Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
ZANZIBAR INAJIBANZA KWA MGONGO WA MUUNGANO
MTANGANYIKA ANALIPA KWA KILE ASICHOTUMIA
ZIGO LA UENDESHAJI WA SMZ NI LA MTANGANYIKA
Sehemu ya I
Wanajamvi
Katika mambo yasiyozungumzwa au kugusiwa katika suala la muungano ni gharama. Gharama hazimaanishi kuendesha muungano tu, zinaenda mbali na kugusa kila sehemu ya nchi na mtu binafasi.
Prof Shivji katika uzi amezungumzia msingi wa muungano ni KUGAWANA MADARAKA. Hii ndiyo dhana ya wazanzibar katika suala la muungano
Ukweli ni kuwa msingi wa muungano ni uchumi.
Mijadala yote imejikita katika dhana ya uchumi na laiti mambo ya uchumi yasingekuwepo tusingekuwa na mjadala mrefu kiasi hiki
Kwanini uchumi? Kwanza ni kutokana na mabadiliko ya kisiasa duniani ambayo uchumi ndiyo siasa. Tanzania na Afrika imeshapita kipindi cha ukombozi na mambo ya kisiasa na sasa tunakwenda katika uchumi.
Muungano wa EU, NAFTA, BRICKS, ASIAN n.k yote imekikita katika uchumi na si siasa. Hata NATO imejiondoa katika ulinzi zaidi kwa kuelewa ulinzi mahdubuti uliopo dunia ya sasa ni uchumi.
Kwetu sisi ni kutokana na upande mmoja kuona unaonewa au una haki zaidi ya upande usiokuwepo( Tanganyika)
Zanzibar wanadhani wanayo haki zaidi katika mambo ya uchumi, kwabahati mbaya Mtanganyika hana kauli kwasababu yeye ni Mtanzania ambaye ndani yake yupo mzanzibar.
Hii maana yake ni kitu kimoja kinachoitwa kwa lugha ya kigeni 'fiscal autonomy' kwamba, ni uwezo na uhakika wa sehemu ya jamii kupewa uhakika huo kwa kuamua mambo yao kwa kuhakikishiwa na serikali au katiba(kwa tafsiri isiyo rasmi)
Prof Shivji jana kasema suala la uvuvi halikuwa la muungano na hivyo JMT iliingilia mamlaka ya znz. Hapo ndipo fiscal autonomy inapokuja kuwa Zanzibar wana haki kikatiba ya kutumia maliasili zao kiuchumi kwa kuhakikishiwa na katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.
Kwa upande mwingine Tanzania bara haina fiscal autonomy kwasababu mambo yote yanayohusu Tanzania yanahusu Zanzibar.
Ni kwa msingi huo watalii(wabunge) kutoka znz wanapokuja Dodoma, wanalipwa kwa pesa ya Tanzania ambayo ni ya Mtanganyika.
Zanzibar ina uwezo wa kuamua idadi ya wajumbe wa BLW kwasababu ina fiscal autonomy.
Ni kwa msingi huo, BLW lina wajumbe 50 na Watalii wa znz katika bunge la JMT ni 81.
Hii maana yake ni kuwa Tanganyika haina fiscal autonomy katika mambo yake. Imeuza autonomy kwa muungano ili hali znz ina autonomy katika mambo yanayoihusu na yanayomhusu Mtanganyika
Mfano wa pili katika kufafanua mada hii, pesa za madini zinatumika katika mambo ya muungano bila kujali lipi la muungano na lipi lisilo kwasababu Tanzania ndiyo Tanganyika ambapo znz ina mkono wake.
Tunapokuja katika suala la kodi, Tanganyika inachangia kodi zake katika muungano ambapo kodi hizo zinaitwa za Tanzania na znz ikidai haki kwasababu ni sehemu ya Tanzania. Hilo ndilo linapelekea znz ipewe 4% ya pato la taifa kwasababu ni sehemu ya Tanzania.
Kwasasa wanadai wapewe 11% ya pato la taifa kwasababu nao ni sehemu ya Tanzania. Haki hiyo wanapewa na katiba kwasababu ni sehemu ya JMT na ndicho kinaitwa fiscal autonomy kwa upande wao.
Kwa upande mwingine, znz ina ZRA inayokusanya kodi zake na kubaki huko huko hivyo kuwa na fiscal autonomy iliyopewa na katiba yao au kuchakachua kama ilivyotokea mwaka 2010.
Hili linaeleza kwa undani kabisa namna kodi za Mtanganyika zinavyovuka bahari kwenda kuendeleza nchi jirani.
Zaidi zinaeleza matumizi mbaya ya kodi za Watanganyika. Nitoe mfano;
Watalii 81 wa znz katika bunge la JMT wanalipwa takribani milioni 10 kwa mwezi, sawa na jumla ya milioni 810 kwa mwenzi na bilioni 9.6 kwa mwaka kama mishahara na marupu rupu.
Ukiweka na viinua mgongo kiasi kinakwenda na kufikia bilioni 9.6 kwa kiwango rahisi sana cha Ts Milioni 100 kwa kila mmoja.
Jumla ya fedha kwa miaka mitano inakwenda kwa hesabu za makadirio ya 9.6 B x 5 + 9.6 ambayo ni karibu na Bilioni 50 Ths
Bilioni 50 zinatoka katika JMT inayochangiwa na Tanganyika 100% kwasababu znz haijachangia kwa miaka mingi at least 10 iliyopita.
Rais Kikwete akiwa Muheza Tanga alitangaza serikali kutenga kiasi cha sh milioni 500 kwa halmashauri 41 nchini kujenga nyumba za Walimu
Hadi hapo unaweza kujiuliza iweje kwa miaka mitano watalii 81 kutoka znz wapokee bilioni 50 halafu halmashauri 41 zipewe bilioni 500 kwa pamoja.
Hii maana yake ni kuwa Tanganyika haina fiscal autonomy ya resources zake kiasi cha kutoa mabilioni kwa watu 81 wasio na mchango wowote katika bunge la JMT zaidi ya utalii huku walipa kodi wa halmashauri 41 wakipewa milioni 500 ambazo ni pungufu ukilinganisha na milioni 800 kwa mwezi wanazopewa watalii 81.
Tuangalie muungano kama wa Scotland na UK unakuwaje
Inaendelea