Mwalimu, post: 19224548, member: 11689"]Trump kwa nafasi yake hawezi kukubali 100% kinachosemwa na intelligence agencies wake sababu atakuwa anajikaanga mwenyewe pia.
Mkuu, Trump ame miss opportunity. Tulisema hapa kuwa alichopaswa kufanya ni kukaa kimya au kuungana na wenzake kuwa kulikuwa na cyber attack na hilo ataliangalia
Jana baada ya kupata briefing za Intel community, akasema ataunda tume ya cyber security
Yaani alimalizia pale alipopaswa kuanzia. Tulijadili hili na NN.
Kinyume chake Trump akaanza malumbano na Intel community akiwa hana evidence yoyote ya ku back up madai yake.
Alichokifanya ni spinning kwamba hacking haikubadili matokeo
Hoja hiyo ilipoteza mashiko pale ambao Dem, Rep, media na Intel comm zote ziliposema ameshinda kwa kura na hakuna wizi katika upigaji.
Akabadili na kusema wanataka ku delgitimize urais wake
Hoja ikafa kwamba, ameshinda ndiye pres elect na hakuna wizi ni legit pres elect
Mwisho akaanza tweets za ku denigrate intel community.
Hapo ndipo walipokaa sawa kwani walijua kosa moja tu atalitumia vema.
Wamempa hadi go between wa Russia na Assenge anaowaamini
Bado ana tweet wanaotaka mahusiano mabaya ni stupid hata baada ya evidence zote
Sasa hivi ana 'vita' na intel community, Republican achilia mbali adversary wake Dem
Unaweza kuona alivyo drag na poor handling itakavyo mgharimu siku zijazo
Trump aje na uchunguzi mbadala utakaobaini wahusika udukuzi kuwa sio warusi basi tuhuma zilizotolewa na CIA & FBI zitaendelea kusimama
Uchunguzi mbadala alisema Jumatano au Alhamisi. Kumbe alisubiri mahojiano ya Assenge na Fox akidhani atapata mahali.
Hana evidence ya kukabiliana na hoja za 16 security agencies ambazo unanimously zimeafiki kuwa ipo hacking na ilitoka Russia na imefanyika sehemu nyingine pia.
Obama ameitwa majina mengi kwamba anaunga mkono magaidi wa kiislamu, mjamaa etc kutokana na sera zake juu ya Iran, Cuba n.k. Hivyo tusishangae sana Trump naye akiandamwa na tuhuma kwamba ni puppet wa Urusi... Ndio siasa hizo!
Obama ni smart sana.
Kila alichofanya alikuwa na majibu tayari
Iran, aliuliza wenye mbadala wauweke hadharani.
Hakuna aliyekuwa nao na in fact wengine wanakubaliana naye.
Kilichotokea na hasa Trump alisema deal ya Iran Obama alitoa pesa cash
Ukweli ni kuwa pesa za Iran zilikuwa zimezuiliwa na suala hilo lilifika mahakama za dunia
Kuendelea kukaa nazo ni kuongeza interest kwasababu mwisho wa siku watalipa
Akatumia nafasi kuibana Iran, kwa kamba waliyokuwa nao Iran na kuwatia kitanzi
Cuba: Obama ameeleza sanction zipo miaka 50 na ushee, nini kipya kimetokea?
Uhusiano wake na Cuba ni approach mpya ya kuingia Cuba na kufanya instigation
Ndivyo US walivyofanya mataifa mengi.
Obama hatakuwepo lakini 20 yrs to come outcome itaonekana. USSR haikuanguka na Reagan,ilianza mika mingi Ronald akamalizia tu
Ujamaa: Walimtuhumu sana, akuliza ni nchi gani ya kibepari iliyofanya tofauti na yeye
Obamacare: Hadi jana aliuliza, kama Obamacare ni mbaya mbadala upo wapi?
Sote tunajua Trump hana na Republican wanahangaika kutengeneza sasa hivi
Kwahiyo kuna tofauti ya u-smart kati ya wawili hao katika hatua za mwanzo tu.
Tofauti zitaendelea kujadiliwa kutokana na maamuzi ya Trump , anaweza kufanya vizuri au vibaya hilo ni suala lisiloweza kujadilika akiwa hana power.
So far bado anajifunza. Vita na intel community itamweka pagumu
Maamuzi yote yataangaliwa kwa jicho la shaka sana na hilo litakuwa tatizo
Wiki hii wanaanza confirmation ya cabinet.