Tetesi: Edward Lowassa kuongea na vyombo vya habari kesho kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam

Tetesi: Edward Lowassa kuongea na vyombo vya habari kesho kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam

Status
Not open for further replies.
Naendelea kuhifadhi maneno mpaka nikapojua nini kiko nyuma ya pazia kwa tukio la leo. Ngoja nisikilize ngoma za bakulutu (Polo Tika Tika) kwanza wakati nasubiri. Kitaeleweka tu.
 
Wala sitaki hata kumsikia huyu mtu kuanzia leo. Kaniharibia siku hakuna kunacholika wala kunyweka mpaka muda huu. Heri nikapumzike kambi za alshababu!!
Mkuu hukujua kwani ulishawahi kumuona Mh . Lowassa kala gwanda? Mbowe hoiiiiiiiii
 
Hiyo sababu ya kwanza ina maana akiachiliwa ni sawa na kusema kuwa either madaraka yalitumika vibaya katika kumuweka ndani or upendeleo umechangia kutolewa kwake (ni sawa na rushwa in kind). Inatoa picha gani kwa wananchi wa kawaida?
Mbona wale wabakaji wa watoto wasiojiweza hata kujitetea wametoka na kukaribishwa lunch mahali patakatifu ilileta picha gani kwa wabakaji watarajiwa mtaani na wananchi wa kawaida wenye watoto wadogo mashuleni na mtaani?
 
  • Thanks
Reactions: Mj1
Ngoja aunge mkono juhudi za Magufuli, sijui makamanda watamuita fisadi tena, halafu wale wakijani watamsafisha, hapa patamu, akivuka upande wa pili hamna aliye salama wote wataonekana wanafiki, yetu macho😀
Hizi ndio siasa zetu zinachanganya kichwa kama mtu aliyepata Cannabis
 
Kuwa mpinzani Africa ni sawa na kuzimu kwa hili Mbowe anastahili pongezi ana kifua cha kiume na ngozi ngumu kama nyegere
True, na ni mmoja wa watanzania wachache wanaoishi bila unafiki. Na unajua nini...kila siku inayoenda kwa Mungu anaiishi kwa ukamilifu wake
 
Ngoja aunge mkono juhudi za Magufuli, sijui makamanda watamuita fisadi tena..
Kwa nilichokiona leo, huyu sio fisadi tena as far as CCM is concerned. Leo JPM kampa sifa za nguvu sana mpaka nikahisi muda si mrefu EL atafanya maamuzi magumu kwa mara ya pili.
 
Hivi Lowassa ni mtu wa kuitisha press Serena? Halafu aongee dakika mbili?
 
Ninapenda kusubiri sana jambo la masaa machache tusubiri!
 
Mimi nina pesa ambazo nikizatandaza barabarani zinaanzia dar to dodoma halaf unasema unataka kuninunua nihamie....nikuambie tu ntahama kwa mapenzi tu au sababu nyingine ya kisiasa ila sio PESA

Bwahahahahahahaaaa[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwanini?Kama anapigania Tumbo lake kwanini uache kunywa na kula?

Hivi ng'ombe akirudi zizini alikozoea kuna shida?Rafiki huyo si mwenzetu pigana na hali yako
Mnajiriwaza poleni sana. Endapo hatahama mtamfurahia na kumpongeza sana. Poleni sana, naona furaha zenu ni za msimu. Dah, Polepole mliyemdharau kwa upole kutokana mwendo pole wake naona taratiiiibu anawamalizia watu pumzi. Kazi imebakia kukalia kujiliwaza na Lissu.
 
Wape faraja kesho... Wanakupenda sana. Kumbuka zile kura million 6 na ushee kumbuka matusi kashfa na kejeli na tuhuma lundo ulizotupiwa... Usije ukawa mwepesi kusahau... Utawaumiza na kuwaliza wengi sana... Usijiwazie wewe... Wawazie hawa watu wanaokupenda sana
Muda unayoyoma watu wamejawa na kihoro kuwa kesho utaongea nini.. Baadhi wanasema maandalizi ya leo kule Pugu hayakuwa ya hasanali bali wewe... Safari yako ya ikulu na matamshi yako yale tayari yameshawasononesha wengi sana... Ni simanzi kila mahali...
Una utashi msimamo na maamuzi binafsi lakini una tafakuri na hekima pia... Kama ukiamua kurudi ccm waweza kwenda.. Hakuna atakayeweza kukuzuia... Lakini utaleta Maumivu kwa mamilioni ya watanzania waliohangaika nawe bega kwa bega usiku na mchana.. Kuna watu si haba wameumizwa kuteswa na kudhulumiwa maisha na mali zao kwa sababu tu ya kukuunga mkono wewe... Usije kuwasahau hawa... Wengine bado wako mahabusu na wengine wanatumikia vifungo usiwasahau pia...
Watanzania wanapitia kipindi kigumu sana.. Wana sononeko na majonzi hawahitaji kuumizwa zaidi.. Wape faraja wafurahi....
Ikishindikana kabisa waweza kwenda.. Watakaobaki wataukomboa wakati...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom