Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Wape faraja kesho... Wanakupenda sana. Kumbuka zile kura million 6 na ushee kumbuka matusi kashfa na kejeli na tuhuma lundo ulizotupiwa... Usije ukawa mwepesi kusahau... Utawaumiza na kuwaliza wengi sana... Usijiwazie wewe... Wawazie hawa watu wanaokupenda sana.
Muda unayoyoma watu wamejawa na kihoro kuwa kesho utaongea nini.. Baadhi wanasema maandalizi ya leo kule Pugu hayakuwa ya hasanali bali wewe... Safari yako ya ikulu na matamshi yako yale tayari yameshawasononesha wengi sana... Ni simanzi kila mahali...
Una utashi msimamo na maamuzi binafsi lakini una tafakuri na hekima pia... Kama ukiamua kurudi ccm waweza kwenda.. Hakuna atakayeweza kukuzuia... Lakini utaleta Maumivu kwa mamilioni ya watanzania waliohangaika nawe bega kwa bega usiku na mchana..
Kuna watu si haba wameumizwa kuteswa na kudhulumiwa maisha na mali zao kwa sababu tu ya kukuunga mkono wewe... Usije kuwasahau hawa... Wengine bado wako mahabusu na wengine wanatumikia vifungo usiwasahau pia.
Watanzania wanapitia kipindi kigumu sana.. Wana sononeko na majonzi hawahitaji kuumizwa zaidi.. Wape faraja wafurahi..
Ikishindikana kabisa waweza kwenda.. Watakaobaki wataukomboa wakati!