TANZIA Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea Urais wa CHADEMA 2015) afariki dunia

Nepi Na-Iwe atakanyaga msibani?
Nepi Naiwe atadhubutu kusikitika au kusaini daftari la maombolezo?
 
Apumzike kwa amani Mpendwa wetu EL.
Hakika tutamkumbuka kwa ujasiri na uhodari wake katika kuchapa kazi kwa bidii na maarifa lakini ndiye Kiongozi peekee ukimwacha mzee Ruksa ndiye aliye onyesha uwajibikaji.
Pumzika kwa amani mzee wetu.tutakuombea daima.
 
Huo unakuwaga uongo huyo babayake na Lowasa alikuwa na mali gani miaka hiyo? Na alifanya biashara gani?
Lowasa alikuwa mwizi kama mimi na wewe tukipata fursa ya kufanya hivyo!
Mungu atuokoe! RIP
 
Kwaheri Mzee mwema

Ulisalitiwa na uliowasaidia kuingia ikulu

Ugomvi wenu ukatuepushia yule fisadi mwenzao membe

Mungu akatupeleka kwa mzalendo Magufuli

Wewe na magufuli kazi yenu bado haijakwisha yupo mzalendo ataimalizia
R.I. P Mzee Lowassa. Ni jambo la kufurahisha kuona umetamatisha maisha yako nyumbani, katika hospitali yenye jina la rafiki yako wa muda mrefu, Jakaya Kikwete. Hujawahi kumkosea heshima Kikwete, bila shaka unafahamu zaidi juu ya kilichotokea kati yenu ndo maana mkaendelea kuheshimiana licha ya wapumbavu na wajinga kujaribu kuzusha kila waliloweza....kisa tu kwa sababu wanamchukia Kikwete. Wewe kamwe hujawahi kuwa sehemu yao hao wajinga.

Jema zaidi, uliamua kuwasaidia watu fulani kuinuka kisiasa baada ya kuungana nao kwa muda na kuwapatia wabunge wengi. Baada ya kuondoka mijinga hii inaendelea na ujinga wao km hivi....... Tafadhali iombee ipate akili.
 
R.I.P Mh Edward Lowasa nikikumbuka enzi za kampeni 2015 hasa pale Cruzin Inn ..ile Iman tuliyokua nayo juu yako ..ule Umoja uliokua pale.. lala kwa Aman Mzee wetu
 

Hizi ndio huitwa hoja za nguvu.
 
Huo unakuwaga uongo huyo babayake na Lowasa alikuwa na mali gani miaka hiyo? Na alifanya biashara gani?
Lowasa alikuwa mwizi kama mimi na wewe tukipata fursa ya kufanya hivyo!
Mungu atuokoe! RIP
Kwenye siasa, siku zote kuna watu fulani ambao wao hufananishwa na kete, kisha kuna kundi jingine linalofananishwa na wasuma kete.

Waliopo jikoni na wanaielewa vizuri siasa za hapa Tz hawawezi kumuita Lowassa fisadi kwa sekeseke lile la RICHMOND, yeye alikuwa mfanikishaji tu ila ngoma ilipikwa na KIKWETE na mwisho wa siku ikabidi ajiengue ili kulinda jina la mwenye nguvu wakati huo.

Ulaji ni kawaida unapopata fursa na kila mtu hufanya hivyo kwa nafasi yake, inakuwaje LOWASSA ndio achorwe kama fisadi mkuu wa taifa hili?

Wewe ulielishwa propaganda huko kijijini uliko, endelea kuamini unavyoamini, lakini unatakiwa ujue siasa ni bahari kubwa sana.
 
Wewe pia uliyelishwa hizo propaganda zako endelea kuamini hicho ulichopangiwa kuamini.

R.I.P Lowassa,
Long live JK.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…