Mwaalimu wangu hapa Jukwaani
Nguruvi3, hivi unaona jinsi demokrasia ya wenzetu (US) ilivyo na mushkeli. Sasa watu kwa uhuru wao wa kidemokrasia waliamua kutompa kura Hillary Clinton lakini kwa kitendo hicho wamepigwa fine. Sasa hapo hauoni kuwa demokrasia zetu na zao mapungu ni yale yale tofauti 'rangi' tu!?
===========
Four Washington state electors who broke their pledge to vote for Democratic candidate Hillary Clinton are each being fined $1,000, after 3 chose to vote for ex-Secretary of State Colin Powell, and one for Native American tribal elder Faith Spotted Eagle.
They will all be fined next week, and have 60 days to pay, according to the spokesman for Washington Secretary of State Kim Wyman, who spoke to the AP. He added that an appeals process is being formulated in case of a challenge.
This is the first time anything like this has happened in the state in 40 years, when one elector went rogue and voted for Ronald Reagan instead of Gerald Ford, who won in Washington but lost the general election to Democratic candidate Jimmy Carter in 1976. It was that year that the penalties for going rogue were signed into law, but 2016 is the first year they will be enforced.
Washington state’s rogue electors make history – fined $1,000 for not voting Clinton
Mkuu naona bado unatafakari hoja hapo juu.
Nichangie hoja kwa maana mbili, kwanza, dhana ya uchaguzi na pili dhana ya demokrasia
Kwa hoja yako' waliopigwa faini wameonewa' wana uhuru wa kumchagua wamtakae'
Mantiki yako inaongozwa na hoja hizi
1. Wamepigwa faini kwasababu ya kutompigia kura Hillary Clinton,ni kukiuka Demokrasi
2. Kwamba, wana uhuru lakini kuna mizengwe inawekwa kwavile wamekwenda kinyume
3. Kwamba faini waliopigwa inatoka kwa Democrats
4. Kwamba, electors wapo huru kumchagua wamtakaye
5. Hayo 1-4 ni ukiukwaji mkubwa wa demokrasia kama tufanyavyo sisi
Majibu ya dhana ya hoja zako
1. Uchaguzi mkuu wa Marekani:
Kama tulivyojadili utaratibu upo ngazi za vyama,state na federal
Tulisema kuiba kura hakuwezekani kitaifa ingawa inaweza katika county au state
Kila state ina bunge na senate,uchaguzi wa N.Carolina ni tofauti kwa utaratibu S.Carolina
Ndio maana yapo malalamiko(voter suppression) NC tusiyoyasikia South Carolina
Afisa tawala wa state( sec of state) ndiye msimamizi wa chaguzi katika ngazi ya state.
Huyu ni mtu wa tatu kwa wadhifa baada ya state Governor na Lieutenant
Ukisoma article kwa umakini faini wamepigwa na Washington sec of state $ 1000
Ni mara ya kwanza, si kwasababu ya Clinton bali utaratibu kutumika katika state husika
$1000 haikubuniwa, ipo sheria ya Bunge, kuanzia 1976 Reagan akiwania na Ford
1976 electors walimpigia Reagan na siyo Ford(alishinda state)ya Washington si kitaifa
Ndipo Washington state ikaweka utaratibu electors wampigie aliyeshinda state
Uchaguzi wa 2016 Clinton alimshinda Trump na electors waliwajibika kumpigia kura
Kwavile walikwenda kinyume na sheria, sec of state akawapiga faini, si Clinton Vs Trump
Kila state ina utaratibu unaoongoza electors wanavyokusanyika na kupiga kura
Kwa maana hiyo Maine na Nabraska wanatumia congressional district tofauti na Ohio
Article haikuwa na details kwa utaratibu na hivyo kudhani Dem na Clinton wanahusika
Kilichokuongoza ni dhana ya Clinton na Trump kuonyesha ''upendeleo au uonevu''
Kwa bahati mbaya uka igonore ukweli wa taratibu zilivyo, adhabu na nani katoa
Mwisho ukatoa conclusion Clinton/Dem wamekikuka misingi ya 'watu huru kuchagua'
2. Demokrasia tumeijadili, haiwezi kuwa uniform Duniani na hili tulikueleza kwa kina.
Demokrasia ni taratibu za jamii husika kupanga, kuamua kuchagua wanayokubaliana
Ukitazama uchaguzi wa US, utaiona demokrasia bila miwani wala lens
Unapolinganisha na kwetu inashangaza kwasababu hata tuliyokubaliana hautendi
Fuatilia tume ya uchaguzi ya US katika federal level, rudi katika state hadi county
Ukimaliza, ulinganishe na tume ya uchaguzi ya Tanzania ambayo mwenyekiti anateuliwa na mwenyekiti wa chama na kuapishwa na kwa kofia ya Urais ili mwenyekiti wa tume asimamie haki kati ya mwenyekiti alimteua na mtu mwingine!
Mkuu Chungwa na nazi koroma ni vitu viwili tofauti,kulinganisha ni kutafutia watu kicheko
Tusemezane