Nakubaliana na wewe ndugu Mkandara,however ni wazi kwamba mfumo wa kibepari pekee,yani bila social elements, una "foster" hizo tabia za ulafi...Ndo maana kwenye mfumo huo,gap ya masikini na tajiri ni kubwa.
Let's be honest.. Ebu nambie ni nchi gani duniani iwe ya Kijamaa/Kibepari ambayo matajiri Wanaoshika uchumi ni asilimia hata 10%? - Nambie hiyo nchi iwe ya kijamaa au Kibepari!, nadhani bila shaka hakuna kitu hii.. that's the truth on the ground tuache hizi siasa za maandishi ya kiimani.. Dunia nzima nchi zote ziwe ktk Ujamaa au ubepari, Utajiri umeshikwa na watu wasiodizi asilimia 1 hardly 2..Kinachotazamwa zaidi ni ktk siasa hizi mbili ni ujenzi wa middle class yaani kundi la kati baina ya Wafanyakazi na matajiri. Yaani kundi linalotoka ktk umaskini na kwenda kati na ukichunnguza sana utaona Ujamaa unawaondoa watu toka ktk Utajiri kuwarudisha ktk umaskini. Ujamaa ni wa wanyonge, maskini kama nchi ni tajiri huwezi kukuta wanazungumzia Ujamaa. Ujamaa ni kwa wale walioonewa, kuporwa mali zao na sio kwa nchi tajiri inayotaka kuwapa wananchi wake maisha bora..then first youmake them your enemy number baada ya mkoloni..
Hivyo katika Ubepari kuna matajiri wachache na Ujamaa pia kuna matajiri wachache vile vile.. Na mkuu wangu - ULAFI humpata yule anayezuiwa zaidi ya yule alokuwa huru.. Kama friji Open huwezi kuwa mlafi sema yule ambaye chakula kwa kuhesabiwa lazima kuuna walafi wengi zaifdi..Mtoto unayemfungia ndani kila siku akiishi kwa amri kama kuku, siku zote ndiye mlafi na siku ukimwachia kidogo tu ndio siku anaondoa shauku zake zote kwa ulafi ulokuwa nao. Huyu ndiye Mlafi zaidi ya yule ambaye yuko huru unless ana matatizo ya akili,, amini maneno yangu sii tunawaona watoto wa ma gate makali, Wasomali na Waarabu huku majuu wnavyoharibikiwa. Hawa ni wabaya zaidi ya unavyofiria kwa ulafi maana wanataka kumaliza vyote kabla hawajarudi handakini. Hii ndio hekima aloificha Mungu juu ya umuhimu wa Uhuru wa mwanadamu, unampomkataza sana kitu, ukamnyima ndivyo anavyozidi kuwa curious, anavyokitamani zaidi na kuwa sehemu ya fikra zake kila siku.. Just set them free, weka miiko na maadili then let them face the music - akiharibu anakuwa grounded!
That's another fact on the ground twende Russia, China au Korea kwa kina Mao, Lenin, Kim hawa wote walikuwa Putin hawa wote they lived large all the time, wakiendesha maisha yao ya juu sana. Pengine waliokuwa wasafi ni Revolutionary na Pan Africanist kina Nyerere hapa nampa sifa zote mzee wetu maana hawa waliweka goals back then lakini nao wakawa victim of the same Ulafi wa wengine baada ya hapo hawakuwa na mwendelezo zaidi ya Idea za Kujikomboa. Na wataondoka hawakukamisha lolote maana walafi wameisha ingi
Ujamaa kwanza tulikuwa na serikali kubwa sana ku run everything under their watch na kila kiongozi ngazi zote walikuwa matajiri ukitazama asilimia ya uzalishaji vs fedha wanazotumia wao ni zaidi ya asilimia 70 kuendesha maisha yao wao.. Walikuwa wakipewa nyumba bure, usafiri bure na dereva, mpishi, gardener, shopping ya nguo na Chakula utadhani they were Mafia Mob. Akipita kiongozi lazima msimame wima kwa nidhamu ya woga na kuushusha uso chini ati tukiitana ndugu..Haya mambo yalitakiwa tuwafanyie wakoloni na walowezi sio kuwageuzia kibao wananchi wako na kuwa nyie tena ndio mabeberu, mkiwakunja mwananchi wa kawaida wanyonge hawawezi kumshitaki kiongozi wa chama cha zidumu fikra za mwenyekiti!.
JMushi! tumeishi ktk maisha hayo ya kuogopa hata kukutana na polisi ukiwa na mfuko wa khaki wa sukari..Wengine tumelala ndani kwa amri ya Meya tu ati ulitembea na mwanaye basi unaenda kulala jela siku saba. Tunapigishwa push up na kurushwa kichura kwenye mageti kwa sababu hujamkatia mlinzi wa mzee ulipochukua binti yake out..na mambo haya yanaendelea hadi leo huko North Korea. Na kibaya zaidi ktk Ujamaa watu wanaficha mali ili ku create Uhaba wakati vitu hivyo vinasafirishwa nchi za jirani. Mwananchi hana Unga lakini wazee wa Ikulu wanakula kuku kwa mrija, Champagne na Carviar kina Kim na Cuban Sigar hawajawahi kula ugali wa njano na harage!
Mkuu tumeishi maisha hayo japokuwa mimi mpenzi mkubwa wa Nyerere lakini sikubaliani kabisa na fikra za serikali kushika umiliki wa mali za watu hasa wananchi wake.. Hapana hii ni dhulma isipokuwa serikali inaweza shika njia kuu za Uchumi kama vile Usafiri, umeme, maji, elimu, Afya, Mazingira, Usalama na mambo muhimu ya utoaji huduma kwa wananchi cause that's all we ask for -ni UHAI wetu, huko kwingineko serikali inatakiwa kutunga tu policies ambazo zinawalinda wananchi wote na sio majority au matajiri wachache bali policies zinazoweka uwanja tambarale kwa watu wote kushindana, kuweka malengo, goal, ndoto n.k
Ninaamini ili kuondoa hizi tamaa na ULAFI ni lazima kuwepo na control ya mapungufu yetu sisi wote kwa sheria na taratibu ambazo kwa nchi maskini tunamhitaji DIKTETA ndani ya Ubepari ambaye anaamini ktk Miiko na maadili lakini sio kuwanyang'anya wananchi urithi wao ambao ungewawezesha kuwa matajiri wa kesho, Waajiri wa kesho, wawekezaji wa kesho badala ya serikali inayowategemewa kutajirika ilihali yenyewe ni maskini.
Huu ndio ukweli ya kwamba ULAFI ni moja ya mapungufu ya binadamu na both Ujamaa na Ubepari ume fail somehow..Tofauti inakuwa tu kwamba Utajiri hauwezi kuzaliwa nao unless iwe urithi lakini uta struggle from senti moja hadi kuwa na millioni wakati Ujamaa unamkabidhi kiongozi Utajiri na fimbo mkononi. By the way, naomba nielewe nazungumzia Ujamaa ule unaotafsiriwa na mabepari kama ukomunist..
Kwa nini tulishindwa wakati wa Nyerere?. Ni kwa sababu Ujamaa wetu ulipoteza vipaumbele vyetu kiuchumi baldala ya kuwatazama mabepari kama maadui tuliwalenga wananchi na hasa viongozi waliofikiria wamekua kurithi nafasi za mkoloni.. hawa walitakiwa kupigwa stop tu, badala ya kupipwa fadhila kwa kuwakandamizia wananchi. Kwa sababu hiyo tuliwafilisi hadi wananchi ili kuwa wote level moja kumbe hata tungewaacha wananchi wamiliki property bado nchi za magharibi zingetupiga chini tu.. Kushuka kwa mazao malighafi zetu haikuwa coincidence, bad timimg au bahati mbaya.. They wanted us to go down on our knees na tuwasujudie kwa kuputa mkono wao uendao kinywani. At the time you either with them or with the enemy hapakuwepo na maswala ya Neutral, who own what, au sijui nchi zote zisizofungamana na upande wowote. Was all about who U with? - East or West! basi.. Sisi tulijiita hatufungamani mbona mbona tuliitwa wajamaa kwa sababu tulifunga milango.
Nguruvi3, Dah mkuu wangu Usimba na UYanga hauwezi kutuondolea matatizo yetu..Lugha zinazotumika kule kwenye siasa kusema kweli imefikia mahala nasema huu sasa ni utoto.. Napenda sana kubishana kimjadala, kutazama picha mbili za mitazamo ktk jambo lolote ili kunijenga zaidi ktk kufahamu wengine wanafikiria nini lakini kusema kweli nimefikia mahala nashindwa hata kuelewa huu UADUI umetokea wapi na sasa tumefikia kuonyeshana hadharani.. It's like, the chicken has come home to roost!