kaligopelelo
JF-Expert Member
- Jun 20, 2013
- 2,832
- 4,070
Haji Manara naye na uchambuzi wake
Hajis Manara, "Muitaliana Roberto Baggio alifunga goli kama hili kwenye Seria A Msimu wa 1991/92 na liliimbwa sana hilo goli duniani".
George Hagi, Mromania Star zaidi katika football na aliyetamba sana World Cup ya 1994 kule USA, alifunga goli kama hilo wakati akiitumikia Barcelona. Ilikuwa ni Mechi baina ya Barca na Granada kwenye kombe la Mfalme. Hagi alipasia kwa kuuswitch mpira kwenye nyavu ndogo, ilikuwa ni hadithi ya ukumbusho wa goli la Baggio.
Lakini bingwa wa kupasia nyavu duniani alikuwa Gary Lineker, Muingereza aliyetamba na Tottenham, Everton na Barcelona, style hii ya kufunga aliipenda sana na ilizoeleka Kwa kila shabiki wa soka kwa wakati huo.
Mabibi na Mabwana, sasa namleta kwenu Aziiz Stephen Kii, namba 10 mgongoni na style ile ile ya Lineker, Hagi na Baggio, hao pia walikuwa wavaa jezi namba 10 kama anayovaa Aziz.
NB: Sorry nimewakumbusha story ambazo hamwezi kupewa na wachambuzi wa mchele, ni lazma uwe umeiishi football ndio hata uwajue kina George Hagi wa dream team ya Barcelona Ya mwaka 1992.
@az_stephane10 🙌
#Bugati