Edmund Mndolwa: Awamu ya Tano tulilazimishwa kukalia misumari

Edmund Mndolwa: Awamu ya Tano tulilazimishwa kukalia misumari

Akizungumza kwenye kikao cha Wakuu wa Shule za Wazazi za Chama cha Mapinduzi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Dk Edmund Mndolwa, amedai kwamba kwenye awamu iliyopita walilazimishwa kukalia misumali na wala hakukuwa na hata chembe ya Utawala bora.

Kikao hicho kimeitishwa na Katibu Mkuu wa CCM, ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi.

Chanzo: MwanaHalisi

Swali: Je, wale watetea Legacy bado wangalipo?
Tuwekeeni VIDEO ya hayo Maneno ya Dk. Edmund Mndolwa anayosema hayo, mimi namfahamu Dk Mndolwa ni kiongozi mwenye weledi msomi aliyebobea siamini kama anaweza kuzungumza maneno hayo
 
👇😁😁😁
16409521842520.jpg
 
Akizungumza kwenye kikao cha Wakuu wa Shule za Wazazi za Chama cha Mapinduzi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Dk Edmund Mndolwa, amedai kwamba kwenye awamu iliyopita walilazimishwa kukalia misumali na wala hakukuwa na hata chembe ya Utawala bora.

Kikao hicho kimeitishwa na Katibu Mkuu wa CCM, ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi.

Chanzo: MwanaHalisi

Swali: Je, wale watetea Legacy bado wangalipo?
Hayo ni majungu na kujipendekeza kwa Samia. Mbona hawa wapigaji wanatumia nguvu kubwa sana kupambana na Magufuli asiyekuwepo duniani? Tunajua mwamba alivyowafix kwenye miradi ya CCM hadi wengine wakakimbilia Chadema wakakuta hali ni ngumu wakarudi CCM wakiwa wamekatwa mikia. Huyo huyo Mndolwa Novemba 2019 aliitisha kikao cha kumpongeza Magufuli kwa kazi kubwa alizozifanya na kusema wataenda na Magufuli 2020
 
True and fact, ninamkumbuka kwa kuidharau COVID 19 na ikampa majibu, pimbi Mkubwa yule
Yule Yuko wapi?

Unamkumbuka tu acha uongo.

Kila ukipita kwenye miundombinu alohakikisha inakamilika unafurahi mwenyewe.
 
Sijasikia akizungumzia Loliondo au hilo ameona sawa pamoja na kukalia sofa.
Uwizi tu ndio unaopigiwa chapuo.
Doctorate yake inafaida gani ? Hana machapisho yanayosaidia jamii. Wapo wapo kuunga juhudi na kushangilia
 
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wanalialia,walalahoi nao wanalialia.Hii nchi ina viongozi wanafiki Sana.
 
Akizungumza kwenye kikao cha Wakuu wa Shule za Wazazi za Chama cha Mapinduzi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Dk Edmund Mndolwa, amedai kwamba kwenye awamu iliyopita walilazimishwa kukalia misumali na wala hakukuwa na hata chembe ya Utawala bora.

Kikao hicho kimeitishwa na Katibu Mkuu wa CCM, ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi.

Chanzo: MwanaHalisi

Swali: Je, wale watetea Legacy bado wangalipo?

Pimbi mkubwa huyu! Ni mmoja wa wale wanafiki wa kiwango cha PhD tulionao nchini. Wao ndio walikuwa enablers wake, waliokuwa wanakaa naye high table wakimpigia makofi. Unakaaje high table na muovu bila wewe kuwa muovu?
 
Akizungumza kwenye kikao cha Wakuu wa Shule za Wazazi za Chama cha Mapinduzi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Dk Edmund Mndolwa, amedai kwamba kwenye awamu iliyopita walilazimishwa kukalia misumali na wala hakukuwa na hata chembe ya Utawala bora.

Kikao hicho kimeitishwa na Katibu Mkuu wa CCM, ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi.

Chanzo: MwanaHalisi

Swali: Je, wale watetea Legacy bado wangalipo?
Kuondoa ujinga ni dhana Pana, haimaanishi kujua kusoma na kuandika tu ndio kuondoa ujinga. Moja kati ya fursa tuliyoipata katika awamu ya tano, ni kujua kwamba, kama taifa, tuna kundi kubwa sana la wajinga, ambalo, limekaa pale, linasubiri mtu alitumie tu, na litampa uhalali wa kutenda maovu makuu ya kuchukiza, ya kihayawani, na ya makufuru. Lakini, maovu hayo yatakuwa na uhalali wa sanduku la kura, kama ilivyokuwa kwa Hitler, na yeye alishinda kwa kura nyingi. Muovu ana uhalali wa kura! Hivyo ni kiongozi halali kikatiba!

Tuna kundi kubwa lililosherehekea utekwaji, mauaji, ukatili, kubambika kesi, kunyanyasa watumishi, dhuluma kwa wafanyabiashara, kundi Hilo kubwa ni la JPM.

Kama taifa, lazima tuwe na mikakati ya kuondoa ujinga katika kundi hili. Ujinga wa kuwafanya waelewe kwamba yale yalikuwa ni matendo ya kihayawani kabisa na hayafai katika nchi hii.
Fikiria mhitimu wa chuo kikuu asiye na ajira aliyekuwa anashangilia JPM kuzuia ajira serikalini na kuua uwezo wa sekta binafsi kuajiri.

Muajiriwa wa mfanyabiashara anafurahia uonevu dhidi ya bosi wake, baada ya mwezi kampuni inakufa, anakosa ajira

Fikiria mkulima wa korosho, mnazi mkubwa wa JPM japo aliona zao la korosho lilivyonajisiwa.

Tafakari mwananchi anayesifu sera za kunyima watumishi maslahi, halafu anaishi kwa kutegemea ndugu zake ambao ni watumishi ... Kila siku kupiga mizinga.

Fikiria watanzania waliokuwa wanashangilia kwa furaha kubwa kuona au kusikia fulani katekwa, mfanya biashara fulani kafilisiwa au kabambikwa mamia ya kesi, au kanyanganywa fedha zake zikizokuwa benki.

Mkuu wa Mkoa anaiba au kudhukumu magari, halafu anayawekea plate number za serikali, na like kundi la wajinga linatopea katika kumsifu sana kwamba ni kiongozi bora,gari ya wizi anaweka plate number za Mkuu wa Mkoa (RC)!

Nadhani kama nchi, tuandae programu maalum ya kuufuta ujinga huu ili kundi hili kubwa la wajinga,lipate uelewa. Haijalishi ni shilingi ngapi itatumika, lakini taifa litaponywa.

Kundi hili bado lipo, lina kiu ya damu ya watanzania wenzetu na halijashiba, ilibidi wengine wafukuziliwe Malawi, maana muda wote walikuwa wanaimba damu! Damu! Damu!.

Tutumie Redio,tv, na wasanii, shule, vyuo, viongozi katika hotuba kuufuta ujinga huu. Kila kiongozi akipata fursa ya hotuba aseme hili.

Kundi hili linahitaji elimu tu na uwazi wa taarifa ili kulivua utando wa propaganda za kipumbavu na kijinga kutoka awamu ya tano.

Kundi hili yule aliyefukuziliwa Malawi alikuwa anahangaika kuliweka pamoja ili limpe kura, jitihada zifanywe kuibomoa gundi iliyolishikamanisha, viongozi wanaoendelea kulitegemea ili wapate kura, wabomolewe kisiasa kabla hawajabomoa taifa.

Mama Samia amefanya makubwa sana kulijenga taifa na kulifanya liwe pamoja ...tumuunge mkono kwa namna yoyote ile
 
Akizungumza kwenye kikao cha Wakuu wa Shule za Wazazi za Chama cha Mapinduzi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Dk Edmund Mndolwa, amedai kwamba kwenye awamu iliyopita walilazimishwa kukalia misumali na wala hakukuwa na hata chembe ya Utawala bora.

Kikao hicho kimeitishwa na Katibu Mkuu wa CCM, ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi.

Chanzo: MwanaHalisi

Swali: Je, wale watetea Legacy bado wangalipo?
Wazee wa Legasi huwa wanatetea ujinga tu. Wenye chama chao wameongea.
Mimi ni nani wa kupinga?
 
Toka mtoto wake akatwe Ubunge kule Korogwe na JPM kwa issue ya ufisadi huyu mzee hana hamu na JPM. Yaani mzee aliamini mtoto angepita kabisa
tena Hayati Mwamba alimjulisha Mzee Mndolwa ambae ni Mjumbe wa CC kabla hata kamati kuu haijaanza kikao kuwa tunaenda kuchagua Mgombea Ubunge wa Korogwe lakini sio Mwanao kwa kuwa ni mtoa Rushwa
 
Hawa watu hawana kabisa hoja za maendeleo?

Kwamba kumsema alie kufa ndo kutapunguza ugumu wa maisha ya waTZ?

Tutegemee kuona Samia akitukanwa baada ya utawala wake.

Wanasiasa wa namna ya Mndolwa hawafai hata kiti cha ujumbe wa nyumba kumi maana hawana vision ya kuangalia mbele badala yake wanafanya mambo yasiyo na tija.
Hawamsemi aliyekufa bali wale waliomfanya vile alivyokuwa ili ujumbe ufike kuwa hawakufanya vyema na ikiwezakana wabadilike.

Dr Edmund sio mjinga
 
tena Hayati Mwamba alimjulisha Mzee Mndolwa ambae ni Mjumbe wa CC kabla hata kamati kuu haijaanza kikao kuwa tunaenda kuchagua Mgombea Ubunge wa Korogwe lakini sio Mwanao kwa kuwa ni mtoa Rushwa
Kwani mwenyekiti ndiye anakata majina ya wagombea? Ndio akamweka Tale tale🤣🤣
 
Hakuna umeme siku ya tano halafu hata uwezo wa kununua sola au generator huna umekalia uchawa tu wa ccm
Upuuzi mtupu, hata Mangula akiongea atakuwa anafanya siasa tu, kama vile tu pro-Chadema unavyoshupalia hizi siasa hapa za majitaka huku mtaani hakuna umeme mchana ni siku ya tano mfululizo sasa, wananchi tunawachora tu na siasa zenu ipo siku ya Gambia kuzidi Srilanka yatawafika tu.
 
Back
Top Bottom