Tetesi: Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM

Lowasa, Sumaye, Kingunge n.k. wakirejea CCM kutokea CHADEMA sitashangaa kusikia kauli kutoka kwa Mwenyekiti wetu kwamba "acha waende kwakuwa hawakuwa na msaada wowote" na kwamba "sisi tulishasema siku nyingi kwamba ni mafisadi".

Siasa za Tanzania ni sawa na biashara nyingine inayoingiza kipato (ruzuku) hasa pale inapoendeshwa na mfanyabiashara mzoefu dizaini ya Mbowe. Haitakiwi jazba kwenye eneo la biashara. Wanaopandwa jazba ni washabiki na waandamanaji wasioijua biashara yenyewe.
 
Kwani hao watu walirudisha kadi za CCM? Bado nibwanachama hai wa CCM ila wamejitenga tu kwa muda, hawajapewa talaka bado
 
Huwa naamini sana information zako. Tunakumbuka wakati wa uchaguzi uliwaacha watu midomo wazi.
Lizaboni namba ingine ndie alikuwa wa kwanza kuleta taarifa humu kuwa Lowasa ananunua chadema ili agombee uraisi na ikawa kweli.Habari zake huwa naziamini sana .Mark his words.Lowasa atarudi CCM kuna presha kubwa sana hasa kutoka kwa watu wake wa karibu na familia yake.
 
Pamoja na Chadema kupoteza mwelekeo lakini bado mna hofu na Chadema kufanya mikutano nchini kwa kuivuruga kupitia polisiccm. Bado mnahofia uchaguzi huru na wa haki kupitia rasimu ya Warioba na Tume huru ya uchaguzi!!!! Kweli Chadema imepoteza mwelekeo kama bado mnaihofia kiasi hiki.

Aiseeee CHADEMA kimepoteza mwelekeo
 
Kamera ya Lizaboni imenasa kikao cha mkakati wa Lowassa kutaka kujiengua na CHADEMA na kurejea CCM.
je kuna ubaya gani kama ni kweli si tutabaki sisi au pia hili hupendi/???????
 

Naomba hilo litokee hata leo niione cdm yangu original isiyo na mawaa na ccm ikimbatie majinamizi yake.
 
Uchawi tu kumbe mme mmisi babu wa watu huyo muacheni ni wakwetu mpaka msimu wake uishe. Na atastaf akiwa timu ya waelevu
 
Lowasa arudi CCM ili iweje. Mtu mwenye akili kama Lowasa hawezi kufikiri hilo kwa sasa.
 
Akirudi Lowasa na Sumaye CCM nitaandamana hadi Dodoma nikiwa nimevaa magunia kuirudisha kadi yangu ya CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…