Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Mkuu Mkandara,
"Pamoja na yote haya binafsi yangu naamini ktk kumfundisha jirani yako uwezo wa yeye kujitegemea, kumwajiri, kumfundisha kuvua samaki badala ya kumpa kipande cha samaki..Na ukiwsha mwezesha umeomndoa mzigo huo machoni na ndio maana nasema sisi wote tunataka uhuru wa kumiliki mali zetu kuwezeshwa kuzalishaji badala ya kuwa wategemea zaka."

Nimekunukuu hicho ulichosema ndicho alichosisitiza Mwalimu Nyerere; siku zote alipigania watu wajitegemee; kwenye suala la zaka nadhani nyote mnaimba wimbo mmoja msichokubaliana ni nani kaimba malaika vizuri, kwenye kutoa zaka wanapewa watu wasiojiweza nini watazafanyia hizo pesa hiyo siyo hukumu yako; hata zikitolewa moja kwa moja kutoka msikitini au kanisani bado watu wanaweza kuzitumia kwenye mambo yasiyotakiwa.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu wangu Mkandara:
1. Si kweli kwamba sijaelewa dhana ya "kukubali kutokubaliana"...nakuelewa vizuri tu! Nilichosema, kwanini tusimame sehemu mbili tofauti hali wanaweza kuwa pamoja? Pia, si kweli kwamba niko Far Left, hata siko huko wala kulia! Nachoamini kama kuna kushoto na kulia, basi kuna katikati(kitovu), juu(kichwa) na chini(miguu), tunaweza kuchagua mojawapo hapo kwani kulia na kushoto tumeshindwa! Yaani, naamini katika kufanya UBUNIFU wa namna gani tuishi, ila, ili tufanye ubunifu sahihi, wenye tija kwa umma, si vikundi vya watu wachache tu, basi hatuna budi kuongozwa na MANTIKI, yaani UTU, yaani UWIIANO SAHIHI, yaani KUFIKIRIANA, yaani NIDHAMU. Uchumi, siasa na tamaduni, iwe UTU kwanza. Pasi kuwa na hilo katika huo ubunifu wetu, basi ni BURE, sawa na kuukimbiza upepo!
Sasa tunaweza hoji, je nisahihi kuwaachia misingi watoto wetu wakaiendeleza? Watoto wetu si hawa wa vyuoni au mashuleni, ni kizazi chetu kijacho "new generation" Tunawafikiria kweli? Maana sisi tumeshazikwa hai, je tuwaache nao wazikwe? Ndio maana nasema, ni lazima tufikie suluisho, si kukata tamaa na kusema "Tuyaache yalivyo"
2. Ni wazi kuwa hakuna Mjamaa 100% ila moyoni tu! Kwani mfumo uliopo unambana kutouishi ujamaa! Analazimishwa kuishi asichokiamini! Je, ni sahihi kwake kujiua ili akwepe hali hiyo? Au ajiunge kuiamini na kuipenda hali hiyo? Au ajaribu japo kwa kijinafasi kadogo alichonacho kupigania imani yake? Ipi ni nafasi yako katika kuipigania imani yako inayokandamizwa?
SITOACHA HADI NAKUFA!
3. Uhuru upi ni sehemu ya UTU? Je, ni ule wa taifa kutoka kukoloniwa(independence), ama huu wa mtu kujiamulia apendavyo kuishi(rights-freedom)? Kama ni huu wa HAKI, basi si sehemu ya UTU, tena ndio chanzo kikuu cha ukiukwaji wa UTU! Hakuna UTU katika uhuru wa mtu kumlisha mbwa samaki na nyama, hali jirani yake hajiwezi aridhini kwa maradhi na njaa! Nyerere alisema huo ni "Wendawazimu"
4. UTU si kitu kinachoweza kupotezwa, UTU u nafasini mwa kila mtu, ni "innate value-a man born with value" upo sawa kwa kila mtu! UTU haupotei, ila unakiukwa tu...kwa maslahi ya wachache wapumbavu! Gharama ya kuulinda UTU, haifanani na gharama ya kulinda tawala zote chini ya jua! Ndio maana nilikupa mfano wa mwizi aliyeiba dhaka! Utafakari vizuri! UTU si kutii sheria zisizo na Mantiki!
5. Mkuu Chama amejibu vizuri kuhusu dhaka! Ngoja niongeze kidogo. Kwanini uamini kwamba UTU wako unaweza kubebwa na watu? Una hakika gani kama dhaka yako itamuokoa jirani yako? Kwani hujui kwamba binadamu ameumbwa na tamaa, tena ameachwa huru kujifikiria binafsi, kwani asitafute ukuu kwa dhaka yako? Kwani hatusikii ubadhirifu huko? Muweka hazina ametamani gari la katibu wa kanisa au msikiti, anajipigania kulipata! Hujamuua jirani yako bado?
6. Tufundishane Kutegemeana, na sisi Kujitegemea! Hata Nyerere na AA, alilenga kujenga taifa linalojitegemea ila raia wake wawe WANATEGEMEANA! Ndio maana kukawa na Villagilizatio. Dhana bora kabisa ya kufanya watu wategemeane ni kufanya mali kuwa za umma!
Mungu wetu anaita!
 
Nakusikia mkuu wangu nakusikia sana..na nitaendelea kusema hivi hakuna makosa kabisa watu kukubali kutokubaliana maana ktk UTU wetu hakuna mfumo mmoja na kama ulivyoongezea wewe kuweko kwa kati, kichwa na miguu mbali kabisa na kushoto ama kulia hizi ni nyenzo ktk ujenzi wa UTU ulopotea kwa wanadamu na haviwezi kutumika kwa wakati mmoja isipokuwa pale inapohitajika na kwa mazingira yaliyopo.

Unaweza kuona kumlisha mbwa ni kosa lakini pia kwa yule asiyethamini UTU wa mwanadamu (Mwenendo wa maisha ya Biinadamu) kwa kutegemea kulishwa basi ni bora umlishe mbwa atakaye kupa ulinzi dhidi ya mahasidi. Ninachosisitiza mimi ni ile akili ya kuelewa kwamba sisi wote tuna ibada za kimaisha tunazotakiwa kufanya ili tuitwe binadamu na kwa matemegemo ya ema ya kibinadamu japokuwa tuna matamanio na fikra tofauti ktk maamuzi yetu, tusote tuna akili na huzitumia tofauti katika maswala tofauti na wakati tofauti, hakuna njia moja kwa kila mtu, ukoo ama nchi..

Nakubali sana upana wa mawazo ya watu Kujitegemea na pia watu Kutegemeana, lakini maneno haya hayana maana zaidi ya kwamba kama wewe unajenga nyumba bila shaka unamtegemea mtu mwingine atatengeneza vifaa vya ujenzi. Mkulima wa mahindi atamtegema mvuvi wa samaki au mchganji kupata kitoeo na mlolongo wa kutegemea ahaina kikomo maadam sote tunaijenga jamii yenye kutegemeana.. Na sii kufikiria mtu asojiweza kama ndiye anayezungumzwa ktk ujenzi wa UTU. Mtu mmoja hawezi kuwa kama ndege wa kujenga kiota chake kwa kukusanya majani na pumba zilizopukutika kujisetiri mwenyewe, kuwalinda wanawe mchezo umekwisha. na hata wao hutegemeanakwa kuitana kwa sauti za nyimbo kuwaelekeza wapi kuna chakula ama hatari... .

Huyu asiyejiweza hupewa Zaka na mara zote zaka haziji kwa fedha bali kwa mahitaji yake. NI makosa makubwa sana kumpa mtu fedha kaa zaka isipokkuwa pale inapobidi. Zaka hutolewa kwa kipimo cha vibaba, mavazi na kadhalika kama unavyoona Foodbanks na Salvation Army. Hawa ndio watoka zaka na kote makanisani na misikitini wanatakiwa kutoa huduma na sio fedha, na kila unapochangia mfuko huu ndio wajibu wako ktk jumuiya. Chama kaeleza vizuri sana tu lakini kashindwa kuelewa zaka haswa inatakiwa kutolewa vipi maana kinachotazamwa ni huduma gani unampa mhusika hata iwe kumlipia matibabu Hospital..

Msisitizo wangu upo sii tu ktk kuelewa maadui wetu, kuelewa pia mapungufu yetu yalosababisha sisi kuwa utumwani na hata kukoloniwa na hivi sasa tunakoloniwa kiuchumi.. Hapa hakuna Utu tena na walka hatuwezi kutoa amri ama kuwalazimisha wakoloni mamboleo wafikire utu kwanza... Hivyo maadam tupo huru leo kinachofuata ni kupanga mikakati bora zaidi baada ya kuwa huru ili kuurudisha UTU ulopotea ndani ya kutawaliwa kiuchumi.. Uhuru wa bendera haukuwa mwisho wa ukombozi, uhuru wa mwanadamu ni hadi pale anapokuwa huru na kuchagua mazuri ktk UTU na kulaani machafu, ile nguvu ya kupambana na machafu inatokana na kumwezesha mwananchi kushiriki moja kwa moja na uchumi wake au uchumiwa nchi yake.. Kumpa mtaji wa uwezo wa kuvua samaki na sii kutegemea kipande cha samaki.. huundio UTU..Na ndio maana nikasema Ujamaa ni dawa ya Ukoloni Mamboleo ukisha fanikisha unaupata uhuru wa watu wako dhidi ya wanyonyaji unatazama sasa ni jinsi gani utawaendelea na sio kuutumia tena Ujamaa dhidi ya wananchi wenyewe maana sii Wanyonyaji bali walonyonywa..

Ni mfumo gani unafaa kutumiwa hilo ndilo swala japokuwa hatuwezi kushusha guards zetu na kuuza Ujamaa ambao utaendelea kuwalinda wananchi dhidi ya wageni na wanyonyaji. Hivyo kuna baadhi ya misingi ya Ujamaa ambayo itakuwepo kuendelea kulinda wananchi na sii tena silaha ya kuwaweka utumwani..nadhani hata katika vifaa vya kivita wanatengeneza vifaa vya kulinda na vifaa vya mashambulizi.. Tusiielekeze mizinga hiyo ya kuwlinda wananchi kuelekea mji majumbani mwao..Hii ndio hoja ya maandishi yangu kuhusiana na matumizi ya Ujamaa..Siku zote nimekuwa advocate wa Ujamaa ktk misingi ya Ulinzi na sii silaha ya kupambana na wananchi.. Miiko na maadili inatosha na hii haichagui mgeni wala raia maana kinachotakiwa ni kulinda kile tulichopigania na kwa malengo tulokusudia..
 
Wakuu Mkandara, chama, Nguruvi3, JingalaFalsafa, Tanzania hawewezi kuchagua mfumo wowote zaidi ya ubepari kwa sababu wa utegemezi sasa umekuwa kama maradhi mila ya utegemezi na misaada mingi huhatarisha uhuru wa huyo ama hao wanaofaidika na misaada hiyo kimsingi misaada inafanya mnakuwa watumwa kwa yule ambao anawapa misaada kufuata anachotaka haina faida, misaada itolewayo na mataifa makubwa au matajiri inadhoofisha nchi inayosaidiwa.

Ubepari ndio umetufikisha hapa kwa viongozi wetu kuwa watumwa utafiti unaonyesha kila dola mia za Marekani zinazoingia kama mkopo au msaada katika nchi masikini ikiwemo Tanzania dola 13 ndio zinabaki nchini na dola 87 hurudi zilikotoka baada ya muda mfupi wanaongoza kuweka fedha nyingi kwenye mabenki ya Uswisi ni viongozi wa kisiasa au watumishi waandamizi wa serikali kutoka nchi za afrika hawa sio wafanyabiashara lakini ndio wanaongoza kuweka pesa nje.

Mfumo wa ubepari unachotaka ni maslahi yao tu Wazungu wanajua kabisa kuwa viongozi wa Afrika wanaiba hizo pesa lakini wanachojali wao fedha yao kuwarudia njia yoyote, hawajali kama imeibiwa alimradi hakuibiwa wao ndio maana wanakubali kuhifadhi mabilioni ya fedha kutoka nchi masikini na wakati huo huo wanajua wanazidai nchi masikini mfumo wa ubepari ndio unavyofanya kazi...kwa nchi masikini haziwezi kupingana mfumo wa kibepari ukijaribu kupingana nao huku huna nguvu za kiuchumi wewe ndio utakuwa adui angalia mfano Fider Castor, Ortega Noriega, nawengine wengi.
 
Last edited by a moderator:

Ndivyo mnavyoamini kwa sababu ndivyo mlivyofundishwa. Ubepari hauna mahusiano kabisa na Unyonyaji japokuwa wanyonyaji huwa huru ndani ya Ubepari pasipo masharti magumu..Hiivyo hatari ya kuwapata wanyonyani ktk ubepari ipo sana tu kama ilivyo ktk Ujamaa ambao nguvu kubwa hukabidhiwa viongozi wake na rahisi kwako kuwa Madikteta kama hawatabanwa na katiba...Ndio maana ni rahisi kwenye Ubepari kuona wanyonyaji nakwenye Ujamaa kuwa na Madikteta..

Hivyo hizi hatari za kutokea Unyonyaji na Udikteta ni vitu ambavyo vinaweza kabisa kuepukwa maadam wahusika wenyewe wataelewa walikotoka na wanataka kwenda wapi. Nimesema wazi huko nyuma mbona Nordic countries waliweza na leo wanaongoza duniani kwa tawala zinazotoa MAISHA BORA kwa wananchi wake. Kwao hutakuwa wanyonyaji wala Madikteta maana walichukua yaliyo bora katika Ujamaa, wakazuia kabisa miaya ya Udikteta, halafu wanakuchukua Ubepari na kuzuia miaya ya mirija na Unyonyaji - Inawezekana.
 
Kujenga ubepari kuna misingi yake hao waliojenga ubapari hawakuanza kwa kukopa walitumia rasilimali zao kuleta mapinduzi ya uchumi; katika kujenga ubepari hakuna njia ya mkato wewe unachotaka kulazimisha ni Tanzania kutumia njia za mkato kitu ambacho hakiwezekani; nadhani unachanganya mada udikteta hauna mahusiano na ujamaa wala ubepari ni mtawala mwenyewe ndiye anayeamua kuwa Dikteta, je Mussolini alikuwa mjamaa?; je Mobutu alikuwa mjamaa; Marcias Nguema na Bokasa walikuwa wajamaa?

Ubepari haukujengwa na mtu yeyote, Ubepari ulikuwepo kabla ya tawala zote duniani na ndio msingi wa UTU wa binadamu..Soma vitabu vyote utakuta ukweli nikwamba sisi tuliumbwa ili kujitegemea, kila mmoja wetu atakula kwa jasho lake...Kifupi ni kwamba nchi zote duniani zilikuwa Mabepari kwanza..Sisi Ukerewe babu zetu walikuwa wakimiliki mashamba yao hata kabla ya mkoloni, walikuwa na mitumbwi, miti ya maembe, mabanda ya mifugo na kadhalika kama mali zao hii toka Nuhu...

Wakaja tokea watu waliokiuka UTU hao wakoloni wakaanza kufikiria cha mwingine maana makwao hawakuwa na resources kama zetu kukidhi mahitaji yao. In fact nisema hivi nchi ni Uingereza, Germany, Holland, France, Spain, Portugal na Italia hawa wote hawa kuujenga Ubepari hta kidogo waliukuta kama tulivyoukuta sisi kwa mababu zetu. Isipokuwa Tamaa za viongozi wao (Kings na Malkia) kushindwa kuwahudumia wananchi wao kutokana na uchache wa resources ndio walofikiria njia za kuanza kwenda kuteka na kutawala mataifa mengine..

Muingereza ana nini? Mfaransa ana nini wote hawa wameishi kwa ujanja ujanja miaka yote na ndio maana Globalisation sasa hivi inakuwa na impact kwao kwa sababu hawana tena makoloni na nchi nyingi zinaanza kuwatajirisha wananchi wao..Wa kwanza kuanguka nihao Wagiriki, Waspanish na Wataliani maana wameishiwa akiba walovuna ktk ukoloni..Mmarekani ndio hivyo yeye analazimisha makoloni hadi kesho maana rasilimali zake anaziacha kwa kizazi kijasho, mafuta wanayo mengi tu lakini hayachimbi - Why?

Kwa hiyo tulichokiona sii Ubepari bali ni Ukoloni na tunachokiona leo sio Ubepari bali Ukoloni mamboleo na ndio maana ukilaani Ubepari nchi za magharibi hawatakuelewa kabisa..Katia Ukoloni hawa jamaa Afrika walitukuta tayari mabepari vile vile, wananchi wake wakimiliki mali zao. Wazungu wakakuta utajiri mkubwa sana huku hivyo wakaziteka nchi zetu, wakaweka vikao Berlin kugawana mipaka toka kwetu Afrika, South Amerika, Arabuni, India hadi China na kwa shangwe na wakiwatukuza Christopher Columbus, Livingston, Speke, Vasco Da Gama na wengineo kuwa mashujaa wao. Kote tuliwekwa utumwani hali na mali zetu, tukawatumikia kwa malipo ya wages huku wakichukua mali zetu makwao.

Wizi huu haukuwa Ubepari hilo nakataa kabisa. Ni sawa na mtu anambie Ufisadi nchini umetokana na Ubepari.. haya ni majibu rahisi sana hatutaki kuuchosha ubongo. Na hata kutokea kwa vigogo kama kina Karl max, Stalin, Mao, Lenin, Ghandi na wengineo ilitokana na fikra za kuondokana na Ukoloni.. narudia tena maneno haya sijui mara ya ngapi..Hawa watu, viongozi wenye vision walikaa na kutafakari ubaya wa kutawaliwa, ubaya wa kukoloniwa, ndipo fikra za mapinduzi dhidi ya wadharimu hawa zikazaliwa. Hizo Fikra za kuwaondoa Wakoloni ndizo zilizozaa Ujamaa baadaye japokuwa mwanzo kabisa wa Ujamaa ilikuwa kuwaondoa wakoloni kama walivyoondolewa Saudia, India au Kenya..

Utanisamehe nitatumia lugha chafu kidogo hapa. Ujamaa ni sawa na matumizi ya condom. Lengo haswa ya matumizi ya condom tumesisitizwa kuwa kinga ya maradhi haswa HIV (Ukimwi) lakini tatizo la Condom ni kwamba sii tu inazuia Ukimwi bali pia inazuia pia Uzazi. Hakuna kinachoingia wala kinachotoka, hivyo kiuchumi tunasema matumizi ya condom mwanamme au mwanamke hawezi zijalisha mwenyewe labda kwa kupandikiza. Haya sii maisha ila ni mateso mengine kwa watu wanaofahamu kabisa wanaweza kuzaa halafu matumizi ya condom ndio inakuwa maisha yao..naomba unielewe sina maana mbaya kabisa ya kukashifu matumizi ya condom laa hasha..Ila ndio ukweli uliopo na zipo njia bora zaidi na ndizo nazojaribu kuelezea hapa..

Kinachotakiwa haswa ni kutafuta njia nyingine ya uzazi, na bora zaidi ya zote ni watu kuwa huru zaidi kuchagua mwenza alokuwa mzima, asiyetaka kuambukizana, anayechukia Gonjwa na sii mgonjwa na kushirikiana naye kimwili kwa malengo ya kupata mtoto sasa sio tena kuogopa Ukimwi. Na ndio maana nasema Ubepari sio gonjwa bali gonjwa ni kukoloniwa kiuchumi.

Mwiho nakubali kwamba kuna uwezekano mmoja wenu anaweza ambukizwa kwa njia nyingi iwe ufisadi au tamaa ile ile walokuwa nayo Mwakoloni, lakini kama tunaelewa adui wetu na njia za kinga, tukaweka regulations ambazo zinatulinda sote bila shaka tutakuwa salama.

Kinachoniudhi mimi kuhusu matumizi mabaya ya Ujamaa ni pale unapomvalia condom hata mkeo kila siku kwa tahadhari ya Ukimwi halafu unasema tunaamianiana. Huku kuaminiana hali hatuaminiani ndiko kunakopelekea watu kuwa washenzi vile vile maana hatuna regulations zaidi ya kuamini condoms tu. Hii ndio ilosababisha watu wakauchukia Ujamaa kwa sababu haukuwaamini wananchi wenyewe japokuwa Uhuru tulopigania ulitokana na sisi kuaminiana kwanza.

Hao ulowataja kuwa Madikteta wakati ni mabepari unashindwa kuelewa kwamba wananchi wake hawakuwa huru kumiliki mali bali wao ndio walimiki mali ama kugawa mali walizopenda kuzigawa kinyume cha pale wao ndio wali own karibu kila utajiri wa nchi hizo. Leo hii huwezi kunambia Saudia ni Mabepari kwa sababu ya kuwa na open market system ilihali Sultan owns almost everything, hata nyumba unapewa na Sultan ati ni haki yako - Hawa Wametawaliwa..
- Sijui kama umenielewa?
 
Mkuu Mkandara,
Nadhani bado sijakuelewa unazungumzia ubepari upi ila ninachofahamu mimi ubepari ni mfumo ambao ulibuniwa na watu jaribu kumsoma Adam Smith; pia ningekushauri usome tena historia ya capitalism; Netherlands ilikuwa ndio nchi kwanza kuwa na capitalism.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu Mkandara, ujamaa wenyewe una matabaka yake kuna Socialism ujamaa wenyewe kuna Socialism demagogic ujamaa wa domo kuna Socialist mjamaa kuna Socialisistic transfromation mageuzi ya kijamaa, halafu kuna ubepari umejichanganya na ujamaa Socialite...kuna Capitalism, Capitalist, Capitalize, Tanzania wapo kwenye mfumo gani na mfumo upi bora ambao unaona ndio utawafaa Watanzania
 
Ndio hapo? nachowaambia ndugu zangu tusitake saana ku complicate mambo..Tunajua Ubepari umekuja itwa mfumo unaojali matajiri, wachache kuwanyonya wengi lakini ajabu ndani ya Ubepari unakuta huo huo unakuta kuna vyama vya Kisoshalist.

Ndio maana tunawaona kina Carter na Obama wanaitwa Wajamaa ndani ya nchi ya Kibepari na wanapinga kabisa fikra za Matajiri wachache kumiliki au kushika nguzo za uchumi. Sasa ikiwa Ubepari ni unyonyaji, hawa wanapinga vipi unyonyaji ilihali wanaukubali Ubepari - Capitalism?.
 
Mkuu Mkandara:
Naomba nirudi nyuma kidogo, na japo kwa ufupi nichangie katika haya.
1. Naomba nikunukuu "Katika UTU wetu, hakuna mfumo mmoja"
Kwanza niseme kwamba, hakuna utofauti wa UTU aidha baina ya mtu na mtu, watu na watu, kanda na kanda, kabila na kabila, dini na dini, wala taifa na taifa. UTU ndio MANTIKI KUU ya maisha! Chunguza tafsiri hii ya maisha "Maisha ni Furaha, kama haipo ni upuuzi. Na hakuna Furaha ya mtu ila watu" huo ndio UTU, yaani Mantiki, yaani Uwiano Sahihi, yaani Kufikiriana, yaani Upendo, yaani Ukweli, yaani Furaha, na ndio Maisha, kama sio basi ni Upuuzi! UTU kwanza! Kwa sasa maisha ni upuuzi, ni lazima tuirudishe kweli ya maisha, yaani FURAHA, kimoja tu kuwezesha hilo, UTU! Mungu wetu yu tayari kutushindia!
2. Umetoa mfano wa mjenga nyumba, amtegemeavyo mtengeneza saruji, bati, nondo, n.k. Ni kweli huko ndio kutegemeana! Lakini kunaweza kukawa sio, kukageuka kuwa kunyonyana pale tu UTU unapokiukwa kuwaongoza! Sote tunakiri kwamba tumeumbwa na tamaa, fursa hii ya kutegemeana kwa sasa imegeuka kuwa unyonyaji kwa sasa! Tumeruhusu kupigania maslahi binafsi, kila mtu yuko huru kujipigania. Uhuru huu wa kujipigania, ukiongeza na hulka za binadumu kujikweza, tunapata UNYONYAJI. Mtengeneza bati, atajifikiri binafsi, atapunguza gharama za uzalishaji, lakini ataongeza idadi ya bidhaa, ni wazi zitakuwa chini ya kiwango "za kichina", na ataziuza kwa bei ghali, na mjenzi atanunua kwenye soko huru! TUTAJIDANGANYA kuweka sheria kali na wakaguzi wa viwango(ubora wa bidha), ni UTOTO...kwani hao wasimamizi wa sheria na viwango vya bidhaa, nao ni watu kama mzalisha bati, wana tamaa za kujikweza, wameruhusiwa kujifikiria binafsi, pia wapo huru kujipigania, watakataa vipi kidogodogo wanachopewa kupitisha bidhaa feki sokoni? Ukishakiuka UTU, usishangae wizi, ulaghai, unyonyaji, rushwa,n.k. UTU - KUFIKIRIANA HAKUPO TENA, unalalama nini? Waache EPA na TAKUKURU wale, Richmond n.k. Ni mitego tu, tumetanguliza kichwa!
3. Ndugu Ritz:
Si kweli kwamba sisi hatuwezi kuishi mfumo mwingine zaidi ya ubepari! NAKATAA! Ila ukweli ni kuwa TUNAWEZA, ila si kazi rahisi! Lazima tufikirie kwanza kuwa "SISI ni Mkwawa na wenzake wa karne nyingi nyuma, pia SISI ni kizazi chetu karne nyingi mbele" Leo hii huwezi sema tujitoe kabisa na ubepari, ni wazi tutafutika kwenye uso wa dunia, kumbe basi si mchezo wa miaka kumi au hamsini, ni zaidi ya hapo! Muhimu ni kutambua kuwa LEO ndiyo itakiwayo kututoa kesho! Binafsi najiamini sana, pia naamini ukuu wa mtu mweusi, naamini uwezo wake wa kufikiri, tukitaka tunaweza! Tukae chini, tutafakari, tuumize vichwa, tufanye Ubunifu, na UTU wapaswa kuongoza tafakari yetu! Tusikate tamaa, kusema hatuwezi! UBUNIFU HAUJAWAHI KUFIKA MWISHO. Nguvu yetu ni Umoja na Kuthubutu! Mungu wetu anaita sasa!
4. Mkuu Mkandara:
Unadai kuwa ubepari hauna mahusiano yoyote na unyonyaji! Sijakuelewa labda! Lakini nachojua ubepari ni pigania mtaji kwa namna yoyote ile! Piagani ukuu, pigania kunyonya! Ni muhimu kuwa na tafakari binafsi ya mambo, kuliko kupekua vitabu, kila aliyeandika anamakusudio yake! Ubepari ni pamoja na ukoloni na ukoloni mamboleo!
Kinachokera zaidi kudai eti unyonyaji wa sasa ni kutokana na tamaa za mataifa makubwa, sasa kama ndio mabepari wenyewe, sasa sisi kiburi cha kuamini ubepari kinatoka wapi? UN=CAPITALIST AGENT, nani tutamlilia wizi unaofanywa na MNC's zao ili akemee?
5. Pia ni kosa kabisa kusema ubepari ndio msing wa UTU, kwani UTU ni KUFIKIRIANA. Hakuna kufikiriana katika ubepari, ubepari ni individual compitition over resources, ni wazi huwezi kumfikiria mwengine! UTU haujawahi kuwepo wala hautakuwepo katika ubepari.
Mungu wetu anaita sasa!
 
Ndio hapo? nachowaambia ndugu zangu tusitake saana ku complicate mambo..Tunajua Ubepari umekuja itwa mfumo unaojali matajiri, wachache kuwanyonya wengi lakini ajabu ndani ya Ubepari unakuta huo huo unakuta kuna vyama vya Kisoshalist.

Ndio maana tunawaona kina Carter na Obama wanaitwa Wajamaa ndani ya nchi ya Kibepari na wanapinga kabisa fikra za Matajiri wachache kumiliki au kushika nguzo za uchumi. Sasa ikiwa Ubepari ni unyonyaji, hawa wanapinga vipi unyonyaji ilihali wanaukubali Ubepari - Capitalism?.

Mkuu Mkandara,
Hii mada unaichanganya sana; na unapoteza mtiririko; ni lini Carter na Obama walipinga fikra za matajiri wachache kumiliki au kushika nguzo za uchumi? Je hao mabepari au matajiri tunao Tanzania? Ubepari ni mfumo wenye misingi ya unyonyaji na ndio sababu nchi kama Marekani pamoja na kuwa ni ya kibepari kuna vyombo vingi vya sheria vinavyoangalia mwenendo mzima wa biashara kuna Antitrust &Trade Regulations commissions, Je ni kwanini kampuni ya simu AT&T ilivunjwa? Je ni kwanini Justice department na EU wana antitrust case na Microsoft Corp wanataka ivunjwe na iwe zaidi ya ya kampuni moja?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu Mkandara:
1. Nashindwa kuelewa unapokataa tusihushe ukoloni mamboleo na ubepari! Ni kweli kuwa ukoloni mambo leo uko ndani ya ubepari, lakini haimaanishi ni tofauti! Ubepari ni mfumo wa maisha, hali ukoloni mambo leo ni njia tu kufanikisha mfumo huo wa maisha! Ubepari ulianza na ulanguzi, viwanda, ukoloni, na sasa ukoloni mamboleo ukikingiwa kifua na utandawazi! Struggle for Capital! Kipi kinachokufanya useme havihusiani? Ipi ni tafsiri ya ubepari na ukoloni mamboleo kwako?
Mkuu Chama, ameeleza vizuri sana! Iko wazi kuwa Ubepari ni tangu Ulanguzi hadi Ukoloni Mamboleo leo hii. Ukoloni mamboleo, silaha yake ya kwanza ni kusambaza utumwa wa kifikra kwa walengwa. Ubepari aunadiwi kama uislamu au ukristo! Ubepari hucheza na hesabu kichwani, mnajikuta mmeshanasa mitegoni.
2. Ukiumiza kichwa huwezi pinga kuwa ufisadi ni zao la ubepari. Mimi naamini, Mfumo mbovu wa Siasa, ni chanzo cha uozo wote katika taifa! Ufisadi ni zao la mfumo wetu mbovu, nao ni demokrasia, nayo ni ubepari! Demokrasia ndiyo yenye kulubuni watu juu ya uwekezaji, ubinafsishaji, soko huria, Haki za Binadamu, n.k

3. Msidanganyike na yatokeayo kwenye nchi kubwa za kibepari, ni viini macho tu! Wapo ktk hatua ya juu ya ubepari, external capitalism, wanachofanya ni ku-maintain hilo kila kukicha!
 
Sasa naelewa kwa nini tunatofautiana.. Ukoloni mamboleo hauko ndani ya Ubepari hata kidogo na wala sii kweli Ubepari ni mfumo wa maisha. Ndio maana nikasema Ndivyo mlivyofundishwa..
Tafsiri za Ubepari hii hapa..
1.Capitalism is an economic system that is based on private ownership of the means of production and the creation of goods or services for profit.

2. Capitalism is an econimic system in which investment in and ownership of the means of production, distribution, and exchange of wealth is made and maintained chiefly by private individuals or corporations, especially as contrasted to cooperatively or state-owned means of wealth.

Zipo mia kidogo na zote zinasema neno moja tu Uhuru wa wananchi wenyewe kumiliki njia za uzalishaji,distribution na exchange of wealth kama nilivyosema awali. Na kwa tafsiri hizo hata dini yangu Islaam imeupitisha Ubepari, biblia na vitabu vyote.

Modern 'colonial era' colonialism -
1. Colonialism in this sense refers to Western European countries' colonization of lands mainly in the Americas, Africa, Asia and Oceania; the main European countries which were active in this form of colonization were Spain, Portugal, France, The Kingdom of England, The Netherlands and from the 18th century Great Britain. Each of these countries had a period of almost complete power in world trade from roughly 1500 to 1900.
2. May be used as a method of absorbing and assimilating foreign peoples into the culture of the imperial country, and thus destroying any remnant of the foreign cultures that might threaten the imperial territory over the long term by inspiring rebellion

Neo -Colonization - This term, usually pejorative, refers to a sort of "unofficial" colonization, in which a country's government is overthrown by larger country and replaced by a government that coincides with the larger country's interests. In effect, this makes the country a colony, dealing with the problem of a revolutionary uprising by delivering the impression that the colony is still self-governed.

Kwa hiyo ndio maana nasema hivi Ujama wetu haukulenga kabsia kuondosha Ubepari bali Ukoloni lakini kwa kujikuta tunaiga siasa za kushoto na Kulia tukachukua ya Urusi na China ambao wao siasa zao zilitokana na kukuta kwamba investment zote zilizopo nchini mwao zilikuwa za wageni na uhuru pekee wa bendera hauwezi kuondoa uhuru wao kiuchumi hivyo wakataifisha mali za wageni na kuziweka mikononi mwa serikali maana huwezi kuzigawa kwa wananchi utaanza vipi? Kwa hiyo sababu ya Ukomunist kuifanya serikali kumiliki njia za uzalishaji ni kuhakikisha wageni hawa own mali hizo lakini bahati mbaya imekula hadi kwa wananchi wake..

Pengine mtu pekee alofanya hivyo alikuwa Idd Amin kuchukua za Wahindi na kuwagawia mawanachi ambao kwa miaka 10 wali struggle lakini leo hii Uganda ndio nchi pekee Afrika Mashariki utakuwa Waganda ndio owners wa mashirika makubwa wal sii kwa kuiba au Ifisadi.

Tazama sasa Ulaya, Walokuwa wadhlimu wa Uhcumiwa Ulaya walikuwa Wayahudi mwanzo wa miaka 1900 hawa ndio walitawala njia kuu za uchumiwa Ulaya. Hitler pamoja na kumchukuia kwao waliweza kuwaondoa kistaarabu Wayahudi kwa kuwatafutia nchi nje ya Ulaya. Lakini kwa sababu hawakuwa na Kinga wayahudi wkaarudi na sasa hivi wamezikama nchi zote za kibepari hadi Marekani na wanalia japokuwa hawana budi.. Ulaya na Marekani zote zimekoloniwa na Myahudi kwa ukoloni mamboleo wakati wao mabepari. Ndio nikasema ktk Ubepari ni rahisi kuwa na wanyonyaji lakini haina maana kina Obama wanaopinga unyonyaji are against Ubepari..
 
Mkuu Mkandara:
Ukiumiza kichwa huwezi pinga kuwa ufisadi ni zao la ubepari. Mimi naamini, Mfumo mbovu wa Siasa, ni chanzo cha uozo wote katika taifa! Ufisadi ni zao la mfumo wetu mbovu, nao ni demokrasia, nayo ni ubepari! Demokrasia ndiyo yenye kulubuni watu juu ya uwekezaji, ubinafsishaji, soko huria, Haki za Binadamu, n.k
Mungu wetu anaita! !
Nichangie kidogo katika mnakasha. Sikubaliani kuwa ufisadi ni zao la ubepari. Hata katika nchi zenye itikadi tofauti na huo bado kuna mafisadi.Nakubaliana kabisa kuwa ufisadi ni zao la mfumo mbovu wa kiutawala na wa wataliwa.

Kuhusu demokrasia, nafikiri tunaelewa vibaya. Demokrasi ni mfumo uliokubaliwa na jamii fulani katika kuongoza maisha yao.Siyo lazima uwe wa magharibi hata wakati wa Watemi kulikuwa na demokrasia. Tofauti ni kuwa demokrasia ya wakati huo ilikuwa ni kwa ajili ya jamii fulani tu hatukuwa na demokrasia 'universal' kama tunayoiona sasa.

Ukifuatilia historia utaona Watemi na machifu walikuwa na taratibu zao zilizolenga kudumisha tawala, kutetea haki za jamii, kulinda haki za wanajamii na kusadia katika kuendelea. Tunaweza kutofautina kiwango cha maendeleo lakini maendeleo ya wakati huo yapimwe kwa nyakati. Unapoitoa jamii kutoka point A kwenda B hayo ni maendeleo.

senti thumuni.
 
Mkuu Mkandara: -
Maisha yapo katika nyanja kuu tatu, Uchumi, Siasa na Utamaduni, hizo ni nyanja za maisha si mifumo. Ili mwanadumu kuendesha maisha yake, anapaswa kuundia mifumo ya kuongoza nyanja hizo kuu! Ndipo demokrasia ikaibuka kuongoza Nyanja ya Siasa, hapo mwanzo ilikuwepo Ntemiship, Kingship hadi leo, Dictatorship, na mingeneyo mingi ambayo haijabuniwa bado, ila ipo! Nyanja ya uchumi ilipitia mifumo kama ujima, ukabaila, ujamaa na hivi sasa ubepari! Uchumi, Siasa na Utamaduni havitengani, vyote hukamilisha tafsiri ya Maisha! Ni kujidanganya kujaribu kuvitenga! Kutegemeana kwao, kunapokiukwa kimoja, huaribu kila kitu!
(Mnaweza kurejea kwenye thread niliyoianzisha humu, mnaweza kung'amua chochote)
1. Kama mfumo wa uchumi unaruhusu Private Ownership, basi mfumo wa siasa unapaswa kutunga sera za kulinda Private Ownership! Watu nao wanatakiwa kujengewa utamaduni wa kulinda Private Ownership!
2. Ubepari ni mfumo wa maisha kuongoza nyanja ya Uchumi, ili kufanikisha ubepari siasa ikabuniwa mifumo, leo hii mfumo wa kisiasa uliopo ni demokrasia, ili kulinda kulinda Ubepari-Private Ownership! Kama ilivyokuwa mnaouita udikteta, ili kulinda Ujamaa-Collective Ownership!
3. Kwanini sasa tunahusisha ufisadi, ukoloni na ukoloni mamboleo na UBEPARI. Hapa ni lazima kuchunguza dhana nzima ya Private Ownership, chanzo chake, jinsi inavyofanya kazi, hadi matokeo yake!
(a) Binadamu yeyote ameumbwa na tamaa, kujifikiria binafsi-kutaka kujikweza-UMIMI!
(b) UMIMI huwakisha tamaa juu ya hisa ya mwingine! Na kutamani kuhodhi zote! Kujifikiria!
(c) Matokeo yake ni wenye nguvu kujilimbikizia hisa za wanyonge!
* Ndivyo ufisadi na ukoloni ulivyoibuka. Ilianza mtu na mtu kumezea mate na kuhodhi hisa za mwenzake, kwa vile yuko huru, akafanikiwa. Ikaja kikundi cha watu kumezea mate hisa za wengine, WAKAZIWINDA wakachukua ili kujikweza! Huo ndio Ufisadi na jinsi ulivyohalalishwa na private ownership(struggle for private gains-individual level). Naita Internal Capitalism!
Kikundi kiliponyonya na kulimbikiza mtaji mkubwa, wakatamani kujikweza zaidi, mifumo ikawaambia wako huru! Ikaibuka taifa kuonea kijicho rasilimali za taifa jingine, ndivyo ukoloni na ukoloni mamboleo ulivyoibuka.(struggle for private gains-national level) Naita External Capitalism. Yaani kuna Internal na External Private Ownership of means of Production. Wakaibuka matajiri wakubwa, na masikini wa kutupwa! Kumuacha mtu huru kupigania maslahi binafsi ni kuhalalisha ufisadi na ukoloni. MSIDANGANYIKE NDUGU ZANGU: HAPA HATUJADILI NANI KASEMA NINI, ILA MANTIKI YA MAMBO-LOGIC - UTU.
3. Mkuu Nguruvi3:
Labda ungemeng'enya zaidi juu ya tafsiri ya Demokrasia. Unadai ni Mfumo uliokubaliwa na watu kuongoza maisha yao. Je, kila mfumo uliokubalika ni demokrasia, Kingship kwa Muswati? Utaifishaji je? Monopartism je?
Tusitoe tafsiri rahisi juu ya haya mambo, ni lazima tuingie kwenye tafakari ya kina juu ya haya mambo, si kuamini tu kila kisemwacho. Demokrasia ni mfumo wa siasa, wenye kuegemea dhana ya uhalali-haki za binadamu-uhuru=ubepari.
*Naomba niwaache na hili: Maisha ni Hatua, Kusiwe na 2 kama hakuna 1 na 1, logically ukipiga hatua ya 2 hali mwenzake hana hata 1, utakuwa ume-undermine fursa ya mwenzako, matokeo yake ni kuwindwa, atatumia nguvu kurudisha hisa yake, ndio maana nasema Maisha ni Furaha, kama haipo ni upuuzi mkubwa, na hakuna furaha ya mtu ila watu-KUFIKIRIANA -UTU. Dhana ya Private Ownership haiwez kutufikisha huku, ila kwenye Unyonge.
Mungu wetu anaita!
 
Mkuu JingalaFalsafa,
Kwanini umefikiria mswati na si malkia Elizabeth au mfalme wa Jordan,Saudia au Norway?
Labda utufafanulie, tatizo la mswati ni nini? na linatofuatiana vipi na la Malkia Elizabeth!

Mkuu Mkandara nimemuelewa vema sana.Ukimsoma vizuri anahoja kuwa hiyo private ownership iwe kwa wenye nchi.
Ukiangalia kwa makini ana mantiki, China walikuwa na state ownership taratibu wanaachia wananchi wao umiliki wa nchi yao. Mabepari wakubwa duniani miongoni mwao ni Wachina, lakini china haijaacha dhana yake ya ukomunist.
Wanachokifanyani kutoka hatua moja kwenda nyingine. Vivyo hivyo kwa Cuba.

Ninachokionani kuwa tunatakiwa tulinde haki za wananchi lakini si kuwalinda wananchi wasizitumie haki zao.
Labda tu utueleze kuwa kinadharia ungekuwa katika nafasi ya kuongoza nchi hii ungefanya kitu gani na kwa namna gani kutetea hoja yako.
 
Mkuu Nguruvi3:
1. Mbona sijamkosoa Muswati, ila kumtolea mfano tu! Nimeuliza je ile ni demokrasia, maana kwa tafsiri yako "demokrasia ni mfumo uliokubaliwa na watu kuongoza maisha yao" Jordan na Saudia ni mifano mingine bora kabisa, watu wameikubali-je ni demokrasia? Tafakarini vizuri juu ya Kanuni za Demokrasia, mtaoona mitego tuliyoekewa humo, naamini mtanielewa! Ndio maana nasema Demokrasia ni Ubepari, Ubepari ni Private Ownership, yaani MIMI KWANZA-KUJIFIKIRIA NA KUJIPIGANIA BINAFSI-kupigania tamaa zako, rushwa, ufisadi, kuwinda kama simba na swala, wizi, n.k haviwezi kukwepeka hapa!
2. Ndugu zangu, embu jaribuni kuelewa dhana ya Internal na Extenal Capitalism. Nchi ni lazima ipitie Internal Capitalism ili ipate mtaji wa kufikia External Capitalism, nchi nyingi za ng'ambo wameshafikia hatua ya pili, hawana haja ya kujinyonya wenyewe kwa wenyewe, kwani sisi tupo! Sasa sisi lini tunafikiri tutaweza kupata mtaji mkubwa wa kunyonya taifa lolote? Hata tukiupata, tutamnyonya nani kama sio waafrika wenzetu Msumbiji na Malawi? Hatuioni Kenya inavyotusumbua? Bidhaa ngapi feki wanatuingizia? Utalii nao? Huo ndio ubepari-private ownership mnayoitaka!
2. Ukishaingia kwenye mtego wa kuthamini neno HAKI, hakika UMEPOTEA KABISA! Na kila utakachotafakari lazima kipate ukinzani mwenyewe kabla hujakosolewa. HAKI ni silaha kubwa kabisa ya kukiuka MANTIKI. Haki ni Msingi mkuu wa Ukoloni Mamboleo! Haki ndio mama wa Utumwa wa Kifikra!
HAKI NI UPUMBAVU!
3. Uongozi ni Ubunifu mkuu wangu: Naamini kabisa, adui yetu wa kwanza ni nafsi zetu wenyewe! Nafsi huongoza akili, akili ikishindwa kuona uovu au ikaona na nafsi ikashndwa kuchukua hatua, basi mwili hautakuwa na pingamizi tena, ila kuumia tu! Elimu, Sanaa na Habari, ni silaha bora kwangu katika kujenga utakacho! Ubunifu Haujawahi Kufika Mwisho.
Mungu wetu anaita sasa!
 
Mkuu JingalaFalsafa,
Kwanini umefikiria mswati na si malkia Elizabeth au mfalme wa Jordan,Saudia au Norway?
Labda utufafanulie, tatizo la mswati ni nini? na linatofuatiana vipi na la Malkia Elizabeth!

Mkuu Mkandara nimemuelewa vema sana.Ukimsoma vizuri anahoja kuwa hiyo private ownership iwe kwa wenye nchi.
Ukiangalia kwa makini ana mantiki, China walikuwa na state ownership taratibu wanaachia wananchi wao umiliki wa nchi yao. Mabepari wakubwa duniani miongoni mwao ni Wachina, lakini china haijaacha dhana yake ya ukomunist.
Wanachokifanyani kutoka hatua moja kwenda nyingine. Vivyo hivyo kwa Cuba.

Ninachokionani kuwa tunatakiwa tulinde haki za wananchi lakini si kuwalinda wananchi wasizitumie haki zao.
Labda tu utueleze kuwa kinadharia ungekuwa katika nafasi ya kuongoza nchi hii ungefanya kitu gani na kwa namna gani kutetea hoja yako.
Nashukuru sana kwamba wewe umenielewa kwa sababu mimi najaribu kufikiria nje ya box hili la elimu tulopewa..Ujamaa kwa kila hali ulitokana na kupinga ukoloni na ukoloni mamboleo ambao wageni wanakuja nchini mwetu na kumiliki mali zetu. Hakuna Ujamaa ulotokana na wananchi wenyewe yaani Azimio la Kijamaa lilotokana na kumtazama mwananchi mzawa - Hakuna. Kwa hiyo ndio maana tukataifisha mali za wageni na kuzifanya zetu, kwa kitendo hicho tukaitwa Masocialist lakini deep inside haikuwa kuwafanyia wananchi. Wale waliowaachia wazungu kuelendelea kumiliki mali zao hawakuitwa Wajamaa...

Na ndivyo nasi tunapokuja ktk Ujamaa, nikasema Ujamaa ni Udikteta kwa maana ya kwamba tulipochukua mali zile tuliotakiwa kuendelea kujikinga na wageni na sio kuwawekea sheria sasa wananchi. Katika Ujamaa tukaona dini zinakatazwa, tukaona ni chama kimoja tu kinaruhusiwa kuongoza, hakuna uchaguziisipokuwa wa viongozi wa chama hicho na fikra za muasisi wake kudumishwa. Yeyote anayepingana na fikra hizo aliwekwa ndani ama kuhukumiwa kifo..

Lakini hivi kweli Ujamaa ndivyo ulivyotakiwa? hapana hata kidogo Ujamaa ulikuwa na misingi tofauti kabisa lakini ukazaa mavitu machafu pia kama tunavyoona ktk Ukoloni. Mugabe leo anaitwa Mjamaa kwa sababu kachukua mashamba ya wazungu na kuwapa weusi, hivi kweli anazuia unyonyaji upi hapa?.

Hakuna ubaya kabisa kuweka kufanya hivyo ikiwa yanamlenga adui wetu sote ambaye ni mgeni alokuja tuibia rasilimali zetu toka watun enzi za utumwa hadi malighafi zetu, lakini Ujamaa failed kote duniani kwa sababu uliacha kulinda gate kubwa ukaanza kuwazuia hata wananchi wenyewe kumiliki mali wala kutoka nje. Sasa utaweza vipi kuondoa Umaskini ikiwa mwananchi mwenyewe unamzuia kuwmiliki mali?.. how sii ndio yale ya kugawana mtaji. Na ndivyo wanavyofikiria hata ndugu zangu.. Ukienda Bongo na Usd 10,000 wanafikira uwagawie kila mmoja wao na sio kwa kuinvest hapana ninmatunda ya kazi ulofanya na halali yao kutumia wakatavyo.

Wadanganyika hawafikirii what Usd 10,000 inaweza kuzalisha na tukagawana faida isipokuwa hawataki faida tugawane Mtaji (capital). Sifanyi kutunga haya maneno ni hali halisi nyumbani. Peleka Lorry semi traile au Daladala, watalinywa kwa sababu wao wanahesabu kuwa haya ni matunda ya kazi yako huko Ulaya..Hakuna mtu anayefikiria kuwa huo ni MTAJI na ndio utajirisho utakao zalisha utajiri ama wao kula faida yake..

Ndio maana nasisitiza ya kwamba turudi nyuma na kutazama maadui wetu ktk kutafuta ushindi wa kuondoa Umaskini, Ujinga na maradhi nchini..
 
Back
Top Bottom