Ebu tujitengezee wenyewe miaka 30 ya bongoflava ya JF. Tujikumbushie mangoma, mastori na moments

Kati ya wasanom
Kati ya wasanii waliopaswa kuwa na mpunga mrefu Tanzania kama tungekuwa tunathamini sanaa na jasho la mtu ni pamoja na Juma Nature.
 
Kati ya wasanom

Kati ya wasanii waliopaswa kuwa na mpunga mrefu Tanzania kama tungekuwa tunathamini sanaa na jasho la mtu ni pamoja na Juma Nature.
Mimi sijawai elewa ngoma za nature Mimi nakubali nature alikua na chorus Kali

Hit song

Hakuna kulala
Sonia
SITAKI demu
Inaniuma sana
Nini chanzo

Nyingine Huwa sizielewagiii
 
Asante! Kwa Upande wangu, Miaka 30 ya BongoFlava Inaanzia katika kumsikia SALEH JABIR na mautundu yake yakubadilisha nyimbo za mamtoni kwa kiswahili katika midundo ileile. Nilikua bwa mdogo sana na nilitokea kuipenda style ya Rap maana kabla ya hapo nilikua mpenzi wa nyimbo za taarabu za kina Issa Matona na Bi Malika Taarabu.

Baadae nikakutana na Album ya kundi lakuitwa ZE KILA KITU, hawa nao ni kama Saleh Jabir alivyokua anafanya ila Tofauti yao wao walikua wanabadilisha nyimbo za Mamtoni tofautitofauti kuanzia Blues hadi Ragamuffing, mfano Careless whisper wao waliimba MZIKI KUACHA NOMA, na Murder She wrote wao waliuita MARA SHINGO, japo katika wadau wengi wa mziki wa zamani ninaokutana nao hawawakumbuki hawa wanamuziki na sijui walikua kina nani?

Nyimbo zao mpaka kesho nazikumbuka nimeshindwa tuu kuzipata tofauti na za saleh Jabir amabazo nimefanikiwa kuwa nazo. 2 Proud nilikuja kumsikia baadae pamoja na kundi la GWM, chakufurahisha hawa wote nimewasikia nikiwa sijafika hata kupafaham Dar.

aliofuata baada ya hapo ni kina Balozi, SOS B, Mack D na Kwanza Unit. nikaanza kuvutia na mimin kuandika verse za rap baada ya kumsikia Caz T maana alikua anarapu kikawaida na akitumia maneno rahisi kiasi nikaona huyu hata mimi naweza kumfunika.

Makundi ya Muziki niliyowahi kumiliki Album zao, ni kama NGONI TRIBE, SWAHILI BY NATURE, HBC, GANGWE MOB, GWM, BWV.

mpaka miaka ya 2000 nilikua tayari na mimi ni mdau wa mziki wa Bongo flava maana nilikua nimemeza nyimbo nyingi na nilikua nawaburudisha wenzangu kiasi tukawa tunashindana nani anaweza kukariri verse za nyimbo mpya kwa haraka, ambapo hadi inafika mwaka 2005 hakuna wimbo wa bongo flava uliokua heat ambao sijaukariri.

Na kwa uzi huu niwaombe wadau kwa yeyote mwenye nyimbo hizi au anaweza kunisaidia kuzipata tafadhari, nitachangia chochote.
1- "MPENZI UMENIKIMBIA WAKATI NAUMWA, USIKU WA MANANE, ULIZANI MI NTAKUFA, ILI MILELE TUSIONANE, SASA YAMEKUKUTA, UNAOMBA TURUDIANE, SINA MUDA MCHAFU, MI NI BORA NIWE MJANE". Kundi liliitwa Wanyamwezi Family.

2- "AKIJA KWANGU ATADATA" By Lady Luu

3- "WANGU MAHABUBA, WANGU WA NDANI KIDANI, NAKULA NA WEWE SAHANI" By Keegan

4- "KILA MMOJA MIKONO HEWANI, NATAKA NISIKIE MKISEMA, OOH YEEAH" By John Mjema ft Solothang na Jose Mtambo

Na 5- Ni nyimbo za Hao wakuitwa ZE KILA KITU, kama vile " MZIKI MIMI KUACHA NOMA, JAPOKUA NAKUPENDA WEWE, MZIKI KWANZA PENZI BAADAE, WAKATI WEWE UPO MBALI NAMI, MZIKI NDIO MPENZI WANGU" huu waliigiliza Careless Whisper. Pia kuna ue una maneno "NIMEKUSHINDA KWA KARATA, YAKUBIDI UENDE KWA MGANGA HUYO"

Asanteni sana.!!
 
Wasanii wa zamani wengine miyeyusho.
Juma Nature yupo kwenye peak kaja pale Fire saa mbili usiku katukuta tunakula supu ya pweza kaliungisha naye anagonga soup ya pweza kisha anatuuliza kuberi na tambuu atapata wapi pale Fire.
Pale sheli Morogoro road kwenye fremu pembeni ya Kituo Cha Mwendokasi Cha Fire..🤣🤣
Nilimdharau.
Imagine Diamond sasa hivi anafanya hivyo?!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…