Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Kama ulifikiria imekujengea historia yoyote ya maana, basi aliyekushauri amekudanganya/amekupoteza. Hata huyo aliyekupokea naye anaingia katika historia za wanasiasa wa hovyo katika historia ya siasa za Tanzania. Kama kuna historia concrete itaandikwa na wana vyuoni, basi jina lako litaandikwa kwnye karatasi za mawe!
Ungeli retire siasa labda ingelikujengea heshima zaidi. Kashifa za ufisadi unaotuhumiwa nao hakuna mwenye ushahidi usiokuwa na mashaka! Hivyo bado heshima yako ingelisimama
 
Kuna siku nilihoji humuhumu JF
Huyu mzee mbona havai sare za chadema[emoji1321]‍♂️
Mtazamo wangu mwingine ni ameamua kurejea huko,baada ya kuona Lisu njia moja kugombea na anakubalika kikweli kweli,akaona hapa hamna tena nafac ya urais[emoji38]aliutema ubunge wa viti maalum kwa chadema ili agombee tena urais 2020.sasa kaona maji yanazidi kuwa marefu,ni bora arejee tu huko CCM[emoji38]
 
Best hoja yangu ni kuwa, Jiwe alijinasibu kuwa aliingia Ikulu pasi msaada wa mtu, akimaanisha hakukuwa na mkono wa “The King Maker” katika ushindi wake.

Sasa huu ukaribu wake nae sasa hivi ni kuwa anatafuta nguvu ya ziada kutoka na na hali ya siasa za Tanzania nje na ndani ya nchi?

Ameharibu uchumi

Ameishiwa fedha

Anadhan hao wanafedha kumtoa alipokwama?

Tsunami yaja to hell uchumi na atapata tabu sans
 
siasa za afrika ni ngumu sana hasa kwa wapinzani. View attachment 1035581

Sent using Jamii Forums mobile app
Lowassa ambaye alikuwa mpinzani mkuu wa Rais John Magufuli katika uchaguzi mkuu uliopita, aliondoka CCM na kujiunga na Chadema, kupitia mkutano wake na waandishi wa habari wa tarehe 28 Julai 2015, katika hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Alichukua hatua hiyo, wiki moja baada ya jina lake kuenguliwa katika orodha ya wagombea urais wa CCM.

Niliwekewa mizengwe, kuhakikisha jina langu halifiki Kamati Kuu na Halmashauri Kuu (NEC). Nia yangu ni kuleta mabadiliko na kuondoka kwangu na kujiunga na Chadema, ni kuendeleza dhamira hiyo,”

“CCM siyo Baba yangu, wala siyo Mama yangu. Kama Watanzania wameyakosa mabadiliko CCM, basi watayatafuta kwingine. Ninaondoka. Sijakurupuka.”
 
Baada ya yote yaliyotokea, la msingi ni vyama vya upinzani kujitafakari, kujenga mshikamano kwa wale watakao baki ili kuwe na upinzani imara Tanzania. Kwa hili la Lowasa kuna ambao tulijiuliza huyu mheshimiwa ana simamia nini kitu gani hapo CDM, hadi leo sijapata jibu. Ni wakati wa CDM na washirika wake kujibrand upya kwa maneno na vitendo zidi ya Lichamadola. MUNGU WETU HAJA WAHI KUSHINDWA.
Karibu ndg, ulikuwa kimya siku nyingi. Naona upepo huu haujakuacha salama, umekuibua.
 
Kama ulifikiria imekujengea historia yoyote ya maana, basi aliyekushauri amekudanganya/amekupoteza. Hata huyo aliyekupokea naye anaingia katika historia za wanasiasa wa hovyo katika historia ya siasa za Tanzania. Kama kuna historia concrete itaandikwa na wana vyuoni, basi jina lako litaandikwa kwnye karatasi za mawe!
Ungeli retire siasa labda ingelikujengea heshima zaidi. Kashifa za ufisadi unaotuhumiwa nao hakuna mwenye ushahidi usiokuwa na mashaka! Hivyo bado heshima yako ingelisimama
 
Hawana umakini wowote sema Jeshi la polisi linawasaidia. Kama wanajiona Makini,Wairuhusu CHADEMA ifanye siasa kama wao tuone nani makini kati yao na CHADEMA.
 
Back
Top Bottom