Miaka nasikiliza huu music sisi wengine tulianza na michano ya Saleh Jabir ambaye yeye aliziimba nyimbo za miaka hiyo kwa kiswahili kama Ice ice baby n.k
Then Diplomatz, Gangster With Matatizo. GWM, kulikuwa na Weusi Wagumu Asilia, 2 Proud na nyimbo za Ni Mimi, Nachekelea kwenye Chezo n.k
Wakati huo alikuwepo Jos Mtambo na wimbo Kithaa thaa, Solo Thang alikuwa na wimbo wake mmoja umenitoka... Miaka ya 90s hiyo kama sikosei 94 au 95...
Hard Blasters walikuja kuwika baadaye kidogo late 90s nadhani kama sikosei 98 au 99... Kipindi hicho nami nlikuwa natunga mistari sikuwahi enda studio. Ila nlikuwa mdau mzuri wa Hip Pop... So akina Dully hawakuwa sehemu ya watu naowasikiliza nliona wanaimba nyimbo nyepesi za mabitozi.
Music wa nje miaka hiyo tunawasikiliza akina Nas, Mase, Puffy Daddy, 2 Pac, Naughty By Nature, Coolio. LL. Cool Jay, Notorious BIG etc tunapozea na akina Keith Sweet, R. Kelly, Boys 2 Men, etc