Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Huu ni muda kwa vyama vya upinzani kuonyesha ukomavu wa kisiasa, pia ni wakati muwafaka kuonyesha demokrasia mnayoipigania.

Maendeleo hayana chama

Leo babangu kaona chozi langu😂😂later akasema huyo ndo ashajimaliza kisiasa nijajihis nimekiwa mwepesi..nyoko sana..bora aende
 
Nilikuwa nikijiuliza Lowassa yuko Chadema ila kimuonekano kama yupo CCM yaani yupo kimya vyama vya upinzani visiludie tena kosa kama hili walitumia nguvu kubwa kumsafisha.
Kweli kabisa katika jambo walilokosea sana ni hilo na ni bora amerudi, tofauti na uchaguzi mkuu sijaona jipya alokuwa nalo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LOWASA KURUDI CCM
Lowasa kurudi ccm ni ushahidi kuwa ana uchu wa madaraka. Aliondoka ccm kwa kuwa hakupata fursa ya kugombea urais akiwa ccm na alipoona kuna uwezekano wa kugombea kupitia UKAWA, akafanya uamuzi wa kwenda ukawa ili apate fursa hiyo.
Lowassa alitarajia kuwa atapewa nafasi ya kugombea tena urais kwa tiketi ya Chadema lakini siku za karibuni upepo ndani ya Chadema umemgeukia Tundu Lissu kuwa ndiye kipenzi cha wengi kugombea urais wa Tanzania. Baada ya Lowassa kuona hakuna uwezekano wa yeye kugombea tena urais kwa tiketi ya Chadema ameamua kurudi ccm.
Sio kuwa Lowassa akiwa ccm ana uwezekano wa kugombea urais mwaka 2020 lakini kule ccm kuna maslahi na vyeo. Huenda pia Lowassa anawaza miaka saba ijayo wakati JPM anamaliza muda wake. Huenda akajaribu tena karata zake za kugombea urais kwa kupitia ccm
Kuhama kwa Lowassa ni pigo kwa upinzani kwa vile kuna baadhi ya wana Chadema walijiunga na Chadema kwa sababu ya Lowassa lakini pia inaweza kuwa fursa ya Chadema kujipanga upya. Shutuma kuwa Chadema wanapokea mafisadi sasa zitaondoka.
Ni fursa pia kwa chadema maana kama kuna weaknesses zo zote za kurekebisha basi Chadema wasisite. Kwa mfano wahahakikishe mchakato wao wa kuchagua mgombea urais uwe wa wazi kwa kutumia vigezo vinavyojulikana na kukubalika na uwe wa kidemokrasia.

SWISSME
Mungu mbariki Lowassa.
Cc: Erythrocyte
 
Aisehh siasa za Bongo nyoko. Mimi ntahama Chadema ikiwa mbunge wangu Mbowe akikitoka basi na siasa ntaacha
tapatalk_1551087179830.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Taarifa mbaya sana kwa Dr slaa hizi sijui atahama ccm,ahamie Act alisema hawezi kaa chama kimoja na Lowasa
Sio kweli Dr. Slaa alitaka lowassa aje awe Kama mwanachama was kawaida Ila mkakimbilia kumtukana Leo yametimia
 
Hili gamba fisadi linajali tumbo lake tu na si maslahi ya Watanzania.

 
<blockquote class="twitter-tweet" data-lang="en"><p lang="in" dir="ltr">Lowasa karudi CCM. Karibu tena nyumbani Mheshimiwa. CCM hoyeee! Magufuli hoyee,,,,,,,,</p>&mdash; Reginald Mengi (@regmengi) <a href="">March 1, 2019</a></blockquote>
<script async src="https://platform.twitter.com/widgets.js" charset="utf-8"></script>

Hili pigo la leo pale ufipa ni kama bomu la nyuklia vile.
 
Back
Top Bottom