Nguruvi3,
Mkuu wangu turudi nyuma tuachane na dhana maana hapa nakuona unachoongea wewe ni fikra zako. What will happen if.. if nyingi sana badala ya kuzengumzia hali halisi. Nimekupa mfano wa CCM wa kina AbdulWahid umeanza kudai pasingekuwa na amani? Hivi kweli unataka kusema watu wa leo hawana ueleo mzuri zaidi ya wale wa zamani maana nijuavyo watu wa zamani ndio walikuwa ngumi mkononi na swala la demokrasia halikuwepo. Udikteta ndio ulitawala mataifa leo hii Chadema warushiane ngumi kwa sababu Zitto anataka kuwa mwenyekiti?.
Statement kama hizi ndio zinanifanya nijiulize kama kweli chama hiki kina wenyewe, japo sipendi kabisa niamini hivyo. Kwenu wapenda mpira yule Suerez wa Liverpool hakufukuzwa bwawa la maishi kwa sababu timu ile inatazama ushindi, kuchukua Ubingwa na sii kashifa za mwenyekiti ama kocha. Tena wako radhi kumfukuza kocha ikiwa haleti ushindi kuliko kunfukuza mchezaji bora japo utaona mchezaji mmoja sii timu nzima ya wachezaji 11.
CCM wale pale sii walisema watawafukuza magamba watatu? wa,mefanya hivyi? na tulishangilia sana tukisubiri wafukuzwe maana tulijua ndio kifo cha CCM lakini kwa busara zao CCM wakashtuka, wakajiweka sawa kufuta lugha ya Ufisadi na leo wanaendelea kupeta. Ufisadi sasa umekuwa lugha ya kila mtu kwa kila chama, kila kiongozi na kila dhulma ya jasho la watu. Imekuwa jambo la kawaida yaani sasa hakuna chama wala mtu msafi. Wanatumia mwanya huu kuonyesha kuwa hata sisi sio wasafi.
Kifupi tu, naomba majibu ya swali langu la kwanza.. Kila shilingi ina pande mbili. Tumeyajua makosa ya kina Zitto na Kitila sawa lakini je yale waloyadai kuwepo ndani ya chama mbona hayana majibu? hadi leo sijamsikia kiongozi hata mmoja akielezea swala moja baada ya jingine.
Ikiwa madai yao ni ya kweli basi hata mimi ningeunga mkono mageuzi afanyike japo si kwa kiti cha mwenyekiti pekee bali mfumo mzima wa UONGOZI iwe katiba ama sheria. na kibaya zaidi umnaendeleza madai ya kuheshimu katiba...jamani katiba ya makaburu ilidumisha Aparthied, ina maana walopinga mfumo huu baina yao utawaita Wahaini na Wasaliti kiasi kwamba hata wewe ulokaa pembeni hutakiwi kuwaunga mkono? Pia zamani nchi zote za magharibi - UTUMWA ulikuwa ruksa kikatiba na wakatokea watu kama kina Zitto ndani ya vyanma vyao walopingana na katiba hiyo na wakafanya mageuzi makubwa. Maswala ya haki za wanawake na kadhalika yote haya yameanza within vyama kisha yakaenda hatua nyingine. Kutambua garamu ama makosa siku zote hutupa hekima ya kutorudia makosa. Hekima hutokana na uvumilivu wa maswala kama haya ukayaona nje ya box. Naweza sema kwamba mageuzi hayakutoa roho za watu wengi kama ilivyokuwa sheria hizo zikitumika iwe Apartheid ama Utumwa.
Mkuu namalizia na kuuliza tena zile sababu waloorodhesha kina Mkumbo hadi kufikia maamuzi ya mageuzi ni ya UONGO?.. Je Ukweli ni upi naomba maelezo kwa mtu yeyote anayefahamu undani wa kile kinachofanyika huko. Na ikiwa madai hayo ya waraka ni kweli tupu, wewe unaridhika na mfumo huo wa uongozi kiasi kwamba bora tufumike kombe (Zitto) wana haramu wapite(wanachama)
Wanajamvi,
Kimweri ametoa angalizo zuri sana.
Kasema wapo wanaoamini lolote kutoka kwa Lissu au Mnyika hata kama halina maana
Mkandara#169 kasema wengi wameifanya siasa kama Man U na Asenali.
Nami naongezea kuwa wapo wanaoamini fulani ni kiongozi mzuri sana hata kama hawana sababu za kutosheleza.
Hadi hapo tutakapoondoka katika mitazamo hiyo, tuna safari ndefu ya kuikwamua nchi hii.
Mkandara kwanza uniwie radhi kwa 'if nyingi' mkuu .
Nimeandika kwa fikra zangu nikiamini kile wanachosema ' kila mmoja yupo entitled to his/her own opinion'
Nimezungumzia mengi kwa uhalisia na wala si hisia.
Uhalisi niliouzungumzia miongoni mwa mengi ni haya
1. Kwamba Zitto na Kitila wameandika waraka wa siri -Uhalisia
2. Katika waraka huo wamemshirikisha Mwigamba na wengine-uhalisia
3. Ndani ya waraka wametoa hoja zao na nimezianisha katika bandiko#14- uhalisia
4. Kwamba waraka ulikuwa na kejeli, matusi na mipasho-uhalisia
5.KwambaKitila amekiri kushiriki kuandika waraka-uhalisia
6. Kwamba Zitto hajibu hoja zitokanazo anatembelea vituo vya redio kujisafisha-uhalisia
7. Kwamba Zitto ametumia hoja ya ukaguzi kwa manufaa yake-Uhalisia
8. Ametumia njia alizotumia kupokea milioni 10 za Barrick-uhalisia
9. Waraka umemshauri Zitto afanye mapenzi kwa siri na nepotism-uhalisia
10. Na waraka umelaani mapenzi kwa viongozi wa CDM-uhalisia
11. Bandiko#2 nikaweka vifupisho vya lugha zilizotumika-uhalisia
12. Nimeonyesha upotoshaji wa data-uhalisia
n.k.
Madai ya akina Zitto na Kitila tumeyaona, bandiko#14.
Kinachotukwamisha tusiyajadili hayo 10 ni baadhi yetu kuamini kuwa waraka ulikuwa na usahihi na ni halali.
Katika bandiko#10,11,12, nimeweka kwa mtazamo wangu makosa ya waraka.
Hapa sina maana makosa ya maoni ya waraka bali makosa ya waraka kama ulivyoandikwa na wasomi waliobobea, pili njia zilizotumika katika kufikisha maoni kwa wanademokrasia watarajiwa, upungufu wa hoja, tatu njia walizopaswa kutumia kama viongozi, upotoshaji uliopo ndani ya waraka na mwisho usaliti wa waandikaji kama viongozi
Leo tupo bandiko karibu la 200 hakuna hata mmoja, nasema hata mmoja aliyejibu makosa niliyoyaanisha na kunionyesha kuwa ima nimezua, sikutenda haki, sikuwaelewa au nimewabambikizia.
Kinachosemwa ni kuwa waraka ni halali na tatizo ni ueneykiti wa Zitto.
Hilo ndilo jibu na wala si yale yatokanayo na tuhuma alizopewa au zilizo katika waraka vyote viwili vikifanana sana.
Labda mtu auchukue waraka au aje na maoni ya kuonyesha kwanini akina Zitto walikuwa sahihi kuandika waraka.
Kuhusu historia za za vyama kama TAA na TANU
Mkandara na
Zakumi wanajenga hoja za kuvumiliana kwa kutumia historia za vyama hivyo wakiwataja akina Abdul Sykes na mapinduzi yao.
Wanatusaidia kujenga hoja kuwa TAA ilianza ikafuatiwa na TANU. Wapo wanachama ambao hawakuridhika na mwenendo wa TANU wakajimega na kuunda AMNUT.
Wengine wakaona sera si sahihi wakajiengua na kuunda UTP.
Hawa waifanya mambo yao hadharani baada ya kuyasema na kuona hawasikilizwi.
Hakuna sababu za kusema hawakuwa sahihi kwa mujibu wao, muhimu ni kutambua uhuru waliokuwa nao wa kuzungumza na hata kujiondoa katika vyama.
Kitila na Zitto ni vongozi wa ngazi za juu sana. Niltarajia wangekuwa mfano mzuri wa demokrasia ya karne ya 21 kwa kuwa wawazi pale wasiporidhika. Hawakuchukua mkondo huo, walichokifanya ni espionage na kutumia nafasi zao kutaka kuleta mageuzi ya kitu walichokisimamia kukiandaa na kukishauri kama naibu katibu mkuu na mshauri wa chama.
Sijui historia mnayoizungumzia inasemaje kuhusu hilo.
Hata kama wangefuata nyao za Abdul Sykes bado walipaswa kuvunja milango Kinondoni na kuwaondoa kama historia inavyosema. Hawakufanya hivyo, walichokifanya ni uchochezi ndani ya mitandao huku wakikaa katika vikao na kupanga yale wasiokubaliana nayo lakini walishiriki kuyaandaa. Sijui kama si unafiki na ni kitu gani kwa lugha ya kiswahili(Bandiko# 92)
Tukubaliane tu kuwa kuna matatizo na nashangaa kwanini watu waone hili wakati wengine tulishaliongelea miaka 2 iliyopita huku tukitahadharisha mtafaruku mkubwa ndani ya miezi 18 kama uongozi hautachukua hatua za makusudi za kujenga nidhamu ndani ya uongozi wenyewe na si kwa watu mmoja mmoja.
Tusione haya au kuwa na mapenzi yasiyo na sababu. Tuweni wakweli ili tusizidhulumu nafasi zetu kwa mapenzi tu.
Ukweli usemwe hata kama unauma. Ukweli utatuweka huru.