Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Hoja Za Prof Lipumba kuhusu Lowassa sasa zimeeleweka

Ma Prot sio watu wa mchezo mchezo
 
Naambiwa Mzee Edward Lowassa mwamba wa siasa za Tanzania amerejea CCM.

Huu ni ushindi mkubwa kwa Lowassa mwenyewe na vyama vya Upinzani.

Lowassa atapata posho zake za uwaziri mkuu bila mizengwe.

Lowassa kwa umri wake na hadhi yake si mtu wa kushinda mahakamani au gerezani kwa mapambano ya kidemokrasia.

Mkwe wake Sioi Sumari kama sijajosea jina yupo ndani kwa kosa la uhujumu uchumi tangu 2016.

Kwa kipindi chote hicho,binti wa Lowassa anaishi kama mjane kwa kumkosa mume wake,

Kurejea kwa Lowassa CCM ni fursa kwa mwanae kumpata mume wake mapema ndani ya miezi mitatu ya mwanzo.

Hivi mlitaka Lowasa abaki upinzani huku akijua chaguo la Upinzani ni Lissu au Zitto halafu abaki huko kwa faida gani wakati mkwe wake anateseka gerezani?

Mzee Lowassa kajitendea haki yeye,familia yake pamoja na mkwe wake.

Mzee kaamua kuzichanga na kubani kuwa kurudi CCM kuna faida nyingi kuliko kubaki upinzani ambako si chaguo lao tena kwenye uchaguzi mgumu saana wa 2020.

Kwa upande wa upinzani nako ni sherehe.

Kuondoka kwa Lowassa kumetoa fursa kwa upinzani kujipanga mapema.

Upinzani ungeumizwa endapo Lowassa angejiondoa Upinzani katikati ya kampeni za mwaka 2020.

Kuondoka kwa Lowassa kwa hiyari yake kumeunusuru upinzani na Migogoro ya ndani ambayo kwa sasa ipo ndani ya CCM kuliko upinzani.

Kama wangemuengua Lowassa kwa nguvu na yeye kuamua kuwavuruga kama anavyofanya Lipumba,hakika upinzani ingebidi usubiri hadi 2025.

Lakini kwa kitendo cha kiungwana alichofanya Mzee Lowassa kutotaka usumbufu na kuvunjiwa heshima,ameamua kujiondoa mwenyewe .

Kurejea kwa Lowassa CCM ni sawa na kuamua kustaafu siasa akiwa ndani ya chama kilichomlea. Hii ni faida kwake binafsi kwakuwa ataendelea kunufaika na mfumo ikiwa CCM itadumu nadarakani.

Familia yake haitataifishwa mali zao hata siku Lowassa akiaga Dunia siku mwenyezi mungu akimuita.

Vijana wa upinzani sitegemei mumtukane ,kumzodoa na kumkejeli Mzee wetu huyu ambae ameusaidia upinzani kupata viti vingi bungeni kutokana na ushawishi wake.

Siasa ni wakati,Mzee amesoma vizuri alama za nyakati.
You nailed. Mkwe soon atarudi. Hata ningekua ni mimi
 
Zipo nadharia mitaani kuwa Lowasa alikuja ukawa kimkakati ili kuokoa ccm isife 2015 wakijua atashinda Lkn awe ni MTU wa kuyakubali matokeo kuliko upinzani angesimama Mbowe asingekubali kuibiwa ushindi, thus hakuwahi rudisha kadi ya ccm,hivo kurudi ni kusadikisha haya.Ngoja tuone upepo wa 2020 utakavokuwa.Ccm mpya haiuziki mtaani imevuruga kila sehemu haina uwezo wa kupambana na Lissu
Ni kweli japokuwa uraisi watashinda
 
Kwa heri Ruge karibu Lowasa, liko wazi Lowasa angerudi Ccm thus alianza kumtanguliza Karanga ili jimbo LA Monduli lirudi ccm,wanaweza wakawa wamerudi kwa jiwe ili wamuangamize kumbuka hawa mapacha watatu ni watoto wa mjini wako kitambo hawajaja mjini wakubwa,ngoja tuchek sarakasi zitakavopigwa uenda jiwe akaliwa kichwa akiingia 18 ya mapacha hawa.Muda ni mwalimu
 
Mbona hatuzioni Twitter za kina Zitto na Lissu. Au tuungojee waraka mrefu wa Lissu akianza na historia ya kumsafisha Slaa, na kumkebehi Lowasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona hatujaziona Twitter za harakaharak za kumsema km jabali la mafisadi?, vipi kaponaa kujinyea mlikomdhalilisha 2015?, mkumbushee alaa sasa choo ipo meza anapolia chakula. Je ataisikia au?
 
Wew
Mbowe aliiua cdm hasilia ameua misingi ya chama kwa kumleta lowasa na alitoa fedha nyingi sasa chama kimekufa ata gerezani uko asitoke tena maana dhamira yetu wanacdm inatusuta,mbowe hajiuzulu kwa kushindwa kusimamia chama apo ndo naanza kumuelewa zitto,slaa yani hata bora lipumba sio mbowe ,damu za wana cdm waliokufa kukipigania hiki cham zitamtesa mbowe ,

@ mbowe out
MBOWE out
MBOWE out

Sent using Jamii Forums mobile app
ni sawa na Lowassa mnapenda kuwa penye mteremko, ndio maana watz wataiacha ccm madarakani mpaka kizazi chenye akili kizaliwe.
 
"Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu " Lowassa ameondoka chadema kama Alivyoondoka kalanga
sasa ni wakati wa kufukuzwa kwenye majengo yenu yote mliyopanga maana mlipa kodi amechoka,kaamua kurudi nyumbani
 
Zipo nadharia mitaani kuwa Lowasa alikuja ukawa kimkakati ili kuokoa ccm isife 2015 wakijua atashinda Lkn awe ni MTU wa kuyakubali matokeo kuliko upinzani angesimama Mbowe asingekubali kuibiwa ushindi, thus hakuwahi rudisha kadi ya ccm,hivo kurudi ni kusadikisha haya.Ngoja tuone upepo wa 2020 utakavokuwa.Ccm mpya haiuziki mtaani imevuruga kila sehemu haina uwezo wa kupambana na Lissu
Jidanganye
 
Huo ndio mkakati unaoenda kufanywa now na Team Lowassa as perfect as Lowassa anapambana kuweka heshima yake pale pale juu.

Aidha:

1. Njia ya diplomasia itumike Magufuli aishie awamu moja tu, ama
2. Lowassa wakishirikiana vizuri na Rostam Aziz wakafanya wafanyalo CCM imteme Magufuli 2020.

Ukweli:

Lowassa anawajua na ana mashabiki zaidi wa CCM kuliko Magufuli. Pia, Magufuli kawaumiza zaidi wana CCM kuliko hata wapinzani.

Kama, Lowassa akashindwa kupenya 2020, basi kwa ushirikiano na The King Maker #Rostam Aziz wanaweza kumweka mtu wao ama 2020 au 2025 na kuendelea.

Nimemaliza.

Siasa ni ujasiriamali kama ilivyo ujasiriamali mwingine.

The battle is on, if you can't fight them join them and fight within them!
 
Kama Lowassa Karudi CCM na mimi namfuata kokote aendako narudi CCM nimechoka siasa za kupinga kila kitu narudi nyumbani
20190301_182544.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lowassa karudi CCM kabla ya Lowassa Mwenyewe kujua Kuwa karudi CCM

Lowassa karudi CCM Siku Rostam alipokaribishwa Chai Ikulu Na Mzee Baba

Nguvu ya Rais Magufuli Kwenye Uchaguzi wa 2020 panapo uhai haimithiliki!

Kushoto Jk, kulia Rostam, Pemben Ngoyai
Hahahahaha
Habari mkuu...

Mwendo wa codes tuu..[emoji3][emoji3][emoji41]
 
Back
Top Bottom