Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #221
Romney aliweka mapesa kwenye mabenki ya nje ya nchi yake, hilo si kosa lakini kama mzalendo hakupaswa kufanya hivyo kwani hapo tu atakuwa amekwepa kodi hata kama ni halali. Pili, democrat wanataka waonyeshe kiasi cha kodi na cha wafanyakazi wake ili wajenge hoja kama kweli yupo na middle class. Na tatu wanataka ijulikane wakati anaua kampuni alipata kiasi gani, alilipa kodi kiasi gani ili waonyeshe jinsi gani dhana yake ya umahiri katika small business na job creation ilivyo na utataMkandara;4415626]Jmushi1, utajiri wa Romney unajulikana wala sio siri isipokuwa wanajua kuna mambo ambayo Romney hawezi kuyaweka wazi ndio maana wanambana ili kuharibu profile yake, lakini hakuvunja sheria isipokuwa yataleta picha mbaya kwa wananchi wapiga kura ujio uchaguzi mkuu. Kama kungekuwa na baya, IRS (Renevue) wasingemwacha hata kidogo isipokuwa lengo ni image yake as a President ikijulikana alikuwa anatengeneza ngapi kwa mwaka akiwa CEO halafu mashirika yale yakafa, watu wakapoteza fedha zao itamweka pabaya ktk uchaguzi
Umenena, hawa wanaotuletea utandawazi n.k. na wanaupinga ujamaa, ukweli ni kuwa wao ni wajamaa. Walichokifanya ni kuchukua element nzuri za ujamaa na kuzichanganya na zile zao. Kwa mfano, chimbuko la social welfare siyo magharibi ni nchi za mashariki ya kati na linahusiana na dini.Labda nimalizie kwa kusema unajua Marekani na Ulaya hawa ni WAJAMAA kuliko hata sisi. na ndio maana utaona Liberal wanashinda kwa matumizi halisi ya neno lenyewe kwa sababu hawa hawajatawaliwa.. Ujamaa wao umetokana na kutukuza traditional zao..wanathamini KAZI kiasi kwamba unemployement rate tu ikipanda inamwangusha kiongozi ktk urais..Priorites zao ziko wazi kabisa, iwe system yenyewe jinsi wanavyosaidiana toka welfare hadi job creation huwezi kulinganisha na sisi.. wakati mwingie husema hawa Mabepari ni wajamaa kuliko sisi maana Just Imagine how much monies Bill Gates anatoa kusaidia nchi maskini ktk maradhi?.. Anatumia billions kuliko bejeti ya nchi zetu ktk huduma ya Afya.. Kina sisi ni michango ya harusi, hata kwenda hospital tu kutembelea wagonjwa tunashindwa ila kwenda kupiga picha za wagonjwa, madaktari walipogoma kuonyesha unyama wa serikali!..What did you do to help the sick ones?.. NOTHING! Ujamaa wetu umetokana na experience ya kukoloniwa na tumeshindwa hata kutetea mila na desturi zetu wenyewe tumebakia kuiga kila kitu kiasi kwamba tunaogopa hadi vivuli vyetu wenyewe..
Walichokifanya ni kuchukua muundo na kuufanya u-fit mazingira yao na hilo wamefanikiwa.
Unemployment ni sehemu nyingine ya kulinda jamii zao. Wanajua kuwa unemployment inaweza kuleta unrest na hivyo jamii ya mabwanyeye kuwa matatani. Wakaweka Employment insurance ili kuhakikisha kuwa jamii inalindwa.
Mfano mwingine ni wa Insurance ziwe za auto, house n.k. Tunajua wazi kuwa makampuni ya insurance ni ya kibepari na kazi yao ni kukamua walaji na watumiaji. Lakini pia serikali imeweka taratibu zinazomlinda mlaji au mtumiaji pindi linapotokea lisilotarajiwa.
Huko mahospitalini sasa wanaweka insurance za watu wao na hilo ndilo tatizo Obama analokabiliana nalo. Nia ni kuhakikisha kuwa huo ubepari katika matibabu hauvuki mipaka ya kuwaumiza watu.
Wamefikia hata ku-regulate wall street ili kuhakikisha kuwa jamii haipati misuko suko kama ile ya mwaka 2006-2008 iliyosababisha mtikisiko wa uchumi duniani.
Katika yote hayo sisi hakuna hata kimoja tunachoweka kumlinda mtu wetu. Tumemeza ubepari na ujamaa kama ulivyo na kuimba ubinafsishaji bila hata kuangalia mazingira yetu. Fikiri auto insurance yako Tanzania inakulinda vipi na linganisha na ya wenzetu. Fikiria health system yetu inakulinda vipi ukilinganisha na wenzetu.
Kwa maneno mengine, tumemeza kila kitu bila kufikiria au kuangalia kama kila tunachomezeshwa kinawiana na jamii yetu. Tumeshindwa kufikiri kwasababu tuna hoja rahisi kuwa ubepari au ujamaa ndiyo mifumo inayopaswa kutuongoza.
Ikifika hapo nakubaliana kabisa na jmushi1 kuwa hivi hakuna uwezekano wa sisi kutengeneza kitu kinachofanana au kuwiana na mazingira yetu na kwa manufaa ya jamii yetu bila kumeza maelekezo tu ya uwekezaji, ubinafsishaji holela,ujamaa n.k!
Najua hoja hapa ni kuwa wakubwa watatumia marungu yao ya WB, IMF kutukwaza. Mimi huwa najiuliza Malaysia wamewezaje kutoka pale tulipokuwa nao na kutuacha? Scandinavia wamewezaje kuwa ni mifumo inayolingana na jamii zao? Wahindi wamewezaje kuchomoka katika mitego ya wakubwa? Kwanini sisi tusifikirie na tubaki tukilalama tu.
Hivi tunawezaje kuwa na kiongozi anayekwenda kuangalia utalii nasi kufikiria namna gani ya kuendeleza tulio nao?