Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Mkandara;4415626]Jmushi1, utajiri wa Romney unajulikana wala sio siri isipokuwa wanajua kuna mambo ambayo Romney hawezi kuyaweka wazi ndio maana wanambana ili kuharibu profile yake, lakini hakuvunja sheria isipokuwa yataleta picha mbaya kwa wananchi wapiga kura ujio uchaguzi mkuu. Kama kungekuwa na baya, IRS (Renevue) wasingemwacha hata kidogo isipokuwa lengo ni image yake as a President ikijulikana alikuwa anatengeneza ngapi kwa mwaka akiwa CEO halafu mashirika yale yakafa, watu wakapoteza fedha zao itamweka pabaya ktk uchaguzi
Romney aliweka mapesa kwenye mabenki ya nje ya nchi yake, hilo si kosa lakini kama mzalendo hakupaswa kufanya hivyo kwani hapo tu atakuwa amekwepa kodi hata kama ni halali. Pili, democrat wanataka waonyeshe kiasi cha kodi na cha wafanyakazi wake ili wajenge hoja kama kweli yupo na middle class. Na tatu wanataka ijulikane wakati anaua kampuni alipata kiasi gani, alilipa kodi kiasi gani ili waonyeshe jinsi gani dhana yake ya umahiri katika small business na job creation ilivyo na utata
Labda nimalizie kwa kusema unajua Marekani na Ulaya hawa ni WAJAMAA kuliko hata sisi. na ndio maana utaona Liberal wanashinda kwa matumizi halisi ya neno lenyewe kwa sababu hawa hawajatawaliwa.. Ujamaa wao umetokana na kutukuza traditional zao..wanathamini KAZI kiasi kwamba unemployement rate tu ikipanda inamwangusha kiongozi ktk urais..Priorites zao ziko wazi kabisa, iwe system yenyewe jinsi wanavyosaidiana toka welfare hadi job creation huwezi kulinganisha na sisi.. wakati mwingie husema hawa Mabepari ni wajamaa kuliko sisi maana Just Imagine how much monies Bill Gates anatoa kusaidia nchi maskini ktk maradhi?.. Anatumia billions kuliko bejeti ya nchi zetu ktk huduma ya Afya.. Kina sisi ni michango ya harusi, hata kwenda hospital tu kutembelea wagonjwa tunashindwa ila kwenda kupiga picha za wagonjwa, madaktari walipogoma kuonyesha unyama wa serikali!..What did you do to help the sick ones?.. NOTHING! Ujamaa wetu umetokana na experience ya kukoloniwa na tumeshindwa hata kutetea mila na desturi zetu wenyewe tumebakia kuiga kila kitu kiasi kwamba tunaogopa hadi vivuli vyetu wenyewe..
Umenena, hawa wanaotuletea utandawazi n.k. na wanaupinga ujamaa, ukweli ni kuwa wao ni wajamaa. Walichokifanya ni kuchukua element nzuri za ujamaa na kuzichanganya na zile zao. Kwa mfano, chimbuko la social welfare siyo magharibi ni nchi za mashariki ya kati na linahusiana na dini.
Walichokifanya ni kuchukua muundo na kuufanya u-fit mazingira yao na hilo wamefanikiwa.
Unemployment ni sehemu nyingine ya kulinda jamii zao. Wanajua kuwa unemployment inaweza kuleta unrest na hivyo jamii ya mabwanyeye kuwa matatani. Wakaweka Employment insurance ili kuhakikisha kuwa jamii inalindwa.

Mfano mwingine ni wa Insurance ziwe za auto, house n.k. Tunajua wazi kuwa makampuni ya insurance ni ya kibepari na kazi yao ni kukamua walaji na watumiaji. Lakini pia serikali imeweka taratibu zinazomlinda mlaji au mtumiaji pindi linapotokea lisilotarajiwa.

Huko mahospitalini sasa wanaweka insurance za watu wao na hilo ndilo tatizo Obama analokabiliana nalo. Nia ni kuhakikisha kuwa huo ubepari katika matibabu hauvuki mipaka ya kuwaumiza watu.
Wamefikia hata ku-regulate wall street ili kuhakikisha kuwa jamii haipati misuko suko kama ile ya mwaka 2006-2008 iliyosababisha mtikisiko wa uchumi duniani.

Katika yote hayo sisi hakuna hata kimoja tunachoweka kumlinda mtu wetu. Tumemeza ubepari na ujamaa kama ulivyo na kuimba ubinafsishaji bila hata kuangalia mazingira yetu. Fikiri auto insurance yako Tanzania inakulinda vipi na linganisha na ya wenzetu. Fikiria health system yetu inakulinda vipi ukilinganisha na wenzetu.

Kwa maneno mengine, tumemeza kila kitu bila kufikiria au kuangalia kama kila tunachomezeshwa kinawiana na jamii yetu. Tumeshindwa kufikiri kwasababu tuna hoja rahisi kuwa ubepari au ujamaa ndiyo mifumo inayopaswa kutuongoza.
Ikifika hapo nakubaliana kabisa na jmushi1 kuwa hivi hakuna uwezekano wa sisi kutengeneza kitu kinachofanana au kuwiana na mazingira yetu na kwa manufaa ya jamii yetu bila kumeza maelekezo tu ya uwekezaji, ubinafsishaji holela,ujamaa n.k!

Najua hoja hapa ni kuwa wakubwa watatumia marungu yao ya WB, IMF kutukwaza. Mimi huwa najiuliza Malaysia wamewezaje kutoka pale tulipokuwa nao na kutuacha? Scandinavia wamewezaje kuwa ni mifumo inayolingana na jamii zao? Wahindi wamewezaje kuchomoka katika mitego ya wakubwa? Kwanini sisi tusifikirie na tubaki tukilalama tu.
Hivi tunawezaje kuwa na kiongozi anayekwenda kuangalia utalii nasi kufikiria namna gani ya kuendeleza tulio nao?
 
Mkandara,nakubaliana kabisa na wewe,kuwa hata Obama ni bepari,na kwamba hayo ambayo tunayaona ama wanayaona kuwa yataleta picha mbaya lakini ni ya kisheria.Kwa upande mwingine,kuna mabepari wazuri na wabaya depending on your position.Kuna mabepari wanaokubaliana kuwa walipe kodi zaidi ama sawa na watumishi wao ie secretary.Mfano ni Warren Buffet ambaye pamoja na kwamba ni mmoja wa matajiri wakubwa duniani,bado anaona si fair kulipa kodi ndogo zaidi ya secretary wake,licha ya kwamba si uvunjifu wa sheria,bali tu ni reasoning ya kibepari.Na ndo maana nikasema wengine wanaweza wasielewe inakuwaje hizi practices ni za kisheria?Kiukweli kuoutsource jobs ni part of free market,lakini consequences zake ni sawa tu na kuhujumu uchumi,lakini ni halali chini ya ubepari,so issue inapelekwa kwa wananchi ambao ndiyo wapiga kura,which that's "democracy"...Lakini endapo vitatungiwa sheria kali vitendo kama hivyo,wanadai kuwa ni udikteta kupingana na free market na democrasia na unaitwa msoshalisti na anti west.

Mkuu mimi nipingane na ubepari nina uwezo huo?mimi na analyse tu,that's it,na kutoa mapendekezo,lakini asilani sina uwezo wa kupingana na haya mambo ambayo ni kama "forces of world"

Mfumo wa ubepari umeshatake over and there is nothing to do zadi ya kujaribu kuya cover yale "mapungufu" yake.
 
Nguruvi3,very well said kwenye post yako #268,I always admire your intake,kwakweli wewe ni among great thinkers na kwa jinsi unavyoelezea,una kipaji cha kutumikia wananchi kwasababu una sifa ya kueleze issue ngumu kiurahisi na ukaeleweka.Shukran for real.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu wangu Mkandara, jmushi1 na Nguruvi3 nawapata vilivyo, lakini sitaacha kusema kuwa.....
HII NI MITEGO, tunatembea bila tahadhali, tunaiona tunapuuza kuchukulia hatua mahususi kwa Kujifikria binafs, UMIMI wetu badala ya WATOTO WETU! Mantiki ya UTU inapokiukwa kwa kufuata hisia na tamaa zake mtu, matendo ya mwanadamu hugeuka kuwa ya kinyama, kinyama, kinyama kila kona! Ni UNYAMA! UTU haujawahi patikana kwenye Ubepari, kwani UTU si UHURU wala HAKI kama asemavyo Mkandara! UTU ni MANTIKI, NAYO NI UWIANO SAHIHI, yaani ni KUFIKIRIANA!
Mnapopata shida sana kunielewa, ni kuingia ndani ya Ujamaa na Ubepari na kuanza kuhoji yaliyomo humo! MNAKOSEA! Kaeni nje yake! Anzeni na kujiuliza binafsi, wewe ni nani, maisha ni nini, kipi ni kipi? Na kinatakiwa kiweje, na kwasababu gani na ili iwe nini? Anzeni chini kabisa! Baada ya hapo, njoo karibu na hoji yale yaliyopo katika mizani ya tafakari yako ya kwanza! Je, yana mashiko au laa? Nasema tena, UTU si HAKI wala UHURU! Hivyo Ubepari hauna UTU hata siku moja! Hata ujamaa tuliouishi vile vile, japo katika falsafa kuu ya Ujamaa nauona humo! Swala ni vipi watu tunaupokea na kuuweka katika vitendo!
Muhimu ni kuwa, mfumo wowote lazima usadifu yaliyomo katika Eneo husika, yaani MAZINGIRA na NYAKATI mahususi! Ubepari hauna unachosadifu kwetu! Mbaya zaidi, umekiuka msingi mkuu wa maisha, UTU(ni kwa imani yangu), Ujamaa umesadifu Msingi mkuu wa maisha-UTU, kilichotakiwa ni kuusadifisha na eneo letu, yaani mazingira na nyakati zetu, hapa ndipo alipojaribu Nyerere, lakini kwa bahati mbaya akashindwa, na sababu kuu ni kutaka matokeo ya haraka, asingeweza kamwe, kwani hata mwanae asingeyaona! Lakini hiki kisitufanye tugeukie UOVU! TUKAE CHINI, TUTAFAKARI. Ubunifu haujawahi kufika mwisho.
Mungu wetu anaita.
 
Wakuu wangu Mkandara, jmushi1 na Nguruvi3 nawapata vilivyo, lakini sitaacha kusema kuwa.....
HII NI MITEGO, tunatembea bila tahadhali, tunaiona tunapuuza kuchukulia hatua mahususi kwa Kujifikria binafs, UMIMI wetu badala ya WATOTO WETU! Mantiki ya UTU inapokiukwa kwa kufuata hisia na tamaa zake mtu, matendo ya mwanadamu hugeuka kuwa ya kinyama, kinyama, kinyama kila kona! Ni UNYAMA! UTU haujawahi patikana kwenye Ubepari, kwani UTU si UHURU wala HAKI kama asemavyo Mkandara! UTU ni MANTIKI, NAYO NI UWIANO SAHIHI, yaani ni KUFIKIRIANA!
Mnapopata shida sana kunielewa, ni kuingia ndani ya Ujamaa na Ubepari na kuanza kuhoji yaliyomo humo! MNAKOSEA! Kaeni nje yake! Anzeni na kujiuliza binafsi, wewe ni nani, maisha ni nini, kipi ni kipi? Na kinatakiwa kiweje, na kwasababu gani na ili iwe nini? Anzeni chini kabisa! Baada ya hapo, njoo karibu na hoji yale yaliyopo katika mizani ya tafakari yako ya kwanza! Je, yana mashiko au laa? Nasema tena, UTU si HAKI wala UHURU! Hivyo Ubepari hauna UTU hata siku moja! Hata ujamaa tuliouishi vile vile, japo katika falsafa kuu ya Ujamaa nauona humo! Swala ni vipi watu tunaupokea na kuuweka katika vitendo!
Muhimu ni kuwa, mfumo wowote lazima usadifu yaliyomo katika Eneo husika, yaani MAZINGIRA na NYAKATI mahususi! Ubepari hauna unachosadifu kwetu! Mbaya zaidi, umekiuka msingi mkuu wa maisha, UTU(ni kwa imani yangu), Ujamaa umesadifu Msingi mkuu wa maisha-UTU, kilichotakiwa ni kuusadifisha na eneo letu, yaani mazingira na nyakati zetu, hapa ndipo alipojaribu Nyerere, lakini kwa bahati mbaya akashindwa, na sababu kuu ni kutaka matokeo ya haraka, asingeweza kamwe, kwani hata mwanae asingeyaona! Lakini hiki kisitufanye tugeukie UOVU! TUKAE CHINI, TUTAFAKARI. Ubunifu haujawahi kufika mwisho. Mungu wetu anaita.
Mkuu, sasa hivi ni dhahiri kuwa hakuna mfumo unaoweza kusema unasimama wenyewe. Wajamaa wanalegeza uzi, mabepari nao wamegeugia ujamaa.

Kama ujamaa ndio kiini cha utu kama usemavyo, nina mashaka kwasababu unapo mbana mtu mpaka akajichukia halafu useme huo ndio utu inanishangaza.Unapomnyima mtu fursa ya kuchagua maisha kutokana na juhudi zake eti huo ndio utu napata taabu kukuelewa.

Unaposema mfumo unaosadifu mahali na nyakati nadhani unaaungana nami wengine kuwa lazima tuwe na kitu chetu kinacholingana na mazingira yetu. Kuna ubaya gani kuiga mazuri ya ujamaa na Ubepari ili uwe na kitu chenye mazuri unayoyataka?

Nisichokubaliana nacho ni kumeza kila kitu bila kuwa na chembe ya tafakari. Tumeambiwa ubinafsishaji, sisi tumeacha Ikulu na Magereza tu, lakini huko ulikotoka wamekataa Reli na miundo mbinu isibinafsishwe. Kilichomuondoa Thatcher ni kutaka kubinafsisha reli. Leo sisi hatujifunzi tumewapa wahuni kutoka India wameng'oa hata iliyokuwepo!

Kwa upande mwingine kwanini tumzuie mtu asilime ekari 100 eti kufanya hivyo ni ubepari. Kwanini tumzuie mtu asifanye biashara anayoweza eti kufanya hivyo ni kujenga ubepari na anayepaswa ni NMC na RTC.

JingalaFalsafa kama ubunifu haujafika mwisho, sasa ndio wakati wa sisi kuwa wabunifu wa miundo na mifumo inayolingana na mazingira yetu siyo imported from east to west.
Juu ya yote hayo nakubaliana nawe kuwa ili kufanikiwa ni lazima utu uwepo na kuleta utu ndio hoja yangu ya misingi ya sheria, taratibu na maadili inapohitajika.
 
Mkuu Nguruvi:
Nimesema naikubali Falsafa kuu ya Ujamaa, sio kusema nakubali walivyoishi Cuba, Tanzania, Korea, Urusi ama China! Hata hivyo Thamani ya UTU haiwezekani kufananishwa na hata gharama uhai wa watu wote duniani, iweje hisia za watu zilizojengwa kwa tamaa zao mbaya, eti zinavunja UTU kwa kudai UHURU & HAKI?
Nilisema awali, kuwa CHUNGUZENI KWA MAKINI NENO "HAKI", mtaona HILA na FITINA zilizojaa humo!
Hakika hakuna MANTIKI ya mtu kupiga hatua ya 3 hali jiraniye hana hata moja! Ni Ukandamizaji, kwanini uwepo wako juu, NI LAZIMA UTEGEMEE UWEPO WANGU CHINI, kwenu ni HAKI/HALALI, kwangu ni HILA na ni upumbavu!
Ndio maana nakubali Falsafa kuu ya Ujamaa, nayo imo kwenye maneno haya "From Each According to His Ability. To Each According to His Needs" yalishanenwa haya, na huu ndio Ujamaa, si kusema watu walikuwa wanapigwa, rais alikuwa dikteta, au kiongozi alijifanya mungumtu, au alikuwa amehodhi utajiri mwingi, UKIWA UNAHOJI UJAMAA KWA MISINGI YA NANI ALIISHI VIPI, HAKIKA UNAPOTEA, na hutoacha kubisha!
Na kama hayo yote yamekuwa yakifanyika ili kulinda Mantiki ya UTU inayopatikana katika Falsafa kuu ya Ujamaa, basi hatuna budi KUYABARIKI kwa mikono miwili!
HAKIKA, ubunifu haujawahi Kufika Mwisho, na Hautafika kamwe! Nafasi tunayo! Ninaposema Falsafa Kuu ya Ujamaa, yaani UTU inayojidhihirisha kwenye kauli ya Marx na Engles hapo juu, sina maana kuwa nimei-copy na kui-paste akilini mwangu, HAPANA! Hakika kuikubali kwangu ni zao la tafakari zangu huru, pasi kufungwa na chochote chini ya jua na hata huko tunakoamini Mungu yupo! Baada ya tafakari yangu, ndipo nikang'amua kipasacho kuniongoza katika kila jambo, nacho si HISIA zangu bali ni MANTIKI ya Mambo, yaani UTU, hapo ndipo napokubali uwepo wa Mungu, na Maisha! Na kwa kuzingatia mantiki hiyo ipi ni maana ya maisha, kuisi, na tuishije, ili iwe nini kwa nani! Baada ya hapo, ndipo nikaingiza tafakari yangu katika kila nikionacho, nikisikiacho ama kukihisi, yaani imani, falsafa, dini, sera, mifumo, itikadi, mitazamo, matendo, na kila kitu, na matokeo yake vyote vilivyopo ni UPUUZI! Yaani maisha ni UPUUZI, kwani vilivyomo havifuati Mantiki kuu, yaani UTU, UWIANO SAHIHI-KUFIKIRIANA, ambako kupo hata katika Falsafa kuu ya Ujamaa, "From Each According to His Ability. To Each According to His Needs" kama Ujamaa ni kinyume na hapo, basi nao ni Upuuzi!
Ubunifu wetu na uwe wa kuratibu jinsi gani ya kuratibu yaliyomo kwenye kauli hiyo, tuishije kulinda kauli hiyo. Tuanze wapi kusimika kauli hiyo katika maisha yetu? Tuanzeje? Hayo ndio maswali magumu kwetu, yanayohitaji mimi na wewe tukae chini tuumize vichwa, tufanye maamuzi na kuchukua hatu stahiki, baada ya kula kiapo moyoni mwako mwenyewe! Binafsi, naamini Utamaduni ndio mama wa Siasa na Uchumi, tungeanza huko!
Adui yangu wa kwanza, ni nafsi yangu mwenyewe!
Mungu wetu anaita sasa!
 
MAREJEO NA TATHMINI

Wanajamvi na wadau wa duru za siasa.
Niwakumbushe kuwa nyuzi yetu ya duru za siasa itafikisha mwaka mmoja Augut 26 mwaka huu.
Nimeonelea ni wakati muafka wa kupata usuli(feedback) na kuangalia wapi tunaelekea na maboresho yanayohitajika.

Kwanza niwashukuru sana wasomaji, na wachangiaji ambao kwa lugha ya staha,heshima na mantiki wameweza kufanya ukumbi huu kuwa na staratarajiwa katika kiwango cha JF.

Lakini si lugha tu bali maudhui ya hoja yanafurahisha, kupingana bila kupigana na kukubaliana kutokubaliana.
Binafsi huwa nafurahi sana kwa jinsi ninavyodokoa vitu kila uchao.
Kama kuna mtu anakwambia elimu ina mwisho basi 'run the other way'.

Ukumbi huu ni wa wazi na unaojadili na kubalishana mawazo kuhusu masuala mbali mbali yanayotuzunguka yawe ya kitaifa au kimataifa. Ni sehemu ya mawazo huru na haifungamani na upande wowote wala kuathiri itikadi ya mtu kwa jambo lolote na namna yoyote. Tunaendelea kuwakaribisha wote wenye mawazo hasi na ya stara kushiriki nasi.

Tumekuwa na maboresho siku za karibuni kuhahakisha kuwa mada inapewa uzito na heshima stahiki.
Tukakubaliana kuwa hoja iachwe iendelee ili kuinanga kwa kina na vina.
Wazo hili zuri limeweza kutusaidia kunyumbulisha mada kuanzia sehehmu moja na kutokea kwingine katika mtiririko mwanana.

Nimepokea PM kuwa mada zingine zinakuwa ni endelevu kiasi cha kufanya matukio moto moto yasifikiwe kwa urahisi.
Ninaelezwa kuwa linapotekea jambo utamu wa kulijadili ni pale likiwa la joto.
Aidha ili kuwa na vionjo na kumgusa kila msomaji kwa namna tofauti ni vema tukaangalia muundo wa duru za siasa ili kutoingilia na kuvuruga mtiririko wa mada na wakati huo huo kutoacha masuala moto hadi yapoteze ladha yake.

Nakubaliana na maswala yote mawili kwa dhati kabisa. Nimefikiria, ili kuweza kuleta uwiano mzuri na kuhakikisha kila mmoja anapata alichokusudia kwa minajili ya kwenda pamoja kuna umuhimu wa kuliangalia suala hili kwa mtazamo mpya.
Nimeliangalia kwa mtazamo wangu na napenda niwasilishe nilichofikiri ili nipate michango yenu kwa nia njema ya kuboresha.

1. Tuwe na duru za siasa kama ilivyo kwa madhumuni ya kujadili mada muhimu na endelevu kama ilivyo sasa.
2. Tuwe na duru za siasa (matukio) kwa maana ya kujadili kile kinachojiri kwa wakati fulani na kwa mjadala mfupi tu unless mjadala huo utarejewa kutokana na kujirudia kwa tukio.

Kama wazo hili litaafikiwa na wadau basi tutafungua duru za siasa matukio na kuendelea na duru za siasa mada endelevu.
Vinginevyo, wadau nawapa ukumbi ili niweze kupata maoni yenu ni jinsi gani twaweza kusonga mbele kwa ari na kasi ya JF. Lengo hasa ni kurudisha JF kama sehemu huru ya maoni 'opinion place'

Nawaalika wote na kwvile sitaweza kuwa tag wote niwaalike wote kwa uchache akina Jasusi, Jokakuu, Iza, Pasco, Ritz, Ben Saanane,JouneGwalu, Nyunyu, Mag3,kaa la moto, Nguvulisonzo,Zakumi, Mwakalinga,Mzee Mwanakijiji,lulu mnango, Elizabeth Donminic, BAK, fyddell na mwingine ambaye simkutaja na tunayethamini ushiriki wake

Wadau ukumbi wa maoni sasa ni wenu

Nguruvi3.
 
Mkandara,nakubaliana kabisa na wewe,kuwa hata Obama ni bepari,na kwamba hayo ambayo tunayaona ama wanayaona kuwa yataleta picha mbaya lakini ni ya kisheria.Kwa upande mwingine,kuna mabepari wazuri na wabaya depending on your position.Kuna mabepari wanaokubaliana kuwa walipe kodi zaidi ama sawa na watumishi wao ie secretary.Mfano ni Warren Buffet ambaye pamoja na kwamba ni mmoja wa matajiri wakubwa duniani,bado anaona si fair kulipa kodi ndogo zaidi ya secretary wake,licha ya kwamba si uvunjifu wa sheria,bali tu ni reasoning ya kibepari.Na ndo maana nikasema wengine wanaweza wasielewe inakuwaje hizi practices ni za kisheria?Kiukweli kuoutsource jobs ni part of free market,lakini consequences zake ni sawa tu na kuhujumu uchumi,lakini ni halali chini ya ubepari,so issue inapelekwa kwa wananchi ambao ndiyo wapiga kura,which that's "democracy"...Lakini endapo vitatungiwa sheria kali vitendo kama hivyo,wanadai kuwa ni udikteta kupingana na free market na democrasia na unaitwa msoshalisti na anti west.

Mkuu mimi nipingane na ubepari nina uwezo huo?mimi na analyse tu,that's it,na kutoa mapendekezo,lakini asilani sina uwezo wa kupingana na haya mambo ambayo ni kama "forces of world"

Mfumo wa ubepari umeshatake over and there is nothing to do zadi ya kujaribu kuya cover yale "mapungufu" yake.
Mimi nadhani watu wengi sana huchanganya Uhafidhina na Ubepari kuwa ni kitu kimoja badala ya Ubepari kama mfumo wa wananchi kumiliki njia za uchumi na sio mtazamo wa uhafidhina unaoweka utajiri kuwa ni haki ya mwananchi kama yalivyo maisha bora. Na zaidi ya hapo watu huchanganya pia ulafi na tamaa za watu kama ndio ubepari wakati havihusiani, hata Mjamaa anaweza kuwa na tamaa na ulafi wa madaraka badala ya mali na hivyo kuwa kitu kile kile mwisho wa siku..

Sheria ya kulipa kodi ni mfumo wa Kibepari haupo katika Ujamaa. Kama unakumbuka wakati wa Nyerere hatukulipa kodi isipokuwa uzalishaji, usambazaji na mauzo ulifanywa na vyombo vya serikali vyenyewe. Na ndio maana wakati wa Nyerere serikali ilikusanya fedha nyingi zaidi wakati wake kwa mauzo kuliko wakati wote wa Ubepari tunapotegemea kodi za wananchi. Hivyo, kuna tofauti za kimfumo kati ya Ubepari na Ujamaa na huwezi kutumia tofauti za malipo ya kodi ktk Ujamaa maana hakuna kodi ila mchango wako mzima ndio unahesabika ili kugawanya kwa wananchi wote.

Hivyo swala la Warren Buffet, ni la kimtazamo ndani ya Ubepari wa wahafidhina, hivyo hata huyo Secretary wake ni bepari lakini yeye liberali anataka matajiri walipe kodi zaidi ya wao.(Binafsi sikubaliani na ulipishaji kodi zaidi Matajiri).. Again nitasema kwamba Kuwa Liberal haina maana sio Ubepari ama wanapingana na Ubepari, bali wanapingana na imani ilitangulia kupatikana kwa Utaifa wao iwe kuhusu mila na destiuri za wazawa na Uhafidhina lakini haipotezi kabisa maana ya mfumo wa biashara unaowapa wananchi haki ya kumiliki mali na sio serikali.

Hivyo hapa naweza sema pengine wewe hukubaliani na Uhafidhina lakini haina maana kabisa inahusiana na Ubepari, wewe ni mgeni Marekani unachotaka ni Kutambuliwa kama mwenyeji, uchangiwe wewe kuishi kirahisi ndani lakini amini maneno yangu ungekuwa born and raised MUzungu, ungechukia sana Uliberali kama sisi tunavyochukia kuona wazungu wanavyokuja wekeza nchini wanachukua almost everything halafu kuna watu wanaowatetea.
 
Mkuu jmushi1, Na pia kumnyima mtu uhuru, nafasi na fursa si dhambi kwa ujamaa.

Licha ya kwamba umekuwa a bit "vague" kuhusiana na "uhuru,nafasi na fursa",bado siamini mfumo mmoja persee unafaa...ndo maana nikasema we should mix em up,zile tunazoziona zinafaa.
 
Mkuu jmushi1, Na pia kumnyima mtu uhuru, nafasi na fursa si dhambi kwa ujamaa.

Sawa kabisa, japo Utii pasipo Uhuru ni Utumwa, lakini Uhuru pasipo Nidhamu ni Wendawazimu! Ujamaa ni mama wa nidhamu hiyo!
Mungu wetu yu hai, tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!
 
Mkuu jmushi1 n JingalaFalsafa,
Hoja yangu kuu ni kuwa katika mifumo yote sijaona unaoweza kusimama wenyewe.
Ninachosema ni kuwa kwanini tusiwe na kitu chetu kitakachochota mazuri na kuacha mabaya?
 
Mkuu jmushi1 n JingalaFalsafa,
Hoja yangu kuu ni kuwa katika mifumo yote sijaona unaoweza kusimama wenyewe.
Ninachosema ni kuwa kwanini tusiwe na kitu chetu kitakachochota mazuri na kuacha mabaya?

Ndio maana nasema "UBUNIFU HAUJAWAHI KUFIKA MWISHO" Tukae chini, tuingie katika tafakari ya kina, tuumize vichwa na vipasuke! Lakini katika pendekezo langu ni kwamba, katika hiyo tafakari yetu, kusiwe na chochote kutufunga ila MANTIKI, nayo ni UTU! Si HAKI, Dini, Uhuru, Hisia, Mazoea, Mtazamo, Imani, n.k ni Mantiki tu, yaani UTU ndio uwe frame yetu, tuishibishie nyama sasa, za siasa, uchumi na tamaduni!
UTU ndio utuongoze kusema tunataka uchumi wetu uweje, siasa zetu ziweje, na tamaduni zetu pia ziweje, kitu ambacho hakipo! Ubunifu wetu ukikiuka tu UTU, basi tusitarajie kumaliza rushwa, wizi, utumwa, unyonyaji, ukandamizaji, magonjwa, vita, chuki na visasi, matabaka ya ubora wa maisha, na kero za kila aina! TUKITAKA...TUNAWEZA! Nguvu yetu ni Umoja na Kuthubutu! TUAMUE SASA! Ni wewe na mimi sio mwenzetu!
Mungu wetu anaita sasa!
 
Sawa kabisa, japo Utii pasipo Uhuru ni Utumwa, lakini Uhuru pasipo Nidhamu ni Wendawazimu! Ujamaa ni mama wa nidhamu hiyo!
Mungu wetu yu hai, tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!
Utii mpasipo Uhuru ni Utumwa haya maneno ni exaclty hutokea ktk Ujamaa. Watu tuliwatii viongozi wretu pasipo Uhuru na ndioa maana tulilazimishwa kujipanga barabarani na kupiga makofi Nyerere akipita, tulifunga biashara na kazi Nyerere akipita, tulisimama wima bendera ya taifa ikishushwa, tuliogopa askari waliotakiwa kutulinda, Hii nidhamu ndio nasema ni NIDHAMU ya WOGA, ambayo kweli Ujamaa ndiye mama wake. Ukweli haijufichi maana tumeishi ktk maisha hayo ya Kijamaa.
 
Mkuu jmushi1 n JingalaFalsafa,
Hoja yangu kuu ni kuwa katika mifumo yote sijaona unaoweza kusimama wenyewe.
Ninachosema ni kuwa kwanini tusiwe na kitu chetu kitakachochota mazuri na kuacha mabaya?
Nguruvi3, Binafsi yangu naamini kabisa kwamba Ubeari na Ujamaa ni sehemu ya maisha yetu toka zamani. tatizo la mifumo hii ni pale inapowekewa kuwa ni elimu ya Uvumbuzi ambao siku zote hutegemea WATU na MAZINGIRA.

Hakuna elimu ambayo haikuwepo, isipokuwa tunavumbua usiri wa vitu ambavyo hatuwezi kuviona, kuvinusa wla kuvisikia pasipo utafiti wa hali ya juu ktk misingi ile ile ya kukidhi mahitaji yetu. Hivyo kama tutatawaliwa kutakuwepo na mfumo unaolenga kutawala, nakama tunapingana na kutawaliwa tutavumbua mfum unaopingana na kutawaliwa. Vivyo hivyo kwa walio huru wakakosa Uhuru haki, nafasi na fursa sawa baina yao hutafuta njia za kupingana. Kwa maana hiyo UJAMAA na UBEPARI ni miundo ya kiuchumi itakayowezekana tu kulingana na mahitaji ya watu na mazingira yaliyopo. Haya ni maandalizi ya safari ndefu ya kumwezesha mwananchi kujikomboa kiuchumi hivyo itategemea na mahitaji ya WATU na MAZINGIRA yaliyopo maana siwezi kutegemea Mmasai alozaliwa Serengeti, kwa asili mfugaji afikirie zaidi ukulima wa vyakula ama mazao ya kuuza ktk mbuga za Serengeti, isipokuwa fikra zote za mageuzi zitalingana na mahitaji ya mfugaji na mazingira yake dhidi ya utawala unaojaribu kuwazuia fursa hizi walizojaaliwa..

Masai akilazimishwa kulima ataiharibu mbuga ya Serengeti, wanyama watahama na pengine hata kupoteza vipaji walivyojaliwa, hivyo utaanza kuwaona mjini wakibangaiza ulanguzi.. Binafsi I always believe kwamba sisi sote binadamu tumeumbwa kwa vipaji tofauti na ktk vijapi hivyo ndipo elimu dunia ilipozindukia. Na ni katika vipaji hivi ndipo mataifa mengine hujifunza na kuipata elimu ambayo inaweza kuendelezwa kisayansi zaidi na zaidi pasipo uwa na mwisho. Kwa kila tunachovumbua ni muendelezo wa kitu kilichokuwepo tangu zamani.

Naamini wazungu walikuja tuchukua sisi Utumwa kwa sababu tulikuwa wajuzi wa kilimo na ndio maana ni WABANTU pekee waliochukuliwa utumwani toka Afrika tukiwaacha mateka wa vita. Utumwa ulikuwepo dunia nzima na ilikuwa economic system ya wakati ule, Wayahudi walichukuliwa utumwa kwa vipaji vyao ktk ujenzi, Wahindi ktk ufuaji vyuma na kadhalika. Kwa hiyo mazingira yao ndio yalisababisha njia gani ya uchumi itumike ktk kuboresha maisha yao kamwe haikutokana na kuwepo kwa mfumo wa utumwa, Ubepari ama Ujamaa.

Kwa maana hii nachoweza kusema ni kwamba hakuna mbadala wa njia ya kiuchumi, sii Utumwa, Ubepari wala Ujamaa maana hizi ni njia tu na zilikuwepo hata kabla ya waandishi wa falsafa hizi isipokuwa walionekana magwiji tu kutokana na kwamba itikadi hizi zilipingana na mazingira walokuwepo na zikafanya kazi. Leo hii maadam Tanzania tumekwama ktk uchumi wa Ukoloni mamboleo, Uchumi unaopelekea sisi kuwategemea wawekezaji toka nje ambao sii watumwa bali mabwana zetu. Sii wajuzi bali wenye mitaji, tukitegemea elimu zao ambazo hazihusiani kabisa na mahitaji yetu ama mazingira tulokuwepo isipokuwa rasilimali iliyopo, hapa ndipo tunapo poteza muda mwingi sana kujadili.

Tunachokihitaji ni mfumo unaolingana na sisi wenyewe (Maskini na Wajinga) wenye vipaji ktk Ukulima, Uvuvi na Ufugaji hapa ndipo tulipotakiwa kuanzia na ndivyo Mh. Nyerere aliweka vipaumbele. Kwa wale wote wanaopingana na Nyerere ktk siasa zake za UCHUMI ni watu wasiopenda kutazama vitu kwa undani zaidi na marefu ya viganja vyao, lakini Nyerere was RIGHT on the Money! kupambana na umaskini, ujinga na maradhi kwa kutumia vipaji tulivyokuwa navyo kama hatua za awali za kumkomboa Mtanzania ambaye hakuwa na elimu wala mtaji.

Tatizo la Ujamaa wetu lilikuwa tu pale tulichukua chembe chembe za mfumo wa Warussia na Wachina kuondoa uhuru wa wananchi na kuwajenga nidhamu ya woga ambayo hadi leo ndio kikwazo kikubwa cha Mtanzania. na nawahakikishieni hatutaweza kwenda mbele hata siku moja kwa nidhamu ya woga hasa kwa kutegemea wananchi waliokuwa maskini na wajinga hata kama mtawapa kiasi gani cha MTAJI na RASILIMALI. Utajirisho wa mtu maskini mwenye kipaji cha kilimo, uvuvi na ufugaji kinatakiwa kutazama work force iliyopo wakati huo huo tukipambana na UJINGA kwa nguvu zote ili kesho tuweze kuwekeza wenyewe..Na ndio maana napingana na mfumo wa ELIMU na AFYA uliopo kwa sababu unaondoa Ulazima (compasory) wa vita hii na kuifanya elimu na afya kuwa privilege. Biashara imechukua nafasi ya Kilimo, uvuvi na ufugaji wakati hatuna elimu wala mtaji wa viwanda..Kwa kudharau priorities hizi, hatutatoka iwe kwa kutumia Ubepari ama Ujamaa, tuwe na mafuta au Uranium - HATUTOKI ng'oo!..
 
Wakuu,

Nimekuwa nikiufuatilia mjadala huu kwa muda mrefu na ama kwa hakika nimeelimika mno kwa shule nzito zinazomwagwa humu...big up kwenu nyote!

Nashawisahika kukubaliana na Jingalafalsafa kuhusiana na mfumo unaotufaa hapa kwetu; Bahati mbaya sisi kama binadamu tumejikuta tumefungwa katika system ambayo ni 2-dimension. Katika system hii tunalazimishwa kuchagua kati ya pande mbili pekee;

-Ama rangi Nyeusi au Nyeupe
-Ama Ujamaa au Ubepari
-Ama Mrengo wa Kulia Au kushoto Na kadhalika....

Huku kila upande ukitumia nguvu nyingi sana kuhubiri mazuri ya upande wake na maovu ya upande mwingine. Wakati wa ujamaa tulihubiriwa maovu ya ubepari na ujamaa ulipoanguka na ubepari kushika kasi tumehubiriwa maovu ya ujamaa. Sasa ubepari nao umetikiswa kutokana na uchumi na hii inatupa funzo kuwa kumbe hakuna mfumo mmoja ambao ni fool proof.

Wakati sasa umefika kwa sisi kufunguka na kutoka kwenye mfumo huu wa 2-dimension na kuingia katika 3-dimension au zaidi...Tusifungwe na haya maneno UJAMAA & UBEPARI bali tuanze upya na mawazo mapya.
 
Mkuu jmushi1 n JingalaFalsafa,
Hoja yangu kuu ni kuwa katika mifumo yote sijaona unaoweza kusimama wenyewe.
Ninachosema ni kuwa kwanini tusiwe na kitu chetu kitakachochota mazuri na kuacha mabaya?
Tuko ukurasa mmoja kwenye hilo.Nadhani nilitumia neno "mix em up".Lakini linahitaji mkakati haswa na kupasua kichwa kama alivyosema jingalafalsafa.Na pia ili tufanikiwe,ni lazima tupate watu wenye nia ya dhati kabisa ya kulitumikia Taifa.Kuna elements za kuwaburuza wananchi ambazo zipo kwenye mfumo wa kijamaa na kisoshalisti.Where as kwenye ubepari,kikubwa ni utapeli wa mawazo na kutumia uhuru ukiwemo wa ku misslead wananchi.

Upande wa ujamaa,unaweka more emphasis on state ownership of major means of production,tatizo ni kwamba,head of state ana madaraka makubwa kiasi kwamba ni kama anaiown nchi.Hilo ni tatizo...

Kwa upande wa ubepari,major means of production ni privately owned,na empahis ni kuhakikisha kuwa serikali haina mkono kwenye hizo means.Lakini again ukiangalia,hayo makampuni private ndo huwa yana dictate direction ya nchi na kuinfluence maamuzi ya state/nation.Kwahiyo again unakuta ni kama nao ndo wanaiown nchi.Somewhere in btn,there should be a balance,and that's just a start.Tatizo ni kwamba kuna interests ambazo zinalindwa by anymeans na wanaonufaika ambao tayari ni very powerfull.

Tatizo lilojitokeza la dalili za ukatili kwenye uongozi wa kijamaa na kisoshalisti,ni kwasababu vita hivi viligeuka vikawa ni kama vita vya kiimani.Ndo maana kwa wasoshalisti na wacommunisti walihakikisha wanaimpose hizo leadership styles ambazo zina constitute brutality...where as wenzetu pia nao walihakikisha ukomunisti haupati upenyo,na ndiyo maana hata FBI iliazishwa,na wale wenye idea hizo walikuwa prosecuted kama materrorist ama maadui wa taifa.Katika mazingira kama hayo,kuzienforce hizo ideas kwenye jamii husika inaweza kufikia mbali na kuisupress jamii husika ili tu kuweza kuimpose ideas kama jinsi walivyofanya miaka ya nyuma wakati wa kuspread dini kulikofanyika,kuhakikisha kwamba imani moja inakuwa enforced ama kuwa imposed upon nk
 
Tuko ukurasa mmoja kwenye hilo.Nadhani nilitumia neno "mix em up".Lakini linahitaji mkakati haswa na kupasua kichwa kama alivyosema jingalafalsafa.Na pia ili tufanikiwe,ni lazima tupate watu wenye nia ya dhati kabisa ya kulitumikia Taifa.Kuna elements za kuwaburuza wananchi ambazo zipo kwenye mfumo wa kijamaa na kisoshalisti.Where as kwenye ubepari,kikubwa ni utapeli wa mawazo na kutumia uhuru ukiwemo wa ku misslead wananchi.

Upande wa ujamaa,unaweka more emphasis on state ownership of major means of production,tatizo ni kwamba,head of state ana madaraka makubwa kiasi kwamba ni kama anaiown nchi.Hilo ni tatizo...

Kwa upande wa ubepari,major means of production ni privately owned,na empahis ni kuhakikisha kuwa serikali haina mkono kwenye hizo means.Lakini again ukiangalia,hayo makampuni private ndo huwa yana dictate direction ya nchi na kuinfluence maamuzi ya state/nation.Kwahiyo again unakuta ni kama nao ndo wanaiown nchi.Somewhere in btn,there should be a balance,and that's just a start.Tatizo ni kwamba kuna interests ambazo zinalindwa by anymeans na wanaonufaika ambao tayari ni very powerfull.

Tatizo lilojitokeza la dalili za ukatili kwenye uongozi wa kijamaa na kisoshalisti,ni kwasababu vita hivi viligeuka vikawa ni kama vita vya kiimani.Ndo maana kwa wasoshalisti na wacommunisti walihakikisha wanaimpose hizo leadership styles ambazo zina constitute brutality...where as wenzetu pia nao walihakikisha ukomunisti haupati upenyo,na ndiyo maana hata FBI iliazishwa,na wale wenye idea hizo walikuwa prosecuted kama materrorist ama maadui wa taifa.Katika mazingira kama hayo,kuzienforce hizo ideas kwenye jamii husika inaweza kufikia mbali na kuisupress jamii husika ili tu kuweza kuimpose ideas kama jinsi walivyofanya miaka ya nyuma wakati wa kuspread dini kulikofanyika,kuhakikisha kwamba imani moja inakuwa enforced ama kuwa imposed upon nk
Yote haya tisa, kumi sisi tunatakiwa kutafuta mfumo unatufaa sisi kulingana na mahitaji yetu na katika mazingira yetu. Hii Tanzania pekee ni kubwa kiasi nkwamba wanachokihitaji Arusha na Moshi sio sawa na dar au Mwanza, rasilimali na maliaisili hazifanani hivyo utajiri wake haufanani.

Tunahitaji mfumo unaotazama msingi huu pekee na sii Ujamaa wala Ubepari uloandikwa na intellectuals wa nchi za magharibi kwa sababu hazifungamani na mahitaji wala mazingira yetu..Ni sawa na kujaribu kupanda miti ya Christmas nchini kutafuta kivuli, wataalam watakuja na vitabu vya kila aina na hata kutulazmisha kutumia mbolea lakini haikuhitaji nguvu yote hiyo, tungepanda tu michongoma na ingeleta kivuli bila matatizo wala gharama kubwa. Muarobaini tunao isipokuwa tumekodolea macho madawa ya maabara hata kama yametokana na muarobaini - Fikra hizi ndizo sikubaliani nazo..

Ubepari una elements za ULAFI maana watu wanashiba lakini bado hawatosheki kuhitaji zaidi na zaidi. lakini pia Ujamaa tatizo lake watu wana njaa na serikali kutuweka mduara ktk sinia moja hapo pia hakuna ustaarabu bali ni ULAFI ue ule wa maskini utatumika wakati viongozi wamekaa meza kubwa. Sijui unaiona logic ya hoja zangu ktk hili?.. kama tutaweza kuzuia ULAFI wa watu basi kuna ubora zaidi ktk kulenga kuwashibisha watu kwanza halafu tukaweka vikwazo kwa wale walafi wanaotaka kula zaidi ya kipimo, kuliko kuondoa njaa kwa kugawana kidogo kilichopo ilihali watu hawa hawana elimu wala uwezo wa kuzalisha unachokitaka isipokuwa kwa vipaji nwalivyonavyo wao..Unakumbuka msemo wa mwenye njaa ukimpa samaki au kumfundisha kuvua ina mafao gani!..

Napinga huu mpango wa kugawana Umaskini kwa kumweka mlinzi na mgawaji wa chakula (serikali) kwa sababu serikali ni watu vile vile wenye njaa.. serikali sio machine ama Miungu watu ni wale wale wenye njaa ya utajiri. It all ends up kuwa na Walafi, hizi ni siasa ambazo sisi hatukuwa nazo ktk mila na desturi zetu. Hatukuwa tunaficha chakula wala kuogopa kula na majirani kila mtu akileta mapishi yake. Ujamaa wetu ulijkuwa ziadi ya kupambana na wakooloni bali Udugu wa kijamii..Hii tabia ya kuiga Ujamaa ulichongwa kama kinyago ndio uliotuponza otherwise Ujamaa wa Nyerere ulilenga tu kuondokana na ubeberu (Imperialism), lkn tumejikuta tuna form another imperialist wa ndani kwa ujamaa ule ule na hawa ndio wanaotuongoza leo wengine wana miaka 80 kuingia 90 hawataki kuachia madaraka.

Its very simple, sisi tuna maadui wa ndani na nje..wa ndani tumeisha sema ni Umaskini, Ujinga na Maradhi hili halina ubishi wala mjadala ni lazima tulifanyie kazi kwanza lakini kikwazo kilichopo ni WALAFI ambao miiko na maadili yanatulazimu kuyafuata upya na kila mmoja wetu awe Accountable.. Na maadui wetu wa nje ni Ukoloni mamboleo, na kama nilivyosema hapo nyuma kwamba ni hali ya kiuchumi inaopelekea sisi kuwategemea wawekezaji toka nje ambao sii watumwa wetu bali ni mabwana zetu. Sii wajuzi bali wenye mitaji (capitalist), tukitegemea elimu zao ambazo hazihusiani kabisa na mahitaji ama mazingira yetu isipokuwa ni interest zao ktk rasilimali yetu ndio zinawavuta.

..
 
Mkuu Mkandara hili jambo la kuhusu wawekezaji linanitatiza kidogo.Wamarekani wenyewe walitaka uhuru kwasababu sheria ilikuwa ikiwataka wapeleke mapato mengi in forms of taxes nk,back to the "mother land" yani kwa malkia uingereza.Walipokwa wakipinga,makampuni ya marekani yakawekewa vikwazo.Wakati ule biashara kubwa ikiwa ni chai.

Kampuni ya uingereza ambayo haikuwekewa vikwazo,ilikuwa na mzigo ya chai kwenye bandari ya Boston,wafanyakazi wakamwaga chai yote kwenye maji na ndipo ikaanza ile kauli ya "Taxed enough already" aka tea party...Haya ni baadhi ya matukio tu yaliyo highlight path waliyoichukuwa wamarekani ili kupambana na mwekezaji beberu wa uingereza ambaye aliwacolonise.Baadae wamarekani walipata uhuru baada ya kumwaga damu dhidi ya mwingereza.Na pia mmarekani aliyegombea uhuru ni mwingereza pia aliyehama kutoka uingereza akitafuta uhuru wa kujiamulia mambo na kuwa na mawazo ya tofauti.Lakini cha kushangaza kwasasa,ni kama the same thing is going on,especially dhidi ya Africa,bado tusitegemee eti kuwa wawekezaji wataleta maendeleo kama hawatabanwa.Na hakuna kampuni ya nje ambayo hailinufaishi taifa ilikotoka,ndo ubepari huo,yale mambo ya "mother land" yapo lakini kwa namna ya tofauti.Kwa wenzetu,kampuni hizo hata kama zinakwenda kuwekeza nje,bado zina majukumu kwa motherland kwasababu ndo wenye kuzilinda na kuzipatia ile "superiority" ndo ubepari huo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom