Mkuu Mkandara,
Kujenga ubepari kuna misingi yake hao waliojenga ubapari hawakuanza kwa kukopa walitumia rasilimali zao kuleta mapinduzi ya uchumi; katika kujenga ubepari hakuna njia ya mkato wewe unachotaka kulazimisha ni Tanzania kutumia njia za mkato kitu ambacho hakiwezekani; nadhani unachanganya mada udikteta hauna mahusiano na ujamaa wala ubepari ni mtawala mwenyewe ndiye anayeamua kuwa Dikteta, je Mussolini alikuwa mjamaa?; je Mobutu alikuwa mjamaa; Marcias Nguema na Bokasa walikuwa wajamaa?
Chama
Gongo la mboto DSM
Ubepari haukujengwa na mtu yeyote, Ubepari ulikuwepo kabla ya tawala zote duniani na ndio msingi wa UTU wa binadamu..Soma vitabu vyote utakuta ukweli nikwamba sisi tuliumbwa ili kujitegemea, kila mmoja wetu atakula kwa jasho lake...Kifupi ni kwamba nchi zote duniani zilikuwa Mabepari kwanza..Sisi Ukerewe babu zetu walikuwa wakimiliki mashamba yao hata kabla ya mkoloni, walikuwa na mitumbwi, miti ya maembe, mabanda ya mifugo na kadhalika kama mali zao hii toka Nuhu...
Wakaja tokea watu waliokiuka UTU hao wakoloni wakaanza kufikiria cha mwingine maana makwao hawakuwa na resources kama zetu kukidhi mahitaji yao. In fact nisema hivi nchi ni Uingereza, Germany, Holland, France, Spain, Portugal na Italia hawa wote hawa kuujenga Ubepari hta kidogo waliukuta kama tulivyoukuta sisi kwa mababu zetu. Isipokuwa Tamaa za viongozi wao (Kings na Malkia) kushindwa kuwahudumia wananchi wao kutokana na uchache wa resources ndio walofikiria njia za kuanza kwenda kuteka na kutawala mataifa mengine..
Muingereza ana nini? Mfaransa ana nini wote hawa wameishi kwa ujanja ujanja miaka yote na ndio maana Globalisation sasa hivi inakuwa na impact kwao kwa sababu hawana tena makoloni na nchi nyingi zinaanza kuwatajirisha wananchi wao..Wa kwanza kuanguka nihao Wagiriki, Waspanish na Wataliani maana wameishiwa akiba walovuna ktk ukoloni..Mmarekani ndio hivyo yeye analazimisha makoloni hadi kesho maana rasilimali zake anaziacha kwa kizazi kijasho, mafuta wanayo mengi tu lakini hayachimbi - Why?
Kwa hiyo tulichokiona sii Ubepari bali ni Ukoloni na tunachokiona leo sio Ubepari bali Ukoloni mamboleo na ndio maana ukilaani Ubepari nchi za magharibi hawatakuelewa kabisa..Katia Ukoloni hawa jamaa Afrika walitukuta tayari mabepari vile vile, wananchi wake wakimiliki mali zao. Wazungu wakakuta utajiri mkubwa sana huku hivyo wakaziteka nchi zetu, wakaweka vikao Berlin kugawana mipaka toka kwetu Afrika, South Amerika, Arabuni, India hadi China na kwa shangwe na wakiwatukuza Christopher Columbus, Livingston, Speke, Vasco Da Gama na wengineo kuwa mashujaa wao. Kote tuliwekwa utumwani hali na mali zetu, tukawatumikia kwa malipo ya wages huku wakichukua mali zetu makwao.
Wizi huu haukuwa Ubepari hilo nakataa kabisa. Ni sawa na mtu anambie Ufisadi nchini umetokana na Ubepari.. haya ni majibu rahisi sana hatutaki kuuchosha ubongo. Na hata kutokea kwa vigogo kama kina Karl max, Stalin, Mao, Lenin, Ghandi na wengineo ilitokana na fikra za kuondokana na Ukoloni.. narudia tena maneno haya sijui mara ya ngapi..Hawa watu, viongozi wenye vision walikaa na kutafakari ubaya wa kutawaliwa, ubaya wa kukoloniwa, ndipo fikra za mapinduzi dhidi ya wadharimu hawa zikazaliwa. Hizo Fikra za kuwaondoa Wakoloni ndizo zilizozaa Ujamaa baadaye japokuwa mwanzo kabisa wa Ujamaa ilikuwa kuwaondoa wakoloni kama walivyoondolewa Saudia, India au Kenya..
Utanisamehe nitatumia lugha chafu kidogo hapa. Ujamaa ni sawa na matumizi ya condom. Lengo haswa ya matumizi ya condom tumesisitizwa kuwa kinga ya maradhi haswa HIV (Ukimwi) lakini tatizo la Condom ni kwamba sii tu inazuia Ukimwi bali pia inazuia pia Uzazi. Hakuna kinachoingia wala kinachotoka, hivyo kiuchumi tunasema matumizi ya condom mwanamme au mwanamke hawezi zijalisha mwenyewe labda kwa kupandikiza. Haya sii maisha ila ni mateso mengine kwa watu wanaofahamu kabisa wanaweza kuzaa halafu matumizi ya condom ndio inakuwa maisha yao..naomba unielewe sina maana mbaya kabisa ya kukashifu matumizi ya condom laa hasha..Ila ndio ukweli uliopo na zipo njia bora zaidi na ndizo nazojaribu kuelezea hapa..
Kinachotakiwa haswa ni kutafuta njia nyingine ya uzazi, na bora zaidi ya zote ni watu kuwa huru zaidi kuchagua mwenza alokuwa mzima, asiyetaka kuambukizana, anayechukia Gonjwa na sii mgonjwa na kushirikiana naye kimwili kwa malengo ya kupata mtoto sasa sio tena kuogopa Ukimwi. Na ndio maana nasema Ubepari sio gonjwa bali gonjwa ni kukoloniwa kiuchumi.
Mwiho nakubali kwamba kuna uwezekano mmoja wenu anaweza ambukizwa kwa njia nyingi iwe ufisadi au tamaa ile ile walokuwa nayo Mwakoloni, lakini kama tunaelewa adui wetu na njia za kinga, tukaweka regulations ambazo zinatulinda sote bila shaka tutakuwa salama.
Kinachoniudhi mimi kuhusu matumizi mabaya ya Ujamaa ni pale unapomvalia condom hata mkeo kila siku kwa tahadhari ya Ukimwi halafu unasema tunaamianiana. Huku kuaminiana hali hatuaminiani ndiko kunakopelekea watu kuwa washenzi vile vile maana hatuna regulations zaidi ya kuamini condoms tu. Hii ndio ilosababisha watu wakauchukia Ujamaa kwa sababu haukuwaamini wananchi wenyewe japokuwa Uhuru tulopigania ulitokana na sisi kuaminiana kwanza.
Hao ulowataja kuwa Madikteta wakati ni mabepari unashindwa kuelewa kwamba wananchi wake hawakuwa huru kumiliki mali bali wao ndio walimiki mali ama kugawa mali walizopenda kuzigawa kinyume cha pale wao ndio wali own karibu kila utajiri wa nchi hizo. Leo hii huwezi kunambia Saudia ni Mabepari kwa sababu ya kuwa na open market system ilihali Sultan owns almost everything, hata nyumba unapewa na Sultan ati ni haki yako - Hawa Wametawaliwa..
- Sijui kama umenielewa?