Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Labda akihama Mbowe na Lissu ndiyo kidoogo nitapatwa na kizunguzungu cha muda tu lkn lowasa wacha arudi zizini akaokoe mali zake
Kwa ufupi Waziri Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Frederick Sumaye amesema uamuzi uliochukuliwa na Edward Lowassa kurejea CCM hauwezi kuwateteresha

In God we Trust
 
Sasa mbowe akijitoa tu chadema hata uenyekiti tu basi chama hakuna kwa akili za akina lissu,mdee,angalau mnyika na lema kidogo wanaweza wakakiendesha chama ila hao wengine harahara/malolota sana.

Mbowe and hekima despite michezo yake michafu kama walivyo wale wa CCM tu
Hata Mbowe nae ni suala la muda tu. Hasa kama atapokonywa uenyekiti nadhani baada ya masaa 72 atakuwa tayari ashapewa kadi ya CCM na uwaziri wa TAMISEMI kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji44]
Screenshot_20190301-185710~2.jpeg
 
Mzee kaona ameingia hasara kununua chama.
Bado Yule mwingne nae atarudi uchaguzi ukikaribia.
Stay tuned,
Devils can't be Angels and vice versa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itakuwa faida kwa upinzani 100%....

Nilishapiga kelele sana hapa kuhusu Lowassa na Sumaye....

Hawa ni watu walioshiriki kila aina ya ufisadi ndani ya ccm .

Angalia sasa tamaa ya mbowe sijui na Dr slaa uso wake atauweka wapi?....

Niwakati wa Lissu kapewa chama na kumshawishi Bi Fatuma karume wagombee 2020 tuchukue nchi mapema...

Fukuzeni na Sumaye kwenye chama ungana na Zitto awe waziri mkuu baada ya uchaguzi hapo tutawapigania kwa hali na mali.

Sent using Jamii Forums mobile app

Best comment brother.
 
Yeye anawazaga URAISI tu basi.
Hana jambo lingine.
Alimharibia tu Raisi wetu kipenzi, Bermad Kamilius Membe.
Zaidi ya Urais, hana ndoto au wazo lingine.
Anataka 2025 Magufuli ampe mafasi ya kugombea Urais,
Lowasa anahaha kuupata Uraisi tu Basi.
LowasaLipumbavuprofesa


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanangu Busha mbona mimi siamini kama Lowassa alipenyeza hela yoyote?

Siamini kabisa!

Labda wewe unihakikishie kwa kuniwekea evidence hapa isiyokua na shaka!

Tukianza kusema kwa maneno generally tu juu juu kua aligawa pesa tutakua tunafanya insinuation!

Kwa kipindi ukimchukua Dr Slaa na Lowassa,Lowassa alikua amempita Dr Slaa kwa approval rating,Mbowe alifanya logical choice ya kumchukua Lowassa maana alikua na kundi kubwa sana la watu wa CCM!

Logic ya Lowassa kutoa hela hai-make any sense kwa minajili hii!
Ahaa kumbe umeweka kigingi kwenye ushahidi,, basi ushahidi upo na utakuja kuuona tu,vuta subira,,,

Sasa watu aliokuja nao ed low walipewa nafasi za juu ndani ya chama na wakahaminiwa,, sasa wote wameludi ccm.

Utakubaliana na mm kua mwenyekiti alivunja demokrasi ndani ya chama kwa kutoruhusu mchakato wa kuchagua mgombea urais ndani ya cdm,?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo tunahesabau masaa tu kama siyo siku
Najaribu kuwaza tu,huenda Lowassa kurejea CCM kuna uhusiano na mkwe wake kuwa lupango kwa kesi ya uhujumu uchumi!
Lowassa huenda kajifunza jambo toka kwa Rostam ambapo Rostam alipotinga tu ikulu tukaona maamuzi ya DPP kufuta mashtaka ya utakatishaji fedha na akabaki na mashitaka aliyoambiwa alipe faini!!!

Wenye kuona mbali,muda utaongea!

In God we Trust
 
Mkuu hawa wanasiasa ambao hawako consistent wanachefua sana ...afadhali angejivua uanachama na sio kurudi CCM what a traitor??!!!

Mkuu ni bahati mbaya sana wanasiasa wengi sana ni malaya namna hii!

It is unfortunate!


CCM hii ambayo inacheza na Maisha ya watu tangia uhuru, watu ambao wanatumia serikali kujipigia, kabla hujasupport this foolish government , umewahi kufikiria kuna ndugu zako kijijini wanakufa sababu ya kukosa madawa na kabla huja support hii serikali ya kidhalimu je umeangalia watu wanaokuzunguka wanaishije ? Watu hawa afford 3 meals a day halafu unali support hili liserikali lako?!! My dear are you blind?
Exactly my sentiments!

Cha ajabu mambo muhimu kama haya watu hua hawayaoni kabisa!

Watu wanao-support CCM ni aina fulani ya watu ambao mimi hua hata siwezi wa-define!

I tried atleast to understand them,ila nilishindwaga miserably!

I’m also with opposition, people who despite being harassed and humiliated and sometimes jailed,they continue to fight for democracy of this country

You are all exceptional and noble people!

I feel them deeply and I will always support them,iwe mchango,etc!
 
Heshima kwenu wana jamvi,

Leo imekuwa siku muhimu katika siasa za Tanzania na pengine nchi ikaingia katika historia mpya katika medani za siasa za ushindani.

Mheshimiwa Lowassa waziri mkuu mstaafu na mgombea urais wa UKAWA mwaka 2015 kajiengua CDM na kurejea CCM.Ukweli mchungu siasa za upinzani katika nchi za dunia ya Tatu hasa Afrika zinahitaji ngozi ngumu kweli kweli.Ikiwa umezoea raha upinzania si mahali pake,kaa mbali kabisa kwasababu zinaweza kukuletea umaskini ikiwa wewe ni mfanya biashara na zinaweza kukulaza ndani ikiwa wewe ni mwanasiasa.

Sote tunajua Rostam Aziz mdogo wake alifunguliwa kesi mbaya sana na tulitarajia angeweza kuhukumiwa kifungo cha muda mrefu.Baada ya Rostam kwenda Ikulu mdogo wake alihukumiwa kupigwa faini na sasa yuko nje akiendelea na biashara zake.

Leo Lowassa karejea ndani ya chama natarajia atarejeshewa tena heshima zake ikiwemo ya kijana wake kuachiwa mara moja na kesi kufutwa.Sitashangaa iwapo Sioni Sumari akiachiwa huru na mambo yakaendelea kama kawaida.

Naomba nisiendelee sana kwa leo naomba kuishia hapa muda ni mwalimu mzuri sana.
 
Back
Top Bottom