"Nyani Ngabu, post: 19148042, member: 188"]Ni kweli kabisa kuwa denial ya Trump inalipa kiki suala zima.
Angecheza kisiasa kwa kukaa kimya au kuwaambia hakubaliana na suala la kuingiliwa uchaguzi na uchunguzi uendelee ili achukue hatua akiingia madarakani.
Kukataa kuwa si Russia akiwa hana ushahidi kunaipa 'kick' hili suala.
Mbaya zaidi anajikuta hapambani na Dem bali IC na Congress
Unakumbuka suala la IRS na Obama. Alichokifanya ilikuwa kuwahi na kusema uchunguzi ufanyike na ikibainika wote waliohusika wachukuliwe hatua. Moto ukapungua
Ila mimi naamini kabisa kuwa suala zima liko politically motivated pia.
Dems kukomalia koo hizo habari kunawanufaisha kisiasa. Kunawanufaisha kwa sababu kunamjengea taswira rais mteule kuwa kasaidiwa na Urusi na hivyo ni kibaraka wa Putin.
Na hasa yeye kuwa 'mtetezi' wa Russia ndiyo kabisa siasa inapata miguu
Na zile kauli zake kuhusu Putin na ile perceived 'bromance' iliyopo kati yao [Trump na Putin] ina play vizuri sana katika hiyo narrative ya kwamba Urusi ili hack ili kumsaidia Trump ashinde.
Na hapa anaingia sec of state kwa ku insinuate kuwa wote wawili wana masilahi.
Lakini mbaya ni pale anapohusishwa na suala la tax return, makampuni yake na uhusiano wake na Russia. Hapa ndipo patamsumbua kama si leo ni down the road
Mwisho wa siku, mimi naamini, hakutakuwa na lolote lile la maana hapa. Ni kama tu ilivokuwa kwenye zile recounts za Jill Stein na zile juhudi za kuwa lobby wale electors wamtose Trump. Nothing will come of it kwa sababu suala zima liko politically motivated.
Whatever the outcome, hili litakuwa 'strings' mbele ya safari.
Hillary na emails ilikuwa hivi hivi, likarudi kwa kasi sana wakati wa uchaguzi
Ni kweli lina sura ya kisiasa kama ilivyokuwa kwa emails za Clinton.
Marekani ndivyo siasa zilivyo watakumbuka kura iliyopigwa miaka 30 na ikaleta tatizo
Emails zilitumiwa kisiasa na Trump hadi Comey alipobadilisha mwelekeo wa uchaguzi kabisa na kuwa sehemu ya anguko la Hillary.
Trump anasema anakwenda Washington to drain the swamp ikiwemo makosa kama ya Hillary. Watu wanapoangalia na kuona hataki uchunguzi,wanaomwamini wanaanza kupata shaka na anakaribisha curiosity hata kwa waliokuwa na doubt
Emails za Clinton the same will happen to Trump kama hatafanya damage control mapema. Hizi tweets zinabaki kama kumbu kumbu
Hivi mazee wewe huoni kama ni ajabu kidogo kama ingekuwa ni kweli kabisa Russia ndo imefanya hiyo hacking na Marekani kukiri hadharani?
Manake kukiri hadharani ni kukiri madhaifu yenu. Na tena si kukiri tu madhaifu yenu...ni kukiri kuwa mmezidiwa kete na hasimu wenu mkuu.
Kukiri hadharani ni katika kutafuta kuungwa mkono na hilo limefanikiwa.
Republican ndio wamekomalia kuliko Dem
Hapa ni ku insinuate jambo litakaloanzisha hisia za 'inferiority' na US hawakubali hilo
Sidhani washauri wa Trump wanakubaliana na tweets zake na jinsi anavyo handle suala . Kwasasa it's OK lakini linaacha alama.
Nakuhakikishia miaka 4 baadaye litakuwa silaha dhidi yake.
Unakumbuka TPP ya Clinton ilivyogeuka silaha ya Bernie na Trump dhidi ya Hillary.
Unakumbuka Seccession na suala la ujaji .
Atakuwa confirmed lakini hana uhuru wa kazi kwasababu kuna prejudice dhidi yake
Unakumbuka kauli ya 'Najua zaidi ya majenerali' inavyomsumbua.
Kwasasa haipo obvious lakini failure of any military mission itakuwa associated
Katika hali inayoonyesha tatizo, Trump anasema ana habari zaidi ya watu wanazojua
Tayari kuna swali, ni kutoka source zipi? Na anaweka wapi IC zake?
Tatizo ana 'drag' na kulifanya story kila uchao mwenyewe