Duru za siasa - Matukio

Duru za siasa - Matukio

Sidhani
Mimi binafsi sijajua nimekuwa mentioned mahsusi kwa mintarafu gani
Kila mwisho wa bandiko tumekuwa tunaafnya mialiko tu kama sehemu tu ya kutambuana. Haihusiani na wala haina maana yoyote na mada inayojadiliwa kwa namna yoyote.
Nadhani hili linaanza kuwa blown up out of proportion na sikusudio au mintaarafu ya nyuzi hii.

Naomba nikutake radhi kwa kukutaja hata kama kufanya hivyo ilikuwa kwa nia njema kabisa.
Tumefanya editing ili kumaliza suala hili kwa upendo. Natumaini hoja itakuwa imefika mwisho.
 
TATIZO LA UHAMIAJI HARAMU

SEHEMU YA PILI

Tunaendelea na mjadala tulioanza jana na tuwatake radhi kwa kwa kuingiliwa na hoja zisizohusiana.
Tuyaayangalie kwanza mambo tuliyoyasema ni sehemu ya mambo yanayohusiana na uhamiaji haramu halafu tujaribu kujibu maswali tuliyojiuliza

1. Usalama : Tanzania kama nchi nyingine za ulimwengu wa tatu hazina namna bora ya kutafuta rekodi ya wahamiaji haramu. Na ni ukweli kuwa wahamiaji haramu wanatoka maeneo ya vita na uwepo wao unaongezeka gharama za ulinzi na usalama.

2. Huduma za jamii : Tanzania kama nchi nyingine inapanga maendeleo kutoka na idadi ya watu.
Huduma kama za afya na elimu ni mifano michache. Uwepo wa wahamiaji haramu unaweka shinikizo katika huduma hizo (strain) na pengine kuwaumiza wananchi zaidi kuliko wahamiaji.

Mtafaruku uliozuka ni wa kuwaondoa wahamiaji haramu na si kuondoa wahamiaji halali.
Ingawa unaonekana kama sehemu ya mgogoro wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda(Diplomatic row) ukweli utabaki kuwa ni zoezi lialohusu wahamiaji haramu. Rwanda inaonekana kuwa nao wengi na kuonekana walengwa

Tanzania ina sababu za kuwaondoa wahamiaji kutokana na sababu kubwa mbili zilizotajwa hapo juu, kiusalama na kupunguza mzigo unaotokana na raia wasiokuwepo katika mipango ya maendeleo ya nchi.

Tangu wahamiaji haramu na wakimbizi walipoingia nchini hali ya usalama mikoa ya kanda ya magharibi imekuwa ni mbaya sana. Silaha zimezagaa hovyo,wakazi wengine wakilazimika kukimbia makazi yao kutokana na nguvu walio nayo wahamiaji haramu. Usalama wa usafiri umekuwa wa mashaka huku watu wakiporwa mchana na usiku.

Lakini pia wahamiaji haramu wengi wao ni askari na hatujui uwepo wao ni kwa madhumuni gani.
Wanaweza kuwa ni watu wenye kutumiwa na serikali za nchi zao kama wapalelezi au wahusika wa matukio ya hatari.

Na inatisha ziaid pale wahamiaji haramu kukaa maeneo karibu na kwao, wakikataa hadhi za ukimbizi au kuomba vibali vya kuishi nchini. Ni kwanini kundi fulani liamue kuishi sehemu fulani likiwa halitaki kupewa hadhi yoyote?

DRC waliwakaribisha wahamiaji haramu ambao wamegeuka kuwa hatari na kufikia mahali pa kutaka nchi ya DRC igawanywe ili nao wawe na nchi yao. Hili lazima limtie wasi wasi mtu mwenye akili timamu kwasababu ni mwendo huo huo unaonekana katika mikoa ya magharibi ya Tanzania. Je, hakuna sababu za kuchukua tahadhari?

Kuhusu huduma za jamii, mashule yamekuwa na watoto wa wahamiaji haramu wakishindana na wazawa kwa rasilimali chache sana zilizopo. Tummeshuhudia mfumo wetu mbaya ukitoa nafasi kwa maafisa wa serikali ya Rwanda ya leo ambao wamesoma kwa kodi za Watanzania kuanzia msingi hadi chuo kikuu.

Vituo vya afya na zahanati hupewa masanduku ya dawa (kit) kwa mwezi kulingana na idadi ya watu. Uwepo wa wahamiaji haramu unapunguza huduma hizo kwasababu idadi yao inazidi idadi halisi iliyopo serikalini.
Pengine kit imekadiriwa kwa watu 20,000 lakini eneo lina wahamiaji haramu 5,000 unaweza kuona robo ya rasilimali inakwenda kusikotarajiwa.

Madhara ya wahamiaji haramu kuachwa ni ya kiusalama na kijamii na uwepo wao bila kujulikana una halalisha uvunjaji wa sheria, hii ikiwa ni pamoja na migongano kati ya wazawa na wahamiaji haramu kama tunavyoshuhudia kule Goma na Kivu. Tayari madhara ya kuhama kwa wananchi wa Kagera yapo wazi na kuendelea kukaa kimya ni kuwanyima wananchi hao haki yao ya kikatiba ya kulindwa kama raia wengine.

Ni zipi haki za wahamiaji haramu?
Mhamiaji haramu ni mhalifu na haki ya kwanza ni kupelekwa mbele ya sheria.

Miongoni mwa haki walizonazo wahamiaji haramu ni kumiliki watoto wao. Tanzania inasheria zinazolinda watoto kwa kuwapa uhuru wa kuishi hadi miaka 18 watakapokuwa na uwezo wa kuamua ni uraia wa nchi ipi kati ya ile ya asili na Tanzania wanaoutaka.

Wahamiaji haramu hawana haki ya kupata uraia kwasababu wameoa au wameolewa Tanzania.
Haki hiyo ipo kwa wale wanaoishi kwa njia halali. Na wala wahamiaji haramu hawana haki ya kudai mali waliochuma wakiwa Tanzania kwasababu uwepo wao ulikuwa haramu na mali zao zaweza kuwa ni zao la uharamu

Tanzania na nchi za EAC hazijaridhia mkataba wowote wa kuruhusu watu na mitaji yao kuondoka kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Madai kuwa Tanzania imekiuka makubaliano ya EAC si ya kweli ya ni uzushi mkubwa.

Kwanini kuna tatizo na Rwanda?
Ukiacha mzozo wa kidiplomasia uliopo, wahamiaji wengi ni raia wa Rwanda ambao wamekimbia makwao nyakati za maujai ya kimbari au kutoafikiana na serikali yao. Wengine wapo miaka 50, wengine ni wageni hata miezi 6 haijapita n.k. Kwahakika hakuna anayeweza kusema nini kinatokea katika nchi yao kiasi cha kuwazuia kutorudi au kukimbia.

Makosa ya wahamiaji hasa wa Kinyarwanda ni kukataa kupewa hadhi ya aina yoyote. Wamekataa hadhi ya ukimbizi na hawataki kuomba vibali vya ukazi au uraia. Inashangaza mtu ana miaka 50 bado hajaweza kupata hati ya kuishi kwa uhalali. Kwa mwenye nia njema hilo lingeshafanyika na hatuoni kwanini iwepo huruma kwa uzembe.

Pamoja na uwepo wao miaka mingi jambo wanalojivunia ni kuwa na ardhi, mashamba na kumiliki majumba.
Hayo yote hayawezi kuwafanya wawe wakaazi wa kudumu au raia wa Tanzania. Ni mali zilizpopatikana kwa kutumia njia haramu za uhamaji haramu. Hakuna halali inayotokana na uharamu.

Hoja kubwa ya Wanyarwanda ni kuoa, kuolewa na kuwa na watoto. Hoja hizo haziondoi ukweli kuwa wahusika ambao ni watu wazima wake kwa waume hawakufuata taratibu na ni wahalifu kwa kuishi kinyume cha sheria.
Watoto au ndoa siyo kigezo cha kupata uraia au ukazi ingawa vinaweza kusaidia kupata vitu hivyo.

Wahamiaji wamepewa muda wa kuondoka na hiyo ni favor wala si haki. Haki yao ilikuwa kutokea mahakamani kama tunavyofanya kwa raia wa nchi nyingine. Hakuna aliyeburuzwa na askari hadi tunaandika na hivyo madai ya kukiukwa kwa haki za binadamu hayana mashiko. Huwezi kukiuka haki kwa mtu anayereja nyumbani kwake.

Suala hili limeumiza sana Wanyarwanda na serikali ya Kagame. Wanyarwanda wengi wanajua hatima yao ipo mashakani kwasababu zilizowafanywa wakimbie.

Serikali ya Kagame ina wasi wasi kuwa huenda miongoni mwao ni wapinzani ambao wanaweza kuleta matatizo ndani ya nchi, na pia kuogopa wimbi la hasira kutoka kwa watu hao kwa matamshi yake dhidi ya Tanzania.
Na muhimu zaidi ile fursa ya kufanya uhalifu kama kupora mali za watu na ardhi sasa haitakuwepo.

Lawama za wahamiaji haramu wa Rwanda zibaki kwa Kagame aliyesababisha waondoke nchini mwao kwanza, na si Tanzania inayowashauri warudi kwao tena bila kuwachukulia hatua za kisheria.
Ni muhimu wakaangalia chanzo cha tatizo na kuacha kudhani hifadhi waliokuwa nayo ndio chanzo cha matatizo yao.

Tusemezane
 
ATATIZO LA DAWA ZA KULEVYA
KWANINI MWAKYEMBE ATASHINDWA VITA ALIYOIANZA ?

Sote twafahamu sakata la madawa ya kulevya na lilivyochafua nchi katika uso wa dunia. Kwasasa, Watanzania wanaonekana kushukiwa kila wanapokuwa na hilo linaongeza ugumu wa kupata visa na hata kusafiri kawaida

Madawa yanayopita katika viwanja vyetu ni kiwango kinachotisha.
Tatizo halikuanza leo au jana, lina muda kidogo. Kinachotisha ni jinsi linvyongezeka kwa kasi kama mradi mkubwa kwa vijana watumiaji na wasafirishaji.

Maelfu ya vijana wamefungwa nje ya nchi na mamia wamepoteza maisha kwasababu ya madawa hayo.
Wapo wabeba unga wajulikanao kama punda wa wafanyabiashara wakubwa.
Punda hawa wapo katika tasnia mbali mbali ziwe za michezo au za sanaa.

Kishindo kikubwa ni kile kilichotokea Afrika kusini kwa shehena kubwa kunaswa.
Ni kilo 150 za madawa ambazo hazijulikani ziliwezaje kupita na kuingia katika ndege kwa kupitia uwanja wa JNIA.
Kwa wasafiri wa kawaida kupitisha zawadi kama laptop ni suala la mjadala na sijui ilikuwaje kilo hizo zikapita.

Hakuna shaka mabinti waliotumiwa hawakuwa na uwezo wa kumiliki shehena hiyo yenye thamani ya dola mil 6.
Hawa walikuwa ni punda tu wa kupitisha mzigo na wala hawakuhusika katika kuratibu shughuli nzima.

Tangu tukio kutokea viongozi wa kisiasa na serikali wamerudi nyuma katika kulizungumzia.
Hatujamsikia waziri mkuu, waziri wa mambo ya ndani, mkuu wa Polisi, mkuu wa usalama na hata rais kuliongelea

Mtu pekee aliyepewa jukumu hilo ni kamanda wa kikosi cha kuzuia madawa bwana Nzowa ambaye maelezo yake ni ya kubabaisha na ni wazi hana la kuumbia umma.

Kiongozi pekee aliyejitokeza ni waziri Mwakyembe ambaye siku za karibuni amekuwa maarufu kwa utendaji na ufuatiliaji wa shughuli zinazo gusa maeneo yake ya kazi

Juzi alifanya ziara uwanja wa JNIA na kubaini madudu mengi ikiwa ni pamoja na upotoshaji wa taarifa, au taarifa za kuumba umba kama zile za kukosekana vitendea kazi. Kumbe basi mkanda wa jinsi gani tukio hilo lilivyotokea upo.

Kwa taratibu za kawaida mkanda huo hupitiwa kila siku kuona utendaji wa uwanja wa ndege kwa siku iliyopita..
Ni wazi kile alichokiona Mwakyembe kilionekana na viongozi husika na wao wakakaa kimya makusudi.
Hata uchunguzi ulioagizwa umeonekana kuruka sehemu muhimu sana na ni ubabaishaji wa kawaida tu.

Hii maana yake ni kuwa biashara hiyo si ndogo na inahusisha mtandao mzito sana.
Kuna uwezekano mtandao ukahusisha viongozi wa kitaifa au ukawa na uwezo wa kutishia amani na maisha ya viongozi.Ndiyo maana tunaona wote wamejificha na kulikimbia suala hili.

Kwa waziri Mwakyembe, tumpongeze kwa kuthubutu lakini ni ukweli usio na kificho kuwa zoezi lake litashindwa.
Litashindwa kwasababu ya kukosa kuungwa mkono na viongozi wenzake tena wenye mamlaka husika.

Hivi waziri wa uchukuzi atawezaje kumkamata mtuhumiwa wa uhalifu? Atatendaje kazi bila kuungwa mkono na wakuu wa usalama na Polisi? Atatendaje kazi na kuvuka mipaka ya waziri wa mambo ya ndani? Atatendaje kazi kukwepa kiunzi cha waziri mkuu?

Ni kwa kuangalia ukweli huo duru za siasa tunasema zoezi la Mwakyembe litashindwa.
Tunamtakia kila la heri lakini kushindwa ni wazi zaidi kuliko kushinda.
Timu yake imemsuasa na inakwepa kupambana na ukweli.
Mwakyembe ameachwa mwenyewe

Tusemezane
 
MASHARIKI YA KATI (MISRI)

Duru za siasa tulisema kutokana na mfungo mtukufu wa Ramadhan hali ya mambo itatulia nchini Misri, lakini si suluhu ya tatizo lililojitokeza la kumuondoa Rais aliyechaguliwa kidemokrasia Morsi.

Tulisema pia, utaratibu uliotumika wa jeshi kuingilia kati na kumuondoa Morsi ulikuwa unajenga mazingiara hatarishi ''precedent' kwa mustakabali wa Misri. Tukauliza je, ikitokea kuna kundi haliridhiki na utawala suluhu ni kuita jeshi?

Hadi tunaandika watu 700 wakiwa wafuasi wa Brotherhood ya Morsi wameshapoteza maisha. Tukumbushe kuwa Brotherhood ni jamii yenye mrengo wa kidini na kisiasa inawakilishwa na chama cha 'Freedom and Justice party'.Hivyo tunaongelea Brotherhood na FJP kama kitu kimoja na tawi lake

Vurugu hizo zimesambaa nchini Misri, kuanzia miji ya Cairo hadi Alexandria.
Polisi na Jeshi wanawatanya wanachama wa Brotherhood kinyume na kile walichokifanya kwa Morsi

Endapo kungekuwa hakuna upendaeleo jeshi lingechukua hatua zile zile ilizochukua kwa Morsi.
Tatizo tuliloliandika huko nyuma sasa ni dhahiri na hali inaonekana kuwa mbaya.

Kutokana na hasira na chuki, wananchi wameanza kuhamishia hasira zao kwa jamii ya Wakristo kwa kuchoma nyumba za Ibada. Mpango huo haufanywi na Brotherhood bali makundi tu yenye hasira.
Brotherhood ni werevu sana na wameonyesha kuchukizwa na kitendo hicho ambacho kitaharibu taswira ya chama chao. Jitihada za kuzuia uhalifu huo zinaendelea.

Aliyekuwa waziri wa serikali bwana Mohamed Albaradei (mkurugenzi wa zamani wa shirika la Nyuklia) na mpinzani wa Morsi amejiuzulu jana kama hatua ya kupinga yanayotokea. Albaradei anachokifanya ni karata ya kisiasa akielewa hataki kuhusishwa na tatizo hili katika siku za baadaye.

Hapa kuna funzo muhimu sana tunalopaswa kuliona. Kwanza, ni kutambua kuwa lazima tuwe na muongozo wa nchi ili kila mmoja aufuate na si kutegemea taasisi moja kama ilivyo jeshi la Misri.

Pili, tuwe na utaratibu unaozingatia sheria na utawala bora. Leo Jaji mkuu aliyepewa jukumu la nchi kwa mategemeo kuwa angeweza kuleta utangamano ndiye ameongoza serikali kuleta maafa zaidi.
Ni wazi Misri haina utaratibu ulio wazi wa kuziba pengo la uongozi la taifa na hiyo inaleta mvurugano

Tatu, lazima tujifunze kuwa vyama vya siasa lviwe vya kisiasa kwa maana iliyokusudiwa na siyo siasa iliyochanganyika na dini. Vurugu za kuchoma makanisa hazikuandaliwa na Brotherhood kwa uchache wa kusema na wala hazina uhusiano kati ya imani moja na nyingine. Kwa bahati mbaya wananchi wanaohusisha Brotherhood, Uislam na siasa wamekwenda mbali na kushambulia eneo lislohusika

Je sisi tunamwelekeo huo wa dini na siasa?
Mwelekeo upo wa wazi na wakujificha. Tumeona viongozi wakimiminika kumjulia hali sheikh aliyejeruhiwa. Wangeweza kufanya hivyo kama raia wengine na wala hilo si tatizo.
Tatizo ni pale wanapokwenda kumjulia hali kama wa wawakilishi wa vyama vyao.

Duru za siasa tunasema Sheikh aliyejeruhiwa anapaswa kutendewa haki mbele ya sheria na si kuhukumiwa kwa njia za utata kama ilivyotokea Morogoro. Hilo haliondoi ukweli kuwa hisia na huruma zilizoonyeshwa zinatokana na imani zaidi ya utanzania na uraia wake.

Ndio maana tunaonya vyama vya kisiasa kuacha kulifanya suala hili la kisiasa bali liwe la uhalifu kama uhalifu wa Mwangosi, Kibanda, Ulimboka au lile la kanisani Arusha na mkutano wa Chadema.

Tunaendelea kutahadharisha kuhusu vyama kuliangalia tatizo la Sheikh kisiasa zaidi ya kibinadamu. Wapi CUF iliyoungana na Polisi kuwalaani Chadema eti kwa kujilipua ipate huruma, na CUF iliyoomba ipewa hadhi ya upinzani rasmi wakati chadema inaomboleza, eti ipate huzuni na hisia kwa Sheikh Ponda kutotendewa haki? Ubinadamu umegawanyika katika vigezo gani ?

Tutakkapoendekeza mambo hayo tutakuwa tunapalilia mgogoro kwa njia za siri na ipo siku itakula kwetu(mungu apishilie mbali). Mambo ya kisiasa yasiambatanishwe na dini kwasababu ipo siku kundi moja litakuwa na ugomvi na serikali na vurugu zikahamia miongoni mwa imani tofauti kama tunavyoona wahuni wa Misri walivyofanya.

Kama Brotherhood walivyokosa gurantee nasi hatunayo kuwa wapo watu watakaotofautisha imani zao na itikadi za kisiasa. Na wala vyama vya kisiasa havina gurantee hiyo na hivyo ni bora kuepuka tatizo kabla halijatokea.

Tusemezane
 
KWANINI CCM WAMEINGIWA NA ULEVI HUU USIO NA MFANO?

Katika mambo yanayonivutia na siasa za nje kama Marekani, Ujapan, India na Uingereza kwa uchache ni kiwango cha demokrasia ndani ya vyama vya siasa na masilahi ya taifa mbele kuliko kitu kingine.

Kuna mifumo inayotumika katika nchi hizi inayohakikisha kuwa masilahi ya vyama vya kisiasa yanalindwa lakini kwa namna yoyote ile hayapunguzi nguvu ya masilahi ya umma hata nukta.

Mathalan, unaweza kusikia shauri linakuwa partisan ndani ya seneti au bunge likimaanisha kuwa ni msimamo wa chama. Kuna masuala ya bipartisan yakimaanisha kuwa kuna haja ya kufikia muafaka kwa pande zinazohusika.

Kuna kitu kinaitwa binding resolution kwa maana kuwa maamuzi yanayo fungamanisha mtu na chama chake, na non binding resolution ambayo hayafunagamanishi mtu na maamuzi ya chama.

Tutolee mfano kidogo ili dhana hiyo ieleweke. Msimamo wa CCM ni serikali mbili na Chadema(serikali 3) huku CUF ikiwa inababaika. Misimamo hiyo yote ni Partisan.

Rais JK alipotangaza kuhusu rasimu ya katiba lile lilikuwa suala nje ya msimamo wa chama na lisilofungamana na siasa za chama(Non-binding resolution).

Alipowaalika Chadema na vyama vingine kuhusu suala la muafaka wa pamoja pale ilikuwa (Bipartisan) na kwa maana hiyo suala la katiba ni Bipartisan na non-binding resolution, kwa mfano mdogo.

Ni kwa msingi huo viongozi kama mawaziri wakuu, wakuu wa nchi n.k. wamekuwa wanalitolea maoni yanayopingana na misimamo ya vyama vyao. Hii ni kwa kuelewa suala la utaifa linatangulia na vyama ni baadaye na kwamba ni Bipartisan no-binding resolution.

Ni jambo la kusikitisha na kutia aibu sana kuona kijana na kiongozi kama Nape Nnauye amelifanya suala la katiba kuwa binding na partisan kwa chama. Hata wabunge wengi vijana tunaona wamekaa kimya bila kutoa misimamo yao kwa kuogopa vyama vyao kama CCM na Nape wanavyowatisha.

Katiba ni muongozo wa taifa usiojali mitazamo ya kiitikadi. Ni chombo kinachogusa maisha ya kila mmoja awe CCM, Chadema au CUF. Vyama vya siasa ni maeneo ya mapito lakini nchi ni makazi ya kudumu. Hakuna anayeweza kuweka masilahi ya vyama mbele ya masilahi ya taifa.

Kitu kibaya zaidi ni kuwepo kwa upotoshaji wa makusudi ili kukidhi matakwa ya kisiasa na hapa CCM. Nape alipaswa kueneza elimu ya uraia na suala la misimamo ya wananchi liachwe kwa wananchi.

Hakuna kamati yoyote iliyoundwa kushughulikia suala la muungano iliyokuja na msimamo wa chama. Hili Nape anapaswa kulifahamu. Hakuna kongamano lolote lililowahi kufanyika klkatoka na msimamo wa chama.

Kwa maneno mengine suala la katiba ni la kitaifa zaidi kuliko chama na wala halimfungi mbunge, waziri, mjumbe wa chama au balozi wa nyumba kumi kulitolea msimamo wake kwa maono na utashi wake

Hivi sasa wazanzibar wanaongelea kuhusu suala na mustakabali wa nchi yao.
Nape hana nchi ya kuiongelea bali chama cha kuongelea.

Ukweli inasikitisha sana na duru za siasa tunamwambia Nape huu ni usaliti wa hali ya juu sana wa utaifa na taifa lake. Hakuna mtu mwenye chama bila utaifa.

Tunajenga taifa la vizazi vyetu hivyo masilahi yetu yasitupeleke mahali pa kulisaliti taifa.
Nape anaamini nchi yake ni CCM na hivyo masilahi yake yapo CCM.

Nape sisi tupo na tunapita lakini Tanzania na Tanganyika zitakuwepo daima. Vyeo na nyadhifa ni mapambo ya kupita, walikuwepo, wapo na watakuwepo. Kipimo cha kiongozi bora si kuhusu antakeleza nini bali anasimami wapi linapokuja suala la utaifa.


Tusemezane


 
Last edited by a moderator:
TUNAPATAJE VIONGOZI ? UPANDE TUSIOUJUA

Kila siku uchaguzi unavyosogea tunashuhudia tambo, majigambo na kila mbinu za wanatarajia kugombea nafasi wakipigana vikumbo kujinadi kwa njia zisizo rasmi ili kuungwa mkono.
Kampeni za kichini chini zinafanyika kila mahali, harambee, misaada n.k.

Eneo linaloonekana kuchukua uzito wa kampeni hizo ni vyombo vya habari viwe magazeti, TV au social media kama forum na mablogu. Hizi zimetumika kikamilifu na watarajiwa.

Kuna mbinu ya kutumia vijana kwa kuelewa ni wapiga debe wazuri na wana njia (access) za vyombo mbali mbali. Makongamano yanafanyika, vijana wanakusanywa na kutoa matamko kuhusu kiongozi fulani.

Kinachoshangaza hoja ya matamko 'fulani anafaa kuwa rais'', yakitolewa pengine wanajua au hawaju maana ya uongozi.Tatizo wasilolijua ni kutoelewa kiongozi wa kitaifa.
Tumewazoea wabunge na madiwani wakisema' wanataka maendeleo'' kama kitu katika makontena

Kiongozi wa kitaifa anapatikana kwa kuangalia mambo mengi.
Inaonekana sasa kiongozi anapatika kwa kelele na wala. Watanzania hatujifunzi kutokana na makosa.

Kiongozi wa nchi hubeba dhamana kubwa ya maisha ya wananchi, alama ya taifa na ni chanzo cha ustawi wa jamii kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Awaniaye uongozi ni lazima ajiridhishe na aridhishe wananchi uwezo wake wa kubeba dhamana kama ilivyotarajiwa na ilivyo kisheria.

Kuna sifa za kiongozi zilizoanishwa kitalaamu na kijamii.
a)Kijamii kiongozi hajitambui hadi atakapoambiwa na umma awaongoze
b)Kiongozi husita sana kupewa jukumu kwa kujua uzito wa dhamana aliyopewa
c)Aanatakiwa aielewe jamii anayotaraji kuongoza katika matarajio na matatizo yake
d)Awe mwadilifu binafsi na kwa wenzake
e)Ajitambue kama kiongozi na si mtawala

Kwa kuzingatia sifa za kiutawala
i) Awe na maono na malengo (mission and vision)
ii)Uwezo wa kufanya maamuzi
iii)Aongoze kwa mifano 'active Member wa team yake ya uongozi'
iv)Uzoefu katika shughuli za umma hasa utawala(management)
v)Historia isiyo na shaka katika utendaji wake
vi) Alichowahi kufanya na kufanikiwa (achievement)
vii)Mwenye suluhu ya mambo yanayoonekana kutokana na maamuzi yake
vii)Sifa za kitaaluma zinazopambua uwezo wake wa kuyaangalia mambo tofauti

Hizo ni baadhi ya sifa ambazo hubadilika kutokana na mitazamo mbali mbali na hapa nasema si lazima ziwiane na kile mtu mwingine alichosoma au kusikia. Lakini kwa minajili ya mjadala hiyo ni inatosha

Nchi za wenzetu rekodi ya kiongozi katika kuongoza na kutoa maamuzi pamoja na vigezo vingine zinapatikana pale kiongozi huyo anapowania uongozi. Hapa kwetu ni ngumu kwasababu huko bungeni hakuna namna ya kubaini nani ana msimamo gani katika masuala ya taifa.

Ni kutokana na kukosekana kwa kumbu kumbu imekuwa ni vigumu kujua nani anasimama wapi na kwasababu gani katika mambo ya taifa. Ni kwa msingi huo mambo mazito kama rasimu ya katiba, ya kijamii kama madawa ya kulevya na kiuchumu kama miradi kushindwa malengo hayatolewi maoni bali viongozi hujificha nyuma ya vyama vyao.

Duru za siasa tunashangazwa sana na makundi au watu wanaopita wakisema kiongozi fulani antaufaa! swalli ni kuwa kiongozi huyo antufaa kwa vigezo gani? Kwanini tuambiwe anatufaa bila kuambiwa sifa zake alizo nazo? Tena wanaose haya ni wasomi,sajui huko vijijini hali ikoje.

Vyombo vyetu vya habari navyo ni matatizo tu. Katika hatua za kuchuja 'vetting' vyombo vya habari ni sehemu muhimu sana inayoweza kusaidia katika upataikanaji wa habari. Tunashangaa navyo kama wasomi hovyo vimejiunga katika kampeni za kipuuzi huku vikijiita mhimili wa nne wa dola.

Watanzania lazima tubadilike, tuache kupata viongozi kwa njia za khanga,pilau, bahasha au umaarufu tu wa mtu. Vinginevyo ipo siku tutapata viongozi wenye historia za uhalifu, ubakaji, wizi, uharamia na hata wageni wasio na sifa.

Kabla mtu hajasema fulani anafaa, tungependa atueleze kwanini anadhani anafaa na wala si kutamka hovyo 'abcd' ni kiongozi mzuri. Kiongozi si bwana harusi na hutahitaji uzuri wake.

Tusemezane



 
KWA HILI CHADEMA WAMEONYESHA UONGOZI

Suala la kuandaa katiba mpya ni moja ya mambo katika ilani ya Chadema. CCM hawakuwa na ilani hiyo.Chadema waliachia ajenda hiyo kwa serikali baada ya shinikizo la wananchi kuhusu kuidurusu kaiba.Kosa la Chadema ni kuacha likatekwa nyara na serikali lilikuwa kosa kubwa na duru tuliwalaumu

Mchakato ulipoanza Chadema walizembea kwa kuruhusu CCM kuutekwa tena bungeni na kuandaa mazingira ya kushinikiza hoja zao kupitia mabaraza ya kata na pengine bunge la katiba.
Hiyo ndio mbinu walioyabaki nayo kwasababu hawana ilani na wala hawakuchaguliwa kwa ilani hiyo

Rasimu ilipotoka CCM wakaanda waraka na kuusambaza kwa wananchama wao wakitaka serikali moja kama ilivyo sera(haikuwa katika ilani) ya chama chao. Waraka huo ni wa kushangaza kwasababu umeandikwa na kikundi cha watu bila ridhaa ya halmashuri kuu au hata mkutano mkuu wa chama.

Waraka huo unatokana na kauliza za mwenyekiti wa CCM aliyeanzisha mchakato pasi kuwa na maelekezo ya chama chake, wala kutokuwa katika ilani ya uchaguzi. Rais anatokana na chama tawala sasa sijui ni lini wanachama walipewa nafasi ya kuamua kuanza kwa mchakato wa katiba mpya, pili kuandikwa kwa waraka.

Pamoja na hayo katiba ni mwongozo wa mwananchi bila kujali itikadi ya kisiasa. Leo mwana CCM anaweza kuwa CDM na vivyo hivyo wa CUF kuhamia CCM. Katiba si jambo la chama ni jambo la utaifa, kulifanya la kichama ni hatari kubwa kwa mustakabali wa taifa.

Chadema pamoja na makosa ya nyuma hili wanonekana kulifanyia kazi kama uongozi na viongozi na inabidi tuwapongeze.

Chadema walikuwa na ilani , baada ya rasimu kutoka sasa wanazunguka kwa kazi kuu tatu.
1.kuwafafanulia wananchi nini kilichomo katika rasimu kwa lugha nyepesi na ya kueleweka.
2.Kukusanya maoni yao bila kujali itikadi za kisiasa baada ya ufafanuzi huo
3.kueleza wao wanafikiraje kuhusu suala zima.

Hiki ndicho kilipaswa kufanywa na chama tawala. Hata kama hawakuweza kuwa na ilani, mwenyekiti alipochukua agenda na chama kubariki ingawa ni ya mtu mmoja, CCM iliapswa kuonyesha leadership katika suala nyeti na la utaifa kama hili. Kwa bahati mbaya hawakufanya hivyo.

Kwa mshangao wao CCM wamewatuhumu Chadema kuendesha mikutano kwa minajili tuliyoeleza hapo juu. Upungufu wa CCM usiwe na kinga ya kutuhumu Chadema. Siasa za ushindani ndivyo zilivyo,mpinzani hutumia udhaifu wako. Hakuna shaka wananchi wana wawelewa vizuri na kupata taswira ya uongozi na viongozi.

Tume ya Warioba imesema haitafanyia kazi maoni ya mikutano ya hadhara.
Hatujui walilenga nini, ukweli unabaki kuwa maoni wanayokusanya Chadema watayafikisha kama baraza la maoni ya katiba.Bila kujali utaratibu unaotumika Chadema wamesimama vema na hawapaswi kubezwa.

Katika bandiko #308 tumeonyesha kwa uchache sifa za uongozi na kiongozi.
Sijaona mwanachama wa CCM aliyejitokeza japo kukemea utaratibu wa watu wachache kuwa chama, lakini eti bado tunapata majina lukuki ya watu wanaofikiriwa kuwania uongozi!!!

Hivi jambo kama hili halitoshi kubaini nani kiongozi na nani mviziaji?

Tusemezane
 
KWANINI TUNAFANYA KAZI ZA ZIMAMOTO KILA SIKU?

Kazi za idara ya zimamoto ni kukimbia katika eneo la tukio ili kuokoa na kuzuia uharibifu unaowezatokea.Katika siku na muda huo, zimamoto wanakuwa 'bize' kuliko wakati mwingine.
Baada ya tukio hurudisha magari na zana zao karakana na kusubiri tukio jingine pengine baada ya mwezi au mwaka.

serikali ya awamu ya nne ndivyo inavyoonekana kufanya kazi. Awamu hii ilianza kwa utaratibu wa kuunda tume kuchunguza matatizo na kwa bahati mbaya sana tume zikawa ni nyingi kiasi cha wananchi kuhoji kazi nyingine ya vyombo vya dola.

Kilichoishtua serikali ni taarifa ya tume ya Mwakyembe iliyoondoka na waziri mkuu Lowassa.
Hapo ikaonekana tume zinageuka kuwa shubiri.

Utaratibu ukawa kuunda tume na kufunika matokeo.
Leo hatuna majibu ya tume zifuatazo
1. EPA iliyoundwa na Mwanasheria mkuu, mkuu wa PCCB na IGP
2. Tume kuchunguza mikataba ya deep green, Meremeta na ufisadi mwingine
3. Tume kuchunguza wanyama walivyotoroshwa KIA
4. Tume ya kuchunguza mateso ya Kibanda na Ulimboka
5. Kamati ya polisi kuhusu ulipuaji wa bomu kanisani
6. Tume ya kuchunguza kufeli kwa wanafunzi

Hizi zikiwa ni baadhi tu ya mamia ya tume ambayo taarifa zake haziwekwi wazi hata siku moja.
Ujanja wa kuunda tume umejificha katika kupooza hasira za watu na pengine kuficha ukweli chini ya zulia kwani tume hizo huambiwa nini cha kufanya kabla ya kufanya uchunguzi.

Imefika mahali kila tukio linaundiwa tume kana kwamba nchi hii haina vyombo vya dola au kama vipo haviaminiki au havijui kazi zake. Nchi imebaki kuongozwa na tume na si utawala wa sheria.

Leo tumesikia wabunge wakichachamaa kuhusu tatizo la madawa ya kulevya lilivyoshamiri na kuharibu taswira ya nchi. Waziri husika anatoa majibu ya kutokuwa na uhakika na kile anachozungumzia. Siajabu kesho tutasikia tume inaundwa kuangalia wa tatizo.

Kila jitihada zitafanyika kuhakikisha kuwa suala hilo nyeti linamalizwa kama mengine ya meremeta na deep green. Tume iwe ya bunge au serikali itakalia taarifa na ''upepo utapita''

Inashangaza kwanini serikali iwe infanya kazi za zimamoto kila siku. Kuna taarifa za kufunga mitambo ya kukagua madawa siku za karibuni. Swali ni kuwa ni kwanini hakukuwa na uchunguzi siku za nyuma kuhusu suala hilo? Vyombo vya usalama vinafanya kazi gani hadi hali imekuwa mbaya kiasi hiki?

Wabunge wamechachamaa kuhusu madawa ya kulevya, huu nao ni uwajibikaji wa ajabu sana. Wabunge hao hao hakuna anayefuatilia kwanini tume zilizopita hazijatoa taarifa zao za awali?
Kuna tofauti gani kati ya kutoroshwa wanyama na madawa ya kulevya katika uhalifu?

Ni wazi kuwa bunge halijaiwajibisha serikali husika na limekuwa sehemu ya uzembe ule ule.
Labda hapa tuseme bunge la CCM kwasababu kila mara ni wabunge wa CCM wamekuwa wanapinga hoja za wapinzani wao wenyewe au kupitia Spika na naibu wake.

Hiawezekani nchi ikaendeshwa na kamati na tume. Vyombo vya usalama vinafanya nini?
Waziri husika kama wa mambo ya ndani kwanini asiwajibike japo kuonyesha uchungu kwa yanayotokea

Rais kwanini asiwawajibishe wakuu wa vyombo vya usalama au wateuzi wake kisiasa kwa kushindwa kumsaidia kutekeleza majukumu hadi yafanywe na tume au kamati? Ni lini rais atachukua hatua kama kiongozi wa nchi kuonyesha kuwa haridhiki na wimbi la maovu linaloshamiri nchini?

Matatizo yetu hayahitaji tume, kamati wala kongamano. Kinachotakiwa ni uwajibikaji wa vyombo husika. Msimamizi wa vyombo hivyo ni serikali na pale vinaposhindwa basi ni kushindwa kwa serikali.

Wananchi wa tanzania hawakuchagua viongozi wa kuongoza tume au kamati, wamechagua serikali ya kutatua matatizo yao kwa muda muafaka na mbinu muafaka wala si kazi ya zimamoto kama ilivyo sasa.

Tusemezane
 
MTAFARUKU WA SYRIA

Habari kubwa duniani ni endapo nchi za Magharibi zitaishambulia Syria kufuatia matumizi ya silaha za sumu zilizoua mamia ya watu hasa wanawake na watoto.

Marekani inaongoza jitihada hizo, kwa bahati mbaya mshirika wake mkubwa Uingereza imekataa kupitia kura ya bunge hilo iliyomtaka waziri mkuu Cameron kutotumia nguvu ya kimamlaka kutimiza azma hiyo(Prerogative power)

Mashabulizi yanonekana kuchagizwa na utumiaji wa silaha za sumu ingawa mgogoro upo muda mrefu sana na mamia wamepoteza maisha. Swali ni je, kuuawa kwa bunduki kuna unafuu kuliko silaha za sumu?

Rais Obama yupo katika shinikizo kubwa apeleke majeshi. Obama anakumbu kumbu zilizosababisha vita ya Iraq kwa tuhuma 'feki' za matumizi ya silaha za sumu. Yeye alikuwa mahiri katika kampeni kwa kulaani vita hiyo.
Kinachomtisha ni historia kutojirudia ingawa timu ya UN inakamilisha uchunguzi.

Pamoja na timu hiyo yapo madai kuwa wapinzani walitumia njia hizo ili kuhalalisha kuondolewa kwa Asaad.
Wapo wanaoamini kuwa aliyefanya hivyo ni Asaad kwani hata ndege za kivita zilitumika kuua watu seuse silaha

Obama alisita kuingilia mgogoro wa Syria kwasababu ilikuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe(civil war) ambayo wapinzania hawajulikani ni akina nani. Zipo taarifa kuwa Wasyria wenyewe siyo wapinzani bali makundi ya Alqaeeda yanayotaka kutumia fursa hiyo.

Swali ni kuwa baada ya kumuondoa Assaad ni nani atachukua nchi?
Woga wa Obama ni nchi kuangukia mikononi mwa Alqaaeda na kuwa tatizo kwa Marekani siku zijazo.

Kama ni hivyo je marekani itakapotumia mabomu ya mbali (Tom Hawk Missile) lengo litakuwa ni nini. Je, ni kumuadhibu Assad na kumwacha au kumuondoa na nchi iwe mikononi mwa watu wasiojulikana ni akina nani?

Hoja hizo ndizo zipo mezani kwa Obama na inaonekana hali ni tete sana. Wakati Obama akitafakari kuna uwezekano wa Syria kuishambulia Israel kama kulipa kisasi na wakati huo huo Iran kumuunga mkono.
Israel inaweza kutumia fursa kumshambulia Iran (vinu vyake vya Nyuklia), azma ipo isipokuwa Obama anaizuia.

Ikitokea Iran ikaishambulia Iran,mashariki yakati kutakuwa na hesabu za kuchanganya sana(complicated equation). Mgogoro utahusisha na kuvuta pande zisizohusika na kusambaa mashariki ya kati yote.

Duru tutaendelea kufuatilia kwa ukaribu hali inavyoendelea.

Kesho tutaangalia mzozo wa Jumuiya ya Africa Mashariki (EAC)

Tusemezane
 
asante mkuu kwa uchambuzi wa Syria, nasubiri kwa hamu uchambuzi kuhusu mzozo wa EAC
 
MGOGORO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Sehemu ya kwanza
Tunaelewa jumuiya ilianza kama pendekezo la shirikisho la kisiasa la Afrika mashariki wazo la Nyerere lililosababisha hata kuchelewesha uhuru wa Tanganyika.Kwa bahati mbaya wazo lilipingwa na Kenya na katika wabunge waliolikataa mmoja wao ni Mwai Kibaki mbunge wa Mkadara wakati huo ambaye alikuja kuwa Rais.

EA community ikaundwa mwaka 1967 ikiwa na nchi tatu. Kenya kama colon ilikuwa mbele kiuchumi na viwanda. Shughuli nyingi za kiuchumi zilikuwa nchini Kenya, washirika wengine wakiwa na sehemu tu ya shughuli hizo. Kupinduliwa kwa Obote na mzozo wa Tanzania na Uganda mwaka 1973 bado hakukutetesha jumuiya.

Aliyekuwa waziri wa sheria na mwanasheria bwana Charles Njonjo, tajiri na mtu mwenye ushaiwshi mkubwa alimshauri Kenyatta kuua jumuiya kwa hoja ya Kenya kuwa mbali kiuchumi na wengine kuwa tegemezi. Mwaka 1977 Kenya ikazuia kila kitu na kupeleka jumuiya kufa

Wakati huo uchumi wa Uganda chini ya Amin ulikuwa katika hali mbaya sana.Tanzania hali haikuwa mbaya kiasi hicho na niwakumbushe wana duru kuwa katika miaka hiyo noti ya sh 20 iliyojulikana kama pound sawa na pound 1 ya UK.Chimbuko la jina la dala dala ni kutokana na magari kufanya trip za mjini kwa kuiba iba wapiga debe wakisema safari ni dollar dollar ndipo neno dala dala likatokea. sh 5 ilikuwa sawa na dollar moja ya Marekani.

Baada ya kuvunjika kwa jumuiya Tanzania ilianza upya kwa kila kitu. Ununuzi wa mabehewa na Injini za treni, mawasiliano ya satellite posta na simu na ilibidi tuazime ndege kutoka msumbiji.Uchumi ulianza kuvurugiga kwasababu ya mikopo na ujenzi mpya wa miundo mbinu.
Nchi marafiki zetu kama China, Hungary zilitusaidia kuanza upya ujenzi wa uchumi

Kwa bahati mbaya mwaka mmoja tu uliofuata tukajikuta katika vita na Uganda jambo lililodidimiza kabisa uchumi wa nchi. Baada ya vita miundo mbinu ilikuwa katika hali mbaya na uzalishaji wa kilimo ulipata mtikisiko kwa kuzingatia kuanguka kwa bei katika masoko ya dunia kwa Pamba, Korosho na Katani.

Kuvunjika kwa jumuiya kulilazimu kufunga mipaka na Kenya.Kenya ikatumia fursa ya (black market) ikichukua 'advantage' ya uchumi mbaya wa Tanzania.

Hata hivyo kifo cha EAC kilikuwa na matokeo mazuri kwa upande mwingine. Tuliweza kuwa na viwanda vya bidhaa zetu wenyewe kama za nguo, mafuta ya kula, katani, vifaa na bidhaa (betri, viberiti, zana za kilimo,sabuni) , Mang'ula, Tancut Almas, Mufindi saw mill, Saruji, viwabda vya nguo n.k. Ilituchukua muda mfupi kuanza kujijenga bila kutegemea uagizaji wa bidhaa kutoka nchi za jirani ingawa hatukuweza kujitosheleza jambo lililozua ulanguzi wa bidhaa.

Rais Mwinyi alianzisha sera ya soko huria ikiwa na kufungua mpaka. Kenya ilipata soko kubwa la bidhaa zake Tanzania na kujifunza kuwa haiwezi kuwa na uchumi hutegemeana.

Makubaliano ya Rais Moi, Mwinyi na Museveni yalilenga kuijenga EAC kwa masilahi ya wananchi na si ya kisiasa, ushirika wa kisiasa ufuate baadaye. Ikaamuliwa kuwe na hatua za kufuata kuepuka matatizo ya awali

Viongozi walikubaliana kuwa kwanza taasisi za kiuchumi ziiimarishwe kama soko la pamoja la bidhaa, kuweka uwiano wa viwango vya ushuru, kuwepo kwa taasisi za elimu na afya katika miundo inayofanana na kuwa na benki kuu zinazowasiliana.

Nchi zilikubaliana kuwa makao makuu yawe Arusha yalipokuwa makao makuu ya jumiya ya kwanza.
Rais Museveni akaja na wazo la kuwa na jumiya kubwa kwa kushirikisha Rwanda na Burundi.
Wazo hilo lilileta mgongano kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa hofu ya instability ndani ya jumuiya.

Ikumbukwe kuwa wakati marais wakiwa Moi, Mkapa, Museveni na hata waliokuwa Kibaki, Kikwete, Museveni hali ya jumuiya ilikuwa tulivu sana na mipango ilikuwa inakwenda vema bila mitafaruku.

Tanzania ikaamua kuwa na maoni ya wananchi kupitia naibu wa waziri wa EAC Deod Kamala wakati huo. Wananchi wakaonyesha wasi wasi hasa kwa Rwanda baada ya kuhisi matatizo kuletwa na mataifa hayo mawili.

Ikaamuliwa Rwanda na Burundi ziwe washiriki wa mazungumzo. Wakati huo huo jitihada za kusuluhisha Burundi zikiwa zinaendelea Tanzania ikichukua usukani na Rwanda ikiwa inajikusanya kutoka mauaji ya Kimbari.

Ni rais JK aliyekubali nchi hizo zipewe uanachama akisema hilo ni jambo zuri hata pale wananchi.
Museveni akaitumia karata ya kuingia Rwanda na Burundi ili kupunguza ushawishi katika kupiga kura.

Ghafla Museveni akataka liundwe shirikisho la EA na yeye awe Rais wa Kwanza kwa kuzingatia ukongwe.
Wazo lilileta sintofahamu na kumalizwa kidiplomasia.Ni Tanzania iliyoonyesha shaka mataifa mengine yakiwa kimya.

Inaendelea shemu ya Pili...................................
 
Sehemu ya Pili
Kuingia kwa Rwanda na Burundi

Baada ya kupewa uanachama rasmi tukaanza tena kusikia mambo tofauti na msimamo wa marais walioianzisha jumuiya.Rwanda ikaja na madai kuwa makao makuu ya jumuiya yahamishwe kutoka Arush Sababu kubwa eti Nairobi ni kati kati .Wazo hilo halikuwepo kuanzia mwaka 1967 au ilipoanzishwa nyingine miaka ya 1990.
Ile AICC ilikuwa ni makao makuu tangu enzi na hoja ya Rwanda haikuwa na mashiko.

Kenya walikaa kimya kama beneficiary wa mpango huo, Uganda ikakaa kimya ikitegemea kutoa rais wa kwanza wa jumuiya na hivyo kuungwa mkono na Rwanda na Burundi. Ndiyo maana Tanzania ilihoji kulikoni?

Mtafaruku ukawa mkubwa baada ya viongozi kuazimia uundwaji wa shirikisho uanze haraka na suala la mwanzo ni kuifanya ardhi kuwa ya soko la pamoja. Tanzania ikauliza endapo hatujafikia kiwango cha soko la pamoja vipi tuanze na suala nyeti kama ardhi?Ikumbukwe kuwa katika nchi zote Tanzania ndiyo yenye rdhi kubwa.

Ilishangaza kuona Kenya na Uganda zilikuwa tayari kuingia vitani kwasababu tu ya kugombea kisiwa cha Migingo chenye squre km 1 kwa maana ya kutoweza jenga hata uwanja wa ndege. Vipi basi wenzetu wasionyeshe mfano wa pamoja wa soko la ardhi la pamoja?

Kenya ina eneo la km za mraba 580,327, asilimia 95 ya ardhi ikimilikiwa na asilimia 10 ya watu. Yaani asilimia 90 ya watu wanamiliki asilimia 10 ya ardhi. Uganda: Ina eneo la 236,040 km za mraba ikiwa na population ya 241/sqkm kwa kila watu 1000.Rwanda na Burundi twakimu zawo ni mbaya zaidi katika population/sqkm rwanda ikiwa na 430/sqkm in 1000

Tanzania ilikataa wazo hilo kwa msingi wa kuwa ardhi iondolewe ikifahamu kuwa nchi nyingine zilitaka kuchukua advatange ya kuhamisha raia wao kiholela na kuleta mizozo huku tayari tukiwa na mizozo ya ardhi.
Hili liliwachukuiza sana wanachama wengine.

Kenya ikaanza kampeni za kuichafua Tanzania kwa kutumia msemaji asiye rasmi ambaye ni mwandishi wa makala za magazeti Kamau Warigi. Tanzania ikaandikwa katika magazeti kama the Economist ikichafuliwa kwa lengo la kusihinikiza ikubaliane na matakwa ya ardhi. Huo ni ukweli usio na shaka.

Ikaja hoja nyingine ya kuruhusu watu kwenda sehemu moja kwa kutumia vitambulisho. Hoja hii ililenga kuzunguka ile ya ardhi kwa kutambua kuwa vitambulisho vinaweza kuchongwa popote. Kiusalama hilo halikuwa jambo jema na hasa tukizingatia Tanzania haina vitambulisho. Ni hoja ile ile ya ardhi inayoletwa kwa mlango wa uani. Tanzania ikasema kama wapo walio tayari basi wanedelee na sisi tutaungana tukiwa tayari.

Kenya ikaanzisha utaratibu huo na Rwanda bila wanachama wengine.
Ikjazuka hoja ya visa za wageni kutolewa sehemu moja na kuwaruhusu waingie sehemu nyingine.
Tanzania na Kenya ndizo zenye watalii wengi. Kenya ilitaka kuchukua advantage hiyo kwa kukusanya mapato ya watalii kisha waingie Tanzania bila malipo kama watemebeaji na kurudi Kenya pengine baada ya siku moja.

Tanzania ikasema haiwezekani ni muhimu kila nchi ichukue visa kivyake kwasababu haitarajii kunufaika.
Hili nalo limewaudhi hasa Wakenya. Juzi wakaamua kuwa na single visa entry lakini Kenya imeikatalia Rwanda kwasababu zile zile za Tanzania kuikatalia Kenya. Kwamba hakuna manufaa ya single visa entry na Rwanda isiyo na watalii. Hapo unaweza kuona kwanini mtafaruku unazuka.

Ni hoja za kiuchumi na kijamii ingawa haziwekwi wazi. Kinachosemwa ni Tanzania kusita 'dithering' katika kufikia shirikisho halisi. Ukweli ni kuwa Tanzania ipo tayari lakini kwa kuzingatia historia ya nyuma ya EAC na ujanja unaotumika na wanachama wengine ni lazima ichukue hadhari mapema ili isije ikawa exploited.

Lakini pia lazima yujuilize endapo tulishindwa kuwa na ada za viwango sawa kwa wanachama katika Unibersity kwanini tudhani single visa entry inaweza kufanya kazi?

Tujiulize hivi tunawezaje kukimbilia shirikisho huku tukiwa hatujaweka mambo ya taasisi kama za kibenki, miundo mbinu na sarafu katika hali inayokubalika. Na kwanini yawepo mambo ya kipaumbele nje na yale yaliyoazimiwa na akina Museveni, Mwinyi na Moi kuhusu kujenga jumuiya kwa msingi wa wananchi?

Je, tumefikia hatua gani katika kuhakikisha kuwa watu na mitaji vinaweza kuhamishwa bila kueteteresha chumi za nchi husika? Na je, leo tunapoona kuna wahamiaji haramu 21,000 kulikuwa na umuhimu wowote wa kukimbilia suala la ardhi bila kwanza kuhakiki raia na uaratibu wa kuhama kwa watu na mitaji?

Vipi kama leo wahamiaji hao 21,000 ambao ni idadi chache wangepata vitambulisho vya uraia wa Tanzania, je, huo ndio utaratibu unaotumika katika jumuiya kama EU? Na je nani angekuwa katika wakati mgumu miongoni mwa wanachama wa EAC?

Tutaendlea na sehemu ya TATU Kuhusu mzozo huu na hapa ulipofikia.

Tutaendelea......
 
Mkuu Nguruvi3, nashukuru kwa uchambuzi wako murua kabisa, nasubiri sehemu ya tatu ili utuweke kwenye 'board' na sisi wengine. Hata hivyo, ningependa pia uhusishe juu ya "Mediation Agreement" baada ya kuvunjika ile ya mwanzo iliyosainiwa mwaka 1984 ikibidi na kilichokuwemo kwenye hayo makubaliano.

Wakati nikiwa nasubiri sehemu ya tatu, ningependa kugusia maeneo machache ikiwa pamoja na kujumuishwa Rwanda na Burundi. Kimsingi si kosa kuzijumuisha nchi hizo katika Jumuiya na nimepitia Mkataba wa Jumuiya japo kwa haraka, nimebaini kwamba Mkataba uko vizuri katika kuruhusu wanachama wapya ila huenda unakosa tafsiri sahihi kutoka kwa wataalamu wetu. Hizi nchi zimeruhusiwa mapema sana kuwa mwanachama kamili mwenye nguvu sawa kama walivyo sasa, hili ndilo kosa la kwanza lililofanywa (ambapo umeelielezea vizuri kwamba kulitokana na sifa za kirafiki zaidi na si za kijumuiya). Vilevile, kutokana na kukosa tafsiri sahihi ya Mkataba wa Jumuiya na pia kuwepo kwa "specific goals" kutoka kwa baadhi ya nchi wanachama kunachangia sana katika kudhorota kwa Jumuiya hiyo kwa sasa.

Hakukuwa na sababu za kutaka "kuandika rekodi" ya kuwa Rais wa kwanza wa Jumuiya; hakukuwa na sababu ya kuzungumzia ushirikiano wa kisiasa pasipo kuwa na uimara wa ushirikiano wa kiuchumi; hakukuwa na sababu za kufikiria ushirikiano wa suala la ardhi pasipo kufikiria uzalishaji unaotokana na ardhi; hakukuwa na sababu za kufikiria namna rahisi ya watu kutembeleana pasipo kuwa na sababu za msingi za watu hao kutembeleana(rejea matumizi ya vitambulisho).

Ni kutokana na "specific goals" hizo kutoka nchi wanachama ndizo zilizoifanya Tanzania kufikiria tofauti katika ushiriki wake katika Jumuiya.

Kwa muda mrefu kumekuwa na jitihada za kuwa na Community-based integration badala ya inter-governmental organization kama ilivyo sasa ili kufanikisha jitihada hizo baada ya kuona Tanzania imeshtukia mbinu hizo (sidhani kama Tanzania itakubaliana na wazo la kuachana na Intergovernmental organization model). Kuwapo kwa "trilateral agreements" ni uthibitisho kwamba hizo ndizo nchi ambazo zimekuwa na "specific goals" ndani ya Jumuiya, na kwa kuwa malengo hayo yameelekea kutofanikiwa, wanarudi kwenye malengo ya msingi ya Jumuiya ambayo ni "economic", lakini kwa kutaka kuitenga Tanzania ambayo imetibua malengo yao.

Katika hali hii, Tanzania ina namna kadhaa nzuri za kufanya kwa sasa ili kujiweka katika nafasi nzuri. Kwanza isifikirie kujitoa kwenye Jumuiya kwani inaweza kupata kilichoikumba UK kule Ulaya; badala yake ifanye "sailent reforms" kwa kuondokana na dhana ya ushirikiano wa kisiasa na kujiimarisha kiuchumi ili kuendelea kufaidika na makubaliano yaliyopo (Customs Union, Common Markets). Ifanye uchambuzi wa kuangalia ni bidhaa gani ndizo kipusa kwa kuuza soko la Afrika Mashariki na bidhaa gani inaagiza zaidi kutoka nchi hizo ili kuimarisha sekta hizo. Kuimarisha miundombinu ya Reli, Barabara, Bandari na Nishati ili kukidhi mahitaji ya Viwanda na Baishara.

Mashirikiano ya kibiashara ni 'dynamic trends" kwa sasa kwani hayataegemei Serikali inaamua nini bali inafanya nini. Kwa msingi huu, biashara inategemeana na faida watakayopata wafanyabiashara sio maadui iliyonayo serikali. Tanzania ikijipanga katika namna hii ni wazi kwamba, Trilateral Agreements itakufa kifo cha kawaida na kurejea kwenye ujenzi wa Jumuiya ya kweli yenye kuimarisha uchumi sio uhuni.

Lakini pia wataalamu wa Tanzania waandae hoja madhubuti ya kupata tafsiri ikibidi iingizwe kwenye Mkataba maana ya "....ultimately political federation...". Kwa kuwa hakuna timeframe, maana halisi ni kwamba kufikiwa kwa hatua ya ushirikiano wa kisiasa ni kuimarika kwa hatua za mwanzo lakini inaonyesha nchi nyingine hazitaki kuelewa hivyo kwa kuwa wao macho yao kwenye "shirikisho la Kisiasa". Tafsiri sahihi ya kiwango cha kuingia katika shirikisho la kisiasa kitasaidia pia katika kuimarisha uchumi kama kweli wana nia hiyo.

Sasa hivi, nimesikia wanajadiliana kuanzishwa kwa sarafu moja, lakini nikiangalia economic trends hususan macroeconomic indicators, sioni viability ya kuhimili sarafu ya pamoja.

Vilevile, wasifanye kosa la kuruhusu Sudan Kusini na Somalia kuwa wanachama kamili wa Jumuiya kwani kwa kufanya hivi wata-divert trade movements kutoka central corridor to northern corridor ambayo itachangia kuwepo kwa return ndogo katika uwekezaji wa kimiundombinu kwa Tanzania. Hizo nchi ziwe observer tu na zijue kwamba anayekataa kwa wao kutwaa uanachama kamili ni Tanzania ili waanzishe bilateral talks na Tanzania ziwaridhie kwa "masharti". Kwa kufanya hivyo, Tanzania itaweza kuwa na fursa ya kuandaa masharti ya kidiplomasia na nchi hizo kabla ya kuwa wanachama ili zisje kuwa "crisis" nyingine kwa Tanzania kama tulivyokuwa wepesi kuwakubalia Rwanda na Burundi pasipo masharti ya kidiplomasia.

Pia, kuna haja ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara na Burundi ikiwa pamoja na kutoa conscesional rates kwa wafanyabiashara wao kwa huduma za kibiashara zinazotumia miundombinu yetu (strategic move) ili kuwahakikishia utayari wa Tanzania katika kushirikiana nao kibiashara. Aidha, mchakato mwingine... (wacha nisubiri part three yako mkuu).
 
MGOGORO WA AFRIKA MASHARIKI
Sehemu ya tatu

Kabla ya kuendelea na sehemu ya tatu, tuungependa kurejea hoja za Zinedine katika bandiko lake #314.
Tukumbuke kuwa uhusiano wa nchi za Afrika mashariki haukuanza leo(Kenya, Tanzania, Uganda).
Kulikuwa na taasisi nyingi zilizoziunganisha nchi hizi hata kabla ya uhuru.

Bila shaka mkoloni alielewa kuwa tamaduni, uchumi na maisha ya kijamii yaliwiana sana katika nchi hizi.

Ujenzi wa reli ya Kenya-Uganda ulianza mwaka 1897-19001, makusanyo ya ushuru 1900, Bodi ya fedha 1905, Posta 1905, mahakama ya rufaa 1909, muungano wa forodha 1919,bodi ya magavana ya EA 1926, Bodi ya mapato ya pamoja 1940 na baraza la pamoja la uchumi mwaka 1940.

Mwaka 1977 mkataba wa kuizika rasmi iliyokuwa jumuiya ulifikiwa.
Sababu zilizotajwa za kuvunjika kwa EAC zilikuwa kukosekana kwa utashi wa kisiasa(lack of strong political will), kushindwa kushirikisha sekta binafasi na vyama vya kijamii katika shughuli za jumuiya, mgawanyo usio sawa wa faida miongoni mwa wanachama kutoka na tofauti zao za maendeleo na kukosekana kwa sera za kutafutia ufumbuzi matatizo yaliyojitokeza.

Kifungu hiki ni kuhimu sana kwasababu matatizo yanayojitokeza leo ni sawa na yale ya mwanzoni na viongozi hawaonekani kujifunza kwa hilo.

Tatizo moja ni hili la kukosekana kwa utashi wa kisiasa. Tulipokuwa na EAC ya wanachama watatu tuliweza kutafuta suluhu kama ilivyokuwa kwa mgogoro wa Kenya wa kisiasa. Tutalifafanua vema mbele ya safari


Tarehe 14/5/1984 ulisainiwa mkataba wa suluhu ''the mediation agreement'' kwa ajili ya mgao wa mali na madeni ya iliyokuwa jumuiya hiyo na kuvunjika mwaka 1977.

Katika mkataba huo nchi husika zilikubaliana kuangalia maeneo mengine ya ushirikiano na kuweka utaratibu wa ushirikiano huo kwa siku za baadaye.

Mwaka 1993 ikaanzishwa tume ya kudumu ya nchi permanent tripartite commission' ili kuanzisha ushirikiano wa kicuhumi, kijamii, kisiasa, kiulinzi na utamaduni kwa azimio lilifikiwa na marais wa nchi hizo.

Tarehe 26/11/1994 ndipo itifaki ya kuanzisha sekretariati ya kudumu ya nchi hizo iliafikiwa ili kuangalia mambo ya uhamiaji, fedha,miundo mbinu na huduma uliosainiwa na marais wa nchi tatu 26/4/1997 na kupitisha mpango mpango wa maendeleo kwa mambo tajwa kwa mwaka 1997-2000.

Kwa kumbu kumbu hapa ndipo passport za EAC zilipoanza, kulegezwa kwa masharti ya kusafiri, kuwa na ujenzi wa miundo mbinu kama ule wa Arusha Namanga, Namanga-Nairobi ambao unajulikana kama Thika super highway.

Katika mpango huo wa 1997-2000 nchi za EAC zilikubaliana kuweka mazingira ya maendeleo ya watu, kuvutia wawekezaji, jumuiya za kiraia na mpango wa maendeleo kwa kuzingatia menejemnti kama ulivyo katika mkataba wa Marrekesh wa shirika la biashara duniani (WTO)

Ni kutokana na spirit hiyo ya ushirikiano, Kenya waliweza kuingia katika soko la Tanzania kama wawekezaji namba mbili baada ya Uingereza, na vivyo hivyo kwa nchi nyingine
Hadi hapo nadhani Tutakuwa tumejaribu kujibu baadhi ya hoja za mwanaduru Zinedine japo kwa uchache.

Ni wazi kuwa nchi tatu zilikuwa zinaendelea vizuri sana kwa kutengeneza ushirikiano uliohusu wananchi kwa misingi ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni.


Hii haina maana kuwa kulikuwa hakuna matatizo, la hasha, yalikuwepo lakini yalishughulikiwa kidiplomasia na kumalizwa kabisa.
Kwa mfano, Kenya walitaka mambo ya kiuchumi yaende haraka haraka bila kujali nchi zingine, Uganda ikitaka kuwepo na shirikisho la kisiasa na Tanzania ikisema twende kwa uangalifu ili kuepuka matatizo ya mwaka 1977 ambayo ni sehemu kubwa sana ya uchumi wa taifa hili kuangauka.

Tukumbushe kuwa wakati wa mzozo wa Kenya , Tanzania ilishiriki sana katika kutafuta suluhu kama mwanachama wa EAC. Na katika uchaguzi uliopita wa Kenya, Tanzania ilisimama kidete kuiomba jumuiya ya kimataifa imwache Uhuru agombee urais kwa kutumia ushawishi wa EAC licha ya kwamba alikuwa na kesi kwa moyo wa EAC(Spirit of EAC)

Nchi hizi tatu zilifikia mahali pa kuwa na makubaliano ya kijeshi kuwa mmoja akishambuliwa ni jumuiya yote imeshambuliwa. Katika nyanja za kimataifa nchi hizi zilikubaliana kulingana na matakwa ya EAC.

Kwa mfano Kenya ilishiriki IGAD wakati Tanzania ikifundisha askari wa Somali, Uganda nayo ikiwa na jeshi Somali kama sehemu ya AU. Yote yalifanywa bila kunyoosheana vidole, matusi au kejeli.

Ni ushirikiano wa aina hiyo ulioruhusu wananchi wa Kenya, Uganda na Tanzania kufanya shughuli zao bila vikwazo na kuwavutia Rwanda na Burubdi kuomba kufikiriwa uanachama

Nini kimetokea baada ya Rwanda na Burundi kupewa uanachama wa kudumu?

Tuangalie sehemu inayofuata hapo Kesho.......

Itaendelea...







 
MZOZO WA AFRIKA MASHARIKI
Inaendelea...

Mkataba wa awali ilikubaliwa kuwa jambo lolote lazima lipate baraka za washirika wa jumuiya na kwamba nchi anzilishi zilikuwa na kura ya 'veto'

Kujiunga kwa Rwanda na Burundi kuliongeza nguvu ya upigaji kura wa baadhi ya masuala.
Hicho alichokuwa anakitaka Museveni na Kenyatta ili kusukuma ajenda zao, Museveni akitaka shirikisho na Uhuru nguvu za kiuchumi kwa nchi zao.

Suala lililoleta utata zaidi ni la ardhi ambalo kila mmoja atanufaika nalo isipokuwa Tanzania.
Ardhi ya Kenya inamilikiwa na masetla, Uganda Rwanda na Burundi zikiwa na mifumo isiyojulikana na population zinazokuwa kwa kasi

Kurudishwa kwa wahamiaji haramu ni ushahidi kuwa wenzetu walishatanguliza watu wao na sababu za kutaka vitambulisho vitumike kwa raia kusihi popote zilikuwa na manufaa ya siri kwao na si kwa Tanzania.

Tanzania ilisema anayetaka kuwa na ushirikiano na mwingine aendelee wakati ukifika tutaungana nao.
Hii ni kufuatana na kifungu cha mkataba wa EAC kinachosema nchi wanachama wanaweza kuwa na mashirikiano nje ya yale ya EAC

Kenya wana mashirikiano na Rwanda kuruhusu watu wao kwenda kufanya kazi kwa vitambulisho tu bila kuzuiwa. Tanzania ilikuwa na mashirikiano na Kenya kuhusu ujenzi wa miundo mbinu kama bara bara ya Arusha-Namanga-Nairobi. Hilo halijawahi kuwa tatizo

Kenya wana ushirikiano na Uganda,na Tanzania ilikuwa katika mpango wa kujenga reli ya Dar-Isaka-Kigali hadi Bujumbura. Zote ni jitihada za kuimarisha ushirikiano wa kimakundi ndani ya EAC.
Ushirikiano wa makundi ni sehemu ya mkataba wa EAC.

Pia kuna kifungu kinachoeleza ujirani mwema na kusuluhisha mizozo miongoni mwa wanachama kwa njia za majadiliano na maelewano

EAC imekuwa na mizozo ya kisiasa ikihusisha mambo ya ndani. Mzozo wa Uganda na Kenya ulisuluhishwa katika spirit ya EAC. Kuleta makundi kinzani nchini Burundi ilikuwa ni sehemu za kazi za EA kama ilivyo Rwanda

Kipengele hicho ndicho kilitumika na Rais JK kuishauri Rwanda ikae pamoja na waasi.
Ushauri una pande mbili kukubaliwa au kukataliwa. Hata kama kungekuwa na hitilafu miongoni mwa wanachama bado njia za kidiplomasia na ujirani mwema kama ilivyoanishwa katika mkataba zilipaswa kutumika.

Ndivyo Tanzania imekuwa inafanya miongoni mwa wanachama wake.

Mzozo uliozuka kati ya Rwanda na Tanzania ni katika kukosa umakini wa kuangalia vifungu vya mkataba. Rwanda ikachukua hatua za kupotosha maana ya ujirani mwema na usuluhishi kwa njia za amani.
Ikaingia katika siasa za mapambano kama inavyoendelea kujidhihiri.

Tulitegemea wanachama kama Uganda na Kenya kuingilia kati suala hili. Kukaa kwao kimya kuna maana mbili, ima kuuunga mkono Rwanda au kutaka kutimiza haja zao za kisiasa na kiuchumi ambazo Tanzania imeonekana kama kikwazo. Hapa tunasema kulikuwa na jitihada za chini kwa chini za kuidhoofisha Tanzania kimsimamo kilichokuwa kinasubiriwa ni sababu tu!

Sababu imepatikana na haraka haraka tukasikia ushirikiano wa nchi Tatu, Tanzania ikiwa imeachwa.
Tunaweza kusema pengine ni kwasababu Tanzania ilisema wanaoweza kuendelea na waendelee na hiyo ni haki yao, au inawezekana ni kutaka kuishinikiza ili ijiunge na ushirikiano huo kukiwa na shinikizo la wanachama hao watatu juu ya Tanzania kulegeza msimamo wao hasa katika mambo ya ajira na ardhi.

Wapo wanaosema Tanzania imetengwa. Hili si sahihi kwasababu ushirikiano wa Kenya na Rwanda haukuitenga
nchi zingine wala ushirikiano wa reli ya Dar Isaka haukulenga kutenga nchi nyingine.

Kinacholeta utata ni masuala ya kiuchumi kufanywa kuwa ya kisiasa zaidi na hapo ndipo hatari ya shirikisho ilipo. Siasa hutoa suluhu ya muda mfupi na uchumi hutoa suluhu ya muda mrefu.

Jambo la wazi ni kuwa wanachama wengine pengine ukiacha Burundi wameshabikia mzozo bila wao kujua madhara yake ndani ya shirikisho. Yes wanaweza kuwa na mikakati ya pamoja na ya haraka lakini swali ni je, mikakati hiyo ni 'people centered' kwamba ni kwa manufaa ya mwananchi wa kawaida kabisa wa EAC?

Jambo moja la kubaini hapa ni kuwa wakati nchi tatu (Kenya, Rwanda na Uganda) yamekuwa na mashirikiano ya haraka suala la ardhi halipo katika ajenda zao. Suala hilo huzuka pale tu Tanzania inapokuwa mezani.
Kwanini basi wao wasianze nalo kama lilikuwa muhimu kwao?

Tunachokiona ni ushirika wa hasira kwasababu za kisiasa. Kenya wanaushindani wa kiuchumi na Tanzania na hivyo Suala lolote linaloidhoofisha Tanzania linaonekana kuwa na manufaa kwa Kenya.

Uganda inacheza karata zake kwa Kenya na kuiangalia Rwanda zaidi Kisiasa na si kicuhumi.
Nchi hizi zinatafuta manufaa ya kisiasa na kiuchumi huku Rwanda ikitafuta manufaa ya kisiasa zaidi.
Je, Rwanda inafaidika kiuchumi zaidi ikishirikiana na Kenya au Tanzania?

Kiuchumi hapa tunaongelee watu wa kawaida wa mataifa hayo si matajiri wenye biashara za mitaji mikubwa.
Kwa mwananchi wa kawaida ushirikiano huu unaopigiwa debe sasa una manufaa kwa muda mfupi na si mrefu.

Tanzania ina mpaka na nchi zote za EAC pamoja na 4 wanachama wa SADC.
Bado inabaki kuwa kiungo muhimu sana katika jumuiya.
Kwa hali yoyote shughuli za kicuhumi za Kenya ni kubwa nchini Tanzania kuliko nchi nyingine.
Ndivyo ilivyo kwa nchi nyingine pia.

Kinachoamua ushirikiano si matakwa ya kisiasa ni nguvu za soko na uchumi. Kwa mwananchi wa kawaida uhuru wa kufanya shughuli zake nchi zote ni muhimu sana kuliko katika baadhi ya nchi.
Hivyo ni nguvu ya soko itakayozilazimisha nchi hizi kurudi katika mstari na si maamumuzi ya kisiasa.

Leo kuna wawekezaji wa Kenya kwenye soko la watu milioni 43 Tanzania.
Hawa hawataridhika kama kuna misuguano au Kenya itakata mahusiano ya kicuhumi na Tanzania kwa ajili ya soko la Rwanda au Uganda pekee.

Lakini pia ieleweke kuwa katika nchi hizo ushindani utakuwa mkubwa na lazima wananchi watatafuta fursa nyingine. Ni wananchi hao watakaoshinikiza nchi zao kurudisha mahusiano na Tanzania kwasababu ni wao wanaoathrika na si Watanzania peke yao.

Katika hali iliyopo ni makosa kwa Tanzania kuhamaki na kutafuta njia za kuwafariji watatu hao.
Ili mradi bado ni sehemu ya EAC, Tanzania ifanye yale yenye manufaa kwake na kuacha mengine yaendelee kwa kila mmoja.

Uingereza ni mwanzilishi wa EU lakini hatumii sarafu ya nchi hiyo na hilo si kosa.
Zipo nchi za EU hazitumii visa ya Shengen n.k. Tanzania inaweza kuwa sehemu ya EAC lakini isiwe sehemu ya maamuzi yasiyo na tija kwa upande wake

Ikiwa Tanzania itahamaki, basi hilo litawapa nguvu washirika wengine kushinikiza mambo wanayotaka wao na wala si kwa manufaa ya Tanzania.

Tanzania itumie fursa zake kijiografia kwa kuwa sehemu ya SADC na EAC, kuimarisha miundo mbinu na kuweka mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji. Nguvu ya soko ndiyo itaamua hatima ya ushirika na wala si kisiasa.

Tumeshaona tayari kumekuwa na maamuzi ya kuatatanisha kuhusu visa ya pamoja(single visa entry) miongoni mwa wanachama hao watatu. Tayari Kenya inaikatalia Rwanda kuhusu mapato.

Kitendo cha ujenzi wa bandari hakitaweza kuwa kivutio cha wafanyabiashara.
Umbali na gharama ndizo zinaamua wananchi watumie njia gani.

Tanzania ikijizatiti katika hilo kama kuimarisha miundo mbinu ni rahisi kwa wananchi wa nchi jirani kutumia miundo mbinu yetu na soko letu na hivyo kutuhitaji. Hakuna mfanyabaiashara au taasisi ya huduma itakayokuwa tayari kuacha soko la watu milioni 43 na kujikita katika soko la ushindani lililojengwa katika misingi ya kisiasa.

Tusemezane

 
Asante sana mkuu Nguruvi3 kwa uchambuzi makini wa hii ishu ya EAC.
Watu wamehamaki sana kutokana na Rwanda na Uganda kujitoa kutumia bandari yetu ya Dar Es Salaam wakihisi kwamba tunatengwa na tutatetereka kiuchumi. Mimi nadhani ni wakati muafaka wa kujipanga na kutumia fursa zetu zilizopo kujiimarisha. Kama jumuiya ya mwanzo ilipovunjika mwaka 1977 ilitusaidia kujitambua na kuimarisha vyanzo vya uchumi, ni wakati muafaka sasa kutumia fursa zilizopo kujiimarisha zaidi. Hawa jamaa bado wanatuhitaji sana tu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3 asante kwa bandiko lako makini.Ombi maalumu je inawezekana ukachapisha nondo hizi kwenye magazeti kama Raia mwema,Mwananchi..... na magazeti mengine mengi ili wananchi wasiotembelea mitandao ya kijamii wakachota elimu ?.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom