Ndugu wana jamvi.
Siasa ndani ya nchi ni mali ya GENGE.Genge (syndicate) tafsiri yake ni kundi la mwisho lililo na mamlaka katika kuendesha jambo.Kiuhalisia magenge yako kala mahala penye maslahi,kuanzia serikalini hadi kwenye maisha yetu ya kawaida mtaani.
Hivyo basi katika swala zima la kisiasa kuna kundi la juu ambalo lenyewe pamoja na vizazi vyao ndio huwa wanufaika na michakato yote ya kisiasa na utawala ndani ya nchi!.Katika tasnia nzima ya siasa kuna msemo maarufu usemao "Kula lakini usilize meno",hapa wanasiasa wanamaanisha mwanasisa yoyote hutazama tumbo lake kwanza na si la mwananchi lakini usiibe kiholela wananchi wakaona!
Kiuhalisia raia ndio wamiliki wa mali zote za nchi lakini wanasiasa kupitia sanaa iliyotungiwa sheria za kuheshimiwa kuliko vitu vyote nchini ndio wanufaika wakuu wa mali hizo,kikubwa ni kuwa bingwa wa kucheza na maneno!.Hapa ndio maana tunawaona watu wote kuanzia wasomi,wafanyabiashara na raia wa kawaida tunazitolea macho fursa za kisiasa!
Swala lililotokea hivi karibuni la mh.Edward N.Lowassa kurudi CCM ni fundisho tosha kwa Watanzania juu ya kufahamu michezo ya wanasiasa!.Hapo mwanzo Lowassa na timu yake walipishana maneno na wanagenge wenzao,hali iliyopelekea Lowassa na timu yake kutimka.
Lakini tuje katika ukweli halisi,CCM ni mali ya Genge.Genge ambalo limejitosheleza katika mbinu na silaha za kujilinda.Genge hili linamiliki idara ya usalama TISS,l jeshi la polisi,jeshi la wananchi na majeshi mengineyo,hivyo inakua ngumu kwa mtu anaepingana na genge hili kupata ushindi kirahisi.
Kutoka na kurudi kwa Lowassa kute kunajiri kipindi ambacho inchi inajiandaa na harakati za uchaguzi mkuu.Sasa swali tunalopaswa kujiuliza ni je Lowassa si mtu anaetumika na genge kwa maslahi yao?.Kwa maana sifa kuu ya wanagenge ni kwamba wazungumzayo ndani na nje ni vitu viwili tofauti!.
Hivyo wanachi yatupasa tuwajue wanasiasa na michezo yao,maana yote wayafanyayo ni kwa maslahi yao na si yetu.#Tz tuamke.
Sent using
Jamii Forums mobile app