Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Mkuu Mkandara,
Hapo mwisho umenena ya kuwa ni wakati wa kutafuta ushindi dhidi ya maadui watatu, Ujinga,umasikini na Maradhi.
Ni wapi hasa tuanzie!
 
Mkuu Mkandara,
Hapo mwisho umenena ya kuwa ni wakati wa kutafuta ushindi dhidi ya maadui watatu, Ujinga,umasikini na Maradhi.
Ni wapi hasa tuanzie!
Shukran sana Nguruvi3 kunipa nafasi hii kuzungumzia wapi tunazie ktk vita hii..nadhani tutakuwa pamoja ktk hili.

1. UMASIKINI
Kurudisha DIRA ya Taifa ya UJAMAA na KUJITEGEMEA kwa malengo ya kulinda rasilimali zetu dhidi ya wakoloni au ukoloni mamboleo. Neno UJAMAA litumike kama undugu wetu wa pamoja kama wazawa na wenye haki miliki ya rasilimali zetu (right to own Property) na tuwe na pride ya kuwa WATANZANIA warithi halali wa mali zetu aidha kutokana na KILIMO ama KUFANYA KAZI ili kukidhi shauku kubwa ya maendeleo ya mtu mmoja moja. Na tutaweza hivyo kwa kutazama vipaumbele vyetu hasa kilimo ambacho asilimia 70 ya wananchi wanakitegemea, na hivyo kuhamasisha ujenzi wa viwanda vitakavyo sindika mazao nchini hadi kufikia finished product nyumbani ktk standard ya juu inayoweza kushindana ktk masoko ya dunia. Njia moja kubwa ni kuwavutia wawekezaji ni kuondoa kabisa Ushuru wa kuingiza mitambo ya viwanda na zana za kilimo, kuwapa nafuu ya kodi kwa miaka mitano ya kwanza badala ya kuwapa watu binafsi ardhi wazalishe mazao ambayo sisi wenyewe tunaweza kuzalisha ikiwa soko lipo ndani..

Serikali yetu badala ya kujizatiti ktk mikataba ya mafuta, gesi na madini itazame zaidi mikataba ya mashirika ya usambazaji wa bidhaa za vyakula na cash crops kuwekeza nchini. Kwa mfano, Nescafe wanaweza kununua hisa Africafe ili kuiwezesha kushinda kimataifa. Mashirika ya Chai, Korosho, miwa na mazao mengineyo yaruhusiwe kuweka viwanda vyao nchini na kuzalisha hapa hapa jambo ambalo sisi hatukulitazama siku za nyuma. Ikiwa viwanda vya Ulaya leo vinawekeza China kutengezeza karibu vitu vyote inakuwaje sisi tunasahau kwamba inawezekana viwanda vya Ulaya kuwekeza kwetu kutokana na mali ghafi Cheap inayopatikana toka kwa wakulima wetu?.

Na pia ktk kulazimisha masoko yetu nje Watanzania waishio nje (Diasporas) watumiwe kama ma agent wa kuuza ama ku import mali zetu na kuzitangaza nje iwe ktk maonyesho au kufungua maduka ya uuzaji na usambazaji..Leo hapa mimi nanunua mihogo kutoka Jamaica, Nanunua mbilimbi kutoka South Amerika, nilipokuwa Swiss nilikuwa nanunua ndizio kutoka Somalia lakini maajabu ukienda Tanzania unakuta kuna matunda kutoka South Afrika na juice kutoka Dubai au China.. Hili kwanza lazima tulifanyie kazi kurudisha ile azma ya awali ya Uhuru wetu kutotawaliwa Kiuchumi.

Binafsi yangu nina imani sana kama Nyerere asingefanya makosa ya kuacha rasilimali zetu kwa kizazi kijacho akifikiria tutaweza kuwapa elimu ya kutosha wapate kuziendesha wenyewe, akaingia mikataba yeye kabla ya kuondoka, pengine kuweka mikataba mizuri zaidi ya hii waloingia hawa kina Mkapa na JK. Kwa maana nakumbuka hadi mwaka 1999 kabla ya kifo chake sheria ilikuwa mwekezaji yeyote nchini lazima awe na ushirika (ubia) na Mtanzania usiopungua asilimia 50. Hata hivyo maadam imeshatokea, haya maswala ya kutafuta mafuta, kutafuta gesi na vyanzo vya madini ambayo sisi wenyewe hatuna MTAJI wala elimu ya kuyachimba ni sawa kabisa na mswahili wa Kariakoo aliyeuza nyumba yake kwa sababu mgeni ametaka kujenga Ghorofa na asijiulize kwa nini wajenge wao na sio mimi....

Leo hii Kariakoo ni ya wageni, wenyeji wote wameisha hamishwa kwenda mikoani ama vitongojini na bahati mbaya walipata fedha lakini hawana ELIMU na biashara hivyo wameishia kurudi ktk Umaskini. Na ndivyo picha halisi ya Tanzania kufikia mwaka 2050, tutajikuta hatuna kitu, madini tumeuza yote bila kunufaika. Tunakula ruzuku ya mikataba kuwanufaisha wazungu wakati sisi hizo ruzuku zinakabiri tu matatizo ya matumizi ya ndani kama vile kuweka mkate mezani kwa sababu fedha hizo tunashindwa kuwasomesha watoto wetu bure, tunashindwa kuwalipa walimu na hii leo, tayari tuna mikataba mikubwa sana pengine nusu ya rasilimali tulizokuwa nazo tumeisha gawa ama kuuza. Ardhi ambayo ndio urithi, Mtaji na Utajiri pekee ulobakia kwa Mtanzania nao tunaanza kugawa hovyo. Nachelea kusema mikataba hii tunawauzia wageni viwanja kama Kariakoo na itafika mahala tutajikuta Tanzania sii yetu tena ila ya wageni
- Kurudisha DIRA ya Taifa, hii ni hatua ya kwanza hata kama watatuita Wakomunist, Wasocialist lakini ndivyo China walivyoanza na wamefanikiwa kutokana na kwamba Ujamaa wao walijikita katika kutoa ELIMU bora miaka yote ya Utawala wa Mao Tze Tung...

2. UJINGA -
Inataanza na sisi wenyewe kutambua kwamba Umaskini huambatana na UJINGA..Tuweke vipaumbele vyetu sawa (Substantive equality of opportunity) Ili kumsaidia maskini, maskini hapewi samaki bali hufundishwa kuvua!. Hii ndio iwe poicha ya mikataba, misaada na grants zote tunazochukua..

- Nitaendelea baadaye, nadhani kwanza kama kuna swali, sahisisho, pinzani ktk maoni yangu juu ya Umaskini, naomba tulizungumzie kabla hatujaenda hatua ya pili..
 
Mkuu Mkandara,
Hayo uliyoandika hakika yanasisimua sana, lakini pia nikiri yanatia 'hasira'. Yana hasira kwasababu unapofikiri kuwa kuna kiazi kinatoka Somalia na kuuzwa nje wakati Wasukuma wamekosa soko hadi kutengeneza michembe inaudhi.
Unapofikiri chungwa linauzwa pale nyumba Mtindiro Muheza senti 50 halafu linarudi kwenye mfuko wa sh 1200 inatia maudhi.

Mwezi wa kwanza nilikuwa mahali nikaona maji ya madafu kutoka Thailand na Jamaica, wakati sisi madafu tunaacha yauzwe kwenye matenga na komba walewe mnazi.

Nalirejea tena bandiko lako ili nipate fursa nzuri ya kuliangalia katika mtazamo zaidi.
 
Mkuu Mkandara,
Hayo uliyoandika hakika yanasisimua sana, lakini pia nikiri yanatia 'hasira'. Yana hasira kwasababu unapofikiri kuwa kuna kiazi kinatoka Somalia na kuuzwa nje wakati Wasukuma wamekosa soko hadi kutengeneza michembe inaudhi.
Unapofikiri chungwa linauzwa pale nyumba Mtindiro Muheza senti 50 halafu linarudi kwenye mfuko wa sh 1200 inatia maudhi.

Mwezi wa kwanza nilikuwa mahali nikaona maji ya madafu kutoka Thailand na Jamaica, wakati sisi madafu tunaacha yauzwe kwenye matenga na komba walewe mnazi.

Nalirejea tena bandiko lako ili nipate fursa nzuri ya kuliangalia katika mtazamo zaidi.
Karibu mkuu tuchangie mawazo maanake hadi leo hii sina imani kabisa na biashara hizi za kuita wawekezaji tukasahau kwa nini Mwalimu aliyaacha ardhini.. sababu kubwa ilikuwa ELIMU na uwezo wakuweka mikataba inayotupa umiliki ya mali hizo..
 
2. UJINGA -
Nitaanza na sisi wenyewe kutambua kwamba Umaskini huambatana na UJINGA..Tuweke vipaumbele vyetu sawa (Substantive equality of opportunity) Ili kumsaidia maskini, maskini hapewi samaki bali hufundishwa kuvua!. Hii ndio iwe poicha ya mikataba, misaada na grants zote tunazochukua..

Ikumbukwe kwamba dira yetu ya Taifa baada ya Uhuru ilikuwa kutambua maadui wetu wa ndani, na kubwa zaidi tuliweka Ujinga kuwa nafasi ya pili baada ya kutambua nchi haiwezi kuendelea ikiwa wananchi wake ni wajinga, hivyo kutambua kwamba umuhimu wa kuwa eleimisha wananchi ilikuchukua nafasi kubwa zaidi pengine hata kutangulia Umaskini ktk utekelezaji maana ujinga wa watu hata mkiwa na mafuta, dhahabu na kadhalika hamtaweza kuendelea kutokana na mfumo wa kiuchumi ulotawala dunia.

Yawezekana Nyerere hakufanya makubwa ktk hili lakini kutambua umuhimu wa elimu ilikuwa kigezo kikubwa cha kumkomboa Mtanzania na hivyo yatupasa leo sisi kurudi nyuma na kujitazama wajibu wetu ktk kupata elimu ambayo ndio msingi wa kuondosha Umaskini iwe hata ktk Kilimo au Wafanyakazi, pasipo elimu umaskini unakuwa ni laana.

Leo hii maadam tunazungumzia tufanye nini?.. binafsi yangu swala la ELIMU na AFYA yote nitayaweka pamoja kwa sababu suluhisho la maswala yote haya mawili zinafanana, na sababu za kukwama kwetu zinafanana. Na najua watu wengi sana watanipinga katika maoni yangu lakini ndivyo navyolitazama mimi swala zima la elimu na Afya na wapi yalipofanyika makosa kwa sababu tumeondoa ktk UMUHIMU wa elimu kupambana na maadui wa ndani na kuiga nchi ambazo tayari wananchi wake wana elimu na maisha bora..Hata siku moja mtaji wamaskini hauwezi kuwa sawa na tajiri. Sisi tuna Uhaba wa kila kitu na wao wana shughulikia mahitaji ya kila siku, vipaumbele haviwezi kuwa sawa..

Kosa kubwa lilofanyika ktk utawala huu ni kuanzia AZIMIO LA ZANZIBAR ambalo limezaa kina Mwinyi na Lowassa na wengine wenye mtazamo tofauti na ule ulo asisiwa na chama tawala> hawa wameifanya swala la elimu kuwa ni privilege badala ya kuwa RIGHT ya kila Mtanzania ambaye nimesema mwanzo ni Mnyonge (maskini) - Waswahili wanasema - Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!.. ELIMU na AFYA ni haki (right) ya kila Mtanzania na ndio maana nimetumia maneno ya kiingereza yasemayo Substantive equality of opportunity kama msisitizo wa kumfundisha maskini kuvua samaki badala ya kkumpa kipande cha samaki..

Msaada ni ule unaomfundisha maskini kuvua samaki na sio sadaka ya samaki anayopewa kutuliza njaa ya siku moja..Huu mfumo wa ELIMU na AFYA ulioasisiwa na Mwinyi na Lowassa ndio mwanzo wa matatizo na kama unakumbuka mwaka 1993/94, Tanzania tulikuwa nchi ya chini kabisa ktk kufuta Ujinga baada ya serikali kukabishi chombo binafsi kushiriki kikamilifu ktk uendeshaji wa Elimu na Afya nchini. Watoto chini ya asilimian 60 walijiandikisha kuanza darasa la kwanza kutokana na karo zilizowekwa. Toka wakati ule tulizaa uhaba na hatujaweza kabisa kuondosha matatizo hata madogo ya kulipa mishahara..

Tumefikia kuifanya ELIMU na AFYA kuwa biashara ya Kitaifa badala ya serikali kupambana na maadui hawa. tumeshusha hadi guard zetu na hivyo wanyonyaji wa ndani wamepata mwanya wa kuwanyonya maskini watanzania wasikuwa na uwezo wala sauti. Nachoweza kusema kuhusu ELIMU na AFYA ni kwamba serikali inalazimika kurudisha mfumo wa zamani kuwepo na shule za serikali zinazoendeshwa na serikali 100% na zile za binafsi zinazoendeshwa na watu binafsi.. Serikali itaendesha shughuli zake za elimu na Afya na kuruhusu mashirika binafsi kuwekeza ktk ELIMU na AFYA na hawa watapewa nafuu ya kodi kwa vifaa vya ujenzi na kufundishia..

Wanafunzi waliotihaniwa ktk kivuko cha Std 7, from4 na 6 watakuwa na choice ya kuchagua shule tatu wazitakazo kuendelea na masomo ya juu iwe kwenye Private schools au za serikali na serikali yetu itatoa afueni ya kodi ya mapato kwa shule binafsi zitakazo sajili mwanafunzi wa shule ya serikali pia serikali itatoa fungu kumlipia masomo mwanafunzi huyo kulingana na masomo. Mwanafunzi atalazimika kulipia asilimia isiyopungua 20 ya mahitaji ya shule tukijumuisha na karo. Pia kulazimisha ushindani wa elimu bora kati ya shule za serikali na za watu binafsi kwa kuweka viwango vya shule zenyewe iiwe kuna grade AAA na kushuka..

Mkuu serikali yetu ilazimike kuchukua jukumu hili maana sielewi haswa wanachokifanya zaidi ya mikutano, safari, vikao, semina na upuuzi mwingineo ambayo hayina nia wala malengo ya kumkomboa Mtanzania ktk adha hii.. Fedha nyingi za serikali zinatumika ktk kuendesha huduma wanazolipwa mishahara hawa viongozi.. Kuna wakati hujiuliza hivi kweli mishahara ya viongoziwetu huitumia kwa matumizi gani ikiwa karibu kila kitu kinalipiwa na serikali.. Mshahara wa nini haswa maana wanajiwekea kazi ambazo zinaweza kabisa kuendeshwa na Halmashauri za miji. Matatizo yanayojitokeza leo ktk sekta ya elimu na Afya imetokana namfoimo mbaya unaoendeshwa na vyombo hivi na inabidi tuubadilishe mara moja na haraka iwezekanavyo.

Nitaishia hapo kwa sasa..
 
Well said Mkuu Mkandara, juu ya umasikini! Nichangie kidogo:
Umezungumzia Ujamaa na Kujitegemea, kama dira yetu, irudishwe! Naungana nawe kwa 100%, ila naona kikwazo hapa! Na hiki ndio kiwe kitu cha kwanza kukiondoa kabla hatujaanzisha vita na hivyo vitatu! Inferiority Complex-Mental Slavery-Utumwa wa Kifikra ni mzazi wa Ukoloni Mamboleo ambao nao ni mlezi wa Umasikini, Ujinga na Maradhi! Tuanze kwanza na kutoa Utumwa kichwani mwetu ili kumuandaa mtanzania kuishi sera nzuri za Kujitegemea! Pasi kuondoa halo, sisi wenyewe tutakuwa wakwanza kukwamisha harakati za kuuondoa umasikini! HATUTOFIKA!
Tuanze na Kiini kikuu! Na katika hilo, tutangaze Utumwa wa Kifikra kuwa Adui yetu mkuu wa kwanza, kabla ya Umasikini, Maradhi na Ujinga! (tukumbuke kuwa utumwa wa kifikra si ujinga-labda ulimbukeni na upunguani)
Ni hayo tu ndugu zangu.
Mungu wetu anaita!
 
Mkuu Mkandara,
Kwanza nashukuru sana kwa bandiko lako lenye kina na mizani,nadhani Watanzania tujilaumu kwa mengine lakini si fikra wala watu wa kufikiri.

Kwa mtazamo wangu, mahali muafaka pa kuanzia ni kuwa na utawala unaoheshimu sheria na taratibu, na wananchi wanaofuata utawala wa sheria na haki. Tukiweza kutengeneza mfumo utakao muajibisha kila mtu hapo tutakuwa na msingi imara wa kusimamia maadui watatu ujinga, umasikini na maradhi.

Tatizo letu siyo rasilimali au rasilimali watu, ni utaratibu mbaya wa sheria unaotuzuia kuzitumia fursa zetu kwa maendeleo.
Nakubaliana nawe kabisa kuwa elimu ni jibu la tatizo la umasikini na maradhi. Mahali popote dunia penye maadui hao watatu utaona sababu kubwa sana ni elimu. Ni kwasababu hizo Manzese kuna umasikini na maradhi kuliko masaki, Oysterbay na kwingineko.

Brooklyn kuna maadui hao hata kama ni dunia ya kwanza, kama ilivyo Bristol, mumbai na Kibera kenya.
Ili uweze kupambana na tatizo la elimu, kwanza ni lazima uwe na rasiliamali za kutosha. Kwa bahati mbaya sana nchi yetu elimu ni kipaumbele cha mwisho baada ya VX na makongamanio. Ndiyo maana nasema, kama kuna sheria zinazosimama na si zile za azimio la Zanzibar basi huenda tungekuwa mahali pengine.

Ukitazama bajeti yetu na kiasi cha pesa kinachopotea inasikitisha sana. Kiasi kinachopotea si kwa bahati mbaya ni kwasabau hakuna watu wa kusimamia sheria na kuhakikisha kidogo tulicho nacho tunakielekeleza kule tunakohitaji.
Ufujaji, ubadhirifu ni matokeo ya utawala usiojali sheria. Tumegeuza nchi ya kuunda tume hata pale mwizi anapoonekana dhahiri. Tumeshindwa kuwawajibisha wahalifu kwasababu sheria zetu zinahodhiwa na mtu au watu.

Matokeo yake rasilimali ambazo tungezitumia kuondoa kwanza ujinga hazifiki mahali tarajiwa.
Ni kutokana na usimamizi mbovu wa sheria tumefika mahali kundi la watu wanaamua kwa makusudi kuleta mgao wa nishati ya umeme. Licha ya kwamba hatujaweza kuendeleza kile tulichokuwa nacho kidogo, basi hata huo umeme kidogo sasa ni mali ya watu.

Unapokuwa huna nishati ya uhakika hakuna mwekezaji atakayekuja kuwekeza mamilioni ya dollar halafu anunue jenereata.
Hapa tunalazimika kutokuwa na viwanda vya kutengneza bidhaa zetu wenyewe. Tunabaki kuagiza kutoka Brazil na South Africa. Bidhaa kutoka nje zinakuwa ni rahisi sana ukilinganisha na za kwetu kwasababu ya kutokuwa na nishati ya uhakika achilia mambo kama maji na miundo mbinu mibovu.

Huko nyuma tulianza kujaribu japo ni kidogo. Tulikuwa na uthubutu wa kutengeneza Tanbobd iliyoshindana na bidhaa nyingine. Hatukutegemea rambo kwasababu tulikuwa na kiwanda cha magunia, tuliweza kuuza hata nguo nje ya nchi.
Tulikuwa na kiwanda cha kusindika nyama na tuliuza Saudia, hivi inakuwaje Saudia wasio na ng'ombe leo watuuzie nyama? Ng'ombe wa msukuma na mmasai wanawasaidiaje?

Tukifika hapo tena hatuna jinsi ya kumsadia masikini aweze kusomesha watoto. Wakulima wamebaki kuuza bidhaa kwa bei hafifu sana kwasababu bidhaa zetu zinauzwa zikiwa raw. Wakati huo huo tunaagiza bidhaa hizo kwa bei mbaya tu.

Badala ya kujenga maghala ya chakula ili tujitosheleze, tumeamua kuwekeza katika majengo ya kifahari kama lile la bunge Dodoma. Nchi masikini kama yetu haihitaji jengo la gharama kama lile,tunahitaji maghala Rukwa, Mwanza n.k kwanza ili tujitosheleze. Hii pia ingetoa bei nzuri kwa wakulima na kuinua hali zao.

Ninachotaka kusema hapa ni kuwa hakuna nidhamu ya kusimamia shughuli zetu kwasababu bila sheria nidhamu itoke wapi? Kwangu mimi tratibu na sheria kwanza lazima ziwepo kabla ya kukabiliana na maadui watatu.

Wapi tuanzie katika taratibu, kanuni na sheria?

Itaendelea.....
 
Wakuu Mkandara, chama, Nguruvi3, JingalaFalsafa, Tanzania hawewezi kuchagua mfumo wowote zaidi ya ubepari kwa sababu wa utegemezi sasa umekuwa kama maradhi mila ya utegemezi na misaada mingi huhatarisha uhuru wa huyo ama hao wanaofaidika na misaada hiyo kimsingi misaada inafanya mnakuwa watumwa kwa yule ambao anawapa misaada kufuata anachotaka haina faida, misaada itolewayo na mataifa makubwa au matajiri inadhoofisha nchi inayosaidiwa.

Ubepari ndio umetufikisha hapa kwa viongozi wetu kuwa watumwa utafiti unaonyesha kila dola mia za Marekani zinazoingia kama mkopo au msaada katika nchi masikini ikiwemo Tanzania dola 13 ndio zinabaki nchini na dola 87 hurudi zilikotoka baada ya muda mfupi wanaongoza kuweka fedha nyingi kwenye mabenki ya Uswisi ni viongozi wa kisiasa au watumishi waandamizi wa serikali kutoka nchi za afrika hawa sio wafanyabiashara lakini ndio wanaongoza kuweka pesa nje.

Mfumo wa ubepari unachotaka ni maslahi yao tu Wazungu wanajua kabisa kuwa viongozi wa Afrika wanaiba hizo pesa lakini wanachojali wao fedha yao kuwarudia njia yoyote, hawajali kama imeibiwa alimradi hakuibiwa wao ndio maana wanakubali kuhifadhi mabilioni ya fedha kutoka nchi masikini na wakati huo huo wanajua wanazidai nchi masikini mfumo wa ubepari ndio unavyofanya kazi...kwa nchi masikini haziwezi kupingana mfumo wa kibepari ukijaribu kupingana nao huku huna nguvu za kiuchumi wewe ndio utakuwa adui angalia mfano Fider Castor, Ortega Noriega, nawengine wengi.
Ritz

Hapo kwa kiasi fulani nakubaliana na wewe.Mfumo wa Ubepari ulifanikiwa kutokana na model za Zamani huko Europe na America.

Ila kwa nature ya afrika ilivyo na hasa kuibuka kwa Taifa kama CHINA lenye mfumo lililonao wa kiuchumi ningependa tutumie mifumo ya uchumi kwa ratio.Nilishawahi kuandika hapa JF.

My Ideology is a mix of capitalism,socialism and communism.None of them should be practised to the extreme.
Until recently when the economy of the US,father of capitalism crumbled under extreme patronage of capitalist ideals and the heavy multiplier effects in most economies in western Europe,everyone thought capitalism was the best system.Hata leo US inakaribia kutangazwa Mufilisi kwa sababu GOPs wanashikilia misimamo yao,ikumbukwe hawa Republicans ndiyo conservative kabisa kwenye Ubepari.

However,I would support 45% capitalism coz inspite of everything,people need to know that to reach a certain class,one has to compete.I don't support a classless society,that's my grouch with communism,it leads to laziness which in turn affects both the quantity and quality of production.What belongs everybody belongs to nobody.My grouch with unchecked practice of capitalism is the fact that it leads to corruption,it becoms a dog eat dog affair since everyone wants to make a huge profit at all cost,there has to be some control from the government by way of rules and regulation and also certain aspect of the economy should either be solely government owned or jointly owned with the private sector

This is where I give a 35% support to communism because this prevents total exploitation of the citizenry which is too rife with capitalism.My remaining 30% goes to socialism becoz of its ability to distribute wealth fairly better than the ruthless capitalism and the classless communism.However,socialism also have the attendant problem of communism,lack of competion which leads to reduction in both quality and quantity,the difference is that it's not just at state level like communism.

When it comes to social issue I am more to the right,I believe social change should not be rapid,part of the problem the West is having is as a result of silly views skwed towards the left,issues like legality Same-sex practice,abortion,nudist beaches and other weird social misnormer.

As for funding education,I beliv it is impossible to fund education from primary to tertiary that is not realistic,rather basic education(primary and secondary) should be free or almost free but tertiary can't be free,it should be a combination of student bursaries,scholaships and the likes to deserving students.
Health also should be heavily subsidized but not totally free Because that too is almost impossible.
For system of Government especially as it concerns Tanzania,i strongly believe in a disciplined Federalism tuachane na miko na wilaya. That way there is strong competion to develope without necessarily depending on any region.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara,
Kwanza nashukuru sana kwa bandiko lako lenye kina na mizani,nadhani Watanzania tujilaumu kwa mengine lakini si fikra wala watu wa kufikiri.

Kwa mtazamo wangu, mahali muafaka pa kuanzia ni kuwa na utawala unaoheshimu sheria na taratibu, na wananchi wanaofuata utawala wa sheria na haki. Tukiweza kutengeneza mfumo utakao muajibisha kila mtu hapo tutakuwa na msingi imara wa kusimamia maadui watatu ujinga, umasikini na maradhi.

Tatizo letu siyo rasilimali au rasilimali watu, ni utaratibu mbaya wa sheria unaotuzuia kuzitumia fursa zetu kwa maendeleo.
Nakubaliana nawe kabisa kuwa elimu ni jibu la tatizo la umasikini na maradhi. Mahali popote dunia penye maadui hao watatu utaona sababu kubwa sana ni elimu. Ni kwasababu hizo Manzese kuna umasikini na maradhi kuliko masaki, Oysterbay na kwingineko.

Brooklyn kuna maadui hao hata kama ni dunia ya kwanza, kama ilivyo Bristol, mumbai na Kibera kenya.
Ili uweze kupambana na tatizo la elimu, kwanza ni lazima uwe na rasiliamali za kutosha. Kwa bahati mbaya sana nchi yetu elimu ni kipaumbele cha mwisho baada ya VX na makongamanio. Ndiyo maana nasema, kama kuna sheria zinazosimama na si zile za azimio la Zanzibar basi huenda tungekuwa mahali pengine.

Ukitazama bajeti yetu na kiasi cha pesa kinachopotea inasikitisha sana. Kiasi kinachopotea si kwa bahati mbaya ni kwasabau hakuna watu wa kusimamia sheria na kuhakikisha kidogo tulicho nacho tunakielekeleza kule tunakohitaji.
Ufujaji, ubadhirifu ni matokeo ya utawala usiojali sheria. Tumegeuza nchi ya kuunda tume hata pale mwizi anapoonekana dhahiri. Tumeshindwa kuwawajibisha wahalifu kwasababu sheria zetu zinahodhiwa na mtu au watu.

Matokeo yake rasilimali ambazo tungezitumia kuondoa kwanza ujinga hazifiki mahali tarajiwa.
Ni kutokana na usimamizi mbovu wa sheria tumefika mahali kundi la watu wanaamua kwa makusudi kuleta mgao wa nishati ya umeme. Licha ya kwamba hatujaweza kuendeleza kile tulichokuwa nacho kidogo, basi hata huo umeme kidogo sasa ni mali ya watu.

Unapokuwa huna nishati ya uhakika hakuna mwekezaji atakayekuja kuwekeza mamilioni ya dollar halafu anunue jenereata.
Hapa tunalazimika kutokuwa na viwanda vya kutengneza bidhaa zetu wenyewe. Tunabaki kuagiza kutoka Brazil na South Africa. Bidhaa kutoka nje zinakuwa ni rahisi sana ukilinganisha na za kwetu kwasababu ya kutokuwa na nishati ya uhakika achilia mambo kama maji na miundo mbinu mibovu.

Huko nyuma tulianza kujaribu japo ni kidogo. Tulikuwa na uthubutu wa kutengeneza Tanbobd iliyoshindana na bidhaa nyingine. Hatukutegemea rambo kwasababu tulikuwa na kiwanda cha magunia, tuliweza kuuza hata nguo nje ya nchi.
Tulikuwa na kiwanda cha kusindika nyama na tuliuza Saudia, hivi inakuwaje Saudia wasio na ng'ombe leo watuuzie nyama? Ng'ombe wa msukuma na mmasai wanawasaidiaje?

Tukifika hapo tena hatuna jinsi ya kumsadia masikini aweze kusomesha watoto. Wakulima wamebaki kuuza bidhaa kwa bei hafifu sana kwasababu bidhaa zetu zinauzwa zikiwa raw. Wakati huo huo tunaagiza bidhaa hizo kwa bei mbaya tu.

Badala ya kujenga maghala ya chakula ili tujitosheleze, tumeamua kuwekeza katika majengo ya kifahari kama lile la bunge Dodoma. Nchi masikini kama yetu haihitaji jengo la gharama kama lile,tunahitaji maghala Rukwa, Mwanza n.k kwanza ili tujitosheleze. Hii pia ingetoa bei nzuri kwa wakulima na kuinua hali zao.

Ninachotaka kusema hapa ni kuwa hakuna nidhamu ya kusimamia shughuli zetu kwasababu bila sheria nidhamu itoke wapi? Kwangu mimi tratibu na sheria kwanza lazima ziwepo kabla ya kukabiliana na maadui watatu.

Wapi tuanzie katika taratibu, kanuni na sheria?

Itaendelea.....
Nakubaliana na wewe sana tu ktk hili isipokuwa pengine hukufikiria deep ktk swala la SHERIA na TARATIBU..Ni vigumu sana kuweka msisitizo wa matumizi ya sheria na taratibu ktk nchi ambayo ni corrupted, maana lengo na chimbuko la corruption huanza na ku corrupt viongozi ili kuwepo mizizi ya Imperialism (Ubeberu) na Wanyonyaji (blood sucking parasites) ndio kuweka mirija yao kupitia sehemu zote za sheria na utawala ku corrupt vyombo vya sheria na uongozi.. A cold blooded killer kwa kutumia corruption ya sheria na taratibu lazima atashinda kesi, na ndio tunayoyaona leo yakifanyika ktk mahakama zetu, bunge letu na hata serikali kuu.. Hizi ni sign za kwamba tayari Rushwa kubwa zimeisha ota mizizi mikubwa sana kushika mihimili yote mitatu na hawezi kupona mtu..We are done!

Hivyo tuna kazi kubwa sana ya kuondoa kwanza Corruption, hili ni hatua muhimu sana ktk jitihada zozote ambazo zinafanyika na pengine zinatanguliwa na mawazo ya jingalafalsafa anaposema tupambane na mental slavery kwa sababu fisadi yeyote ni mtumwa wa fedha, mtumwa wa tamaa na ushetani aidha anaufanya yeye au unautumikia. Kwa maana ya kwamba anayetoa rushwa ama anayepokea wote hawa ni watumwa kifikra na virusi vyake vimefika hadi kwa watu wa chini kabisa. Hataona njia ya kutoka ama kukidhi mahitaji yake pasipo kuiba au kufisadi pasipo huruma kabisa..

Njia ya pili ni kubadilisha Uongozi, sidhani kama kiongozi bora ataweza kutoka CCM tena baada ya kuwepo Mafia cartel (Imperialist)wakipanga future ya chama na nchi yetu ktk uongozi. Na bado tena kuna tatizo jingine la wageni waliokwisha ingia na kushika sehemu kuu za kiuchumi. Labda kama tutampata rais mfano wa Nyerere ama Kagame nina hakika tutafanikisha hatua zote mbele mapema zaidi ya kupitia wananchi maanahawana nguvu na umaskini ni kilema. Tunachohitaji ni RAIS mshenzi, dikteta na asiyekuwa na huruma kwa mtu yeyote anayekiuka miiko na maadili ya uongozi kyk Utawala bora.

Labda nirudi ktk swala la Capitalism, unajua mfumo wa uchumi unabadilika kwa kila hatua na mahitaji yanavyozidi na mashindano yanavyochochewa.. Capitalism haikuwa mbaya kabisa kaa ilivyo, isipokuwa pale binadamu tulipoacha asili yake (barter system} ama Gols as medium of exchange na kuanza kutumia masoko ya Chongo street (wallstreet) ambako tunauziwa mbuzi ktk gunia..Hii ndio tatizo kubwa la biashara na Ubepari hasa baada ya big corparates kuingilia haki za watu kumiliki mali wakatumia nafasi ya kila mtu kuwa na share ktk msingi wa neno lile lile la haki ya wa kumiliki mali..

Ukweli ni kwamba ukitazama Ubepari wa leo huu sii Ubepari kabisa ni wizi mkubwa sana baada ya Ukoloni, ambao unawanyima wananchi nafasi ya kumiliki mali zao na ukianzisha kikampuni chako kikaonekana kinaanza kufanya vizuri haya mashirika makubwa yanakuja kukununua utoke ktk biashara yao utake usitake. Hii Biashara ya puto (Bubble) na Mabenki makubwa ndio yanaochukua fedha zetu na kukopesha nchi zinazonunua silaha badfala ya mahitaji na wakichonganisha nchi zigombane ili madeni yenu ndio yawe mtaji wao.

Huu sii Ubepari hata kidogo na ndio maana ulipigwa vita na nchi za east na nasema UTANDAWAZI pia sio kabisa Ubepari ila ni stage nyingine ya wizi kutulazimisha tufungue milango yetu waingie kutukoloni kupitia mlango wa nyuma. Hii sasa sio tena Capitalism ile ya wananchi kumiliki mali bali wananchi kuibiwa mali zao maana wanataka kuja wao na kuhodhi tena njia za uzalishaji, mikopo kuweka rehani rasilimali zetu.Halafu wanaweka mali zetu ktk masoko yao wakiuziana share za Barricks wao wenyewe huko makwao kama duka la rehani (Pawn shop) wakijua hutaweza kulipa..

Na hata hao Barricks wakiingia ktk soko la DSE maadam sisi hatuna share ndani wataweka hesabu ndogo sana za mauzo na binafsi sinto nunua share kwao kwa sababu lazima waonyeshe hawafanyi vizuri kwetu ili tusiwalazimishe walipe corporate taxes. na maadam hatuna share hatuna haki ya kufduatilia matumizi yao hadi wanapowakilisha mahesabu. Hawa jamaa ni wezi sio tena Ubepari. Nawaomba mkipata nafasi kaitazameni sinema ya "The International" tambara safi sana, kuna mahala jamaa anazungumzia benki zinavyotumia madeni utapata msisimko..

Kwa hiyo, japokuwa ningependa sana kuona DSE ikiimarika lakini pia nahofia kwamba DSE inaweza kuwa puto linalokuzwa pasipo Utajiri halali..Na hivyo kuwaibia watu kama hizi NSSF na PPF zinavyo walaghai wananchi kwa fedha yao wenyewe. Mambo yote mabaya yanayoonekana ndani ya Ubepari ni kutokana na ubeberu na tobo zilizopo ktk mfumo mzima wa Ubepari na kama tujuavyo wezi hawakosi mgongo, hata wakati wa Nyerere kulikuwepo na matajiri wezi na mafisadi wakiishi Beach na tuka ukashifu Ujamaa na Kujitegemea kwa kubeza itikadi ile kama ni Unyama na Kujimegea.
Kwa hiyo tupo njiani na I hope tutakuja mpata kiongozi wa ukweli ambaye hakuchomekwa kwa sababu hizi sheria na taratibu pasipo kiongozi imara mwenye msimamo ni sawa na kuwa na Quran mkononi ukitegemea watu wengi watafuata na kuheshimu mafundisho yake kumbe hata huko Saudia kwenyewe wapo watu hawafuati dini.
 
Mkandara,
Hili la kuwa na Rais 'mshenzi' na dikteta nakubalina nalo na ndilo msingi wa hoja yangu.
Kiongozi ambaye atasimamia sheria na taratibu huyo atatuwezesha japo kupiga hatua moja mbele.
Dikteta ninayemuongelea hapa si yule mkatili bali mkatili wa kusimamia sheria na taratibu, kwamba yupo tayari kuchukua hatua dhidi ya mtu yoyote bila kumuonea haya anapokiuka misingi ya sheria au taratibu.

Tunahitaji kiongozi atakayerudisha utu kama anavyosema JingalaFalsafa.
Tukumbuke kuwa hakuna shoka linalokata bila mpini.
Huo unyonyaji (Capitalism) hauwezi kufanya kazi peke yake bila kuwa na mpini ambao ni viongozi wa nchi yetu.
Na wala hayo makampuni au mashirika hayawezi kutuingilia kiasi walichotuingilia endapo tutakuwa na viongozi wanaoongozwa na sheria na taratibu na maono pia (vision).

Nitoe mfano, waziri Clare Short alijiuzulu baada ya kuona kampuni ya nchi yake ikinyonya kinchi masikini kabisa duniani.
Aliyeshiriki katikahaya yote ni B.W.Mkapa na Tony Blair. Hatuwezi kumlaumu Blair kwasababu alikuwa anasimamia kile mabeberu wanachokita. Tunapaswa kwanza kusota kidole kwa BWM kwa kushirikiana na wezi katika kuingamiza nchi.

Hata pale ilipobainika kuwa kuna uhalifu, viongozi wetu na hapa JK, aliudanganya umma kwa kauli za PCCB inafanya kazi na hatua zitachukuliwa. Ushahidi upo wazi kuwa pesa zilichotwa na zimerudi. Pesa hizo hazikutoka hazina zenyewe, wapo wahusika wakuu waliochonga dili. Inashangaza kiongozi wa nchi anaposimama na kusema hakuna uhalifu ni makosa ya mahesabu. Hata kama yapo makosa ya tarakimu za bilioni 70, nani amewajibishwa? nani amechukuliwa hatua?

Kwanini tuone BAE kama Capitalist wanaotunyonya na si hawa wezi tulio nao madarakani tena wengine wakiwa na nafasi za uongozi. Ni nani aliyezuia uchunguzi halali kama si kiongozi wa nchi yetu?

Mfano wa pili, sakata kama la Richmond, Kagoda n.k. ni nani wamefanya madili hayo kama si viongozi wetu, na ni nani ameshiriki kuficha ukweli kama si viongozi wetu. Kuna kampuni gani ya kibepari iliyokuja na kuanza mgao ili iuze umeme kama si viongozi wetu? Kuna kampuni gani ya kibepari iliyokuja kuchota mapesa BoT kama si viongozi wetu wliopo madarakani sasa hivi.

Hivi karibuni tumesikia kundi la watu wanaleta mgao wa umeme wa lazima ili wauze mafuta.
Ukiangalia wote wanaotuhumiwa ni viongozi wa nchi hi.
Hata kama wanatumika lakini bado hatukwepi ukweli kuwa wao ni mpini wa shoka.

Ujio wa Capitalists kuhodhi njia za uzalishaji ni suala lililo katika uwezo wetu kulitanzua.
Capaitalists walikuwepo hata wakati wa Nyerere. Mwalimu aliwaambia acheni hayo madini ipo siku watayachimba wenyewe akiwa na maana hadi wakati tutakapokuwa tayari kusimamia rasilimali zetu na si kuzia ujio wao.

Kwa bahati mbaya tumeshindwa kabisa kusimamia na migodi inabaki kuwa mashimo sisi tukizama katika lindi la umasikini.
Mwalimu alitumia sheria na taratibu na utu katika kulinda mali zetu dhidi ya mabeberu. Nani amaevunja sheria hizo kama si viongozi wetu kule Zanzibar ili kutunisha matumbo na mifuko yao.

Kuna nyakati tunaulaumu ubepari bila sababu na kusahau kuwa sisi wenyewe ni sehemu ya tatizo.
Hivi kiwanda cha mang'ula kama kingechukuliwa na bepari na kubaki mang'ula kikifanya kazi kungekuwa na ubaya gani zaidi ya kuuziana kishikaji na sasa kuwa maghala ya chumvi kama tulivyofanya?
Kwanini tudhani kuwa mabepari watatudhoofisha kwa kila hali tusifikiri jinsi tunavyojidhoofisha wenyewe.

Nimalizie kwa kuendeleza bandiko langu # 254 nililosema wapi pa kuanzia?
Kwa bahati mbaya sana tumekosa fursa ya kutengeneza utaratibu utakaotupa kiongozi 'dikteta' wa kutukwamua.
Fursa ya kuandika sheria na taratibu zetu ili tuwe na Viongozi wanaowajibika kwa wananchi, wananchi wanaowajibika katika nchi yao, mahakama zisizotumika kama vichaka vya wahalifu, bunge linalowakilisha wananchi na kusimamia masilahi yao.

Tumeikosa fursa hiyo kwasababu tumeruhusu viongozi wale wale wasio na maadili wala utashi wa kutukwamua waunde tume ya katiba itakayoandika sheria wanazozitaka wao na pengine zinazokidhi haja za mabepari.
Hapa ndipo tulipo bofoa kwasababu sina imani na utaratibu wetu wa kuandika sheria na taratibu kupitia tume ya maoni ya katiba.

Vita yetu dhidi ya ujinga, maradhi na umasikini ipo pale pale kwa bahati mbaya haionekani kama tuna mbinu za kupambana na maadui zetu. Silaha yetu kubwa ni sheria na taratibu, sidhani kama tunayo au tutaipata.

Tumefikia mahali njia kuu za uchumi kama miundo mbinu tumeshindwa kuziendesha. Hata kama tumekubaliana tuzikabidhi kwa mabepari, je tumefanya hivyo kwa njia nzuri? Si tumeona 10% za wahindi na sasa TRC imekufa.
Hapa tunamlaumu vipi bepari kama si ukosefu wa nidhamu, sheria na taratibu.
Kwanini tumlaumu bepari na si Kikwete ambaye amebaki kushuhudia uhalifu wa TRC.

Na kwa hakika kama ulivyosema hapa tulipo hatuwezi kujinasua tukiwa na CCM.
Sababu kubwa ni kuwa hili ni genge la makuwadi na hata siku moja haliwezi kujitenga au kuacha sera zake za hujuma.
Hivyo kitu muhimu zaidi katika nchi yetu kwasasa siyo rasilimali bali viongozi watakaosimamia sheria na taratibu ili kila mmoja awajibike bila kuoneana haya.
Ni kiongozi dikteta peke yake atakayetunasua katika mtego huu. Dikteata wa sheria na taratibu.
 
Wakuu matatizo yetu ya kiuchumi hatuwezi kuyatatua kwa siasa za kwenye majukwaa; ni ukweli hivi sas hatuna wanasiasa thabiti wenye kusimamia maslahi ya watanzania; ipo mifano ya nchi ambazo zimeshindwa kusimamia rasimali zake na hivi sasa zipo kwenye matatizo ya kichumi na rasimali zimekwisha au zinakaribia kwisha mfano mkubwa ni Yemeni, visima vya mafuta na gesi vimekauka na nchi bado ni masikini na inakabiliwa na madeni makubwa je ni nani aliyenufaika na rasimali za Yemen ni hao tunawaita wawekezaji, ukiangalia upande mwingine nchi za south America mfano Bolivia na Venezuela wameamua kwa sauti moja kutaifisha mashirika makubwa ya nishati na kuyarudisha kwenye mikono ya serikali kwa lengo kuwanufaisha wananchi, na ndicho kinachoendelea kwenye nchi hizo; na hakuna njia rahisi na hakuna njia ya mkato, viongozi wetu wananafasi kubwa sana ya kujifunza na kuhahakisha watanzania tunanufaika na rasimali zetu. Hatuna haja wala sababu ya kukopi mifumo tusiyoielewa tunaweza kuchukua mazuri mabaya tukawaachia wenyewe.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Unajua napowasoma watu hapa ukumbini huwa napata raha zaidi japokuwa tunaweza pingana ktk jambo lakini sio kule kwenye siasa. nadhani inanilazimu sasa hivi kuondoka kule kwenye siasa maana sijui namtetea nani maana kumezuka ushabiki mtupu na mimi siwezi ushabiki wa Yanga wala Simba bali kutazama hali halisi..Nawaomba sana wazee wa baraza muyamwage maswala mazito huku tujadili mustakabali wa taifa badala na kujadili majina ya watu kwa habari za kusadikika. Tuirudishe JF yetu huku..
 
Wakuu Nguruvi3,Mkandara na JingalaFalsafa,kwa maoni yangu,wote mko right kuhusu demokrasia na ubepari.Licha ya kwamba ndugu Mkandara na ndugu Nguruvi3 mna maoni ya tofauti na jingalafalsafa,bado yuko right,kwa mfano kama una Afro-centric point of view,basi huwezi kuutofautisha ukoloni na ubepari as well as ukoloni mamboleo na ubepari.Pia nakubaliana na dhana ya kwamba ubepari ulianza kama mfumo wa maisha,baada ya kuexpand na kuwa kama system inayoongoza dunia kwa sasa,ni sawa na kusema ubepari umekuwa "mainstream" worldwide wise.

Tafsiri alizoleta ndugu Mkandara,nazo ni sawa,ie kuhusu capitalism.Lakini kumbuka hayakuanzia huko kwamba wananchi ni wamiliki wa mali za nchi.Ni baada ya mfumo wa kununua hisa ulipoanza,lakini ukweli ni kwamba njia kuu za uchumi zilimilikiwa na wachache na ndivyo hata ilivyo kwa kiasi flani hadi sasa.

Kuhusiana na demokrasia,pia wote right again.However,ninaamini kabisa kuwa tafsiri ya demokrasia inategemea na mahali uliko,lakini alichosema Jingalafalsafa kufananisha demokrasia na ubepari,kwa upande mwingine yuko sawa tu kwasababu demokrasia inayotawala kwa sasa duniani ni hiyo ya mabepri.Na ukiangalia inapokuja kwenye sera za nje za mataifa hayo,nyuma yake kuna hayo makampuni "corporates",individuals na kadhalika amabao wanainfluence foreign policy,sasa hiyo demokrasia yao kwa wengi ni shida kuitofautisha na ubepari.

Pia kwa kumalizia,ukoloni mamboleo kwa tafsiri yetu sisi rahisi,ni kitendo cha Taifa moja moja kulitawala taifa jingine kiuchumi,na ni mfumo ulioupokea ukoloni...Yani mnatawaliwa bado lakini si directly,maamuzi yenu bado yanahitaji baraka za mabepari,na ndiyo wahisani wetu wakubwa,ndo kama "mirija yetu icu"
 
Wakuu Nguruvi3,Mkandara na JingalaFalsafa,kwa maoni yangu,wote mko right kuhusu demokrasia na ubepari.Licha ya kwamba ndugu Mkandara na ndugu Nguruvi3 mna maoni ya tofauti na jingalafalsafa,bado yuko right,kwa mfano kama una Afro-centric point of view,basi huwezi kuutofautisha ukoloni na ubepari as well as ukoloni mamboleo na ubepari.Pia nakubaliana na dhana ya kwamba ubepari ulianza kama mfumo wa maisha,baada ya kuexpand na kuwa kama system inayoongoza dunia kwa sasa,ni sawa na kusema ubepari umekuwa "mainstream" worldwide wise.

Tafsiri alizoleta ndugu Mkandara,nazo ni sawa,ie kuhusu capitalism.Lakini kumbuka hayakuanzia huko kwamba wananchi ni wamiliki wa mali za nchi.Ni baada ya mfumo wa kununua hisa ulipoanza,lakini ukweli ni kwamba njia kuu za uchumi zilimilikiwa na wachache na ndivyo hata ilivyo kwa kiasi flani hadi sasa.

Kuhusiana na demokrasia,pia wote right again.However,ninaamini kabisa kuwa tafsiri ya demokrasia inategemea na mahali uliko,lakini alichosema Jingalafalsafa kufananisha demokrasia na ubepari,kwa upande mwingine yuko sawa tu kwasababu demokrasia inayotawala kwa sasa duniani ni hiyo ya mabepri.Na ukiangalia inapokuja kwenye sera za nje za mataifa hayo,nyuma yake kuna hayo makampuni "corporates",individuals na kadhalika amabao wanainfluence foreign policy,sasa hiyo demokrasia yao kwa wengi ni shida kuitofautisha na ubepari.

Pia kwa kumalizia,ukoloni mamboleo kwa tafsiri yetu sisi rahisi,ni kitendo cha Taifa moja moja kulitawala taifa jingine kiuchumi,na ni mfumo ulioupokea ukoloni...Yani mnatawaliwa bado lakini si directly,maamuzi yenu bado yanahitaji baraka za mabepari,na ndiyo wahisani wetu wakubwa,ndo kama "mirija yetu icu"
JMushi1, Unajua vitu vingine lazima tuvikubali kwamba ndivyo vilivyo na hatuwezi kubadilisha UTU wa mwanadamu maana tumeumbwa na mapungufu yetu kama viumbe. UTU wetu sio wa mazuri tu bali hata tamaa ni ktk sifa za mwanadamu isipokuwa utaitumiaje hiyo tamaa ndipo tunapokuta ubaya wake. Unatamani Embe hakuna ubaya lakini utakapo Iba embe hapo ndipo tunasema tamaa mbaya..Ukilinunua tamaa yako haitakuwa mbaya so its all about sheria na kanuni za UTU wetu.. mabaya pia ya mwanadamu na tusipoweza kuya control ndio tunapokuwa viumbe wabaya sana kuliko wote duniani..

Na bnafsi yangu siamini kabisa kwamba tunaweza fikia kugawana Utajiri au umaskini sawa.. haiwezekani sisi binadamu tumeumbwa kushindana na unyama wetu ndio unatupa hii mori ya kuzidi kwenda mbele zaidi. ndivyo tulivyoumbwa. Utajiri ni bahati, sii kila mtu anaweza kuwa tajiri kama kipaji na haiwezekani kila mtu awe tajiti au vipaji sawa ila kwa kutumia Utajiri na vipaji vyetu tatuwawezesha wengine kupata ajira anapowekeza kwa malengo ya faida. Wababu zetu sisi wengine walikuwa wavuvi na walikuwa na mashua zaidi ya 10 lakini kila mashua iliajiri wafanyakazi zaidi ya 10 maana mitumbwi ya kwetu hutengenezwa na viti vya mbao across wakikaa wawili wawili, na wakirudi ufukoni samaki wao hununuliwa aidha na walanguzi ama hubadilishana na unga, mahindi au kuku...Na hakika pengine walikuwa na hali nzuri kuliko watu wengine lakini tuliheshimu utajiri wa baadhi yetu..

Kwa hiyo swala la kupinga Ubepari limetokana tu na kwamba wageni walikuja kututawala na kutuibia rasilimali zetu wakatunyonya kwa nguvu ya ubeberu wao hivyo kutafsiri Ubepari ktk mtazamo huo.. Labda nirudi niuweke mfano huu ktk upande wa pili. Hivi mnafikiri hawa MABEPARI wanasema nini kuhusu Ujamaa? (Socialism) unafikri maana halisi ya neno hili au unayoijua wewe ndivyo wao wanaamini?.. HAPANA wanaamini ni Utopia Socialism ni Udikteta wa chama kimoja chini ya mwenyekiti (Mungu mtu) who own all means of production.. waulize Mabepari watakwambia ndio Ujamaa yaani fikra za mtu mmoja tu ndio bora kuliko mamillioni ya watu wote around him/her na hawana sauti juu yake (Dikteta)..

Lakini wewe na mimi tutabisha hadi kesho kuwa hiyo sio maana ya Ujamaa japokuwa haya maswlaa ya Udikteta yamo..Ujamaa pia ulikuwepohata kabla ya Ubepari kwa maana ya watu kuishi pamoja ku organise production na distribution zinakwenda directly kukidhi mahitaji yao na economic demands zao, lakini maadam Ujamaa ulokuja na kina Robert Owen, na Karl max ulikuwa aganst walowezi ndipo Ujamaa ukapata maana nyingine. By the way hata wapigania Uhuru wanaitwa siku hizi Insurgent, mara utasikia Gaidi while infact gaidi ni yule mtawala anayewanyanyasa wananchi hadi wakakimbilia msituni. Wakitoa mhanga kuvaa mabomu na kuzitoa roho zao kwa faida ya kizazi kijacho..

Kina Mandela waliozeekea jela na kuitwa gaidi hadi 2004 ndio wameliondoa jina lake ktk list ya magaidi na leo anaitwa HERO!.. Kwa sababu at the end of the day alisalimu amri wazungu wanaendelea kuiba rasilimali na kuzijenga UK na Holland maana hakuna mzungu Msouth ambaye hana urais wa asili yake..
 
Nakubaliana na wewe ndugu Mkandara,however ni wazi kwamba mfumo wa kibepari pekee,yani bila social elements, una "foster" hizo tabia za ulafi...Ndo maana kwenye mfumo huo,gap ya masikini na tajiri ni kubwa.
 
Unajua napowasoma watu hapa ukumbini huwa napata raha zaidi japokuwa tunaweza pingana ktk jambo lakini sio kule kwenye siasa. nadhani inanilazimu sasa hivi kuondoka kule kwenye siasa maana sijui namtetea nani maana kumezuka ushabiki mtupu na mimi siwezi ushabiki wa Yanga wala Simba bali kutazama hali halisi..Nawaomba sana wazee wa baraza muyamwage maswala mazito huku tujadili mustakabali wa taifa badala na kujadili majina ya watu kwa habari za kusadikika. Tuirudishe JF yetu huku..
Mkuu Mkandara naafiki yote uliyosema isipokuwa hapo nilipo bold. Siafiki kabisa uondoke kwenye siasa! Nyumba ikiyumba unatafuta ufa na kuuziba huondoi nguzo. Kule siasa watu wengi wana access ikiwa ni pamoja visitors, bado kunabaki muhimu.
Sema kile unachokiona na kukiamini na usiendekeze U-simba na U-yanga, we need you there Bro! Yale mazito tutayaleta huku kama ulivyosema.

Nawashukuru sana akina MM, Jokakuu, Jasusi, Kichuguu,jmushi, Ngongo,Ogah, Kiranga,Pasco,Mimibaba,fmpiganaji ,msalagambwe, nng00,Nsiande, n.k kukomaa na kuendeleza kazi Jukwaa la Siasa(JLS).
Ninahakika kuna watu wametumwa kuharibu JF hasa JLS,endapo watu wataondoka basi hawa waharibifu watakuwa wameshinda mbinu chafu, hapo tutakuwa tumeshindwa kutumia silaha yetu ya haki ya kusema na ku-bow kwa presha ya waharibifu.

Na pia nakuhakikishia kuwa bado JLS ni 'public opinion place'.
Unakumbuka mjadala wa kutumia reli za jijini ambao unatekelezwa sasa ulianzia JF.
Umuhimu wa miundo mbinu kuimarishwa ili Moro na Tanga zichukue mzigo wa Dar ulianzia hapa.
Watu wengi sasa wanaelewa kiini macho cha serikali 3 au mkataba kupitia mijadala.
Bado tunawahitaji kule JLS.


Ilikuwa nje ya mada kidogo, tuendelee na mnakasha
 
Nakubaliana na wewe ndugu Mkandara,however ni wazi kwamba mfumo wa kibepari pekee,yani bila social elements, una "foster" hizo tabia za ulafi...Ndo maana kwenye mfumo huo,gap ya masikini na tajiri ni kubwa.
Let's be honest.. Ebu nambie ni nchi gani duniani iwe ya Kijamaa/Kibepari ambayo matajiri Wanaoshika uchumi ni asilimia hata 10%? - Nambie hiyo nchi iwe ya kijamaa au Kibepari!, nadhani bila shaka hakuna kitu hii.. that's the truth on the ground tuache hizi siasa za maandishi ya kiimani.. Dunia nzima nchi zote ziwe ktk Ujamaa au ubepari, Utajiri umeshikwa na watu wasiodizi asilimia 1 hardly 2..Kinachotazamwa zaidi ni ktk siasa hizi mbili ni ujenzi wa middle class yaani kundi la kati baina ya Wafanyakazi na matajiri. Yaani kundi linalotoka ktk umaskini na kwenda kati na ukichunnguza sana utaona Ujamaa unawaondoa watu toka ktk Utajiri kuwarudisha ktk umaskini. Ujamaa ni wa wanyonge, maskini kama nchi ni tajiri huwezi kukuta wanazungumzia Ujamaa. Ujamaa ni kwa wale walioonewa, kuporwa mali zao na sio kwa nchi tajiri inayotaka kuwapa wananchi wake maisha bora..then first youmake them your enemy number baada ya mkoloni..

Hivyo katika Ubepari kuna matajiri wachache na Ujamaa pia kuna matajiri wachache vile vile.. Na mkuu wangu - ULAFI humpata yule anayezuiwa zaidi ya yule alokuwa huru.. Kama friji Open huwezi kuwa mlafi sema yule ambaye chakula kwa kuhesabiwa lazima kuuna walafi wengi zaifdi..Mtoto unayemfungia ndani kila siku akiishi kwa amri kama kuku, siku zote ndiye mlafi na siku ukimwachia kidogo tu ndio siku anaondoa shauku zake zote kwa ulafi ulokuwa nao. Huyu ndiye Mlafi zaidi ya yule ambaye yuko huru unless ana matatizo ya akili,, amini maneno yangu sii tunawaona watoto wa ma gate makali, Wasomali na Waarabu huku majuu wnavyoharibikiwa. Hawa ni wabaya zaidi ya unavyofiria kwa ulafi maana wanataka kumaliza vyote kabla hawajarudi handakini. Hii ndio hekima aloificha Mungu juu ya umuhimu wa Uhuru wa mwanadamu, unampomkataza sana kitu, ukamnyima ndivyo anavyozidi kuwa curious, anavyokitamani zaidi na kuwa sehemu ya fikra zake kila siku.. Just set them free, weka miiko na maadili then let them face the music - akiharibu anakuwa grounded!

That's another fact on the ground twende Russia, China au Korea kwa kina Mao, Lenin, Kim hawa wote walikuwa Putin hawa wote they lived large all the time, wakiendesha maisha yao ya juu sana. Pengine waliokuwa wasafi ni Revolutionary na Pan Africanist kina Nyerere hapa nampa sifa zote mzee wetu maana hawa waliweka goals back then lakini nao wakawa victim of the same Ulafi wa wengine baada ya hapo hawakuwa na mwendelezo zaidi ya Idea za Kujikomboa. Na wataondoka hawakukamisha lolote maana walafi wameisha ingi

Ujamaa kwanza tulikuwa na serikali kubwa sana ku run everything under their watch na kila kiongozi ngazi zote walikuwa matajiri ukitazama asilimia ya uzalishaji vs fedha wanazotumia wao ni zaidi ya asilimia 70 kuendesha maisha yao wao.. Walikuwa wakipewa nyumba bure, usafiri bure na dereva, mpishi, gardener, shopping ya nguo na Chakula utadhani they were Mafia Mob. Akipita kiongozi lazima msimame wima kwa nidhamu ya woga na kuushusha uso chini ati tukiitana ndugu..Haya mambo yalitakiwa tuwafanyie wakoloni na walowezi sio kuwageuzia kibao wananchi wako na kuwa nyie tena ndio mabeberu, mkiwakunja mwananchi wa kawaida wanyonge hawawezi kumshitaki kiongozi wa chama cha zidumu fikra za mwenyekiti!.

JMushi! tumeishi ktk maisha hayo ya kuogopa hata kukutana na polisi ukiwa na mfuko wa khaki wa sukari..Wengine tumelala ndani kwa amri ya Meya tu ati ulitembea na mwanaye basi unaenda kulala jela siku saba. Tunapigishwa push up na kurushwa kichura kwenye mageti kwa sababu hujamkatia mlinzi wa mzee ulipochukua binti yake out..na mambo haya yanaendelea hadi leo huko North Korea. Na kibaya zaidi ktk Ujamaa watu wanaficha mali ili ku create Uhaba wakati vitu hivyo vinasafirishwa nchi za jirani. Mwananchi hana Unga lakini wazee wa Ikulu wanakula kuku kwa mrija, Champagne na Carviar kina Kim na Cuban Sigar hawajawahi kula ugali wa njano na harage!

Mkuu tumeishi maisha hayo japokuwa mimi mpenzi mkubwa wa Nyerere lakini sikubaliani kabisa na fikra za serikali kushika umiliki wa mali za watu hasa wananchi wake.. Hapana hii ni dhulma isipokuwa serikali inaweza shika njia kuu za Uchumi kama vile Usafiri, umeme, maji, elimu, Afya, Mazingira, Usalama na mambo muhimu ya utoaji huduma kwa wananchi cause that's all we ask for -ni UHAI wetu, huko kwingineko serikali inatakiwa kutunga tu policies ambazo zinawalinda wananchi wote na sio majority au matajiri wachache bali policies zinazoweka uwanja tambarale kwa watu wote kushindana, kuweka malengo, goal, ndoto n.k

Ninaamini ili kuondoa hizi tamaa na ULAFI ni lazima kuwepo na control ya mapungufu yetu sisi wote kwa sheria na taratibu ambazo kwa nchi maskini tunamhitaji DIKTETA ndani ya Ubepari ambaye anaamini ktk Miiko na maadili lakini sio kuwanyang'anya wananchi urithi wao ambao ungewawezesha kuwa matajiri wa kesho, Waajiri wa kesho, wawekezaji wa kesho badala ya serikali inayowategemewa kutajirika ilihali yenyewe ni maskini.

Huu ndio ukweli ya kwamba ULAFI ni moja ya mapungufu ya binadamu na both Ujamaa na Ubepari ume fail somehow..Tofauti inakuwa tu kwamba Utajiri hauwezi kuzaliwa nao unless iwe urithi lakini uta struggle from senti moja hadi kuwa na millioni wakati Ujamaa unamkabidhi kiongozi Utajiri na fimbo mkononi. By the way, naomba nielewe nazungumzia Ujamaa ule unaotafsiriwa na mabepari kama ukomunist..

Kwa nini tulishindwa wakati wa Nyerere?. Ni kwa sababu Ujamaa wetu ulipoteza vipaumbele vyetu kiuchumi baldala ya kuwatazama mabepari kama maadui tuliwalenga wananchi na hasa viongozi waliofikiria wamekua kurithi nafasi za mkoloni.. hawa walitakiwa kupigwa stop tu, badala ya kupipwa fadhila kwa kuwakandamizia wananchi. Kwa sababu hiyo tuliwafilisi hadi wananchi ili kuwa wote level moja kumbe hata tungewaacha wananchi wamiliki property bado nchi za magharibi zingetupiga chini tu.. Kushuka kwa mazao malighafi zetu haikuwa coincidence, bad timimg au bahati mbaya.. They wanted us to go down on our knees na tuwasujudie kwa kuputa mkono wao uendao kinywani. At the time you either with them or with the enemy hapakuwepo na maswala ya Neutral, who own what, au sijui nchi zote zisizofungamana na upande wowote. Was all about who U with? - East or West! basi.. Sisi tulijiita hatufungamani mbona mbona tuliitwa wajamaa kwa sababu tulifunga milango.

Nguruvi3, Dah mkuu wangu Usimba na UYanga hauwezi kutuondolea matatizo yetu..Lugha zinazotumika kule kwenye siasa kusema kweli imefikia mahala nasema huu sasa ni utoto.. Napenda sana kubishana kimjadala, kutazama picha mbili za mitazamo ktk jambo lolote ili kunijenga zaidi ktk kufahamu wengine wanafikiria nini lakini kusema kweli nimefikia mahala nashindwa hata kuelewa huu UADUI umetokea wapi na sasa tumefikia kuonyeshana hadharani.. It's like, the chicken has come home to roost!
 
Mkandara,kuna mambo mengine ya kibepari,practice yake unaweza ukadhani ni kinyume cha sheria kumbe wapi.Msimamo wangu ni kwamba kumix ndo vizuri,kuchaguwa yale ambayo ni relevant kwenye jamii husika.Ndo maana unaona kuna watu kama kina Romney,ambao wametajirika kihalali,lakini bado wanaogopa kuweka ukweli mbele za wananchi kwasababu it won't make no sense to them,na kila alichokifanya,he abided by the law.Lakini bado hathubutu kuweka tax records zake nk.Sasa watu wanajiuliza anaficha nini na kila kitu ni halali chini ya free market?
 
Mkandara anasema tusiwatoe watu katika ukoloni na kuwaingiza katika ukoloni tena. Anamaanisha lazima wananchi wawe huru katika kuamua, kutenda na kushiriki shughuli zao za maisha na kimaendeleo bila kukwaza na siasa. Kwamba ukoloni ubebe maana yake na si sura wala rangi akitoa mfano ujamaa ulivyokuwa ukoloni wa aina baada ya kuondoa ukoloni.Ameseme ubepari wala si uadui kama watu walivyoaminishwa na kwamba tuwe na mfumo utakaowaacha watu huru na wakati huo huo kuwepo na sheria za kulinda jamii.

jmushi1 anasema tuwe na model tutakayo pick mazuri na kuacha mabaya (Mixed model) akitolea mfano kuwa hata huo ubepari practice yake ina walakini maana kwanini mtu aogope kusema alicho nacho katika mfumo uliokubaliwa na jamii?

Hebu sasa twende kwenye specifics. Mkandara kagusia nini kiwe cha umma na nini kibaki soko huru.
Je kuna mifano tunayoweza kuiangalia kwa undani zaidi!
Mimi ningeweza sema Scandinavia zimejaribu model anayoizungumzia jmushi1.

Na je inatosha tu kuwa na mifumo bila kuwa na UTU anaoongelea JingalaFalsafa?
 
Mkandara,kuna mambo mengine ya kibepari,practice yake unaweza ukadhani ni kinyume cha sheria kumbe wapi.Msimamo wangu ni kwamba kumix ndo vizuri,kuchaguwa yale ambayo ni relevant kwenye jamii husika.Ndo maana unaona kuna watu kama kina Romney,ambao wametajirika kihalali,lakini bado wanaogopa kuweka ukweli mbele za wananchi kwasababu it won't make no sense to them,na kila alichokifanya,he abided by the law.Lakini bado hathubutu kuweka tax records zake nk.Sasa watu wanajiuliza anaficha nini na kila kitu ni halali chini ya free market?
Jmushi1, utajiri wa Romney unajulikana wala sio siri isipokuwa wanajua kuna mambo ambayo Romney hawezi kuyaweka wazi ndio maana wanambana ili kuharibu profile yake, lakini hakuvunja sheria isipokuwa yataleta picha mbaya kwa wananchi wapiga kura ujio uchaguzi mkuu. Kama kungekuwa na baya, IRS (Renevue) wasingemwacha hata kidogo isipokuwa lengo ni image yake as a President ikijulikana alikuwa anatengeneza ngapi kwa mwaka akiwa CEO halafu mashirika yale yakafa, watu wakapoteza fedha zao itamweka pabaya ktk uchaguzi. Obama ni bepari vile vile mbona yeye hatumzunguzii?..

Unajua kuna muda unatakiwa ku file tax zako unaweza acha miaka mitatu hulazimishwi kila mwaka ila ni lazima u file miaka yote ya nyuma. Makosa makubwa ni kuepa kodi, ku declare pato dogo zaidi ya ulichokipata, kuficha baadhi ya mali zako n.k, lakini kuto file mwaka mmoja au miwili haikatazwi, hata watu wa kawaida tu wapo ambao hawaja file miaka miwili. Besides kama ume file hii ni mali yako unaweza kuanika ama kutoanika na kumpa tu mtu unayetaka kumwonyesha..

Turudi nyuma, nani anajua mapato ya marais ktk nchi za kijamaa? They don't even file for tax, hawakatwi tax na wanachota kiasi chochote wanachokitaka hakuna wa kumuuliza infact most ya viongozi wa Kijamaa ni watawala badala ya kuwa viongozi..Hili ni gonjwa tulolibeba hadi leo hii..Mkuu wangu Ubepari kwa mapana yake una mapungufu mengi tu na yote ni human creation kama Ujamaa na asili yake, lakini yaliyopo ktk Ujamaa yanatisha zaidi. Binafsi yangu nachosema sisi tufuate Ubepari kwa maana halisi ya Ubepari (right to property ownership) na Ujamaa (Undugu wetu) kwa maana halisi ya Ujamaa na sio KUIGA haya maswala ya west na east.

JingalaFalsafa
kaeleza vizuri sana kuhusu UTU ambao binafsi yangu naamini ni FREEDOM, JUSTICE na EQUALITY (equal opportunity) huu ndio mpango mzima. Kuwaweka wananchi wako ktk kifungo cha ndani ukiwatuhumu Ubeberu na unyonyaji wakati hawana kitu, maskini na wanyonge ni kujipandisha Umungu mtu. Huwezi kuupata UTU halisi ktk Ubepari wala Ujamaa wa Europe ambao wanalaani madikteta ilihali wao wanasafiri maelfu ya maili kwenda vamia nchi nyingine kusimamisha Demokrasia wakipandikiza mtu wao. Huu ni mpango ambao haupo ktk UTU.. Ni changa la macho, danganya toto ku vest power kwa watu wakati they aren't directly involved na decision making. Bado tupo ktk dunia ya Kutawaliwa na sio kuwa na viongozi.

Labda nimalizie kwa kusema unajua Marekani na Ulaya hawa ni WAJAMAA kuliko hata sisi. na ndio maana utaona Liberal wanashinda kwa matumizi halisi ya neno lenyewe kwa sababu hawa hawajatawaliwa.. Ujamaa wao umetokana na kutukuza traditional zao..wanathamini KAZI kiasi kwamba unemployement rate tu ikipanda inamwangusha kiongozi ktk urais..

Priorites zao ziko wazi kabisa, iwe system yenyewe jinsi wanavyosaidiana toka welfare hadi job creation huwezi kulinganisha na sisi.. wakati mwingie husema hawa Mabepari ni wajamaa kuliko sisi maana Just Imagine how much monies Bill Gates anatoa kusaidia nchi maskini ktk maradhi?.. Anatumia billions kuliko bejeti ya nchi zetu ktk huduma ya Afya.. Kina sisi ni michango ya harusi, hata kwenda hospital tu kutembelea wagonjwa tunashindwa ila kwenda kupiga picha za wagonjwa, madaktari walipogoma kuonyesha unyama wa serikali!..What did you do to help the sick ones?.. NOTHING!
Ujamaa wetu umetokana na experience ya kukoloniwa na tumeshindwa hata kutetea mila na desturi zetu wenyewe tumebakia kuiga kila kitu kiasi kwamba tunaogopa hadi vivuli vyetu wenyewe..
 
Back
Top Bottom