Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

kuunganisha nguvu kupambana na Membe labda, maana huyo 'jasusi' mambo yake sio ya mchezo inawezekana, yeye ame 'chill' tu huko Lindi wakati huku town dk. Bashiru analialia majukwaani kuwa jamaa anamhujumu JPM! ni matumaini yangu JPM hajapoteza support ya Ben na mzee wa msoga, hao wazee waki 'team-up' 2020 patawaka moto.
 
Really?

Eti Lowassa aliletwa kimkakati CDM!

Hivi alipokatwa Lowassa akawekwa Jiwe Lowassa alikua kwenye hali gani halafu uniambie alitumwa CDM kimkakati?

Mtu mzima kama wewe kua muongo muongo namna hii kishabiki hivi ni upumbavu!
wewe 2015 lowassa angegombea urais ndani ya CCM kwa sifa mbaya alizokuwa nazo CCM ingepata tabu sana pengine vurugu zingezuka inakuaje mtu mchafu namna ile anashinda urais wakati watanzania wanajua ni mchafu,kilichofanyika pale ni kuokoa CCM na maslahi yao kwani urais upo tu,kama hivi sio miaka mingi lowassa na kundi lake wanaweza ongoza nchi....

Huu ndio upambavu wangu,weka hekima yako wewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japo niko tips ila ngoja nijaribu kuifinya medula...

Mwanzoni alitumwa kuja kuivuruga Chadema ndo akaja ila hakubvaa gwanda hata siku moja.

Sasa ametumwa tena kurudi kuivuruga CCM sasa sijui zile jezi za Ulipo Tupo zitavaliwa tena...!!!!

Kwaherini, narudi kwenye Mahaba.

Kasie Chuban Matata.
Lazima avae hapo ni home kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo nitakesha kwenye bar kwa furaha ya Lowassa kuondoka cdm. Alaaniwe Mbowe na genge lake kupokea hela ya Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea urais.
Mkuu mie nishaagiza libapa nalibonyeza kwa furaha, tunaitaka ile CDM yetu imara isiyoyumba... Tukitimua na yule katibu mamluki mambo yatakaa sawa ile nafasi apewe Mh Mnyika.
 
Acha ujinga wewe umewahi kufuatilia ninachoandika humu?

Ndani ya saa keshakuwa fisadi tena...

Wakuu bora tuwaache hawa wanasiasa ...! Hivi vitu tukivichukua tuu personal sie ndio tunaumia.
 
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.

Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.

Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rais Magufuli, Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Humphrey Polepole n.k



View attachment 1035375
View attachment 1035459
View attachment 1035448

Unaweza soma pia:

Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM - JamiiForums

Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto - JamiiForums

Lowassa hana namna zaidi ya kuipigia magoti CCM, Mkwewe Sioi Sumari mpaka sasa yupo lockup - JamiiForums
Kwani alikua ameenda wapi?
 
Leo nitakesha kwenye bar kwa furaha ya Lowassa kuondoka cdm. Alaaniwe Mbowe na genge lake kupokea hela ya Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea urais.
Mbowe ameurudisha upinzani kwa miaka mingi nyuma, hii laana itamwandama sana
 
wewe 2015 lowassa angegombea urais ndani ya CCM kwa sifa mbaya alizokuwa nazo CCM ingepata tabu sana pengine vurugu zingezuka inakuaje mtu mchafu namna ile anashinda urais wakati watanzania wanajua ni mchafu,kilichofanyika pale ni kuokoa CCM na maslahi yao kwani urais upo tu,kama hivi sio miaka mingi lowassa na kundi lake wanaweza ongoza nchi....

Huu ndio upambavu wangu,weka hekima yako wewe!

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu kila mtu ana theory yake!

Theory yako wewe haimaanishi ni ya kweli,na yangu haimaanishi yaweza kua kweli pia!

Huenda ikawa kweli au uongo,hapa tunaangalia kila mtu na opinion yake!

Wewe shika yako na mimi nishike yangu mkuu!

Haina noma,pamoja sana!
 
Kila la heri mzee Lowassa ni haki yako kikatiba japo umeumiza walio wengi waliojitoa kukusapoti wewe na kiukweli kama vijana tuliamini kuwa wewe ndiyo rais wa mioyo ya watanzania na hao uliowafuata walikutangazia hata kufa ndiyo hao waliokuchafua kwa madai umejinyea jukwaani ila vijana na makamanda wa kweli tulijitahidi kulipigania hili kulinda utu na heshima yako ila nachoamini Chadema itasimama na wale walioanzia ndani ya chama, nenda mzee Lowassa nenda kapige push up

Sitegemei kuona viongozi wangu wa chama cha demokrasia na maendeleo wakikusemea mbovu zaidi ya kukutakia heri huko ulikorudi ila tambua CHADEMA itaendelea kusimama na kuimarika kila leo

Wambie kesi ya uchochezi na uhaini wakufutie ila Mbowe na viongozi wote wa chama hawatakatishwa tamaa na kurudi kwako
"
mfano na mbowe akatoka na kujitoa CHADEMA
 
Wimbo ulianza kwa chadema, hakuna kupinga. Kila pembe ilikuwa ni "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" alipokosa kuteuliwa kuwania urais wa tiketi CCM akajitoa CCM na kuhamia chadema, akapewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chadema, ghafla chorus ya "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" ikawa inaimbwa na wana CCM.

Sasa karudi CCM nani ataiimba chorus hiyo?

Siasa ni mchezo mbaya sana.
hili swali alijibu ndugu yetu Mwanakijiji....
 
Back
Top Bottom