Best hoja yangu ni kuwa, Jiwe alijinasibu kuwa aliingia Ikulu pasi msaada wa mtu, akimaanisha hakukuwa na mkono wa “The King Maker” katika ushindi wake.
Sasa huu ukaribu wake nae sasa hivi ni kuwa anatafuta nguvu ya ziada kutoka na na hali ya siasa za Tanzania nje na ndani ya nchi?
Dr slaa alisema hawezi kaa meza moja na waliyemchafua itabidi ahame tena ccm aende kwa Rungwe au updp
Lowassa ambaye alikuwa mpinzani mkuu wa Rais John Magufuli katika uchaguzi mkuu uliopita, aliondoka CCM na kujiunga na Chadema, kupitia mkutano wake na waandishi wa habari wa tarehe 28 Julai 2015, katika hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Alichukua hatua hiyo, wiki moja baada ya jina lake kuenguliwa katika orodha ya wagombea urais wa CCM.siasa za afrika ni ngumu sana hasa kwa wapinzani. View attachment 1035581
Sent using Jamii Forums mobile app
Karibu ndg, ulikuwa kimya siku nyingi. Naona upepo huu haujakuacha salama, umekuibua.Baada ya yote yaliyotokea, la msingi ni vyama vya upinzani kujitafakari, kujenga mshikamano kwa wale watakao baki ili kuwe na upinzani imara Tanzania. Kwa hili la Lowasa kuna ambao tulijiuliza huyu mheshimiwa ana simamia nini kitu gani hapo CDM, hadi leo sijapata jibu. Ni wakati wa CDM na washirika wake kujibrand upya kwa maneno na vitendo zidi ya Lichamadola. MUNGU WETU HAJA WAHI KUSHINDWA.
Kama ulifikiria imekujengea historia yoyote ya maana, basi aliyekushauri amekudanganya/amekupoteza. Hata huyo aliyekupokea naye anaingia katika historia za wanasiasa wa hovyo katika historia ya siasa za Tanzania. Kama kuna historia concrete itaandikwa na wana vyuoni, basi jina lako litaandikwa kwnye karatasi za mawe!
Ungeli retire siasa labda ingelikujengea heshima zaidi. Kashifa za ufisadi unaotuhumiwa nao hakuna mwenye ushahidi usiokuwa na mashaka! Hivyo bado heshima yako ingelisimama
Hahahaha magufuli alisema mafisadi yamekimbilia CDM, ila leo kapokea fisadi kwa bashasha kubwa kabisa!
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]siasa za afrika ni ngumu sana hasa kwa wapinzani. View attachment 1035581
Sent using Jamii Forums mobile app
Sijasema kama ataondoka CCM, nimeuliza atarudi CHADEMA? Aliko mi sjiui.
Siasa ina unafiki sana aisee ukiwa unawaza hayo jaribu kuwaza pia wale walio ondoka nae kwenda cdm vipi nao wanarudi au ndo wametopea huko [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Nawaza ccm mlivyomtukana wakati wa kampeni sijui mtasemaje saivi
Anyway astaafu siasa sasa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Inaweza kuwa mbinu ya JK na Yule mwarabu Rostam kuandaa Mazingira ya Membe.Najaribu kuwaza tu.Lowasa ni mtu mzima sana hajarudi ccm bure bure kuna sababu muda utaongea .
Endelea kutafakari huku ukikijaza kibubu kwa ajili yako na familia yako. Ishi maisha yako, ukiwatafakari sana wanasiasa utapasuka kichwa bure. Siasa ni ngumu kuliko physics.Kuna kitu bado nakitafakari.