10 February 2024
DKT. PHILIP MPANGO :UGONJWA ULIOMUUA LOWASSA NI UTUMBO KUJIKUNJA, TATIZO LA MOYO na MAPAFU - ''BENDERA ITAPEPEA NUSU MLINGOTI SIKU 3''...
View: https://m.youtube.com/watch?v=Fxp57GI_-NA
WASIFU WA MWENDAZAKE HON.
EDWARD NGOYAI LOWASSA
Hon. Edward Ngoyai Lowassa
Na Gabriel Kabamba
Edward Ngoyai Lowassa alizaliwa 26/08/1953, katika kijiji cha Ngarashi Wilaya ya Monduli mkoani Arusha Tanzania na kukulia hapo.
Ndiye mtoto mkubwa wa Kiume katika familia ya mzee Ngoyai Lowasa.
Alipata elimu ya msingi katika shule ya Monduli kati ya mwaka 1960-1966, Jemedari huyu alifaulu kwa kishindo na kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Arusha mnamo mwaka 1967-1971 alipohitimu kidato cha nne.
Nguli huyu alifanikiwa tena kufaulu kwa kiwango cha juu na kuchaguliwa shule ya sekondari Mirambo (Tabora) kwa kidato cha tano hadi cha sita mnamo mwaka 1971-1973.
Mnamo mwaka 1977 alihitimu Shahada ya kwanza ya Sanaa katika chuo kikuu cha Dar es Salaam UDSM, hakuishia hapo bali alifanikiwa kuchukua shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Bath nchini Uingereza mnamo mwaka 1984.
Edward Lowassa amejaaliwa kupata watoto wa tano na mke wake kipenzi Bi: Regina Lowasa. Watoto watatu wa Kiume na wawili wa kike. Wote wamejaa hekima na busara kama baba yao na mama yao.
Bwana Edward Ngoyai Lowasa ni zao la Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada mwaka 1977 baada ya kuhitimu masomo yake aliajiriwa na CCM kama Katibu msaidizi na baadaye Katibu wa Wilaya. Kutokana na umahiri, uhodari na uchapakazi wake makini
Lowasa alipata nafazi ya kuwa msaidizi wa mzee Rashidi Mfaume Kawawa, balozi Daudi Mwakawago na katibu mkuu wa CCM ndugu Horace Kolimba.
Edward Lowassa sambamba na Jakaya Mrisho Kikwete na comrade Abdulrahman Omar Kinana walifanya kazi pamoja jeshini. Mwaka 1978/1979 nguli huyu alipambana vita dhidi ya nduli Idd Amin Dada na kuwa miongoni mwa wanasiasa wachache hapa Tanzania waliopambana vita hivyo kwa uhodari mzuri.Alifanikiwa kutoka jeshini akiwa na cheo cha LUTENI.
EDWARD NGOYAI LOWASSA ALISHIRIKI VITA VYA KAGERA
Ninamfahamu vizuri Edward Lowassa. Nilibahatika kuwa mmoja wa Walimu wake wa Siasa alipokuwa Afisa Mwanafunzi Kundi la Nane (Intake 08) mwaka 1978 katika kilichokuwa kinaitwa Chuo cha Taifa cha Uongozi (CTU), Wilaya ya Monduli. Alipata Kamisheni ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania mwaka huo huo 1978.
Akiwa Luteni, Edward Lowassa alishiriki kikamilifu Vita vya Kagera akiwa 206 KV (Kundi la Vikosi) chini ya Brigedia Jenerali Silas Mayunga. Baadaye Kundi la Vikosi 206, liliongezewa nguvu maradufu na kupewa jina la Task Force, likiongozwa na Meja Jenerali Silas Mayunga.
Task Force ilifanyika kazi kwa weledi na ujasiri mkubwa na kufanikiwa kukomboa maeneo yote Magharibi ya Uganda hadi kuukamata mji wa Koboko uliopo mpakani mwa Uganda na Sudani Kusini, alikozaliwa Nduli Iddi Amin. Koboko ilikombolewa tarehe 3 Juni 1979, siku inayohesabiwa kama ndiyo mwisho wa Vita vya Kagera.
Mimi nilikuwa Afisa Mnadhimu Makao Makuu ya Task Force na kipindi chote hicho tulikuwa naye Lt Edward Ngoyai Lowassa.
Lt Col Patrick Marwa Nyaborogo (Mstaafu)
Tel: 0789 392013
Email:nyaborogopm@gmail.com
Kwa nchi nyingi duniani, hii ni sifa muhimu ya ziada kwa mtu yeyote anayewania uongozi wa nchi kwa sababu kushiriki kupigana vita huchukuliwa kuwa ni kiwango cha juu kabisa cha uzalendo kwa kuwa tayari kuifia nchi.
Edward Ngoyai Lowasa aliingia katika siasa za kiserikali mwaka 1985 alipoteuliwa kuwa mbunge wa vijana, sambamba na aliyekuwa spika Anne Makinda na Jenerali Twaha Khalifani Ulimwengu. Akiwa bado mbunge mwaka 1989 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Arusha (AICC) ambako alidumu hadi mwaka 1990.
Alipishinda ubunge jimbo la Monduli, mh. Edward Lowassa aliteuliwa kuwa waziri katika ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais akishughulikia Mahakama na Bunge 1990-1993, yaani alichaguliwa kuwa Mbunge na papo hapo akachaguliwa kuwa Waziri. Hii ni kutokana na Uhodari wake katika utumishi.
Mwaka 1993-1995, aliteuliwa kuwa Waziri wa nyumba na makazi na Maendeleo ya Jamii. Mwaka 1997 aliteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa waziri katika ofisi ya makamu wa rais akishughulikia mazingira na umasikini. Mwaka 2000 hadi 2005 alikuwa waziri wa maji na maendeleo ya mifugo.
Aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa waziri mkuu 30/12/2005 nafasi aliyodumu nayo hadi i 7/02/2008 alipojiuzulu baada ya kashfa ya umeme Richmond.
Source : Imeandaliwa na Gabriel Gibson Kabamba kwa msaada wa vyanzo mbalimbali vya habari
Source :
'' - I had been privileged to take part in defending our state (Tanzania) where I fought in Uganda war (1978).'' Edward Lowassa.
Maktaba :
2014 8 March
DAKIKA 45 ITV NA MH. LOWASSA
View: https://m.youtube.com/watch?v=E7-hDA6d_4Y
Mh. Edward Lowassa mbunge wa Monduli na aliyekuwa waziri mkuu akiwa ni mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ulinzi, usalama na mambo ya nje ya bunge la Muungano. Sehemu ya kwanza.