Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Watu wa Mungu habari zenu..

Tetesi za ndani za CDM ni maumivu makali baada ya Mh Lowassa kurudi nyumbani kumenoga..!! Yaani ni sawa kuvunjika kwa uti wa mgongo, haiwezi tena kujitutumua hata kidogo kisiasa..!! Poleeeeni..!

CCM haishindwi chochote huwa nasema hivi kila mara.. Sasa mmeona na kudhibitisha..! Chezea kitu kingine sio CCM..!! CHADEMA leo bado wako ktk maruweruwe hawajui nini kimetokea, hawaamini bado..!! Siasa mchezo mchafu sana..!! 😜😂😂
 
Walicheza magarasa ya hovyo hovyo na walikuwa wakiliwa ila hawakuujua mchezo hivyo wakaendelea kucheza.

Walipoona wanaliwa sana wakaamua kucheza karata kubwa ila hawakujua pia kuwa karata kubwa yaweza kuliwa kupitua utaratibu wa karata ndogo!

Sasa wamemchukua Lowasa. Hawakuona yule nabii aliyekuja kwenye uapisho na akaishia kukaa na Lowasa waliyemchukua.
Hawaelewi kuwa wamejipaka kinyesi kiasi kuwa siku wakimaliza kukifuta na wao watakuwa sehemu ya dampo.

Bado tunawachezesha karata tunavyotaka na hiyo meza ya mazungumzo wanayoitafuta kwa kumtumia Lowasa haita kaa.

Ajenda mbili za msingi ni hizi;
1. Itolewe CCM kwenye uongozi!
Hii ndio hoja upinzani siku zote.

2.Huyu mjinga atoke.
Hana faida kwa CCM wala kwa yeyote

Sisi tutaendelea kucheza karata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kwenda na kurudi Ikulu ...na kupewa masharti magumu naona leo mzee kaamua"kusurrender"...
 
Huyo mzee kacheza kama Messi. Tunasubili yale majina yake ya utani "jizi, fisadi n.k" yaendelee baada ya kusitishwa kwa muda.
 
Kwahiyo bashiru na polepole wameandaa jiki kwa ajili ya kumsafisha ENL maana maccm yalidai ni mchafu hawafai ccm?
 
'Move' nzuri sana hii kwa CHADEMA wakijua kuikamua na kuitumia, for what it's worth! Tena imetokea wakati mzuri kabisa kuelekea kwenye chaguzi.

Kama kuna 'strategist' wazuri huko ndani ya chama, wakati ni huu wa kuanza kazi.

Mzee Lowassa hakuwa na mchango wowote wa maana ndani ya CHADEMA mbali na mkakati wa kupeperusha bendera wakati wa uchaguzi uliopita. Sasa kaondoka kuwapisha CHADEMA wajiandae tena bila ya mizengwe toka kwake.
 
Leo nitakesha kwenye bar kwa furaha ya Lowassa kuondoka cdm. Alaaniwe Mbowe na genge lake kupokea hela ya Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea urais.
Umesema vyema mkuu hata.huku cuf inaonekana lipumba hana mana kisa kakataa kufanya kz na lowasa akisema nafsi inamsuta leo yako wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mwanasiasa yeyote aliye mzalendo,wote ni wapigania matumbo tuuu,
 
Back
Top Bottom