Unakumbuuka yamenikuta ya akina gwm na sugu😁Miaka nasikiliza huu music sisi wengine tulianza na michano ya Saleh Jabir ambaye yeye aliziimba nyimbo za miaka hiyo kwa kiswahili kama Ice ice baby n.k
Then Diplomatz, Gangster With Matatizo. GWM, kulikuwa na Weusi Wagumu Asilia, 2 Proud na nyimbo za Ni Mimi, Nachekelea kwenye Chezo n.k
Wakati huo alikuwepo Jos Mtambo na wimbo Kithaa thaa, Solo Thang alikuwa na wimbo wake mmoja umenitoka... Miaka ya 90s hiyo kama sikosei 94 au 95...
Hard Blasters walikuja kuwika baadaye kidogo late 90s nadhani kama sikosei 98 au 99... Kipindi hicho nami nlikuwa natunga mistari sikuwahi enda studio. Ila nlikuwa mdau mzuri wa Hip Pop... So akina Dully hawakuwa sehemu ya watu naowasikiliza nliona wanaimba nyimbo nyepesi za mabitozi.
Music wa nje miaka hiyo tunawasikiliza akina Nas, Mase, Puffy Daddy, 2 Pac, Naughty By Nature, Coolio. LL. Cool Jay, Notorious BIG etc tunapozea na akina Keith Sweet, R. Kelly, Boys 2 Men, etc
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥Asante! Kwa Upande wangu, Miaka 30 ya BongoFlava Inaanzia katika kumsikia SALEH JABIR na mautundu yake yakubadilisha nyimbo za mamtoni kwa kiswahili katika midundo ileile. Nilikua bwa mdogo sana na nilitokea kuipenda style ya Rap maana kabla ya hapo nilikua mpenzi wa nyimbo za taarabu za kina Issa Matona na Bi Malika Taarabu.
Baadae nikakutana na Album ya kundi lakuitwa ZE KILA KITU, hawa nao ni kama Saleh Jabir alivyokua anafanya ila Tofauti yao wao walikua wanabadilisha nyimbo za Mamtoni tofautitofauti kuanzia Blues hadi Ragamuffing, mfano Careless whisper wao waliimba MZIKI KUACHA NOMA, na Murder She wrote wao waliuita MARA SHINGO, japo katika wadau wengi wa mziki wa zamani ninaokutana nao hawawakumbuki hawa wanamuziki na sijui walikua kina nani?
Nyimbo zao mpaka kesho nazikumbuka nimeshindwa tuu kuzipata tofauti na za saleh Jabir amabazo nimefanikiwa kuwa nazo. 2 Proud nilikuja kumsikia baadae pamoja na kundi la GWM, chakufurahisha hawa wote nimewasikia nikiwa sijafika hata kupafaham Dar.
aliofuata baada ya hapo ni kina Balozi, SOS B, Mack D na Kwanza Unit. nikaanza kuvutia na mimin kuandika verse za rap baada ya kumsikia Caz T maana alikua anarapu kikawaida na akitumia maneno rahisi kiasi nikaona huyu hata mimi naweza kumfunika.
Makundi ya Muziki niliyowahi kumiliki Album zao, ni kama NGONI TRIBE, SWAHILI BY NATURE, HBC, GANGWE MOB, GWM, BWV.
mpaka miaka ya 2000 nilikua tayari na mimi ni mdau wa mziki wa Bongo flava maana nilikua nimemeza nyimbo nyingi na nilikua nawaburudisha wenzangu kiasi tukawa tunashindana nani anaweza kukariri verse za nyimbo mpya kwa haraka, ambapo hadi inafika mwaka 2005 hakuna wimbo wa bongo flava uliokua heat ambao sijaukariri.
Na kwa uzi huu niwaombe wadau kwa yeyote mwenye nyimbo hizi au anaweza kunisaidia kuzipata tafadhari, nitachangia chochote.
1- "MPENZI UMENIKIMBIA WAKATI NAUMWA, USIKU WA MANANE, ULIZANI MI NTAKUFA, ILI MILELE TUSIONANE, SASA YAMEKUKUTA, UNAOMBA TURUDIANE, SINA MUDA MCHAFU, MI NI BORA NIWE MJANE". Kundi liliitwa Wanyamwezi Family.
2- "AKIJA KWANGU ATADATA" By Lady Luu
3- "WANGU MAHABUBA, WANGU WA NDANI KIDANI, NAKULA NA WEWE SAHANI" By Keegan
4- "KILA MMOJA MIKONO HEWANI, NATAKA NISIKIE MKISEMA, OOH YEEAH" By John Mjema ft Solothang na Jose Mtambo
Na 5- Ni nyimbo za Hao wakuitwa ZE KILA KITU, kama vile " MZIKI MIMI KUACHA NOMA, JAPOKUA NAKUPENDA WEWE, MZIKI KWANZA PENZI BAADAE, WAKATI WEWE UPO MBALI NAMI, MZIKI NDIO MPENZI WANGU" huu waliigiliza Careless Whisper. Pia kuna ue una maneno "NIMEKUSHINDA KWA KARATA, YAKUBIDI UENDE KWA MGANGA HUYO"
Asanteni sana.!!
P funk alkkuta sound ikiwa disorganized,P-funk pia amepiga sana mabeat mazuri wazee kuanzia mzee wa busara , Nini mnataka mazee?? Hili la Nini mnataka nakumbuka lilikua linatumika kwenye kipindi flani star tv.
Nature nae mzee wa story nyingi kumbe ndo anaimba ivyo huku vioja vingi ndani yake.
Kuna wachuja nafaka 😀 halafu baadae likatokea beef la tmk halisi na wanaume family ikapigwa battle Kali ambalo tmk halisi walishinda.
Ngoma za wagosi wakaya traffic huyo, bush part na dknob elimu mtaani, Bado madojo na domo kaya dingi.
Sitaacha ugoro ndio unanipa stimu nikiwa na mamake adriz de mbusiiKwa hiyo unamshauri aache kupiga ugoro!?
Sio Mzee ni chorus tuu wimbo unaitwa Kikao cha dharuraHuo wa kuomba kura unaitwa NDIO MZEE baadae akatoa mwingine unaitwa SIO MZEEE.
Alioimba na Jide unaitwa NIAMINI
Wamejitahidi ila maandalizi yalikuwa 0 aiseeWabongo shida ubunifu zero na utulivu hakuna kabisa......hii ya miaka 30 imekuja baada ya kuona Jigga kule NY anaadhimisha miaka 30 ya album yake reasonable doubt basi nao wakacopy mpaka tarehe aisee.
Kama yaliyo mtokea mheshimiwa pale mcity 😆🔥🔥🔥 wananchi walikataa kabisa siku hio😁
Ile kitu ilikuwa mchongo mchongo na kutafuta sifa kwa madeeeWamejitahidi ila maandalizi yalikuwa 0 aisee
Lingekuwa na mpangilio aisee ni bonge moja la concert
Hii concert naona kama iliibuka tuuIle kitu ilikuwa mchongo mchongo na kutafuta sifa kwa madeee
Unakumbuuka yamenikuta ya akina gwm na sugu😁
FAGIO LA CHUMA-FAGIO LA CHUMATunapojadili ngoma kali za muda wote za BONGO FLEVA. Tusiache kujadili Mikono (Producers) waliozipika ngoma hizo;
MIKA ALEKSANTERI MWAMBA (MIKA MWAMBA). FM. Studios. Alipiga hii mipini.
Tamara + ni wewe - Hard Mad
Eno maiki - Ziggy Dee (Uganda)
Nakupenda Mpenzi - Dudu Baya
get down - Prezo ft Naziz (Kenya)
Twenzetu - Chege
Baby Gal + wange - Mad Ice
Maria Salome - Saida Karoli
Kamanda + barua - Daz Nundaz
wanoknok + Taswira + dingi - Mandojo na domokaya
Picco - Kikongwe
Kwenye Chati - Balozi
Mtoto wa geti kali - Inspector Haroun
Elimu mtaani + sauti ya gharama - D knob
Mkiwa - K sal ft Ferooz
Salome + Julieta + Hi - Dully Sykes
Raha tu - AY
Mambo vipi - Mchizi Mox
Solid Ground Family - Bush party