mfn Mkoani Mwanza ni wakulima wa mahindi, katika mahindi unaweza kupika ugali au kukoroga uji, tangu enzi ya mababu zetu process ni zile zile, kupanda, kuvuna , kusanga mahindi, kupika ugali au kukoroga uji hakuna zaidi ya hapo.. hakuna msomi anaye take risk kusema let us try this labda kutengeneza mkate wa mahindi,au kutengeza spharghetti za mahidi na nk.. Hakuna, wasomi wetu wako kurundika na maisha yanaendelea......
Dada yangu unategemea kisichowezekana kabisa. Kama nilivyosema awali ya yote, kuwa hakuna chama cha Upinzani kilichoanzishwa kwa kutokubaliana na itikadi ama sera za chama tawala, hivyo sii rahisi kufikiria Usomi ndio muarobaini wa kuleta demokrasia nchini bali ni kukubali kutokubaliana kwa viongozi wetu. Huu ndio msingi wa demokrasia ya Tanzania na pengione nchi zote za kiafrika.

Tena niseme hivi, hao wasomi ndio wabaya zaidi maana ubishi wao sii wa kiitikadi bali hutokana na nafasi zao ktk uongozi hutokana na elimu zao kuwa zaidi ya wale walokuwa juu yao ama umaarufu wao. Kama kina Mtei, Mrema na Maalim Seif walianza hivyo unategemea nini kutoka kwa vijana wake, kama leo vyama vyote vinaikubali itikadi ya CCM, wanakubali mrengo wa CCM na hata katiba yao ila wanapingana na CCM ktk utekelezaji wake, uongozi wake, fitna zao, Ufisadi na mabaya yote ya mtumwa kupewa Unyapala unategemea kweli tutapata chama kinachosimamia itikadi tofauti?. Hivi kweli huoni kuwa uongozi Tanzania sio dhamana ila ni Ubwana nasi ni waja wake! ni sawa na mfungwa mmoja alopewa Unyapala kulinda wafungwa wenzake!Siasa zetu ni za Kiimla tupende tusipende toka majumbani, makanisani, misikitini hadi ktk siasa.

Sisi wenyewe hatuna tofauti sana za kiitikad, asilimia 90 ni wajamaa hadi leo ila hatujui mfumo mzima wa itikadi zaidi ya kwamba Conservative ni wahafidhina wasiotaka mabadiliko.. Je, ni manadiliko gani ya Kiitikadi ambayo ndio chanzo cha Utanzania? bila shaka tutasema ni UJamaa wa mwafirka (tafsiri ya Mwalimu), je kweli kuna chama kinachoshikilia Uhafidhina huo nchini wasitake mabadiliko ya Ujamaa wa mwafrika? sidhani kama kipo! na ajabu ni kwamba Uhafidhina wetu ni viongozxi wasiotaka kuachia madaraka,

Uhafidhina wetu ni kutazama mfumo wa nchi za magharibi ambao ulitokana na Ukristu hivyo hawakubali kubadilika na kuacha imani ya dini zao nje ya siasa lakini kweru kila chama hakina dini, mila wala utamaduni,vyama vyote vinapinga Ushoga ama mabadiliko ya tamaduni zetu japo utamaduni huio hawana. Kwa mtazamo huo CUF wanaweza kuwa Wahafidhina kwa maana ya kusimamia Uzawa na Uislaam huko visiwani lakini wao wanajiita Leberali sasa ni liberali wa itikadi gani? Je, wanaukubali ushoga ama mabadiliko gani ya tamaduni zetu - haijulikani, ila ni kwa uhakika CUF ni wapinzani wa CCM kutokana na historia ya Mwalimu sii siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.

Na kuhusu wasomi wetu hakika walisoma ii wapate AJILA na wanaendelea kusoma kwa malengo hayo hayo hivyo msomi kwetu ni yule alosoma University (Academic) na sii Chuoni (Practical) kwa sababu hatuelewi kuwa ELIMU ni mwanga wa kutuonyesha tunapokwenda maana ktk dunia hii pasipo elimu basi upo kizani. Hivyo elimu ni sawa na mtu alobeba tochi kizani, hii haina maana ndiye huijua njia! tuna safari ndefu sana kama tutategemea wasomi wetu badala ya kutazama mahitaji yetu na jinsi gani tunaweza kuwa wabunifu ili kutosheleza mahitaji hayo.

Majuzi tu nilikuwa nazungfumzia swala la vyoo vya kuchuchumaa maana sisi wengine magoti kwisheni, napokuta choo cha shimo ama kihindi mahala popote kila kitu hufunga!...lakini ajabu ni kwamba Udongo wa mfinyanzi ukichanganywa na Nilu (special material ya kuparaza kuta) tunaweza jenga vyoo vya kisasa kabisa vya kukaa pasipo kuagiza toka China. Hata iwe udongo wa mfinyanzi tu tunaweza jenga vyoo vyetu maana tunaweza kujenga vyungu na mutungi ya maji ambayo haina soko tena. Sasa habari hii kweli nayo inahitajki msomi wa Chuo kikuu kutambua kwamba vyoo vya kisasa vinaweza kuwapata soko kubwa hapa nchini?
 
Wanajamvi, katika kuufuatilia huu mjadala, hizi nukuu za Mkuu mkandala zimeniacha hoi; hakika simuelewi kabisa huyu GT kama yuko serious ama anatania tu.
Mkandara said:
Kila nchi inaunda katiba yake pasipo wananchi wake kufahamu yaliyomo.
Kweli?
Mkandara said:
Ilisemakana kwamba Chadema iliasisiwa kuivunja CUF na watu wakaamini hivyo hadi pale CDM na CUF walipoungana nguvu.
Sina hakika kipi chama kilitangulia kusajiliwa kati ya CUF na Chadema mwaka 1992!
Mkandara said:
Ni NCCR Mageuzi tu ambayo kidogo imeonyesha demokrasia ya kweli nayo imetokana na viongozi wake waasisi kujitoa moja baada ya mwingine ili kuanzisha chama kipya.
Ninavyojua Mrema hakuwahi kuwa muasisi wa NCCR; alikuja kudandia tu mwaka 1995 akitokea CCM...
Mkandara said:
Kitila hajafanya kosa lolote zaidi ya sisi kuonyesha jinsi tunavyohaha na ujio wa ACT kama ilivyokuwa kwa wanachama wa CCM pale iliposikika CCJ imesajiliwa.
Ninavyoelewa makosa ya Kitila ni mawili;

  1. Kupanga njama za kupindua uongozi halali wa Chadema.
  2. Kutaka kumsimika uongozi ACT mtu asiye mwanachama.
Mkandara said:
Hakuna jipya alofanya Kitila tofauti na alivyofanya Mtei, Mrema ama Maalim Seif wote hawa walikuwa na sababu zao za kisiasa ndani ya chama walichokuwa mwanzo.
Hapana, hawa hawakuwahi kupanga mapinduzi ndani ya CCM; walijiondokea tu....
Mkandara said:
Kama nilivyosema awali ya yote, kuwa hakuna chama cha Upinzani kilichoanzishwa kwa kutokubaliana na itikadi ama sera za chama tawala,
Kweli hayo?
Mkandara said:
elimu ni sawa na mtu alobeba tochi kizani, hii haina maana ndiye huijua njia!
Duh! kwa mara ya kwanza naisikia hii!
Mkandara said:
tuna safari ndefu sana kama tutategemea wasomi wetu badala ya kutazama mahitaji yetu na jinsi gani tunaweza kuwa wabunifu ili kutosheleza mahitaji hayo.
Wow, ubunifu bila elimu! This is but a tall order!
hivyo si rahisi kufikiria Usomi ndio muarobaini wa kuleta demokrasia nchini bali ni kukubali kutokubaliana kwa viongozi wetu.
Kwa kweli, watu tunatofautiana kimtizamo.
 
Sheria yoyote ama kanuni husimamma haijalishi ufahamu wa wananchi.
Kama unaamini ktk Demokrasia ni lazima misingi inayojenga Demokrasioa ifuatwe laa sivyo hakuna demokrasia.

Nilivyowasoma mwanzo mnaonyesha wazi kwamba unapounda chama muasisi hawezi kumteua ama kumchagua mtu ashike mamlaka ya Uenyekiti pasipo kupitia uchaguzi.

Hizo sababu nasema hazina maana kabisa kwani Watanzania wana experience kubwa sana ya kuunda vyama toka TAA, ASP, TANU hadi CCM na mfumo huo wa uchaguzi ndani ya chama haujabalika iwe ndani ya demokrasia ama nje.
Mwanzo una tofauti kubwa sana ya uchaguzi wa viongozi waa chama na baada ya kujiweka sawa!

Kifupi ni kwamba chama chochote kinapozaliwa kina ruksa ya kuchagua mwenyekiti wake wa muda iwe kwa kuteuliwa kupendekezwa na waasisi wenyewe. Kitila hajafanya kosa lolote!
Aya ya kwanza unakubali kuwa misingi ya demokrasia lazima ifuatwe.
Nakubaliana nawe kabisa. Tuendelee

Aya ya pili, nakubaliana nawe unaweza kuwa na uongozi wa kuteua au kuteuliwa wakati taratibu zingine zikiendelea.Msemaji wa ACT alisema hayo na wala hakuna aliyehoji tukijua wanaandaa katiba na taratibu za muda.

Aya ya tatu, hapo ndipo kosa lilipo na si kosa ndipo ignorance ilipo the least to say.
Kitila anajua chama chake ni cha uwazi.

Anafahamu alivyoshirikiana na ZZK katika waraka. Amekiri kuwa na mfanano wa maono ya kisiasa. Kitendo cha kusema anamshawishi ZZK ajiunge na ACT ilikuwa kulaghai umma, in fact alikuwa anashawishi wafuasi kumfuata ZZK.
Hilo nalo halina tatizo, shida iliyopo ni kukiuka kauli mbiu ya uwazi kwa kubadilisha uwazi na unafiki. Shida ni kutaka kutufanya sote mazuzu kama wale wanavyolishwa kofia au pilau.
Tofauti ya Kitila na Mwigulu ni skafu.

Kosa la pili la Kitila, ZZK ni mwanachama wa CDM. Yeye amejiunga ACT tu siku hiyo na siku hiyo hiyo akamteua ZZK. Hivi hapo kuna logic au element ya uwazi, ukweli au usomi.
Ni kutokana na hilo, hoja ya kuteua viongozi wa muda unayosema Mkandara haina mashiko.

Kitila alijiunga siku hiyo na hawezi kumteua mwenyekiti anayemjua yeye.
Kilichotakiwa ni kutoa tamko kwa niaba ya kamati ya muda ya kumshawishi Zitto afanye haya
1. Afunge kesi mahakamani
2. Ajivue uanachama wa CDM
3. Aombe kujiunga na ACT

Sasa kama wanampokea akiwa mwenyekiti hilo halina tatizo.
Kitendo cha Kitila kuchukua kadi na kuja na mwenyekiti wake wa mfukoni hakifuati misingi ya demokrasia kama aya ya kwanza inavyosema, hakifuati utaratibu wa kupata uongozi wa muda kama aya namba mbili inavyosema, hakilingani na kauli mbiu ya uwazi.

Mbaya zaidi kile walichokilaani katika WARAKA ndicho wanakitekeleza kupitia ACT.
Unafiki huu hadi lini.

Ubabe, kutofuata demokrasia, kukosa maono na akili ndogo waliyoilaani katika waraka inaonekana sasa wanaitekeleza practically.

Mkuu, spedi iitwe spedi na si kijiko kikubwa.
Huu mbadala wanaosema hakuna, mbadala ni Kitila kuamini kuwa hakuna siasa nchi hii kama Zitto si mwenyekiti. Ni kitila kuamini tatizo la Tanzania ni wapinzani na si CCM.
Ni kitila kutumika kama mpini wa CCM kwa kujua au kutojua.

Tungempa benefit of doubt kama angekuwa gula gula, kwa usomi wake this is lowest point of his political career.

Mimi sina hofu na ACT kwasababu sina upenzi wa vyama.
I take them on kila wanapobofoa. This time ni ACT ambao wameanza kwa mguu mbovu na kuondoa hata matumaini yaliyokuwepo ya kubadili siasa za nchi hii.

Kitila na ACT ni disappointment kubwa ya quater ya kwanza ya mwaka 2014.

Mag3
Kitila amekuja na mwenyekiti wake mfukoni, Mkandara anasema hiyo ni demokrasia. Kumbu kumbu zinaonyesha wakati wa Waraka Mkandara alilaani sana kupindishwa kwa demokrasia na kushabikia maasi ya waraka.
Kama kawaida, mkuu Mkandara anageuza tu, hakuna indicator au honi. Angeuza gari li fit anapotaka ku park.
 
Nilikiri toka mwanzoni kabisa kuwa napata taabu sana kujadiliana na mtu kama Mkandara; sababu ni kwamba ana porojo nyingi hadi mtu unashindwa kujua anatetea nini wala kusimamia nini! Leo kaingiza na ujenzi wa choo (ha ha haa!), sijui kesho atakwea tawi gani! Uzuri wa JF ni kwamba inatupa fursa ya kuichunguza kokoro; je kilichomo ndicho tulidhamiria kukivua? Kutetea kitendo cha Kitila and company na kukiita cha kidemokrasia ni sawa na kusema demokrasia ni free for all; haina sheria, kanuni wala taratibu. Kwamba kiongozi yeyote hata kama itadhihirika anazo njama za kukihujumu chama hiyo ni rukhsa, hata kama itagundulika kwamba anakisaliti chama rukhsa na hata kama kwa vitendo vyake anakidhoofisha chama rukhsa. Kwa Mkandara, hiyo ndiyo demokrasia! Wakati chama kiko kwenye kampeni kubwa ya ubunge, kiongozi mojawapo anaanzisha mapambano dhidi ya uongozi uliopo madarakani...hiyo ndiyo demokrasia!

Kwa sasa Zitto kafungua kesi mahakamani akipinga hatua zilizochukuliwa na uongozi wa Chadema dhidi yake na hapo hapo Luteni wake Mkuu anaanzisha chama kipya na kumpendekeza (kumsimika?) kama kiongozi wake mtarajiwa. Je huyo Zitto anasubiri nini kufuta kesi mahakamani ili aweze kujiunga na kuwaongoza watu wake wanaomsubiri kwa hamu, shauku na tumaini kubwa? Je itakuwaje akishinda kesi? Je, kama kesi yake itatupiliwa mbali, yuko tayari kufungasha virago na kuweka kambi ACT au hatoki mtu hadi Chadema imesambaratika kulingana na tabiri za Wassira and company? Hivi sasa kila mwana CCM anakiombea Chadema kifo; is this incidence, coincidence or enemy action? Mkandara alikubaliana na waraka wa Mwigamba 100% na kukiita kitendo chao (genge la MM, M1, M2, M3) cha kidemokrasia! Kwamba Chadema ilitakiwa iwaache tu waendelee na mipango yao ya siri dhidi ya uongozi halali wa Chadema, naam ndiyo demokrasia!
 
Watu hawajui sawasawa lakini kosa pekee alilotuachia Nyerere ni hili la siasa. Watu wamekuwa wanamlalamikia vitu visivyo kweli. Nyerere alikuwa na utaifa, hakuwa mtu rushwa, mkabila au mdini kama watu wanavohubiri hapa. Alilipenda sana taifa hili aliloasisi na sera zake nyingi zilikuwa zinalenga kuneemsha taifa siyo kujineemesha yeye au familia yake. Alipokosea ni pale tu alipoleta hicho kilichoitwa "CHAMA KUSHIKA HATAMU"; hilo ndilo kosa pekee tutakaloandamana nalo miaka nenda rudi.

Hiyo sera ya Chama kushika hatamu iliwajenga maafisa wa jeshi, maafisa wa polisi, mahakimu na watumishi wa serikali kuwa watumishi wa chama. Kama tunavyoelewa, jambo hilo halijfutika kabisa vichwani mwa makamanda wetu wa polisi na wa jeshi la wananchi, ingawa limekuwa linafutika taratibu kutoka vichwani mwa mahakimu wetu. Wale watumishi wa serikali (Civil Servants) ndiyo basi kabisa, utadhani kuwa wao ni waajiriwa wa CCM. Ili waipinge CCM hulazimika kufanya hivyo mafichoni.

Sasa sera hiyo hiyo ya chama kushika hatamu ya wakati huo imeendelea kubaki vichwani mwa wanasiasa wetu wote hata wale waliozaliwa baada ya Nyerere kutoka madarakani. Wanataka siasa za vyama kwa ajili ya utamu wa kushika hatamu tu, siyo kwa sababu ya nchi hata siku moja.
 
Mkuu Kichuguu
Hilo la kushika hatamu nakubali ni tatizo na hakika linatutesa. Kwa upande wa CCM limekubalika si kwa hiari bali kwa mazingira. CCM imetekwa na kundi la wenye nguvu, watu wanaoweza kumtisha mwenyekiti abadili msimamo na ikawa hivyo.
Case study ni suala la katiba mpya.

Nipo katika kumbu kumbu kuwaeleza CUF kuwa chama kinajengwa kwa sera na si sura.
Nilionya kuwa CUF ni Maalim Seif na siku ikiingia dosari chama kinasabaratika. Ndivyo ilivyo kwa sasa.

Nipo katika kumbu kumbu nikiwaambia Chadema, chama chao kijengwe kwa sera na watu mbali mbali wa kuuza hizo sera na si sura za watu. Nilionya kuwa kumtegemea Dr Slaa au Zitto kuna tatizo mbele ya safari kwasababu chama kitakuwa sura na si sera.
Sipo mbali na ukweli ulivyo.

Hawa ACT ni tawi meguka la CDM. Ugomvi wao wa Waraka ilikuwa kutafuta nafasi ya ZZK kushika hatamu na wala haikuwa tofauti za sera. Ilikuwa ni more sura than sera.

Haionekani ACT kama wanajifunza, kwasababu walichokikataa walikotoka ndicho wanakipia debe.
Kwamba, chama hicho hata kabla ya kuuza sera kinaona umuhimu wa kuuza sura.
Ndipo anaingia Dr Kitila akimtaka mwenyekiti ambaye ni mwanachama wa chama kingine.

Kikubwa zaidi ni ulaghai,kutufanya mazuzu kana kwamba hatujui nini kinaendelea.
Nako huko kilichopo mbeleni ni sura na si sera.

Yes, matatizo yametokea huko nyuma, kuendelea kukaa kimya si kutendea haki kizazi kinachokuja.
Ni lazima tusimame na kukemea kwa nguvu zote ulaghai wa kisiasa ''at the political expediency of the people''

Watu wanapoanzisha chama ili kupata mwenyekiti wanayemtaka, is very unfortunate.
Na juzi katibu mkuu wao wa ACT kasema, chama kimeanzishwa kuua upinzani.
Kwamba hakiwezi kutangaza sera za kupambana na nyangumi anAyetumaliza 50 yrs bali ujio wake ni kumaliza upinzani.

Hii maana yake ni moja, wanachotaka ni kushika hatamu.
Hapana! siasa za kushika hatamu hazikubaliki, Siasa ni sera hivyo waeleze sera zao na si sera za kuua upinzani.
Wataua upinzani, then so what! NCCR ilikufa, taifa lilipata nini. The same to CUF.

Naiangalia ACT sioni tofauti na TLP ambayo wanachama walifuata mtu na si sera. Disaster !
 
Nilikiri toka mwanzoni kabisa kuwa napata taabu sana kujadiliana na mtu kama Mkandara; sababu ni kwamba ana porojo nyingi hadi mtu unashindwa kujua anatetea nini wala kusimamia nini! Leo kaingiza na ujenzi wa choo (ha ha haa!), sijui kesho atakwea tawi gani! Uzuri wa JF ni kwamba inatupa fursa ya kuichunguza kokoro; je kilichomo ndicho tulidhamiria kukivua? Kutetea kitendo cha Kitila and company na kukiita cha kidemokrasia ni sawa na kusema demokrasia ni free for all; haina sheria, kanuni wala taratibu. Kwamba kiongozi yeyote hata kama itadhihirika anazo njama za kukihujumu chama hiyo ni rukhsa, hata kama itagundulika kwamba anakisaliti chama rukhsa na hata kama kwa vitendo vyake anakidhoofisha chama rukhsa. Kwa Mkandara, hiyo ndiyo demokrasia! Wakati chama kiko kwenye kampeni kubwa ya ubunge, kiongozi mojawapo anaanzisha mapambano dhidi ya uongozi uliopo madarakani...hiyo ndiyo demokrasia!

Kwa sasa Zitto kafungua kesi mahakamani akipinga hatua zilizochukuliwa na uongozi wa Chadema dhidi yake na hapo hapo Luteni wake Mkuu anaanzisha chama kipya na kumpendekeza (kumsimika?) kama kiongozi wake mtarajiwa. Je huyo Zitto anasubiri nini kufuta kesi mahakamani ili aweze kujiunga na kuwaongoza watu wake wanaomsubiri kwa hamu, shauku na tumaini kubwa? Je itakuwaje akishinda kesi? Je, kama kesi yake itatupiliwa mbali, yuko tayari kufungasha virago na kuweka kambi ACT au hatoki mtu hadi Chadema imesambaratika kulingana na tabiri za Wassira and company? Hivi sasa kila mwana CCM anakiombea Chadema kifo; is this incidence, coincidence or enemy action? Mkandara alikubaliana na waraka wa Mwigamba 100% na kukiita kitendo chao (genge la MM, M1, M2, M3) cha kidemokrasia! Kwamba Chadema ilitakiwa iwaache tu waendelee na mipango yao ya siri dhidi ya uongozi halali wa Chadema, naam ndiyo demokrasia!
Mkuu huwezi kunielewa kwa sababu unasioma tu maandishi yangu pasipo kufuatilia mjadala. Haya ya choo nimeyazungumza kutokana na mfano wa bibie sasa kama wewe hukumsoma yeye itakuuwia vigumu kunifuata. Na labda nikwambie tu ya kwamba mimi hujibu ama huandika hoja zangu tokana na mtu aloelekeza swali, hoja ama mifano kwangu na pengine kutaka mchango wangu.

Na kisha hutaweza kunielewa kwa sababu unatengemea mimi nisimame a chama iwe Chadema au CCm au ACT na kuutetea upande huo, mimi siko hivyo natazama maslahi ya nchi mbee ya vyama hivyo wakivurunda hata Chadema nawatoa nishai sina mapenzi na chama wala viongozi ila naamini ktk mrengo ambao unaweza kuwaondoa wananchi toka ktk umaskini hivyo nguvu yoyote inayotumika kuwatazama WAKULIMA na WAFANYAKAZI kwanza ndio msingi wa argument zangu, maslahi binafsi hana nafasi kwangu.

Kuna mahala umeandika kwamba nimesema kila nchi huandaa Katiba yake bila wananchi wake kufahamu yaliyomo. Sidhani kama umenielewa aama unaelewa maana ya Kuandaa. Nijuavyo mimi hata katiba byetu ya mwaka 1967, 77 ilivyoandialiwa hatukujua yaliyomo hadi imetolewa wazi na kuipitia. Mapendekezo ya wananchi huwa yapo ktk sheria na sii mwongiozo wenyewe maaa ukiwaachia watu wote waandae mwongozo basi haitakwisha kesho wala kesho kutwa. Hata msahafu na Biblia ni maneno ya Mungu ahakutuuliza sisi tunataka tuishi vipi.
.
mwongozo wa Utawala huwa ni swala la Watawala wenyewe, sii rahis wananchi kuulizwa kama wanataka kuwa wajamaa (kushoto)au Mabepari (kulia)ili katiba yao ikidhi maamuzi hayo. Hata katika ajira inajulikana wazi kwamba pasipo wafanyakazi kiwanda haikiwezi kuzalisha lakini msingi wa kufungua kiwanda hicho na mwongozo wake huandaliwa na wamiliki, wewe na mimi tunaweza tu kuchangia jinsi gani tunaweza kuifanya kazi ile kwa ufanisi zaidi, haki zetu, safety na kadhalika katika management lakini mwongozo na malengo huwekwa na wenye miliki..

Swala la Kitila nimelizungumza wazi kabisa sina ushabiki maana vyama vyote vya upinzani nchini vimeanzishwa kwa misingi sawa kabisa na hii ya Kitila. Malumbano ndani ya vyama yamesababisha mgawanyiko na watu na vyama hadi kufikia 19 sijui 20..Hakuna cha Kustaajabisha!
 
Mag3
Kitila amekuja na mwenyekiti wake mfukoni, Mkandara anasema hiyo ni demokrasia. Kumbu kumbu zinaonyesha wakati wa Waraka Mkandara alilaani sana kupindishwa kwa demokrasia na kushabikia maasi ya waraka.
Kama kawaida, mkuu Mkandara anageuza tu, hakuna indicator au honi. Angeuza gari li fit anapotaka ku park.
Hakuna mahala nimesema hiyo ni demokrasia ila nimesema ndivyo nyama vyote vya Upinzani vilivyo anzishwa ni ktk msingi hiyo na mtafaruku wa viongozi huko walikokuwa.

Hakuna demokrasia ya kweli Tanzania na mifano ndio hii maana Chama Tanzania ni WATU sio MRENGO (itikadi) na hata ukiwauliza wana CCM wote kwa nini wanaamini CCM itawaletea maendeleo watasema kwa sababu kule kuna vigogo na watakupangia list ya wasomi wao kana kwamba msomi ndiye hujiunga CCM ili huleta maendeleo. Waulize Chadema na CUF ni yale yale, Zitto kaondoka ameondoka na watu wake, akiondoka Mbowe naye atabeba wake japo itikadi ya Chadema ni ile ile.

Huyo Mag3 mwambie sijasema kwamba Mrema ndiye alikuwa muasisi wa NCCR, ila kutoka kweke NCCR kama kiongozi ilitokana na Mtafaruku. Swala hapa ni jinsi gani vyama vya Upinzani vilianzishwa nchini! Sio swala la kutokubaliana kiitikadi bali kutokubaliana kwa maslahi binafsi..
 
Wanajamvi, katika kuufuatilia huu mjadala, hizi nukuu za Mkuu mkandala zimeniacha hoi; hakika simuelewi kabisa huyu GT kama yuko serious ama anatania tu.

Kweli?

Sina hakika kipi chama kilitangulia kusajiliwa kati ya CUF na Chadema mwaka 1992!

Ninavyojua Mrema hakuwahi kuwa muasisi wa NCCR; alikuja kudandia tu mwaka 1995 akitokea CCM...

Ninavyoelewa makosa ya Kitila ni mawili;

  1. Kupanga njama za kupindua uongozi halali wa Chadema.
  2. Kutaka kumsimika uongozi ACT mtu asiye mwanachama.

Hapana, hawa hawakuwahi kupanga mapinduzi ndani ya CCM; walijiondokea tu....

Kweli hayo?

Duh! kwa mara ya kwanza naisikia hii!

Wow, ubunifu bila elimu! This is but a tall order!

Kwa kweli, watu tunatofautiana kimtizamo.
Usipoelewa maana hakika hutaelewa maana. Tazama sasa na usomi bado hujaelewa kitu umetoka mtupu bado una maswali mengi wakati kila kitu wazi kabisa...
 
Wakuu Nguruvi3 na Mag3,

Mmehoji zitto anasubiri nini kuhamia ACT. Mtazamo wangu ni Kwamba, kwa vile sasa ni dhahiri Kwamba moja ya Malengo makuu ya ACT ni kusambaratisha chadema (rejea kauli ya mwigamba), ili kufanikiwa, kazi hiyo itamwitaji Mwenyekiti wao mtarajiwa (zitto) awepo chadema japo kwa muda kwa Nguvu za Mahakama.

Kauli ya mwigamba juu ya kusambaratika kwa ukawa Kabla ya 2015 ni kauli ya kuitazama kwa makini sana. Sasa ni dhahiri Kwamba kikwazo kikubwa cha Hawa Jamaa kuihujumu chadema with a final blow ni ukawa. Ni Jambo la kusikitisha sana Kugundua Kwamba zitto na kitila hawafurahishwi na ukawa. Msimamo wa mwigamba Ndio msimamo wa zitto na kitila hasa kwa kuzingatia Kwamba ukawa ni chadema, hasa kwa siasa za bara. ACT Kupinga UKAWA maana yake ni nini Kama sio kuendeleza kuwa mpini wa CCM kuua upinzani?

All that said and done, utafiti wangu mitaani japo ni wa juu juu ni Kwamba - vijana wengi sana vijiweni,mikoa ya dsm, mbeya, Arusha, mwanza, wameshajua nini kinaendelea. Wanamjadili zitto Kama mpiga Dili na mbomoaji wa upinzani. Mtu yoyote akienda Katika miji hii na kutega sikio kila mijadala ya zitto inapojitokeza ataweza verify nachosema.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara,

Ili ueleweke vizuri unasimamia wapi, pengine ungetufanyia swot analysis ya act relative to chadema Kama mshindani wa act. What are the strengths, weaknesses, opportunities and threats za ACT? Kumbuka, strengths and weaknesses ni masuala ya ndani ya chama na opportunities and threats ni masuala ya nje ya chama - yani mazingira yanayokuzunguka chama.

Nina wasiwasi kama kweli lengo la ACT ni kudhoofisha CHADEMA au kuimarisha CCM. Inawezekana kuwa ni moja kati ya mbili, lakini siamini hata kidogo kama itakuwa na maslahi yoyote kwa Mtanzania. Inawezekana kuwa ni mchezo tu.
 
Wakuu Nguruvi3 na Mag3,

Mmehoji zitto anasubiri nini kuhamia ACT. Mtazamo wangu ni Kwamba, kwa vile sasa ni dhahiri Kwamba moja ya Malengo makuu ya ACT ni kusambaratisha chadema (rejea kauli ya mwigamba), ili kufanikiwa, kazi hiyo itamwitaji Mwenyekiti wao mtarajiwa (zitto) awepo chadema japo kwa muda kwa Nguvu za Mahakama.

Kauli ya mwigamba juu ya kusambaratika kwa ukawa Kabla ya 2015 ni kauli ya kuitazama kwa makini sana. Sasa ni dhahiri Kwamba kikwazo kikubwa cha Hawa Jamaa kuihujumu chadema with a final blow ni ukawa. Ni Jambo la kusikitisha sana Kugundua Kwamba zitto na kitila hawafurahishwi na ukawa. Msimamo wa mwigamba Ndio msimamo wa zitto na kitila hasa kwa kuzingatia Kwamba ukawa ni chadema, hasa kwa siasa za bara. ACT Kupinga UKAWA maana yake ni nini Kama sio kuendeleza kuwa mpini wa CCM kuua upinzani?

All that said and done, utafiti wangu mitaani japo ni wa juu juu ni Kwamba - vijana wengi sana vijiweni,mikoa ya dsm, mbeya, Arusha, mwanza, wameshajua nini kinaendelea. Wanamjadili zitto Kama mpiga Dili na mbomoaji wa upinzani. Mtu yoyote akienda Katika miji hii na kutega sikio kila mijadala ya zitto inapojitokeza ataweza verify nachosema.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mchambuzi ebu twende mbele tukitazama nyuma tulikotoka. Inakuwaje leo iwe swala zito kwenu ikiwa Chadema wenyewe waliwafukuza watu hawa kwa majigambo mengi kwamba hawawezi kukisambaratisha chama? kwa madai ya kwamba Chadema haiwahitaji, sasa wanapoanza mavitu yao tunaanza ulalama! Na hivi, toka lini Chadema ndio ikachukuwa maana ya Upinzani? Je hii si kutaka vyama vingine vyote visimkubali ZZK maana unaposema ZZK kuua Upinzani ina maana zaidi ya Chadema.

Binafsi na sintozungumzia ya wengine, lakini baada ya kuwatimua hawa jamaa nilijua -Hili laja! na haitakuwa faida kwa Chadema ila hasara! Nilijaribu sana kuwaonya wanachama, viongozi na wanajamii JF hapa kijiweni petu kuhusu maamuzi yale kuwa hayatakijenga chama ila kukibomoa maana hawa watu hawatakubali hata kidogo kukaa nje ya siasa baada ya kufukuzwa tena kwa kesi ndogo kama ile. Naisema kesi ndogo kwa sababu haikuwa na uzito wowote zaidi ya changamoto ya demokrasia ndani ya chama na jinsi gani tungeweza kuizima moto ule bila kumwagia mafuta.
Hata ktk maisha yetu ya kawaida ukimsingizia sana mkeo kutembea nje ya ndoa na ukaanza matusi na jeuri basi huyo mke atakuja tembea kweli nje ya ndoa maana haaminiwi kwa lolote atakalo fanya. Sasa mke anatembea nje ya ndoa mnaanza kusema sii unaona? tulijua tu kwamba huyu malaya! alaa ubaya upo sehemu moja tu.

Jamani, iCCM waliweza vipi kulizima la Lowassa, hata huyo Nape Mnauye leo hii vita yake sii tena Lowassa wala Kujivua magamba na Wadanganyika wameisha sahau kabisa. Lowassa shujaa tena anajipanga wazi wazi kabisa na wapo watu wanamshabikia kuwa ni haki yake kuweka nia maadam hajaanza kampeni. Hao CCM waliweza vipi kuvumilia ya CCJ na kina Sitta hadi chama hicho kimejichokea chenyewe. Badala ya CCM kufukuzana nao kwa maneno na woga (fear is the key) CCM wameendelea kujipanga kama chama dhidi ya Lowassa ama makundi ya watu na atakaye bisha namwambia asubiri Uchaguzi mkuu maana rais Mtarajiwa wa CCM ni MWANAMKE na kesha andaliwa vema chini ya huyo huyo Lowassa.. Itakuwa changa la macho kwenu lakini sio mimi.

Vioongozi wa Chadema walifanya makosa makubwa kuwafukuza Mwigamba, Kitila na Zitto kwa. Haya hayakuwa maamuzi ya wanachadema na sisi wengine hatukupendezewa kabisa maana tunaamini Zitto asingeweza kushinda Uchaguzi wa ndani hata kama angeenda kumchinja ngamia maana tunajua fika kwamba ZZK hakubaliki ndani ya chama toka mwaka 2009japo nje ya chama anapendwa zaidi. Na hata kama huo waraka wangeusambaza nchi nzima wanaChadema wasingekubali Zitto awe mwenyekiti maana wanaamini ZZK ni pandikizi. Sasa hilo pandikizi liko nje ya chama mnaanza tena kuliogopa, kulalama hivi mlitegemea huyu ZZK afanye nini ili aaminike?..

Sasa maadam Chadema walikubali kurusha jiwe la kwanza tukiitangaza vita tena kwa ushabiki mkubwa sana humu JF, inakuwaje leo tunaanza kusema wao ni wasaliti ikiwa sisi wenyewe tumewakabidhi silaha hizo. Hivi kweli mlitegemea hawa watu wangeondoka Chadema hivi hivi tu baada ya kufukuzwa kwa chuki kama ile maana mara nyingi watu wanaoondoka Chadema hujifukuza wenyewe baada ya kubanwa sana, wakakimbilia vyama vingine na kuanza kulalama ovyo.

Hawa walioondoka wenyewe ndio tunaweza kusema wanakisaliti chama lakini hawa jamaa zetu hatukuwapa nafasi zaidi ya sisi wenyewe kuwachoka na kuzua habari za waraka, wengine wakiaminishwa kwamba Zitto ni CCM hutumiwa kukibomoa chama, alaaa kama hivyo ndivyo toka mwanzo na sababu ya kumtimua kwa nini leo tunashangaa!.

Vita ya kina Zitto ni uongozi ndani ya chama wala sii itikadi, sera ama katiba ya chama isipokuwa waliona kuna mapungufu makubwa ya uongozi wa chama kufikia malengo,na ndivyo wapo wana CCM wengine wanavyoitazama serikali ya JK ktk kuleta maendeleo kwa wananchi. Unapopingana na CCM ni swala jingine, na kupingana na uiongozi wa serikali ya Kikwete jingine hata kama wewe ni mwanaCCM Ni vizuri sana sisi wananchi tujue tofauti baina ya Chama na mgombea Urais ama mwenyekiti. Hapa tunamtafuta mtu ambaye he can deliver na sii vinginevyo, sasa kama hawa watu waliona Mbowe na Dr.Slaa wanakipeleka chama kusikotakiwa wakajipanga wao wachukue uongozi kupitia uchaguzi wa mwaka 2013, kosa liko wapi?

Haya huo uchaguzi uko wapi maana naona hata huu mwaka 2014 unapita kinyemela, hakuna uchaguzi wala harufu yake. Viongozi na wasemaji wakuu wa chama hadi leo hii hawa ndio watakao tupangia uchaguzi ujao na sii katiba wala kanuni inayotazamwa. Je, hizo kanuni za chama hazikukiukwa? na kikao gani kilichowapa mamlaka gani yalowapa hawa viongozi muda zaidi, kupanga na kuchagua siku ya Uchaguzi!.

Kanuni zinapindishwa hovyo hiovyo na hakuna wa kuwaambia kwa sababu tu hawa ni viongozi wa chama kana kwamba chama kina wenyewe. Kila uchaguzi unapokaribia lazima Chadema kuna visa, uzushi na mambojambo yaani huu ukubwa umekuwa dawa! Huu ujinga mtaendelea kuwa nao hadi lini? Mbowe mshikaji wangu sana tu lakini ujinga unaofanyika sasa hivi ndani ya Chadema na hasa hawa vijana waloingia kwa mlango wa nyuma, ndio wanatupelekesha watu hovyo wakitegemea kila mtu atashusha kichwa, tena wanasema hovyo hovyo kumdhihaki mwalimu bila kujali kwamba baadhi yetu sisi ndio wafuasi wakubwa wa baba wa Taifa.

Sisi wengine tunatazama na kupima, tunashangwazwa na visa hivi kila inapotokea uchaguzi Chadema iwe vijana au kukiongoza chama na tatizo ni kwamba hao hao viongozi wa chama ndio wabunge na kila tunaposema mfumo ubadilike tunaambiwa hawa watu walijitolea kwa hali na mali hivyo ndio pekee wanaoaminika! Eeeeh! wanaaminika na nani kama sio kundi fulani maana chama kina wananchama Tanzania nzima sijasikia wala kuona list ya viongozi wanaoaminiwa na wananchama!
 
Mkuu Mkandara,

Ili ueleweke vizuri unasimamia wapi, pengine ungetufanyia swot analysis ya act relative to chadema Kama mshindani wa act. What are the strengths, weaknesses, opportunities and threats za ACT? Kumbuka, strengths and weaknesses ni masuala ya ndani ya chama na opportunities and threats ni masuala ya nje ya chama - yani mazingira yanayokuzunguka chama.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Swala la ACT halinihusu, ni mipango gani walokuwa nayo siijui na wala sina haja ya kuijua unless nitapenda kujiunga nao hivyo nitawasoma na pengine kuuliza maswali mengi tu kama nilivyofanya kwa Chadema miaka hiyo. Kifupi sina tumaini na siasa za Bongo ni kuumizana vichwa tu.

Ila naelewa wazi kwamba Kitila na wenzake wanayafanya madudu yale yale yalotanguliwa na wanasiasa wetu ya kwamba usipokubaliana na uongozi wa chama hiki anzisha chako, na kama kuna mtu anakupa shida fukuza wewe ndio mwenyewe! japo nyote mnaamini itikadi moja! Hizi ndio siasa za Kiafrika na kusema kweli sizijui isipokuwa umaarufu wa mtu ndio mtu!
 
Mkuu nakubaliana na wewe na kuhusu utoto kwenye siasa zetu. Kama wewe si kiongozi basi unakimbhia chama unaanzisha chako. maswali yanakuja, kama wana ACt hawatapenda Zitto awe mwenyekiti na Kitila awe Katibu, wataondoka na kwena kuanzisha chama kingine? ACT ina tofauti gani na CDM au vyama vingine vya kisiasa, na kuhalalisja uwepo wake?
 
Uanachama wa siasa Bongo ni sawa na Ushabiki wa mpira wa miguu siku hizi, maana akiondoka mchezaji basi na washambiki wanahama timu sii kama wakati wetu wa Simba na Yanga. Hivyo kama akiondoka Mbowe ataondoka na watu na ndivyo ilivyokuwa kwa Mtei, Mrema Lipumba na wengineo wote walitokea CCM wakawafuata hawa jamaa. Tatizo ni kwamba tulipoanzisha vyama vingi ndio wakati huo huo tukaingia Ubepari hivyo mambo mengi yalibadiliika yakawaacha watu nyuma. Watu wenyewe ndio hatutaki kuamini kwamba siku hizi hakuna neno UZALENDO, kuna kitu kinaitwa - The right to chose! hii imefikia hata watu kuchagua kumheshimu mzazi au laa!
 
Mchambuzi,
Msimamo wa mwigamba Ndio msimamo wa zitto na kitila hasa kwa kuzingatia Kwamba ukawa ni chadema, hasa kwa siasa za bara. ACT Kupinga UKAWA maana yake ni nini Kama sio kuendeleza kuwa mpini wa CCM kuua upinzani?
Dah kumbe ndio hivi mimi sikujua hili.kumbe Ukawa ni Chadema kwa bara sio umoja wa wajumbe, haya sasa mimi nayepingana na UKAWA pia nipo ni kundi la nani la ACT au sio? Mkuu ieleweke nachopinga mimi sio umoja wa UKAWA ila fikra za kuunda serikali 3 wakiacha mambo ya muungano kuwa 7 badala ya mambo yote yawe ya Muungano.

Kama hivi leo tuna mambo 22 ya Muungano na yale ya Bara yanaendeshwa chini ya muundo huu wa seriikali 2 tusiidai Tanganyika kwa miaka 50, Je inashindikana nini kuwa na yote ya Muungano kuziba kabisa midomo yahawa kina Jussa maana wao ndio wanataka kila siku mambo ya muungano tupunguze, nanyi mnaafikiana nao. Leo tuna saba, kesho yatakuwa matano, na kisha mawili na mwisho hakuna kitu hudhani kwamba hawa jamaa hawakuwa na mwisho hadi waone Muungano umekufa!.

Hili ndilo tatizo langu kubwa na UKAWA ktk mapendekezo ya rasimu ya Warioba. Tulichoomba sisi wananchi ni katiba mpya inayokwenda sambamba na transformation ya TAIFA letu Kiuchumi na kisiasa ili kukidhi mahitaji yetu, jambo ambalo lilitakiwa toka mwaka 1993 na sii swala la kero za Muungano wetu maana mamlaka ya utekelezaji shughuli za serikali ni i za serikali, kila jimbo, kila mkoa na kila wilaya wanayo haki ya kupewa mamlaka hayo ndani ya mfumo huu wa Kibepari..muhimu la lazima kwa serikali zote 2 chini ya muundo wowote na haikomei kwa serikali hiz bai huenda hadi kwa Magavana, Mayor na serikali za mitaa wote wanahitaji mamlaka kamili kwa shughuli zao na sii mlolongo wapaper work na ofisi, hii inaoleta Urasimu na ucheleweshaji wa maendeleo.
 
Mkuu Mkandara
Angalizo,bandiko 118nadhani halipo katika sehemu husika. Hapa tunajadili ACT kama fimbo ya kuua upinzani.

Nimehamisha bandiko hilo kwenda kwenye uzi husika. Ahsante na tunakujibu kule.
 
Last edited by a moderator:
ACT WATENDA WALIYOKEMEA HUKO NYUMA

Katika madai ya waandika Waraka,MM, M1, M2, M3 ilikuwa ni viongozi wa chama kushindwa kumwajibisha Mwenyekiti wa CDM. Literally, walikuwa wanasema katibu mkuu wa CDM hakuwa na kauli mbele ya mwenyekiti na hivyo kuburuzwa tu bila kujua anafanya nini. Hayo ni madai yaliyomo katika waraka na wala si kauli zetu

Majuzi katibu mkuu wa ACT at least kwa anavyojulikana, Mh Mwigamba, amenukuliwa na vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya jamii akisema ujio wa UKAWA umekwaza jitihada za kupambana na CDM.
Kauli hii ilitoka kwa mmoja wa viongozi wa muda ambao hadi sasa wanajulikana.

Ilitegemewa yatokea mambo mawili
1. ACT wakanushe na kujiweka mbali na kauli hiyo(Dissociate)
2. ACT waunge mkono kauli hiyo kwa uwazi bila kificho kama kauli mbiu ya chama chao.

Katika hali ya kushangaza, idara ya uenezi ikatoka na kauli za kujiweka mbali na watu wanaoandika katika mitandao kuhusu ACT na si kauli ya kiongozi wake hata kama ni wa muda.
Idara ikasema kuna taratibu za kufuatwa ndani ya ACT na watu wasitilie manani maneno ya watu.

Katika mahusiano ya kijamii (PR) hili ni jambo la kushangaza.
Kauli iliyotolewa na mmoja wa watu wanaojulikana kuwa vinara wa ACT haiwezi kupuuzwa au kutolewa majibu rahisi namna hiyo.

Tulidhani kuwa, kwavile viongozi walioandika waraka ndio waliopo ACT, lau wangekuwa na uthubutu wa kumkemea yoyote anayekwenda kinyume cha taratibu bila kificho kama kauli mbiu inavyosema ''uwazi'

Kinyume chake inaonekana viongozi wale wale waliolaani katibu mkuu wao wa zamani kuwekwa mfukoni na mwenyekiti nao sasa wamewekwa mfukoni na 'katibu' wa ACT.

Kama hawakuweza kutoka na kuweka sawa kauli hiyo, maana rahisi ni kukubaliana nayo.
Lau hawakubaliani nayo, basi wamebaki nayo tumboni kama vile walivyokuwa wanalaani katibu mkuu wao wa zamani kubaki bila kauli mambo yakienda mrama.

Kuna swali moja tu la kujiuliza, unawezaje kulaani jambo moja na miezi michache ukafanya jambo lile ukituaminisha kuwa huo ni mbadala?
 
Back
Top Bottom