Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shukran sana Nguruvi3 kunipa nafasi hii kuzungumzia wapi tunazie ktk vita hii..nadhani tutakuwa pamoja ktk hili.Mkuu Mkandara,
Hapo mwisho umenena ya kuwa ni wakati wa kutafuta ushindi dhidi ya maadui watatu, Ujinga,umasikini na Maradhi.
Ni wapi hasa tuanzie!
Karibu mkuu tuchangie mawazo maanake hadi leo hii sina imani kabisa na biashara hizi za kuita wawekezaji tukasahau kwa nini Mwalimu aliyaacha ardhini.. sababu kubwa ilikuwa ELIMU na uwezo wakuweka mikataba inayotupa umiliki ya mali hizo..Mkuu Mkandara,
Hayo uliyoandika hakika yanasisimua sana, lakini pia nikiri yanatia 'hasira'. Yana hasira kwasababu unapofikiri kuwa kuna kiazi kinatoka Somalia na kuuzwa nje wakati Wasukuma wamekosa soko hadi kutengeneza michembe inaudhi.
Unapofikiri chungwa linauzwa pale nyumba Mtindiro Muheza senti 50 halafu linarudi kwenye mfuko wa sh 1200 inatia maudhi.
Mwezi wa kwanza nilikuwa mahali nikaona maji ya madafu kutoka Thailand na Jamaica, wakati sisi madafu tunaacha yauzwe kwenye matenga na komba walewe mnazi.
Nalirejea tena bandiko lako ili nipate fursa nzuri ya kuliangalia katika mtazamo zaidi.
RitzWakuu Mkandara, chama, Nguruvi3, JingalaFalsafa, Tanzania hawewezi kuchagua mfumo wowote zaidi ya ubepari kwa sababu wa utegemezi sasa umekuwa kama maradhi mila ya utegemezi na misaada mingi huhatarisha uhuru wa huyo ama hao wanaofaidika na misaada hiyo kimsingi misaada inafanya mnakuwa watumwa kwa yule ambao anawapa misaada kufuata anachotaka haina faida, misaada itolewayo na mataifa makubwa au matajiri inadhoofisha nchi inayosaidiwa.
Ubepari ndio umetufikisha hapa kwa viongozi wetu kuwa watumwa utafiti unaonyesha kila dola mia za Marekani zinazoingia kama mkopo au msaada katika nchi masikini ikiwemo Tanzania dola 13 ndio zinabaki nchini na dola 87 hurudi zilikotoka baada ya muda mfupi wanaongoza kuweka fedha nyingi kwenye mabenki ya Uswisi ni viongozi wa kisiasa au watumishi waandamizi wa serikali kutoka nchi za afrika hawa sio wafanyabiashara lakini ndio wanaongoza kuweka pesa nje.
Mfumo wa ubepari unachotaka ni maslahi yao tu Wazungu wanajua kabisa kuwa viongozi wa Afrika wanaiba hizo pesa lakini wanachojali wao fedha yao kuwarudia njia yoyote, hawajali kama imeibiwa alimradi hakuibiwa wao ndio maana wanakubali kuhifadhi mabilioni ya fedha kutoka nchi masikini na wakati huo huo wanajua wanazidai nchi masikini mfumo wa ubepari ndio unavyofanya kazi...kwa nchi masikini haziwezi kupingana mfumo wa kibepari ukijaribu kupingana nao huku huna nguvu za kiuchumi wewe ndio utakuwa adui angalia mfano Fider Castor, Ortega Noriega, nawengine wengi.
Nakubaliana na wewe sana tu ktk hili isipokuwa pengine hukufikiria deep ktk swala la SHERIA na TARATIBU..Ni vigumu sana kuweka msisitizo wa matumizi ya sheria na taratibu ktk nchi ambayo ni corrupted, maana lengo na chimbuko la corruption huanza na ku corrupt viongozi ili kuwepo mizizi ya Imperialism (Ubeberu) na Wanyonyaji (blood sucking parasites) ndio kuweka mirija yao kupitia sehemu zote za sheria na utawala ku corrupt vyombo vya sheria na uongozi.. A cold blooded killer kwa kutumia corruption ya sheria na taratibu lazima atashinda kesi, na ndio tunayoyaona leo yakifanyika ktk mahakama zetu, bunge letu na hata serikali kuu.. Hizi ni sign za kwamba tayari Rushwa kubwa zimeisha ota mizizi mikubwa sana kushika mihimili yote mitatu na hawezi kupona mtu..We are done!Mkuu Mkandara,
Kwanza nashukuru sana kwa bandiko lako lenye kina na mizani,nadhani Watanzania tujilaumu kwa mengine lakini si fikra wala watu wa kufikiri.
Kwa mtazamo wangu, mahali muafaka pa kuanzia ni kuwa na utawala unaoheshimu sheria na taratibu, na wananchi wanaofuata utawala wa sheria na haki. Tukiweza kutengeneza mfumo utakao muajibisha kila mtu hapo tutakuwa na msingi imara wa kusimamia maadui watatu ujinga, umasikini na maradhi.
Tatizo letu siyo rasilimali au rasilimali watu, ni utaratibu mbaya wa sheria unaotuzuia kuzitumia fursa zetu kwa maendeleo.
Nakubaliana nawe kabisa kuwa elimu ni jibu la tatizo la umasikini na maradhi. Mahali popote dunia penye maadui hao watatu utaona sababu kubwa sana ni elimu. Ni kwasababu hizo Manzese kuna umasikini na maradhi kuliko masaki, Oysterbay na kwingineko.
Brooklyn kuna maadui hao hata kama ni dunia ya kwanza, kama ilivyo Bristol, mumbai na Kibera kenya.
Ili uweze kupambana na tatizo la elimu, kwanza ni lazima uwe na rasiliamali za kutosha. Kwa bahati mbaya sana nchi yetu elimu ni kipaumbele cha mwisho baada ya VX na makongamanio. Ndiyo maana nasema, kama kuna sheria zinazosimama na si zile za azimio la Zanzibar basi huenda tungekuwa mahali pengine.
Ukitazama bajeti yetu na kiasi cha pesa kinachopotea inasikitisha sana. Kiasi kinachopotea si kwa bahati mbaya ni kwasabau hakuna watu wa kusimamia sheria na kuhakikisha kidogo tulicho nacho tunakielekeleza kule tunakohitaji.
Ufujaji, ubadhirifu ni matokeo ya utawala usiojali sheria. Tumegeuza nchi ya kuunda tume hata pale mwizi anapoonekana dhahiri. Tumeshindwa kuwawajibisha wahalifu kwasababu sheria zetu zinahodhiwa na mtu au watu.
Matokeo yake rasilimali ambazo tungezitumia kuondoa kwanza ujinga hazifiki mahali tarajiwa.
Ni kutokana na usimamizi mbovu wa sheria tumefika mahali kundi la watu wanaamua kwa makusudi kuleta mgao wa nishati ya umeme. Licha ya kwamba hatujaweza kuendeleza kile tulichokuwa nacho kidogo, basi hata huo umeme kidogo sasa ni mali ya watu.
Unapokuwa huna nishati ya uhakika hakuna mwekezaji atakayekuja kuwekeza mamilioni ya dollar halafu anunue jenereata.
Hapa tunalazimika kutokuwa na viwanda vya kutengneza bidhaa zetu wenyewe. Tunabaki kuagiza kutoka Brazil na South Africa. Bidhaa kutoka nje zinakuwa ni rahisi sana ukilinganisha na za kwetu kwasababu ya kutokuwa na nishati ya uhakika achilia mambo kama maji na miundo mbinu mibovu.
Huko nyuma tulianza kujaribu japo ni kidogo. Tulikuwa na uthubutu wa kutengeneza Tanbobd iliyoshindana na bidhaa nyingine. Hatukutegemea rambo kwasababu tulikuwa na kiwanda cha magunia, tuliweza kuuza hata nguo nje ya nchi.
Tulikuwa na kiwanda cha kusindika nyama na tuliuza Saudia, hivi inakuwaje Saudia wasio na ng'ombe leo watuuzie nyama? Ng'ombe wa msukuma na mmasai wanawasaidiaje?
Tukifika hapo tena hatuna jinsi ya kumsadia masikini aweze kusomesha watoto. Wakulima wamebaki kuuza bidhaa kwa bei hafifu sana kwasababu bidhaa zetu zinauzwa zikiwa raw. Wakati huo huo tunaagiza bidhaa hizo kwa bei mbaya tu.
Badala ya kujenga maghala ya chakula ili tujitosheleze, tumeamua kuwekeza katika majengo ya kifahari kama lile la bunge Dodoma. Nchi masikini kama yetu haihitaji jengo la gharama kama lile,tunahitaji maghala Rukwa, Mwanza n.k kwanza ili tujitosheleze. Hii pia ingetoa bei nzuri kwa wakulima na kuinua hali zao.
Ninachotaka kusema hapa ni kuwa hakuna nidhamu ya kusimamia shughuli zetu kwasababu bila sheria nidhamu itoke wapi? Kwangu mimi tratibu na sheria kwanza lazima ziwepo kabla ya kukabiliana na maadui watatu.
Wapi tuanzie katika taratibu, kanuni na sheria?
Itaendelea.....
JMushi1, Unajua vitu vingine lazima tuvikubali kwamba ndivyo vilivyo na hatuwezi kubadilisha UTU wa mwanadamu maana tumeumbwa na mapungufu yetu kama viumbe. UTU wetu sio wa mazuri tu bali hata tamaa ni ktk sifa za mwanadamu isipokuwa utaitumiaje hiyo tamaa ndipo tunapokuta ubaya wake. Unatamani Embe hakuna ubaya lakini utakapo Iba embe hapo ndipo tunasema tamaa mbaya..Ukilinunua tamaa yako haitakuwa mbaya so its all about sheria na kanuni za UTU wetu.. mabaya pia ya mwanadamu na tusipoweza kuya control ndio tunapokuwa viumbe wabaya sana kuliko wote duniani..Wakuu Nguruvi3,Mkandara na JingalaFalsafa,kwa maoni yangu,wote mko right kuhusu demokrasia na ubepari.Licha ya kwamba ndugu Mkandara na ndugu Nguruvi3 mna maoni ya tofauti na jingalafalsafa,bado yuko right,kwa mfano kama una Afro-centric point of view,basi huwezi kuutofautisha ukoloni na ubepari as well as ukoloni mamboleo na ubepari.Pia nakubaliana na dhana ya kwamba ubepari ulianza kama mfumo wa maisha,baada ya kuexpand na kuwa kama system inayoongoza dunia kwa sasa,ni sawa na kusema ubepari umekuwa "mainstream" worldwide wise.
Tafsiri alizoleta ndugu Mkandara,nazo ni sawa,ie kuhusu capitalism.Lakini kumbuka hayakuanzia huko kwamba wananchi ni wamiliki wa mali za nchi.Ni baada ya mfumo wa kununua hisa ulipoanza,lakini ukweli ni kwamba njia kuu za uchumi zilimilikiwa na wachache na ndivyo hata ilivyo kwa kiasi flani hadi sasa.
Kuhusiana na demokrasia,pia wote right again.However,ninaamini kabisa kuwa tafsiri ya demokrasia inategemea na mahali uliko,lakini alichosema Jingalafalsafa kufananisha demokrasia na ubepari,kwa upande mwingine yuko sawa tu kwasababu demokrasia inayotawala kwa sasa duniani ni hiyo ya mabepri.Na ukiangalia inapokuja kwenye sera za nje za mataifa hayo,nyuma yake kuna hayo makampuni "corporates",individuals na kadhalika amabao wanainfluence foreign policy,sasa hiyo demokrasia yao kwa wengi ni shida kuitofautisha na ubepari.
Pia kwa kumalizia,ukoloni mamboleo kwa tafsiri yetu sisi rahisi,ni kitendo cha Taifa moja moja kulitawala taifa jingine kiuchumi,na ni mfumo ulioupokea ukoloni...Yani mnatawaliwa bado lakini si directly,maamuzi yenu bado yanahitaji baraka za mabepari,na ndiyo wahisani wetu wakubwa,ndo kama "mirija yetu icu"
Mkuu Mkandara naafiki yote uliyosema isipokuwa hapo nilipo bold. Siafiki kabisa uondoke kwenye siasa! Nyumba ikiyumba unatafuta ufa na kuuziba huondoi nguzo. Kule siasa watu wengi wana access ikiwa ni pamoja visitors, bado kunabaki muhimu.Unajua napowasoma watu hapa ukumbini huwa napata raha zaidi japokuwa tunaweza pingana ktk jambo lakini sio kule kwenye siasa. nadhani inanilazimu sasa hivi kuondoka kule kwenye siasa maana sijui namtetea nani maana kumezuka ushabiki mtupu na mimi siwezi ushabiki wa Yanga wala Simba bali kutazama hali halisi..Nawaomba sana wazee wa baraza muyamwage maswala mazito huku tujadili mustakabali wa taifa badala na kujadili majina ya watu kwa habari za kusadikika. Tuirudishe JF yetu huku..
Let's be honest.. Ebu nambie ni nchi gani duniani iwe ya Kijamaa/Kibepari ambayo matajiri Wanaoshika uchumi ni asilimia hata 10%? - Nambie hiyo nchi iwe ya kijamaa au Kibepari!, nadhani bila shaka hakuna kitu hii.. that's the truth on the ground tuache hizi siasa za maandishi ya kiimani.. Dunia nzima nchi zote ziwe ktk Ujamaa au ubepari, Utajiri umeshikwa na watu wasiodizi asilimia 1 hardly 2..Kinachotazamwa zaidi ni ktk siasa hizi mbili ni ujenzi wa middle class yaani kundi la kati baina ya Wafanyakazi na matajiri. Yaani kundi linalotoka ktk umaskini na kwenda kati na ukichunnguza sana utaona Ujamaa unawaondoa watu toka ktk Utajiri kuwarudisha ktk umaskini. Ujamaa ni wa wanyonge, maskini kama nchi ni tajiri huwezi kukuta wanazungumzia Ujamaa. Ujamaa ni kwa wale walioonewa, kuporwa mali zao na sio kwa nchi tajiri inayotaka kuwapa wananchi wake maisha bora..then first youmake them your enemy number baada ya mkoloni..Nakubaliana na wewe ndugu Mkandara,however ni wazi kwamba mfumo wa kibepari pekee,yani bila social elements, una "foster" hizo tabia za ulafi...Ndo maana kwenye mfumo huo,gap ya masikini na tajiri ni kubwa.
Jmushi1, utajiri wa Romney unajulikana wala sio siri isipokuwa wanajua kuna mambo ambayo Romney hawezi kuyaweka wazi ndio maana wanambana ili kuharibu profile yake, lakini hakuvunja sheria isipokuwa yataleta picha mbaya kwa wananchi wapiga kura ujio uchaguzi mkuu. Kama kungekuwa na baya, IRS (Renevue) wasingemwacha hata kidogo isipokuwa lengo ni image yake as a President ikijulikana alikuwa anatengeneza ngapi kwa mwaka akiwa CEO halafu mashirika yale yakafa, watu wakapoteza fedha zao itamweka pabaya ktk uchaguzi. Obama ni bepari vile vile mbona yeye hatumzunguzii?..Mkandara,kuna mambo mengine ya kibepari,practice yake unaweza ukadhani ni kinyume cha sheria kumbe wapi.Msimamo wangu ni kwamba kumix ndo vizuri,kuchaguwa yale ambayo ni relevant kwenye jamii husika.Ndo maana unaona kuna watu kama kina Romney,ambao wametajirika kihalali,lakini bado wanaogopa kuweka ukweli mbele za wananchi kwasababu it won't make no sense to them,na kila alichokifanya,he abided by the law.Lakini bado hathubutu kuweka tax records zake nk.Sasa watu wanajiuliza anaficha nini na kila kitu ni halali chini ya free market?