Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Itakuwa faida kwa upinzani 100%....

Nilishapiga kelele sana hapa kuhusu Lowassa na Sumaye....

Hawa ni watu walioshiriki kila aina ya ufisadi ndani ya ccm .

Angalia sasa tamaa ya mbowe sijui na Dr slaa uso wake atauweka wapi?....

Niwakati wa Lissu kapewa chama na kumshawishi Bi Fatuma karume wagombee 2020 tuchukue nchi mapema...

Fukuzeni na Sumaye kwenye chama ungana na Zitto awe waziri mkuu baada ya uchaguzi hapo tutawapigania kwa hali na mali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa nawahurumia wale ambao chama kwao ndio maisha wakampokea mzee wakapambana kwenye uchaguzi vurugu zile ukute kuna waliopoteza viungo vya mwili au kuna waliofariki,familia zinateseka na mzee huyo karudi zake chama cha kijani. Ndio maana mimi na siasa mbali mbali nitapiga kura sababu tu ni haki yangu ila si mshabiki wa siasa kabisaaa
 
Fisadi mwingine huyo yeye na Sumaye yalikuwa makosa makubwa sana kuwakaribisha Chadema mafisadi hawa wawili. Hawana impact yoyote ile ndani ya Chadema.

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.

Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hali ya kisiasa inazidi kupamba joto kuelekea uchaguzi mkuu ujao wa 2020 hasa baada ya leo Mh. Edward Lowassa kuonekana katika viwanja vya Ofisi ndogo ya CCM Lumumba sambamba na Mh. Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Taarifa za awali zinasema huenda tayari Mh. Edward Lowassa ameamua kurudi CCM na kuachana na siasa za Upinzani. Hakika hili ni pigo kubwa kwa Upinzani hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020!
IMG-20190301-WA0001.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom