Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Mzee kaondoka na ramani ya ufipa, lazima watafutane. Mtahangaika sana na mzee huwaga hajibu kitu atapiga kimya tu. Tuliwaambia mbn hata gwanda havai Mara ooh Mara ooh, sasa kiko wapi
 
Sasa nadhani rafiki yangu nayemuheshimu Dr Slaa atarudi CHADEMA,maana asiyempenda kaja.

Dah Barafu umeniwahi, sasa SLAA arudi CDM, watoto wa mjini wabaya sana.. ROSTAM on the move.
 
Kumbukizi Mtifuo!
Screenshot_20190301-185710~2.jpeg
 
Wakuu habari zenu

Moja kwa moja tuende kwenye mada

Kwanza rest in peace Ruge

Lakini pia huenda kuna MTU anajiandaa kuzikwa kwa heshima ya kitaifa maana bila hivyo hataipata

Leo Lowasa amerejea nyumbani binafsi kilichomleta chadema ni uraisi tu

Na kitu hicho ndicho kilichomkasirisha slaa akaamua kubwaga manyanga akaenda zake ccm na kupewa ubalozi

Kingine ni ufisadi ambao slaa anaamini lowasa ni mojawapo wa mafisadi papa nchini Tanzania

So akaondoka chadema kisa lowasa na kwenda ccm kwa sababu lowasa ni fisadi na hawezi kukaa chungu kimoja na fisadi wala hayuko tayari kumruhusu fisadi kugombea urais

Sasa lowasa amerejea ccm

Je daktari slaa atarudi chadema au yuko tayari kukaa na fisadi chungu kimoja hapo ccm?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo maana mm sipendi kushabikia siasa kwa upuuzi kama huu.,Africa hakuna siasa.
 
Back
Top Bottom