Tetesi: Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM

Tetesi: Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM

Lowasa, Sumaye, Kingunge n.k. wakirejea CCM kutokea CHADEMA sitashangaa kusikia kauli kutoka kwa Mwenyekiti wetu kwamba "acha waende kwakuwa hawakuwa na msaada wowote" na kwamba "sisi tulishasema siku nyingi kwamba ni mafisadi".

Siasa za Tanzania ni sawa na biashara nyingine inayoingiza kipato (ruzuku) hasa pale inapoendeshwa na mfanyabiashara mzoefu dizaini ya Mbowe. Haitakiwi jazba kwenye eneo la biashara. Wanaopandwa jazba ni washabiki na waandamanaji wasioijua biashara yenyewe.
 
Kwani hao watu walirudisha kadi za CCM? Bado nibwanachama hai wa CCM ila wamejitenga tu kwa muda, hawajapewa talaka bado
 
Huwa naamini sana information zako. Tunakumbuka wakati wa uchaguzi uliwaacha watu midomo wazi.
Lizaboni namba ingine ndie alikuwa wa kwanza kuleta taarifa humu kuwa Lowasa ananunua chadema ili agombee uraisi na ikawa kweli.Habari zake huwa naziamini sana .Mark his words.Lowasa atarudi CCM kuna presha kubwa sana hasa kutoka kwa watu wake wa karibu na familia yake.
 
Pamoja na Chadema kupoteza mwelekeo lakini bado mna hofu na Chadema kufanya mikutano nchini kwa kuivuruga kupitia polisiccm. Bado mnahofia uchaguzi huru na wa haki kupitia rasimu ya Warioba na Tume huru ya uchaguzi!!!! Kweli Chadema imepoteza mwelekeo kama bado mnaihofia kiasi hiki.

Aiseeee CHADEMA kimepoteza mwelekeo
 
Lizaboni namba ingine ndie alikuwa wa kwanza kuleta taarifa humu kuwa Lowasa ananunua chadema ili agombee uraisi na ikawa kweli.Habari zake huwa naziamini sana .Mark his words.Lowasa atarudi CCM kuna presha kubwa sana hasa kutoka kwa watu wake wa karibu na familia yake.

Naomba hilo litokee hata leo niione cdm yangu original isiyo na mawaa na ccm ikimbatie majinamizi yake.
 
Uchawi tu kumbe mme mmisi babu wa watu huyo muacheni ni wakwetu mpaka msimu wake uishe. Na atastaf akiwa timu ya waelevu
 
Lowasa arudi CCM ili iweje. Mtu mwenye akili kama Lowasa hawezi kufikiri hilo kwa sasa.
 
Wadau, amani iwe kwenu,

Ni dhahiri kwamba Lowassa na Sumaye hawana amani ndani ya CHADEMA. Hawana dira wala mwelekeo. Kila wanalopanga halipangiki na CHADEMA hakionekani kuwa chama chenye mwelekeo wa kushika dola.

Kamera ya Lizaboni imenasa kikao cha mkakati wa Lowassa kutaka kujiengua na CHADEMA na kurejea CCM. Kwa sasa anaendelea na mazungumzo makali na baadhi ya wafuasi wake waliobaki CCM ambao wamemgomea kwenda upinzani. Kilichomshtua zaidi Lowassa ni hili wimbi la sasa lililoshika kasi la viongozi na wafuasi wa chama ambao aliona kuwa ni kimbilio lake wakimkimbia na kujiunga na CCM.

Je, viongozi wangu watampokea Lowassa? Mimi nasema wasiwe wepesi kukubali ujio wa Lowassa. Ni vema tukafunga gate valve ili asiruhusiwe kurejea tena chamani. Ameshaivuruga CHADEMA na sasa anataka kurejea tena CCM na kutuvuruga. Nasikia anataka kurejea kabla ya uchaguzi wa ndani wa CCM ngazi ya Taifa. Tusiruhusu jinamizi likatukumba tena ndani ya CCM.
Akirudi Lowasa na Sumaye CCM nitaandamana hadi Dodoma nikiwa nimevaa magunia kuirudisha kadi yangu ya CCM
 
Back
Top Bottom