R.I.P EN Lowassa
Viongozi wa Umma wanapofariki wanaandikwa kwa mema na mabaya, waliishi kwa ''privilege' ya Umma
Katika mazuri aliyofanyia Taifa ni kuongoza nchi za ukanda wa mto Nile (Riparian states) kupinga Mkataba wa Waingereza na Egypt wa mwaka 1929 kuhusu matumizi ya maji ya mto Nile.
Akiwa Waziri wa Maji na Mifugo ,Lowassa alisimama kidete kuhakikisha maji ya Ziwa Victoria yananufaisha Taifa. Mpango wa Maji ya Victoria Dodoma ni matokeo ya kazi hiyo.
Waanaofaidika na miradi wa maji ya Ziwa Victoria ni kazi ya Lowassa, tunamkumbuka na kumshukuru kwa hilo
Katika mambo mabaya aliyofanya ni kusimama Bungeni kama Waziri Mkuu kupinga KATIBA MPYA akisema iliyopo inatosha ingawa alijua si kweli. Alisimama kutetea Uwaziri mkuu wake na si masilahi mapana ya nchi.
Pili, akiwa Bungeni kama Waziri Mkuu alitetea Richmond kwamba hakuna Wizi. Leo tunajua kulikuwa na wizi ya kutisha si kwa Richmond n.k. Lowassa aliogopa sana Uwaziri mkuu wake kuliko masilahi mapana ya nchi. Hakutetea nchi alitetea hali yake ya baadaye ya Urais
Tatu, ENL alikuwa na matamanio zaidi ya uongozi kuliko wito.
Katika hilo, alifanya makosa mengi kwasababu tu alilenga Urais wake na si masilahi ya nchi.
Muda wake umetimu, tumtakie safari njema, kwamba kuna cha kumkumbuka sana!! linabaki swali
JokaKuu Pascal Mayalla Mag3